Mume wangu simwelewi, hataki kabisa nishike simu yake

Mume wangu simwelewi, hataki kabisa nishike simu yake

Naombeni ushauri,

Kuhusu hii hali mume wangu hataki kabisa ushike simu yake na simu zake zina password na ukimuomba kukutajia anakwambia kabisa hawezi maana kwenye simu zake kuna mambo ya ofisi ambayo mimi sitakiwi kuyafahamu ila ya kwangu haina password na huwa anaishika kama simuoni anapekua sana tu sasa sijui anachoficha ni nini.

Umenichekesha kweli eti kama humuoni anapekua sana ... sasa ilijuaje anapekua akama humuoni au huwa unaacha msyuka pale alipokaa kujua anavyoifanya simu yako!! fanya kazi achana na cm yake kwa sababu haitakusaidia kitu sana sana itaharibu mahusiano yenu...
 
Msemee kwa bashite kama bado hataki kutoa password bashite amuorodheshe kwenye list ya wauza unga.
 
Nakushauri km unataka ndoa basi mambo ya simu ya mumeo achana nayo na kama ushamchoka mume basi endelea kufuatilia simu yake soon utakuja na thread ya kuachwa
 
"MWANAMKE MJINGA ATAIVUNJA NDOA YAKE KWA MIKONO YAKE"
Unatafuta nini kwenye simu ya mumeo? ukikutana na vitu visivyo kupendeza utavumilia?
unachokitafuta utakhpata endelea kupekua cm ya mumeo

fanya mambo mengine cmu ya mwanaume iogope na uiheshimu kama chumba cha mkweo!
 
Naww una tatizo kwny ndoa?
Matatizo kwenye ndoa hayahepukiki, hiyo ni hali ya kawaida sana ila yasiwe matatizo yenye sababu za kipumbavu kama za kuwekeana password kwenye simu,sasa mnafichana nini ambacho huwezi kukizuia ili kutunza heshima na uaminifu kwa mkeo, kama ni mchepuko bila shaka unatakiwa uudhibiti usiingilie muda wa mkeo
 
Ukitafuta ubaya wa kitu hata altareni utaupata, na ukitafuta uzuri wa kitu hata kwenye tundu la choo utauona pia.
 
Matatizo kwenye ndoa hayahepukiki, hiyo ni hali ya kawaida sana ila yasiwe matatizo yenye sababu za kipumbavu kama za kuwekeana password kwenye simu,sasa mnafichana nini ambacho huwezi kukizuia ili kutunza heshima na uaminifu kwa mkeo, kama ni mchepuko bila shaka unatakiwa uudhibiti usiingilie muda wa mkeo
Unaruhusu mchepuko uwe na muda wake?!...is this u?!

Pole lkn ndio maisha
 
Unaruhusu mchepuko uwe na muda wake?!...is this u?!

Pole lkn ndio maisha
Itakua ni uongo kudhani kwamba hakuna usaliti mdogo mdogo ambao mume wangu amewahi nifanyia, better believing than not ...... Lakini kitu cha msingi zaidi ni heshima ambayo mume humtunzia mkewe, namshukuru kwa hilo kwa kweli sijawahi kuhisi au kuumia kwa yeye kuonyesha tabia zisizofaa SIJAWAHI
 
Ukiona hivyo jua. Una wake wenzako wanafichwa,mwambie ukweli hupendezewi na anavyofanya.
 
Naombeni ushauri,

Kuhusu hii hali mume wangu hataki kabisa ushike simu yake na simu zake zina password na ukimuomba kukutajia anakwambia kabisa hawezi maana kwenye simu zake kuna mambo ya ofisi ambayo mimi sitakiwi kuyafahamu ila ya kwangu haina password na huwa anaishika kama simuoni anapekua sana tu sasa sijui anachoficha ni nini.
Ukishaishika ukakutana na usichokitarajia utakuwa umejiandaa kisaikolojia?
 
simu yake ya nn vitu vingine mnajitafutia matatizo wenyewe, hivi ukikutana na visivyoonwa kwenye simu ya mumeo upo tayali kuachana nae!
 
simu yake ya nn vitu vingine mnajitafutia matatizo wenyewe, hivi ukikutana na visivyoonwa kwenye simu ya mumeo upo tayali kuachana nae!
Transparency ni moja ya nguzo za ujenzi wa familia imara, ni udhaifu mkubwa kufichaa fichana vitu ambavyo mnaweza kuviweka sawa
 
Umesema simu ni yake...we unaitaka ya nn..si una yako....naona unatafuta ugonjwa wa roho...ya ngoswe muachie mazoea
 
Back
Top Bottom