Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Pole sana Leah kwa yaliyokukuta, jambo kama hili nililishuhudia kwa jirani yangu ambaye ni ofisa mwenye cheo kikubwa kwenye jeshi la polisi, kuna mdogo wa mke wake alikuja kwao kwa lengo la kuendelea na masomo, baada ya muda ikagundilika mume kamtia mimba shemeji yake, mke alihamaki sana nakuamua kuondoka nyumbani, watu wakamsihi sana akaamua kurudi kwake, mdogo mtu akajifungua na sasa mtoto anamiaka minne ameanza nursery, yule shemeji amejengewa bunju na maisha yanaendelea, chukua muda ufanye uamuzi utakaouona wa busara, usifanye maamuzi ya hasira utakayojutia baadae!
 
Duh! Kweli elimu ya mastaz sijui mastaaz haijawah muacha mtu salama. Pole mpendwa ntakushaur bdae ngoja niingie job kwanza

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Inauma Ila sasa kwa sababu maandiko husema adui ni mtu wa nyumbani mwako. Na mmefunga ndoa Na huyo ni mdogo wako wa damu unaonaje ukasamehe na mdogo wako akarudi nyumbani akajifungua tu. Wewe ukaendelea kusoma Na kumaliza na baadaye uzaae watoto wa kwako. Na nikwambie huo ni mtihani ukifanya kosa ukavunja ndoa yako baadaye inaweza kukugharimu pia utakuwa umempa shetani ushindi maana yeye kazi yake ni kuvunja, kuiba Na kuchinja. Hapo Mungu alikufunulia ili uweze kufanya maamuzi sahihi je mdogo wako asingibeba mimba ungejua? Kuwa makini hapa kuna vitu vitatu Kama wewe ni mkristo

Shetani:-
1. Kuvunja
2. Kuiba
3. Kuchinja
Bado haujachelewa

1. Shetani Ana mpango wa kuvunja ndoa yako, kitu ambacho Mimi naamini hajafanikiwa dada usiangalie ulimwengu utasema nini mwangalie Mungu ndani ya Yesu. So shetani yupo kwenye hatua hii ya kwanza Na asifanikiwe ktk jina la Yesu. Maana akifanikiwa hii hatua anaingia hatua ya pili ya kuiba.

2.Hatua hii "kuiba" anataka either akuibie mme au mipango yenu ili wewe ubaki pekee yako Na yeye pekee yake Na labda nikuhakikishie mme wako kamwe hatamwoa huyo mdodo wako. Sasa akimaliza hili anaingia hatua ya tatu.

3. "Kuchinja" hapa unatafutwa either wewe au memo au wote. Kivipi ni rahisi hivi unafikiri ni rahisi kwa mwanamke aliyekwisha olewa kukaa bila mme vivo hivo mwaname? Hapa anaweza chinja mmoja wenu kama si wote kwa magonjwa, stress , suicide Na mengine yanayofanana Na hayo.

Mimi kama mimi nakuombea shetani ashindwe . Alichokiunganisha Mungu shetani wala mwanadam asikitenganishe. Amen
 
Mumeo kusubiri kulimshinda afu we uliweka vitu flan front instead of family... Cha msingi samee ata kama utadill na maisha yako mbona yesu alisamee ata waluomsulubu?? Na alikuwa anajua One day watamsulubu

sent from my iPhone 6
 
Jamani, kweli jamaa amekosea, lakini tusimlaumu kwa kusikia upande mmoja, maana maisha ya ndoa ni siri nzito kati ya wanandoa wenyewe,hatuwezi katu kufahamu kwa nini jamaa aliamua kufanya hivyo,wao ndio wanaojua, lakini mara nyingi wanawake wasomi kama siyo wacha Mungu ni wasumbufu sana kwenye ndoa, anaweza hata akakupangia ratiba ya mambo ya faragha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Isomeke "Mdogo wako amepewa mimba Mume wako"

Kwa Hisani Ya Watu Wa Mbeya!
 
Pole sana dada Leah2

Najua ni kwa kiasi gani una umia kutokana na kilichotokea kati ya mumeo wa ndoa lakini pia na mdogo wako. Kutokana na jina lako naamini kabisa ndoa mliyofunga ni kikristo yenye kiapo kwamba mtakuwa pamoja kwenye shida na raha, afya na ugonjwa...ni mpaka pale kifo kitakapo watenganisha. Kwa alichokifanya mumeo ni dhambi hata kwa Mungu lakini hata kibinadamu amekukosea sana kama mkewe, ila inabidi tukumbuke biblia inasema kwamba, amebarikiwa yule awezae kusamehe bila kujali ukubwa wakosa. Swali moja la kujiuliza, unataka kumfurahisha Mungu au wanadamu (Nafsi yako) kama jibu ni Mungu ni jibu sahihi zaidi kwani yeye ndie awezae kukupa faraja na kukuepushia na aibu ndani yako lakini pia na wale wanaokuzunguka kwa kuwa utakuwa umechagua funguo lililo jema. Ushauri wangu ni vizuri kuomba sana ili Mungu akupe ujasiri katika hili lakini pia ni vyema kwenda kwa viongozi wa dini (wachungaji) wakupe ushauri zaidi katika hili kwani tunaamini hao wana hekima zaidi ya kutuliza moyo wako. Kumbuka hata mkiachana bado kwa Mungu huyo ni mumeo mpaka pale kifo kitakapo mchukua, hivyo kwa maamuz yoyote utakayo chukua kwa Mungu ni batili ingawaje kibinadamu tunaweza ona umefanya sahihi.
Mungu akutie nguvu na ujasiri katika kipindi hichi.
Mungu akubariki. Karibu tena.
Villiky_J

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho kisa kipo exactly kama kilichomtokea mama yangu, alikaribisha mdogo wake, baba yetu akampa ujauzito!!

Kilichofuata ni mtoto alizaliwa alipofikisha miaka miwili akachukuliwa na mama yangu! Akalelewa kama mtoto wa familia yetu!

Hii ilikuwa ni zamani, wanawake walikuwa wavumilivu sana, hakukua na mitandao ya kijamii, cheating kwa mwanaume haikuwa a big deal!
Kwa maisha ya sasa uvumilivu wa hivo ni ngumu sana!

Ushauri wangu fanya kile moyo wako unaona sahihi!

As long as hujazaa na huyo mume, msamaha pekee ni wa kumbadilisha status kutoka kuwa mume na kuwa shemeji, ila sio kuendelea nae!! Hii itajenga chuki zaidi kati yako na mdogo wako!!
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
We endelea kusoma na kufanya kazi tu. Inakuuma nini na wewe hutaki kuzaa? Utajijiua....[emoji30]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee! Pole sana

To accomplish much you must first lose everything..
 
Back
Top Bottom