Fuata ushauri huu ujimalize kabisa.Mie najua unampenda ndiyo maana unaomba ushauri.Je kabla hamjafunga ndoa, hii si ndiyo ilikuwa tabia yake mpaka na wewe akakupata?nauliza tena, sio kwamba mimba ndiyo imemlazimisha kukuoa.Ukiolewa na mwanaume kiwembe, na ndoa yenu ikawa imekuja kwa sababu ya ujauzito, haka ka mchezo ka chovya chovya atachukua muda kukaacha.Sasa kama uliolewa kwa staili hii, pole sana, sijui utafanyaje, maana jamaa ataendelea kuonja na kuacha.Au jamaa kakuchoka ndiyo maana anafanya vituko hivi ili utambae? kwani mna watoto?nadhani hapa maswali ni mengi kabla haujaamua kuondoka.Kucheat ni tabia, kama hujaizoea itakushinda tu.yataka uzoefu, utajiumiza bure kwa kuwa huko utaenda kwa ajili ya kulipiza kisasi na hutakuwa na furaha kamwe.
Pole sana na inaonekana imekuuma... Ushauri, funguka kwake na kwa wakware wake.. Na Kama unao ushahidi wa kutosha anzisha zali kwa wazazi wake... Kumbuka na uwe na Moyo wa kuwa mlango wakuondoka kwako unafunguka nawe usiogope kulikabili Giza la maisha huko mbele, otherwise, anaweza kuua taaratibu kisaikolojia au kimwili..