Hivi kwa nini watu wanafikiri kwamba baada ya kuoana, mtakaa miaka na miaka, kila siku mnalala kitanda kimoja, watu wawili wale wale halafu sex life itakuwa ile ile tu?
Kama umeamua kuingia katika ndoa inabidi ukubali kweli fulani za maisha ya ndoa.
Mojawapo ni hii, ya kwamba kuna uwezekano mkubwa sana wa moto wa tendo la ndoa kupungua.
Watu wanakuwa wakubwa zaidi, kazi zinazidi, majukumu yanazidi, watoto wanaingilia, familia, harufu za maziwa waliocheua watoto, mara mke kapoteza shepu kwa kuzaa, mara baba libido imeshuka kapata kitambi na kashaanza kupata majani meupe mpaka kwenye bustani ya katikati etc etc.
Utategemeaje rigwaride libaki lile lile?
You are just setting yourself up for disappointment.
Kwani mapenzi lazima kila siku kugegedana? Kiutu uzima hairuhusiwi?