Naongea na nyie wanaume wenzangu ambao mnajifanya mnajua kupenda kila kitu ''ngoja nikamuulize waifu'' hata kumtumia mamako chochote unaenda kuuliza waifu uzezeta huo, halafu mbona siku hizi wanaume tumekuwa mdebwedo hivyo hatuna ule uanaume(kichwa cha familia) matokeo yake tunaendeshwa kwa kutumia remote au limbwata zinafanya kazi kumbukeni mwanamke si ndugu yako, na Mungu alisema tuishi nao kwa akili.
1 Petro 3-5
Neno: Bibilia Takatifu
Mafundisho Kwa Wake Na Waume
3 Kadhalika ninyi wake, jinyenyekezeni chini ya waume zenu, ili kama wako wasioliamini neno, wapate kuamini kwa kuvutiwa na mwenendo wa wake zao. Hawatahitaji kuambiwa neno 2 kwa sababu wataona maisha yenu safi na ya kumcha Mungu.
3 Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje, yaani: kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu na kuvaa mavazi maridadi. 4 Bali kujipamba kwenu kuwe katika utu wa ndani wa moyoni, kwa uzuri usioharibika, wa roho ya upole na utulivu. Uzuri wa namna hii ni wa thamani sana mbele za Mungu. 5 Maana ndivyo walivyojipamba wanawake wata katifu wa zamani, waliomtumaini Mungu na kuwa wanyenyekevu kwa waume zao.6 Kama Sara alivyomtii mumewe Ibrahimu, akamwita ‘bwana’. Ninyi sasa ni binti zake Sara kama mkitenda mema pasipo kuogopa tishio lo lote.
7 Kadhalika ninyi waume, ishini na wake zenu kwa kuwahurumia, mkitambua ya kuwa wao ni dhaifu na hivyo muwape heshima, kwa maana ninyi ni warithi pamoja nao wa neema ya uzima. Fanyeni hivyo ili sala zenu zisizuiliwe.
Msilipe Ovu Kwa Ovu
8 Hatimaye, ninyi nyote muwe na nia moja, mhurumiane, mpen dane kama ndugu, muwe na mioyo ya upole na ya unyenyekevu. 9 Msi lipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; ila barikini kwa maana hili ndilo mliloitiwa na Mungu, mpate kurithi baraka. 10 Kwa maana, “Mtu anayependa kufurahia maisha, na anayetamani kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya na midomo yake isi seme uongo. 11 Mtu huyo aepuke maovu, na atende mema; atafute amani na kuifuatilia sana.12 Kwa maana macho ya Bwana huwaele kea wenye haki, na masikio yake husikiliza sala zao. Bali Bwana huwapa kisogo watenda maovu.”
Kuvumilia Mateso
13 Basi, ni nani atakayewadhuru ikiwa mna juhudi katika kutenda mema?14 Lakini hata kama mtateseka kwa ajili ya haki, mtabarikiwa. Msiogope vitisho vyao wala msiwe na wasiwasi, 15 bali mioyoni mwenu mtukuzeni Kristo Bwana. Kila wakati muwe tayari kumjibu mtu ye yote atakayewauliza kuhusu tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa unyenyekevu.
16 Dhamiri zenu ziwe safi ili mnapotukanwa, hao wanaotukana mwenendo wenu mwema katika Kristo, waone haya. 17 Maana ni afad hali kupata mateso kwa kutenda mema kama hayo ndio mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu. 18 Maana Kristo pia alikufa mara moja tu kwa wakati wote; mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili atulete kwa Mungu. Mwili wake uliuawa lakini akafanywa hai katika roho yake. 19 Naye akiwa katika roho alik wenda kuhubiria roho zilizofungwa kifungoni. 20 Roho hizo zamani hazikutii, siku zile Mungu aliposubiri, wakati Noe alipojenga safina, watu wachache, yaani watu wanane, wakaokolewa katika ile gharika ya maji. 21 Maji hayo ni kielelezo cha ubatizo ambao sasa unawaokoa ninyi, si kwa kuondoa uchafu kwenye miili yenu, bali kama dhamana ya kuwa na dhamiri njema kwa Mungu kwa ajili ya kufufuka kwa Yesu Kristo. 22 Yeye amekwenda mbinguni, na amekaa upande wa kulia wa Mungu pamoja na malaika, mamlaka na nguvu zote zikiwa chini yake.
Maisha Mapya
4 Basi kwa kuwa Kristo aliteseka katika mwili, ninyi pia jiimarisheni kwa nia hiyo hiyo kwa maana mtu aliyekwisha kuteseka katika mwili hana uhusiano tena na dhambi. 2 Matokeo yake ni kwamba, kwa muda wa maisha yake yaliyobakia hapa duniani, haishi tena kwa kufuata tamaa mbaya za mwili bali anaishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu. 3 Maana mmekwisha kutumia muda wa kutosha katika maisha yenu yaliyopita mkifanya yale ambayo watu wasiomjua Mungu hupenda kutenda: uasherati, tamaa mbaya, ulevi, karamu za ulevi na ibada ovu za sanamu. 4 Wanaona ajabu kwamba sasa hamshi riki tena pamoja nao katika ufisadi wao wa kinyama, nao huwatu kana. 5 Lakini itawabidi kujieleza mbele zake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. 6 Kwa maana hii ndio sababu Injili ilihubiriwa hata kwa hao waliokufa: wahukumiwe kama wana damu wengine kuhusu maisha yao katika mwili, bali wapate kuishi katika roho kama Mungu aishivyo.
Kuja Kwa Kristo Kumekaribia
7 Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo muwe na akili timamu na wenye kiasi ili mweze kuomba. 8 Zaidi ya yote, pen daneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika dhambi nyingi sana. 9 Karibishaneni pasipo manung’uniko. 10 Kila mmoja na atumie kipawa alichopewa kuwahudumia wengine, kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu. 11 Mtu akisema kitu, basi na awe kama anayesema maneno halisi ya Mungu. Mtu anayetoa huduma na ahudumu kwa nguvu apewayo na Mungu; ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo. Yeye ni mwenye utukufu na uweza, milele na milele. Amina.
Kuteseka Kwa Mkristo
12 Wapendwa, msishangae kwa ajili ya mateso makali yanayowa pata kana kwamba ni kitu kigeni kinawatokea. 13 Bali furahini kwamba mnashiriki katika mateso ya Kristo, ili mpate kufurahi na kushangilia wakati utukufu wake utakapofunuliwa. 14 Kama mkilau miwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa Utukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa juu yenu. 15 Lakini asiwepo mtu ye yote kati yenu ambaye atateswa kwa kuwa ni mwuaji, au mwizi, au mhalifu au anayejiingiza katika mambo ya watu wengine. 16 Lakini kama mtu akiteseka kwa kuwa ni mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu kwa jina hilo. 17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya watu wa Mungu; na kama itaanza na sisi, mwisho wa hao ambao hawatii Injili ya Mungu utakuwaje? 18 Na, “Kama ni vigumu kwa mtu wa haki kuokolewa, itakuwaje kwa mtu asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?” 19 Basi wale wanaoteswa kufuatana na mapenzi ya Mungu, wajikabidhi kwa Muumba wao aliye mwaminifu.
Maagizo Kwa Wazee Na Vijana
5 Ninawasihi wazee waliomo miongoni mwenu, nikiwa mzee mwenzenu na shahidi wa mateso ya Kristo na mshiriki katika utu kufu utakaofunuliwa. 2 Lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, si kwa tamaa ya fedha bali kwa moyo wenu wote. 3 Msijifanye mabwana wakubwa kwa wale mnaowa chunga bali muwe vielelezo kwa kundi hilo. 4 Naye Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa mtapokea taji ya utukufu isiyofifia.
5 Kadhalika ninyi vijana watiini wazee. Jivikeni unyenyekevu, mnyenyekeane kwa maana, “Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa neema wanyenyekevu.” 6 Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu wenye nguvu, ili wakati wake ufaao utakapotimia, awainue.
7 Mwekeeni yeye fadhaa zenu zote kwa maana yeye hujishughul isha sana na mambo yenu.
8 Kaeni macho. Kesheni, maana adui yenu Ibilisi, huzunguka- zunguka akinguruma kama simba, akitafuta mtu atakayemmeza. 9 Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkifahamu kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayo hayo. 10 Na mkisha kuteseka kitambo kidogo, Mungu wa neema yote ambaye amewaita katika utukufu wake wa milele katika Kristo, yeye mwenyewe atawa kamilisheni na kuwathibitisha na kuwatia nguvu. 11 Uweza ni wake milele na milele. Amina.
Salamu
12 Nimewaandikia kwa kifupi kwa msaada wa Silvano, ndugu ambaye namtambua kuwa mwaminifu, nikiwaonya na kuwashuhudia kuwa hii ndio neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.13 Mwenzenu mteule hapa Babiloni anawasalimu pamoja na mwanangu Marko .
source:
Bible Gateway passage: 1 Petro 3-5 - Neno: Bibilia Takatifu