Morning glory
Senior Member
- Mar 20, 2014
- 149
- 55
Wana JF please please nawaomba sana mnisaidie mume wangu amesoma mpaka post degree na Hana ajira nifanyeje? Yaani mi ndo nalisha nyumba na kulipia mahitaji yote, sasa inaniumiza! Binafsi sijamtenga ila namwonea huruma sana hajawahi kuajiriwa since 2011 na kila miradi anao anzisha unaishia njiani, sasa yupo tu home-nimewaza sana kuweka thread hii jamvini coz siko sure sana Kama yuko humu.
======== Updates ================
======== Updates ================
Wadau wote wa JF Nliwahi kupost Uzi Hapa wa mume wangu kutokuwa na kazi na Huu ni mrejesho.Tunaendelea kuumia kadri siku zinavyoenda mbele na msaada wangu unakuwa haitoshi Kwa familia yangu.Watu wengi waliahidi kunisaidia lakini mpaka Leo nimeishia kuambulia ahadi hewa tu na uchokozi na utani mwingi kutoka Kwa wadau humu JF.Wenye nafasi tafadhali msaidieni mume wangu yani karibu tunaumbuka na ukizingatia tunaishi nyumba ya kupanga