Pamoja na kwamba hii imeshatokea, napenda kutoa ushauri kwa wanawake mlioamua kuolewa timizeni wajibu wenu kwa waume zenu!
Biblia inasema Mungu ameumba jambo jipya duniani, mwanamke atakuwa mlinzi wa mumewe.
Nitoe maana chache za mwanamke kumlinda mwanamume,
1) Ni lazima mwanamke adhibiti dalili yoyote inayoashiria mumewe kutoka nje ya ndoa. "Mdharau mwiba mguu humwota tende"
2) Mpatie mumeo kila apendacho kwa ufanisi wa hali ya juu, kama ni chakula mwulize anapendelea nini halafu kiandae mwenyewe kwa ubora wa hali ya juu kwa uwezo wako wote maana huyo ndiye mumeo,
Kama ni penzi mpatie kila anapohitaji hadi aridhike mwenyewe. Ukimnyima au ukimbania ujue kuna siku atatafuta mbadala na atapatiwa anachohitaji kwa ubora anaotaka. Ndiyo maana Mungu amesema" MSINYIMANE isipokuwa MMEPATANA kwa muda ili mpate faragha kwa kusali"
Mwanamke usiamue mambo peke yako bila kuridhiana/kukubaliana na mumeo.
USHAURI WANGU:
1) Msamehe mumeo, huyo ni mume tu sio rahisi kihivyo kumuacha mumeo. Ukumbuke kuwa kuna wanaume wengine wanatembea hadi na mama wakwe zao! Sembuse kutembea na shemeji yake! Lkn hawajagundulika tu. Na baadhi wamegundulika. (Siombei itokee tena kwa yeyote) Leo mumeo katembea na mdogo wako, umeita wazazi, je angetembea na mama mkwe wake ungemwita nani?
Au unauhakika gani endapo utaachana na huyu, yule atakayekuoa hatakuwa zaidi ya huyu?
Narudia nakushauri msamehe mumeo, umpende zaidi na use naye karibu zaidi,maisha yataendelea.
2) Mdogo wako mshauri asitoe mimba(asiue) kumbuka hiyo ni kazi ya mikono ya Mungu, isiharibiwe na mtu yeyote. Mtoto akizaliwe mpende kama watoto wako utakaozaa.
3) Jitahidi kumpendeza mumeo kwa uwezo wako wote, usiseme moyoni mwako "hata nisipomtimizia matakwa yake atavumilia" kumbuka wanaume ni wepesi wa kutafuta alternative ways when they encounter an obstacle! Ndiyo maana ukifuatilia sababu kubwa ya wanaume wengi kuwa na nyumba ndogo ni "KUNYIMWA TENDO LA NDOA NA WAKE ZAO WA NDOA" . Wanawake wengi hudhani wanawakomoa/wanawaadhibu waume zao kuwanyima tendo la ndoa lkn kumbe wanatengeneza mwanya wa mambo mabaya zaidi.
Sent using
Jamii Forums mobile app