Hivi hii kauli ya mwanamke ishi nae kwa akili kwako imeekaaje?

Bin wamakamo

Member
Dec 12, 2021
77
92
Hii inshu ya mwanamke ishi nae kwa akili kwako imekaaje? maana imenifanya nitafakari sana
kiutani lakini kwamba ukiacha kutafuta tu pesa basi tuakikishe tunafuta na akili, eeh hapo hapo tutulie kwanza kwani sisi hatuna akili? Sisi wakina abudala vichwa wazi? Tunazo! na kwanini tusisitizwe hapa kwenye wanawake tu na si mahala pengine?

Sasa naanza kufikilia kuwa ndio tuna akili lakini kuna akili zile za kuishi nao, ndizo zimebeba siri kubwa ya maisha kiujumla, najua unielewi kama nimekuacha endelea kubaki hapo hapo!

Basii kuna jamaa kasikia wanawake ishini nao kwa akili, anajua yule mama fulani tu au yule demu wake wa kule kipalang'anda, eboo! ni wanawake ishini nao kwa akili, wanawake hao ni pamoja na dada, mama, shangazi, na huyo mama fulani, yaani hapo baba ni wanawake

Kuna kitu kinaitwa "Kuishi" alafu kuna "kuishi kwa akili" unaelewa au unasoma soma tu embu twende taratibu "kuishi" unaishi tu kwakuwa umebalikiwa uhai na mungu na uko duniani kwa hiyo wewe unaishi tu

Alfu sasa kunakitu kinaitwa "kuishi kwa akili" huku sasa ndo kuishi huku ukijua nini unataka? Nini unafanya? kwasababu gani ufanye? nini hutaki? kipi ni sahihi? kipi si sahihi? ebwana hapa kwenye kuishi kiakili Kuna mambo mengiii hatuto maliza leo, ndio maana watu wengi wanaishi ishi ishi tu

Sasa tunarudi kwenye kauli yetu "wanawake ishini nao kwa akili" duniani kuna mambo mengi sana, kwanini kwenye wanawake tumesisitiziwa tuishi kwa akili? yupo atajitokeza kusema moja kwa moja kwamba wanawake wana matatizo ndomana tumeambiwa tuishi nao kwa akili, unaumwa wewe! umefikilia kwa kina sana hii kauli, ukiingalia kijuu juu tu na kwakuwa wewe umechagua kuishi ishi tu, kauli hii unaweza usiitazame kwa jicho ambalo mimi naitazama, tubakie hapo hapo tukubali tukatae wanawake ukiishi nao kwa akili dunia yote utaiyona ya babaako!

Sasa ukichagua kuishi ishi tu iyo kauli ya "wanawake tuishi nao kwa akili lazima itakuwa ndo kipoza machungu chako.

Haya wale wenzangu wa kuishi ishi tu tuendelee kuishi ishi tu tutafanyaje sasa!

Ila nyinyi mnaotumia akili kuishi , angalieni msije kujikuta izo akili zenyewe amna!

#wamakamo
 
Kama huna akili maana yake huwezi ishi nao badala yake wataishi na wewe
FB_IMG_16878399836697984.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom