Mungu anaifahamu vema katiba Yetu; alimtwaa JPM huku akijua VP ndiye atakuwa Rais wetu. Watanzania tupokee hii zawadi kwa mikono miwili

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,622
2,459
Mungu hutembea katika maagano, maagano ambayo hufanyika Kati yake na wanadamu aliowaumba akawapa thamani ya Kwanza Kati ya viumbe vyake Vyote.

Mandalio ya moyo ni ya Mwanadamu, lakini jawabu la hayo latoka kwa Mungu.

Mungu anaifahamu fika katiba Yetu, na kwamba hawezi kuruhusu kifanyike kitu bila ya kuwepo mbadala wake!! Alimtwaa mtumishi wake JPM huku akijua ajaye atafiti na atakuwa Bora.

Watanzania, Tumepewa Mama, Tumepewa Rais shupavu, Tumepewa mtu sahihi Kwa nyakati hizi, Tumepewa mlezi na mwenye huruma, hizo ni sifa za mama yeyote duniani.

Ukiachilia mbali hayo, ninalo la kushauri Kwa Raisi wetu.

Mh, Rais, ukweli kwamba, maneno huumba, nyakati za kabla ya uchaguzi 2015, Watanzania wakiongozwa na Upinzani, Kwa ujumla wake, kuna Mahali tulikuwa tumechoka mno, tulichoka na dhuruma, tulichoka na wizi na ufisadi, Tulichoshwa na ujambazi wa Wakati wowote, Tulichoshwa na wauza madawa ya kulevya, Tulichoshwa na rushwa, Tulichoshwa na huduma mbovu kwenye karibu sector zote,tulichoka na Uonevu, tulinyanyasika, mahakamani hapakuwa na haki, Huna hongo husikilizwi, ukweli tulichoka.

Na tulipochoka, Tukaamini kwamba, Wakati tulionao ni wakati wa kuchagua Raisi asiyevumilia hayo.

Tukataja sifa inayombeba huyo mtu atakayetuongoza, Sifa yake kuu, awe ni mithili ya Dicteta, mkali, asiyechekacheka!

Hilo ndilo likawa bango katika myoyo ya Watanzania, na Kwa Mungu Neno Hilo likapigwa mhuri, na matokeo yake kila mtu anajua.

Na sasa, maneno meengi yameanza kupita humu kudai Rais huyu hawezi, sijui tunarudishwa enzi za machozi ya Watanzania kulilia urithi wao kuishia Kwa mabepari, kulilia haki zao n.k, hizi kauli nazikataa kupitia majina yote ya Mungu wetu, wewe unaweza na Mungu amekuamini, simama kama shujaa na usiogope kwani Mungu Yuko upande wako.

Raisi wetu aliyetangulia Mbele za haki, siwezi kumhukumu hata chembe moja, Kwa kuwa tulimuomba kwako Mungu na wewe ukatupatia.

Raisi wetu huyo, amefanya mengi mema na yametufaa Sana kama Taifa, lkn pia ukweli hakuwa malaika, yako na mengine ambayo kafanya ni mabaya.

Nilichojifunza kwake ni kitu kimoja chenye nguvu ya kubadiri kila Hali yetu ya umasikini na kuelekea utajiri, na ndicho nachotaka nikusihi Mh Raisi wetu, hata usipofanya mengine, Ile kauri ya Sisi sio Masikini, Tanzania sio Masikini,Tunaweza kila kitu na kwamba tunaweza siku moja kuwa nchi ya kutoa misaada, hii kauli ni kauli ya kimamlaka na Ufalme usioabudu shetani, maana ukweli ni kwamba, Mungu alitukamilisha na ametupa Vyote hivi vilivyopo ili tujikwamue, Kwa akili alizotupa, tunaweza kila kitu tukiamua kuzitumia akili pamoja na uthubutu na kutoyumba!

Na usimuonee aibu yeyote anayejaribu kukuyumbisha, utafanya makuu Sana, upo hapo kwa kusudi maalmu, ni kama ilivyokuwa Kwa Ester Chini ya mpinzani wao mkubwa Naamani, na wewe Mh upo hapo Chini ya Upinzani mkubwa wa mafisadi ambayo yanatumia kila Mbinu kujaribu kukutikisa.

Tanzania tuko nyuma yako Mh Rais.

Mungu bariki Tanzania
 
Tabia ya kumsingizia Mungu katika kila jambo ni ya hovyo sana.Hivi aliyekuambia Shetani hawezi kusimika Wafalme ni nani? Unawakumbuka akina Julius Caesar, Napoleon, Mafarao, Mobutu, Falme za Ulaya, Xi na wengi wengine waliokuwepo na waliopo?Hawa walisimikwa na Shetani.

Unakumbuka Bwana Yesu alipopandishwa angani na Shetani, akaonyeshwa falme zote za dunia akaambiwa haya yote nitakupa kama ukiniabudu? Bwana Yesu hakukataa kwamba kweli Shetani anaweza kumpa ufalme, ila alimjibu kwamba ondoka kwangu Shetani, imeandikwa kwamba utamuabudu Mungu peke yake. So Shetani anaweza kukupa ufalme ukitimiza masharti yake.
 
Tabia ya kumsingizia Mungu katika kila jambo waliopo,hovyo sana.Hivi aliyekuambia Shetani hawezi kusimika Wafalme ni nani?Unawakumbuka akina Julius Caesar,Napoleon,Mafarao,Mobutu,Falme za Ulaya,Xi na wengi wengine waliokuwepo na waliopo?Hawa walisimikwa na Shetani.

Unakumbuka Bwana Yesu alipopandishwa angani na Shetani,akaonyeshwa falme zote za dunia akaambiwa haya yote nitakupa kama ukiniabudu?Bwana Yesu hakukataa kwamba kweli Shetani anaweza kumpa ufalme,ila alimjibu kwamba ondoka kwangu Shetani, imeandikwa kwamba utamuabudu Mungu peke yake.So Shetani anaweza kukupa ufalme ukitimiza masharti yake.
Kwa sababu huna uhakika na Hilo, wenye Imani tuache tusonge
 
Kwa sababu huna uhakika na Hilo, wenye Imani tuache tusonge
Unajua mkuu,imani zingine misingi yake ni very shaky.Mkuu kwangu mimi imani kwamba mama Samia anaweza kutuvusha salama haipo.
Kwa sababu huna uhakika na Hilo, wenye Imani tuache tusonge
Sawa mkuu,ila imani zingine ziko based on very shaky ground.
 
Kwahio kwa imani yako ni kwamba hayupo Pro-active yaani anangoja shida itokee ndio analeta dawa, Yaani ni Re-active
 
Tabia ya kumsingizia Mungu katika kila jambo ni ya hovyo sana.Hivi aliyekuambia Shetani hawezi kusimika Wafalme ni nani? Unawakumbuka akina Julius Caesar, Napoleon, Mafarao, Mobutu, Falme za Ulaya, Xi na wengi wengine waliokuwepo na waliopo?Hawa walisimikwa na Shetani.

Unakumbuka Bwana Yesu alipopandishwa angani na Shetani, akaonyeshwa falme zote za dunia akaambiwa haya yote nitakupa kama ukiniabudu? Bwana Yesu hakukataa kwamba kweli Shetani anaweza kumpa ufalme, ila alimjibu kwamba ondoka kwangu Shetani, imeandikwa kwamba utamuabudu Mungu peke yake. So Shetani anaweza kukupa ufalme ukitimiza masharti yake.
so shetani ndio ametupa ufalme mpya?
 
so shetani ndio ametupa ufalme mpya?
Usiniwekee maneno mdomoni Detective tafadhali.Nime elezea wazi kwamba Ufalme pia una weza ukawekwa na Shetani,kwa hiyo watu wasi singizie kwamba kila mara Mungu ndiye anaye simika ufalme.Please note,sijasema huu ufalme wa sasa umewekwa na Shetani.I repeat,usiniwekee maneno mdomoni.
 
Back
Top Bottom