Mungu amenipa nafasi nyingine ya kumtumikia na kutumikia watu wake. Praise be to God!

Aug 7, 2014
8
95
Wengi mtakuwa mlisikia juu ya ajali mbaya niliyopata mimi na makamanda wengine watatu tukielekea kwenye mkutano wa hadhara, Geita. Ni moja ya ajali mbaya kiasi kwamba kila mtu akiona gari lilivyoharibika hakuna anayeamini kuna aliyebaki salama.

Namshukuru Mungu sana aliyesikia maombi yetu tulipomlilia tangu gari lilipoacha njia. NI HAKIKA MUNGU ALIKUWEPO NDANI YA GARI LILE NA MUNGU AMETENDA MUUJIZA.
Nawashukuru sana kwa dua na maombi yenu tuko hai na tunaendelea vizuri sana.

Lengo langu kwa leo sio kuiongelea ajari ile, ninachokusudia kusema ni kwamba kama ajari ile ingeniua, kuna mambo mengi ya msingi ambayo yangehairishwa kufanywa. La msingi kuliko vyote nisijamtumikia Mungu vya Kutosha na utoaji wa elimu ya uraia, sijafanya kwa kiwango cha kukata kiu yangu.

Ninacholenga kuongelea hapa ni juu ya kukomboa wakati na kufanya kazi kana kwamba hatutapata muda mwingine tena,kutokuhairisha mambo kwa visingizio visivyo vya msingi maana kesho yaweza kuwa sio yako. Kama tungeunganisha muda wote tunaopoteza kwa visingizio dhaifu tungegundau nusu ya maisha yetu tumepoteza bila kazi za msingi.

Namshukuru Mungu kwa ulinzi wake na kunipa nafasi nyingine,namwahidi kumtumikia kwa nguvu zaidi,Namwomba Mungu kunijalia hekima na maarifa kutumikia watu wake wa dunia hii kwa uadilifu.

Namwahidi Mungu kuendeleza kukemea maovu yanayotendeka na kuwaelimisha watanzania wenzangu juu ya haki na wajibu wao na mimi kujielimisha mwenyewe kwa bidii.

Natoa wito kwenu rafiki zangu tusiwe wavivu,tusiweke matumaini yetu kwa kesho, linalowezekana leo lisingoje kesho.

Nawashukuru sana kwa maombi yenu na salamu za pole nilizopata kwa njia ya simu, Jamii forums, Facebook na njia zinginezo.
Ndugu zangu mmenionesha upendo mkubwa sana, mbarikiwe wote kwa kujali sana. Mmeigusa roho yangu kwa namna ya pekee; Nimejiona napendwa.

Mungu awabariki sana na awape furaha katika maisha yenu.

Mbarikiwe sana,
Upendo Furaha Peneza
 
Asante sana upendo furaha pendeza , Mungu kakuponya sababu anajua kuna mchwa(CCM) wanaotafuna mali za umma hivyo wanahitaji kusambaratishwa,

Hapo mwanzo walizoea kutumia uchawi lakini kwa bahati mbaya kwao ni kwamba imeandikwa kwamba "kizazi cha mwanamke kitamponda yule joka kwa kisigino" so tusichoke kabisa kukiangamiza kizazi hiki cha mchwa na nzige(CCM), kwa kuhakikisha tunatengua mashauri yao maovu juu ya nchi yetu, tuhakikishe kwamba wote tunawatawanya kwa njia saba mpaka kieleweke.

CHADEMA NI FUNGU JEMA
CHAGUA FUNGU JEMA LEO.
 
Last edited by a moderator:
Ni KWELI TUPU Mungu ni upendo na Furaha yake ni nguvu zetu !

Nakutakia uwe na afya njema kama shujaa pamoja na Mungu
 
Last edited by a moderator:
Heko mdada, ni vyema kurudisha sifa na utukufu kwa Mwenyezi Mungu yeye aliyemuumba wa vitu vyote, kwani kila jambo linalotukia hapa duniani ni kwa makusudi yake na wala si kwa mipango yetu sisi wanadamu

Ni wakati wa kutafakari na kujiuliza kama ulivyosema yawezekana mwenyezi Mungu ameamua kuwacha ili kuwakumbusha kazi mliyoapa kuitekeleza mnaikamilisha kwa wakati na kwa nguvu kama mlivyoanza. Yewezekana kuna kulegalega kulikokua kukitokea hivyo tukio hilo la Ajali liwe kengere ya Alarm kukukumbusheni wajibu mlioapa kuutekeleza liwake jua inyeshe mvua. Nikutakie kila Lakheri dada Upendo Furaha Peneza ktk majukumu yako kichama na kimaisha..

God bless you my dada...

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Mungu ni mwema amekulinda na kukupa uhai ili uimalizie kazi. Mungu hawezi kukuchukua kabla haujamaliza kazi aliyokutunuku kuifanya
 
Acheni utapeli mnawatumikia wanasiasa halafu mnajitia mnawatumikia wananchi. Mungu hakuwepo kwenye ajali ya matapeli. Mmepewa pesa na wanasiasa ili muwafanikishie malengo yao ya kula kwa zamu,hayo hamuyafanyi bure
 
Kazi aliyoifanya Mandela si unaiona ndugu yangu wewe asiye elewa! Na yeye alikuwa analipwa na wana siasa! Na hao wanalipwa na wana siasa ili kukamilsha majukumu kama hayo ya Mandela! Fikiri kuliko kuwaza as if umekulia ktk nchi ya jirani!
 
nani wa kumfananisha na Mandela hapo? Mandela is someone else not blabla,aliishi kwa taabu jela kwa msimamo wake,Mandela hakuwa muongo,mzushi wala dikteta. Mandela amewahi kunyang'anya mtu mke? Mandela ni icon ya Africa kama kina Nyerere,Nkurumah,Sekou Toure,Kaunda hata sijui kama unawajua hawa zaidi ya Slaa na Mbowe
 
upendo peneza elimu ya uraia ambayo kwako la ni ra utawapotosha raia manake utawaita laia. Pole kwa ajali lakini usimkufuru Mungu kwani siku zilikuwa hazijatimia au kura hazikutosha vinginevyo ziraili angechukua tu...nakushauri eneda darasani ujifunze lafudhi ili usituchanganye maana hatujui ajari tunajua ajali...
Wengi mtakuwa mlisikia juu ya ajari mbaya niliyopata mimi na makamanda wengine watatu tukielekea kwenye mkutano wa hadhara,Geita. Ni moja ya ajari mbaya kiasi kwamba kila mtu akiona gari lilivyoharibika hakuna anayeamini kuna aliyebaki salama,Namshukuru Mungu sana aliyesikia maombi yetu tulipomlilia tangu gari lilipoacha njia.NI HAKIKA MUNGU ALIKUWEPO NDANI YA GARI LILE NA MUNGU AMETENDA MUUJIZA.
Nawashukuru sana kwa dua na maombi yenu tuko hai na tunaendelea vizuri sana.

Lengo langu kwa leo sio kuiongelea ajari ile,ninachokusudia kusema ni kwamba kama ajari ile ingeniua,kuna mambo mengi ya msingi ambayo yangehairishwa kufanywa. La msingi kuliko vyote nisijamtumikia Mungu vya Kutosha na utoaji wa elimu ya uraia, sijafanya kwa kiwango cha kukata kiu yangu.

Ninacholenga kuongelea hapa ni juu ya kukomboa wakati na kufanya kazi kana kwamba hatutapata muda mwingine tena,kutokuhairisha mambo kwa visingizio visivyo vya msingi maana kesho yaweza kuwa sio yako. Kama tungeunganisha muda wote tunaopoteza kwa visingizio dhaifu tungegundau nusu ya maisha yetu tumepoteza bila kazi za msingi.

Namshukuru Mungu kwa ulinzi wake na kunipa nafasi nyingine,namwahidi kumtumikia kwa nguvu zaidi,Namwomba Mungu kunijalia hekima na maarifa kutumikia watu wake wa dunia hii kwa uadilifu.
Namwahidi Mungu kuendeleza kukemea maovu yanayotendeka na kuwaelimisha watanzania wenzangu juu ya haki na wajibu wao na mimi kujielimisha mwenyewe kwa bidii.

Natoa wito kwenu rafiki zangu tusiwe wavivu,tusiweke matumaini yetu kwa kesho,linalowezekana leo lisingoje kesho.

Nawashukuru sana kwa maombi yenu na salamu za pole nilizopata kwa njia ya simu, Jamii forums,Facebook na njia zinginezo.
Ndugu zangu mmenionesha upendo mkubwa sana,mbarikiwe wote kwa kujali sana. Mmeigusa roho yangu kwa namna ya pekee,Nimejiona napendwa.
Mungu awabariki sana na awape furaha katika maisha yenu.

Mbarikiwe sana,
Upendo Furaha Peneza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom