Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Nilimsikia Fred Lowassa katika salaam zake za rambirambi pale Karimjee Hall, akitoa shukurani zake za dhati Kwa Rais Samia Kwa matibabu ya Baba yake, Hayati Edward Lowassa na kwenda mbali zaidi Kwa kutamka kuwa kama siyo Kwa msaada mkubwa aliotoa Rais Samia, baba yake asingeweza kufikia majuzi, wakati Mungu alipotwaa roho yake
Nimejiuliza maswali kadhaa kuhusu kauli hiyo ya mtoto wa Hayati Edward Lowassa, alikuwa akimaanisha Nini?
Najua wazi kuwa Hayati Edward Lowassa, kutokana na nyadhifa mbalmbali alizoshika hapa nchini, ikiwemo Waziri Mkuu mstaafu alistahili kupata Huduma hiyo ya matibabu katika kiwango Cha "first class"
Sasa najiuliza hivi Rais Samia alichofanya Cha ziada katika matibabu ya Hayati Lowassa ni kipi??
Swali la pili najiuliza, iwapo Rais Samia, aliidhinisha malipo ya ziada Kwa matibabu ya Lowassa, hizo sifa zilipaswa zitujie sote wananchi wa nchi hii, Kwa kuwa yeye Rais Samia, hakutoa pesa hizo kutoka mifukoni make, Bali "alizichota" kutoka kwenye hazina yetu ya Taifa, ambazo ni pesa za walipa Kodi wa sisi wananchi wa nchi hii
Hata hivyo namkosoa Fred Lowassa alipotamka kuwa kama siyo Rais Samia, Basi baba yake asingeweza hata kufikia siku hiyo aliyofariki!
Anachosahau Fred Lowassa, ni kuwa sisi binadamu wote, tunahesabiwa siku zetu za kuishi hapa duniani na Mungu pekee!
Kwa mawazo ya Fred Lowassa, kama Rais Samia, ndiye amerefisha maisha ya baba yake, ambaye amefikisha umri wa miaka 70 hadi pale alipofariki, basi tusingeweza kuwapata maelfu ya wazee masikini wasio na kitu, wanaishi hadi miaka zaidi ya 100
Ujumbe wangu Kwa sisi binadamu, tunapaswa kwanza kutoa shukurani Kwa Mungu aliyetuumba, Kwa lolote jema linalotutokea hapa duniani, badala ya kutoa sifa Kwa binadamu wenzetu, ambao nao wameumbwa na Mungu wetu