"mummy,where is daddy?"

mijanaume bwana yaani inatetea janaume lenzao kutokulea mtoto..........
Mleta mada, zungumza nna mtoto mwambie daddy hawezi kuwa nanyi kwa sasa kwa sababu moja, mbili, tatu (digest in such a way usimuumize mtoto kihisia)

Exactly my point; amwambie baba yuko Japan na anampenda sana. Meanwhile aongee na baba mtoto (tatizo hatujui nini kilitokea) ili afikirie hata kupiga Simu tu aongee na mwanaye.

Unajua starehe zetu halafu tunaleta watoto ambao wanakuwa unhappy inauma sana.

Mwanangu alikuwa ananipa story za wenzake shule; kuna rafiki yake anaumia coz hamjui baba yake. Anampenda step dad lkn anatamani amfahamu biodad wake. My son akasema bora yangu mimi namjua baba yangu; iliniuma sana.
Kuna Mazingira mengi (including failed marriage) yanasababisha watoto wasiwe na wazazi wote, lkn si vizuri kunyima access ya mtoto kwa mzazi mwenzio. Anayeumia zaidi ni mtoto, hawasemi tu.
 
Dah! Apo kama baba kamkataa mwana inakuwa ngumu..inahitaji busara ya ukweli kutoka kwa Mungu!
Ila kwa vyovyote vile usimwambie mtoto kuwa baba yako kakataa kukuona and all that, msaidie kuubeba huo uchungu kama mama, tafadhali!

Kwa sasa mtafute Bujibuji akusaidie kuongea na mwanao hata kwenye simu..baba si lazima yule aliyetoa mbegu tu!!!
 
Last edited by a moderator:
Asante mkuu, nimekupata. Tuzidi kuomba Mungu kwa kweli.
Mwisho wa mwaka mwema Mkuu. Uambar'e Necha.

Sikatai ila omba tu mungu usikutane na kimeo...sio wote wanatelekeza watoto wamependa....inafikia hatua mtu anasema muache akikua atanitafuta...
 
Umenikumbusha mke wa kitombi Beckam,baba ya wanaye akiandikwa kuhusu umalaya wake kwenye magazeti basi Vicky anawakalisha kitako wanae na kuwaambia yote anayosemwa baba yao ni uongo.Anamwagia masifa David he is a good daddy to them.

Namsupport Vicky, children need to be protected hata kwa uovu wa mzazi wao. Wakikuwa wakubwa watajua na wataamua wenyewe!
 

We'll said. Sasa unaweza kuimagine huyo malaika anavyodemand kumjua baba ake ili hali wako eneo moja.. Hii si ni dhambi jamani kah!

Walikuwa kwenye gud times wakatengeneza mtoto huyo sasa makosa ya baba /mama yanamwadhibu mtoto. Wanaume wenye tabia hii acheni bana sio ustaarabu.

Mnajiletega mtoto akishakuwa na life kuja kuchukua mahari, au akiwa amesoma kuwekea heshima bar.. Non sense!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
I knew exactly
What you were going through
,

It's just that I didn't have the
right
To discuss your problems

I
saw you struggling For our education

I saw you
struggling to get us clothes to
wear

mama
This man you got married to is
dead alive


Over the years I asked myself so Many questions

Is he my real
dad or
Was I adopted mama

I know
it's difficult for you mama
But hold on I am a little grown
up now

Lucky dube~hold on lyrics.

Nadhani inaweza kukup mwanga na kujua the way watoto wanavofikiria juu ya wazazi wao wanao behave tofauti.

Ushauri wangu kwako:

Mweleze mwanao ukweli aujue,hiyo itasaidia kuliko unavomdanganya.

Na ukweli uwe kweli ukweli na si vinginevyo.
 
Mpeleke makaburini mwambie amelala hapa muonyeshe kaburi lolote

Aisee hii hapana, bora adanganywe danganywee akishakua kidogo aambiwe ukweli but in apositive way.

Huwezi jua ipo siku baba ake ata demand kumwona hapo wewe ushamwonesha dogo kaburi daaa!
Afu huyo mtoto ni wa 3 years jaman..

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Inanitia hasira kweli hivi vitu. Nikifikiria what a great dad i had when growing up he aint great anymore manake haoni kama na mie nimekuwa mbibi sasa, tunaishia kugombana), ati mwanangu asiwe na baba kwa sababu we are freaking not!
rafiki yangu bintiye wa 5 yrs hivi anakaa na bibi na babu. Out of nowhere alianza kudema babangu alikufa zamani. Wakimumboa baba yupo anasema msinilazimishie. And the sun of a gun yuko mjini anatembeza kengele tu, hajui wanae wanakula nini wala kuvaa nini mwaka wa nne huu. Mie mbona ningemuonyesha na kaburi lisilo na jina kabisa.
 
Mpeleke makaburini mwambie amelala hapa muonyeshe kaburi lolote

Jamani sasa mtoto akikua na kujakujua kuwa baba yake yupo hai si ataumia sana? Kumbukeni kuwa watu hujirudi baadae. Baba anaweza kujirudi na kutaka kuwa karibu na mwanae. Mie nadhani asimdanganye kuwa kafa ila amdanganye kuwa amesafiri kaenda mbali sana na atachelewa sana kurudi. Awe anasema hivyo kila akiulizwa mpaka hapo mtoto atakapopata akili ya kuelewa kwanini baba hayupo pamoja nao.

Btw, mwanaume anayekana au kutelekeza mtoto anaudhi na kuumiza kuliko chochote!
 
Maskini huyo mtoto....ataumia zaidi akienda shule! Nime experiance the same situation but kwangu baba alifariki nikiwa na 3months!! Hebu fanya kumwonesha baba ake bana..!
 

Kumdanganya kuwa babae kafa si vizuri, si sawa hata kidogo. Hata kumzushia kifo mtu yeyote yule si sawa sembuse baba? Hapana kwa kweli.

Btw, mwanaume anayekana au kutelekeza mtoto anaudhi na kuumiza kuliko chochote!

Kila mara humu naongelea uwajibikaji wa wazazi. Na ukweli ni kwamba mzazi yeyote (si wababa tu kwani hata wamama wanaotelekeza watoto wapo wengi tu) anayetelekeza mtoto au watoto ni katili.
 
God give me courage to accept the things can not change, courage to change the things can and wisdom to know the difference


Mwambie ukweli kwamba baba yako yupo na kuna siku atakuja utamuona (dont turn the kid against his father) siku akikua atamtafuta mwenyewe na kama atamkataa hio itakuwa ni makosa yake huyo baba na wewe hapo utafanya kazi tu ya kumuelezea mwanao kwamba baba yake amepotoka na amsamehe
 
Naelewa, lkn Hasira usiniambukize mtoto. Hadi kumpenda baba yake, alikuwa na kauzuri Fulani; so story unazompa ni zile zenye image nzuri, mabaya nayamezea valuer chumbani kimya!

Akiwa mkubwa na uwezo wa kuhandle ukweli mchungu nitamwachia situation aione na aievaluate mwenyewe.

 
tatizo la hao wanaume mtoto akikua na akiwa na nyadhifa fulani,mara huyo mzazi anajigonga,hawajui jinsi gani wanavyowaumiza watoto wakiwa wadogo.kuna kaka mmoja alivyomtelekeza mzazi mwenzake,huyo dada akaenda nje ya nchi.huyo kaka alikuwea hataki hata kusikia habari ya huyo mtoto.mkaka akaoa,hakupata mtoto maisha, wacha aanze kumtafuta yule aliemtelekeza.huyo mtoto wa kike ana chuki na huyo baba,mwenyewe anasema huyu baba wa kambo ndio baba yangu.amenilea vizuri tu{mama yake baadae aliolewa na m congo}huyo baba amemkubali kama mtoto wake.ki ukweli wanaume mnakosea kwa hilo,hata kama hakuna mapenzi na wazazi wenzenu,jaribuni kujenga urafiki ili msiwaumize watoto wenu.u never know in life hao hao watoto wanaweza wakawasaidia wakati wewe mzazi unakuwa huna mbele wala nyuma
 
ki ukweli wanaume mnakosea kwa hilo,hata kama hakuna mapenzi na wazazi wenzenu,jaribuni kujenga urafiki ili msiwaumize watoto wenu.u never know in life hao hao watoto wanaweza wakawasaidia wakati wewe mzazi unakuwa huna mbele wala nyuma

Hapana, siyo wanaume wote wako hivyo na siyo wanawake wote ambao huwapenda watoto wao.

Kwa hiyo wanaume hatukosei kwa sababu wote hatufanyi hivyo. Baba yangu hakukosea hata mara moja. Mimi sijakosea hata kidogo. Wanaokosea ni hao mahsusi wanaowafanyia hivyo wana wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…