Mume wangu anacheat nifanyeje?

Mume wangu anacheat nifanyeje?

pole mamii, nakushauri kusanya vithibitisho vyote kuwa anacheat then ongea nae ukimpa hatua utakazochukuaa.
1) kama anakuhitaji kama mke aache.
2) mwambie utamshtaki kwa mtu ambe anamuheshimu mfano kaka ake, ustadhi au askofu aliyewafungisha ndoa.n.k.
3) ila ckushauri kuondoka huyo ni mume wako komaa nae hao wa nje wezi tu.
4) pia jichunguze kujua chanzo cha kuchet, ongeza mahanjumati, mtt jipambe, yaan zidisha mambo kunako 6*6.


Nikwambie cri...mm wangu alicheat ckuhizi nimejipanga vibaya..yaan nikimkamata kwa kitanda mpaka analia wakati hakuwahi b4.

Hakika mwanamke hodari huwa anajipanga kuyakabili mapungufu ndani ya ndoa nimeipenda hii ya kuongeza maujanja na kujipamba kwani mwanaume jasiri hawezi kuacha kurudi nyumbani kama mke wake atabakia na kiwango kile alichompedea kabla hajamuoa. Ninyi wanawake mnajisahau mkishaolewa kujiremba basi maujanja basi. Unategemea nini akitoka huko barabarani na kukutana na hao wanajua kujipamba wakapambika na wajanja zaidi ya nyoka wawapo chumbani? Lazima mtu apotee nyumbani
 
..kweli kaka watu wengine hawana busara hata kidogo at mtandao wanaoupe...............]
 
Naomba msaada wenu mume wangu anacheat nifanyeje? mbaya zaidi na watu ambao wengine kawatambulisha kwangu,na ilikia hatua nilipokwenda jifungua alileta mpaka ndani nikiuliza tatizo nini hasemi sms kila siku godnight bby love u ukiuliza sina mana ya mapenzi nisaidieni wana jf nianye nini ?nami nianze cheat kama yeye au nifanye nini?

wee kamata kijana akupe raha....utamu kitu cha kushare bwana
 
wala usimuulize!piga kimya...zidisha mapenzi utaona mwenyewe
 
Kwahiyo Wewe ukiishiwa pesa mkeo rukhsa kutafuta kibuzi si ndio? Huyu dada katoka kujifungua Ina maana mume wake kakosa subiri ameenda kutembeza uchi wake badala ya kutulia na mkewe mjamzito.



Hakika mwanamke hodari huwa anajipanga kuyakabili mapungufu ndani ya ndoa nimeipenda hii ya kuongeza maujanja na kujipamba kwani mwanaume jasiri hawezi kuacha kurudi nyumbani kama mke wake atabakia na kiwango kile alichompedea kabla hajamuoa. Ninyi wanawake mnajisahau mkishaolewa kujiremba basi maujanja basi. Unategemea nini akitoka huko barabarani na kukutana na hao wanajua kujipamba wakapambika na wajanja zaidi ya nyoka wawapo chumbani? Lazima mtu apotee nyumbani
 
kabla ya mwaka 1950 wanawake wakiwa ktk hali hiyo walikuwa wanawaambia waume zao waache uzinzi si mzuri lakini wanaume hawakukoma,1950-2000 wanawake wakawa wanapiga magoti mbele za Mungu kuomba waume zao wabadilike lakini wanaume waliendeleza uzinzi,2000 na kuendelea wanawake wakiwa ktk mkasa kama wa kwako WAMEAMUA NA WAO KUTEMBEZA UCHI!nadhani kuanzia mwaka 2050 hakutakuwa na ndoa na mtakuwa huru milele...wote wake kwa waume.jichagulie uamuzi wa kuamua nobody will blame you,una uhuru wa kuamua kuifuata njia ya shetani aliyochagua mumeo

Hapo kwenye bluu nadhani Mwana wa Adam, Mfalme wa wafalme anajiandaa kuja kumlipa kila mtu kadri ya matendo yake
 
Binti inaonekana pepo wa kucheat nawe amekuingia; sasa kwanza kemea huyo pepo kwako then KAA VIZURI SANA na mmeo muelekeze na jiweke VIZURI uvutie kama mwanzo kabla ya kuzaa. Inaonekana haya yameanza wakati una MIMBA, ebu jiangalie vizuri please kwani wengi wenu huwa mnabadilka sana mkishazaa na hampendi kujiweka vizuri zaidi, na kumbuka jamaa alikupenda kabla hujazaa. Ingawa aliaidi kukupenda milele lakini yeye ni binadamu pia kumbuka... bwana Mungu awe nanyi na kuiponya ndoa yenu....Ubarikiwe sana
 
wala usimuulize!piga kimya...zidisha mapenzi utaona mwenyewe

Kwa kawaida, mwanaume ukimuuliza kitu mara nyingi tunakua attention kujihami, kuwa mkali ikiwa miongoni mwa hizo njia.
Katika hali kama hii akisema amuulize, sidhani kama wataelewana. Kwanza mama ana machungu ya yanayoendelea, usitegemee atamuuliza kwa njia ya upole.

Ushauri wako wa kutomuuliza akichanganya na maombi na kuwa mnyenyekevu, nna imani mme atajirudi.
kama umewahi mfanyia mtu kitu kibaya alaf yeye akakaa kimya huku akiendelea kuonyesha utulivi , unaweza omba msamaha mwenyewe.
 
Na wewe cheat,tena mitoko yako wakati unafata bakora hakikisha unapendeza ile mbaya,akigundua unagegedwa vizuri nje roho itamtulia na ataacha upuuzi wake.Kila la kheri..!
 
Kwahiyo Wewe ukiishiwa pesa mkeo rukhsa kutafuta kibuzi si ndio? Huyu dada katoka kujifungua Ina maana mume wake kakosa subiri ameenda kutembeza uchi wake badala ya kutulia na mkewe mjamzito.

Kuna tatizo hapa inawezekana kuna kutoelewana au kuwa na malengo tofauti katika kupata suluhu ya hawa wanandoa. Kilicho chema ni KUVUMILIANA na kuchukuliana mapungufu yaliyopo. Na ndio maana nikasema kuwa nimeipenda hiyo ya kujipamba na kuzidisha maujanja chumbani. Naamini mwanamke mwenye busara hata akiwa mja mzito sio kigezo cha kutojipamba na kuwa mrembo ili awe anamvutia mumewe. Pia ni kipindi ambacho wote wanahitaji kuwa pamoja ili waweze kuilea mimba pamoja kwa upendo. Yapo maudhi wakati wa ujauzito lazima mwanaume ajue jinsi ya kuyachukulia sikumaanisha atoke nje akazurure hovyo HAPANA.
 
Naomba msaada wenu mume wangu anacheat nifanyeje? mbaya zaidi na watu ambao wengine kawatambulisha kwangu,na ilikia hatua nilipokwenda jifungua alileta mpaka ndani nikiuliza tatizo nini hasemi sms kila siku godnight bby love u ukiuliza sina mana ya mapenzi nisaidieni wana jf nianye nini ?nami nianze cheat kama yeye au nifanye nini?


Dada kisa chako kinanisikitisha, najiona mimi kama wewe, japokuwa mimi ni mwanaume, lakini nakushauri ifuatavyo:

  1. Hebu jaribu kurudi nyuma katika historia ya maisha yako wewe na mume wako. Je, kabla ya kuoana, kulikuwa na maandalizi YA KUTOSHA kwa jini ya kuishi kama wanandoa? Je, maandalizi hayo yalifanyika chini ya msingi wa kidini au wa kimila? Hujaeleza kama wewe ni Mkristo au Muislam. Kila dini ina taratibu na misingi yake ya jinsi ya kuishi katika ndoa. Utazame, je, kulikuwa na maandalizi ya kutosha?
  2. Ninasema hivi kwa kuwa wengi wetu, sisi vijana wa leol, TUNAKURUPUKA na kuingia ndani ya ndoa huku tukiwa HATUJAFANYA MAANDALIZI ya aina yoyote yale ya jinsi ya kuishi katika ndoa. Ukweli ni kwamba, wanaume na wanawake wengi siku hizi wanaingia kwenye ndoa na kuendelea kuishi KANA KWAMBA bado hawako kwenye ndoa. Sijui imekuwa FASHENI au kitu gani. Mtu unaoa/unaolewa ili mradi tu uitwe Mr. au Mrs. Fulani, umevaa pete, basi, umependeza, lakini HUJUI MAANA YAKE!
  3. Hapo ndipo chanzo cha mtu kutoka nje ya ndoa kinapoanzia. Bwana yeye anajiendeshea maisha yake kana kwamba hana mke nyumbani. Anaenda huku na huko, anabadilisha wanawake kama mashati. Kinachomrudisha nyumbani, akitubu, mkia kaufyata nyuma, ubabe wote umeisha ni nini? UKIMWI! Keshaukwaa! Labda tena KISHAMWAMBUKIZA mke wake bila hata kujua. Anamwona mke wake kama kimada, lakini aliye ndani ya nyumba. Kwa hiyo hawezi kumtofautisha na yule wa nje. Wote sawa! Hapa, hata ile HOFU YA MUNGU haipo tena. Kama ingekuwa apo, ile amri ya "Usizini" isingevunjwa kabisa.
  4. Najua maneno haya ninayokuambia ni MAGUMU na YANATIA UCHUNGU, lakini ukweli lazima usemwe. Hakuna kufichaficha hapa. Tunaficha nini? Lengo letu ni kutafuta MARIDHIANO kati yako wewe na mume wako, umekuja kutuuliza UFANYE NINI? Sasa sisi tunakuambia... tuseme MIMI ninakuambia, kwanza ANZA KUJICHUNGUZA wewe mwenyewe.
  5. Hebu jiulize: Ni mara ngapi ulimwandalia mume wako chakula mezani? Ni mara ngapi uliandaa maji ya kuoga na kumwita mume wako, mkaingia wote bafuni, mkaoga pamoja?
  6. Jiulize: Ni mara ngapi ulimwambia mume wako: Nakupenda _______ (fulani). Nakupenda honey. Nakupenda switi!
  7. Jiulize: Ni mara ngapi ulimpokea mume wako aliporudi nyumbani akitoka kazini, na kumwambia: Pole mume wangu kwa kazi nyingi.
  8. Sasa jiulize: Ni mara ngapi yote haya, na mengine ambayo sijakuuliza, mume wako alikuwa anakufanyia, na labda wewe hukuyatilia maanani, kwa kuyaona "old fashioned"?
  9. Kumbuka, misingi ya kidini (kwa waumini wa Kikristo) ilihuishwa na tamaduni za makabila mbali mbali, baada ya tafiti mbali mbali kufanyika kuhusu uhuishaji huo wa mila na desturi, ili kuzioanisha na jinsi Kanisa la Kikristo linavyofanya kazi yake hapa nchini, HASWA kwa wanandoa. Kwa hiyo, yale ambayo vijana wa sasa wanayaona "ya kizamani", ni misingi ambayo wazazi wetu waliitumia ili kuishi kwa amani na maridhiano. Hakukuwa na ubaguzi wa nani "mkubwa" au "mdogo" ndani ya nyumba. Wote walikuwa sawa, walielewana, waliridhiana. Hakukuwa na ubabe.
  10. Utakuta siku hizi, binti anatoka kwenye familia yenye UWEZO, kwa hiyo anajua: Wikiendi naenda kwa Mama. Anasahau maana halisi ya "kuwa mwili mmoja" na mume wake. Naye mume kwa kuwa anampenda, anashindwa kumzuia, lakini anaumia moyoni. Anabaki mpweke. Mke anaenda kwa mama yake, kuanzia Ijumaa anarudi Jumapili. Mume anabaki na "beki tatu" nyumbani, unatarajia nini kitokee? Sasa hapo Shetani anaanza kazi yale. Baada ya "kutosheka" kwa "beki tatu" anaanza kutoka nje kabisa ya ndoa. Keshaisaliti, lakini Shetani keshamteka, akili haipo kwenye "network" yake. Hapo mawazo yote ni: Mie si naonekana -----? Mie si naonekana sina lolote? Yeye si anaona wazazi wake ni bora zaidi kuliko mimi? Haya, ngoja mie nikajirushe na washkaji, tukasake madem. Potelea mbali! Kufa kwaja!
  11. Safi sana! Shetani keshafanya kazi yake! Keshawamaliza WOTE!

Sasa dada, unaona kinachotokea hapo? Mie nimekupa "nusu" tu ya mkanda. Wewe hujatueleza kinagaubaga kinachoendelea ndani mwako. Lakini cha kwanza kabisa, BAADA YA KUTAFAKARI, ninakuomba ufanye hivi:

  1. Kwa IMANI YAKO, sali sana. Muombe Mungu akupe moyo wa uvumilivu na upendo. Sali sana!
  2. Kwenye sala zako MUOMBEE MUNGU amrejeshe MUME WAKO kwako, kwani Mungu ndiye aliyekupa mume huyo. Yaonekana bado wampenda, kwa hiyi huna budi kukumbuka kwamba UNAMPENDA na huna mwingine zaidi yake.
  3. Kauli yako ya kwamba kwa kuwa yeye amecheat na wewe ucheat IFUTE KABISA. Ok, amecheat, sawa, na wengine kawaleta hadi ndani. SAMEHE NA SAHAU. Fanya kwamba jambo hilo HALIJATOKEA, kwamba ni Shetani ndiye amempitia. Shetani ni ADUI WA KILA MWANADAM, kwa hiyo kila atubuye na kuungama dhambi zake husamehewa na kufutiwa dhambi hizo.
  4. Tafuta muda, weka mazingira, mwambie mumeo unataka mtoke outing. Toka naye outing, sijui kama bado unalea, lakini kama unaweza, hebu nendeni outing mara moja au mbili, fanya utoke naye outing hata kila wikiendi, kwa mwezi mmoja, kisha tazama nini itakuwa reaction yake.
  5. Pengine wewe ULIKUWA BUSY na kazi, hukupanga muda wa kufurahi na mumeo? Au labda yeye? Sijui. Wajua wewe. Jaribu kujikumbusha, mlivyokuwa wapenzi mlikuwa mnafanya nini? LAKINI USISAHAU KUOMBA NA KUSALI KILA SIKU! OMBA SANA! SALI SANA.

Mimi natarajia kwamba, maombi yako yatamrejesha mume wako nyumbani, na kama wewe ni Mkristo, basi, itakuwa HARAKA SANA. Kwa sasa uko naye, lakini Shetani ameshamteka, tena KAMTEKA SANA, ndio maana anadiriki hata kuwaleta hao vimada, wezi, nyumbani. La sivyo ANGEMUOGOPA MUNGU. Unahitaji sana kufanya maamuzi magumu: Uamue, ndoa imekushinda, uondoke.... sijui utaenda wapi, maana sioni utakapokwenda na sidhani utakuwa na maisha mazuri, kwani utakuwa umevunja ndoa ILIYOFUNGWA NA MUNGU! Kwa hiyo nakushauri, vumilia, kwa busara utakazopewa na Yesu Mwokozi, HAKIKA utafanikiwa. Nakutakia mafanikio mema ili ndoa yako idumu. Kumbuka: Kwa Mungu, HAKUNA linaloshindikana!

Nitakukumbuka kwenye Sala Zangu.

Ubarikiwe sana!

Amina!
 
Punguza mapungufu yako kwenye mapenzi mumeo atarudi! Jaribu pia ule mtandao wanaume wanaoupenda kwa sasa kwa mumeo

Masanilo, lile Kanisa uliloanzisha bado lipo? Nashangaa siku hizi huitwi Reverend tena, kulikoni?
Au wale waumini uliokuwa nao waligoma kuwa na ndoa za mitala?
 
Hehehehe nimejikuta nacheka after kuread comments za hii sred, men are men hawahitaji kuwa na reason ili wacheat, woman hata uwe perfect vipi they wil cheat coz cheating is their nature ,they are never satisfied with a single v thats why iwil never get married in my entire life
 
Punguza mapungufu yako kwenye mapenzi mumeo atarudi! Jaribu pia ule mtandao wanaume wanaoupenda kwa sasa kwa mumeo

Masanilo, lile Kanisa lako ulilokuwa ukichunga bado lipo ama limesambaratika? Kulikoni siku hizi huitwi tena Reverend Masanilo? Au Waumini wako waligomea ndoa za mitala?
 
Ndicho alichofanya mama yako kumkeep baba yako?????

inaonekana mlokole mzuri sana, loh! Kuna watu wanaona rahis kuwapotosha wenzao. Aafu huyu si alikuwa anajiita rev masanilo.?
 
Usikaribishe mafarakano ndani ya nyumba, just do a thing what you think will stops him cheating on you.
 
Back
Top Bottom