Mume wangu nakupenda ila joseph kanikuna

Mume wangu nakupenda ila joseph kanikuna

Ndan ya box

Senior Member
Joined
Jun 2, 2014
Posts
159
Reaction score
44
Mapenzi ndiyo yanaupamba ulimwengu huu,kama huamini hata uwe na pesa kiasi gani,masikini kiasi gani,hata uwe na postion gani serkalini hata kama wewe ni kiongozi mkubwa duniani jamani acheni mapenzi yaitwe mapenzi,

Haya mapenzi yalimfanya Rais mandela asalitiwe,haya mapenzi yamefanya watu wengi maarufu wauwane,eeee mapenzi hivi wewe ni kitu gani?Watu wanafanyiana unyama kisa mapenzi,

Raisi mwinyi aliongea mapenzi yamekaa sehemu ambayo upende usipende pale sehemu utaonja tu ,

kweli yamekaa pale mahala hata ukiona kwa macho,mwili utatamani,akili inapararaizi,moyo unakuruka juujuu,kisa mapenzi,

Mshirikishe mungu na omba sana mungu akupe macho na uone yupi anakufaa kamwe huwezi toa machozi kisa mapenzi,

Kamwe huwezi umia kisa mapenzi ,mazingira ndio tatizo kubwa ,siku ya kwanza ulipompenda je jiulize ulikutana nae wapi ?

mazingira gani?

Mtu unakutana na mtu Bar,club,daladala,njiani,uchouchoroni,sinema,leo hii anakusaliti unalia unalia nini?

Ushauri,mungu ni muweza wa yote,aweza yote,fanya maombi kwa kumaanisha utashinda na hakuna machozi kamwe
 
Hii ni lugha gongana maana kaweka porojo mno !
Joseph sijui Mwinyi mara Mandera mmmhhh.
 
Hili shairi hulijui au nilidhani umeweka ule ubeti wa lile shairi ambalo linazungumzia jinsi joseph alivyomkuna au tukukumbushe.
 
Huyo Joseph mbona hujamtumia tena au ulikuwa unamaanisha Emmanuel Mbasha nini kwa sababu ndiyo hivyo tena yuko mahabusu sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom