Mume anapokataa kuvaa pete ya ndoa

Mume anapokataa kuvaa pete ya ndoa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,638
Reaction score
220,409
Siku ya harusi pete zenu zilibarikiwa na mlivalishana. Kamati ya harusi iliandaa usiku mmoja Kempinski kabla hamjasafiri kwenda Serengeti kwa honey moon.

Mmetoka tu reception bwana harusi anapovua suit yake anavua na pete na anakwambia kabisa hawezi kuvaa pete maishani mwake lakini anaahidi kuwa mume bora.

Pamoja na kuwa havai pete, face book profile yake ameweka picha yenu ya harusi na status amechange kuwa married.

Hii imekaaje na wewe utaichukuliaje?
 
Hana allergie yeyote anasema hapendi tu vidole yake kuvaa kitu chochote na wewe ukipenda vua tu pete yako
Binadamu tunatofautiana katika kuwa na upenzi wa vitu, sehemu au maono. Mambo haya hutokana na aidha malezi au asili nk. Mimi naamini ndoa huanzia katika nyoyo za wawili wapendanao.
Hivyo basi, yanayofuata kuanzia mavazi, malazi na yote yafuatayo ni nyongeza tu. Huyo ambaye hapendi kuvaa pete, anao upendo kwa mwenzi wake? Haigizi ndoa? Kama hayo yapo jumlisha uaminifu wa kweli, wanandoa muishi kwa amani.
 
Mimi naona pete ndio zinaongoza kuletea wake zao wanaovaa matatizo na vitimbi. Bora hasivae tu aonekane kama vile hana msimamo wa nyapuz hata kama ameoa..
Pete muhimu tena lazima mvae kwenye shughuli za maana mkiwa pamoja, au mmoja wenu atakapoona itafaaa.. hapo kuna mengi.
Mwisho wa siku pete haibebi kuonyesha ya kiukweli ya wanandoa.. pambo tu.. muhimu ni ya mioyoni mwenu.
 
Kusema ukweli he is a husband material na amebeba majukumu yake yote, mke akiridjia hakuta kuwa na neno na pete yake ameihifadhi
 
Binadamu tunatofautiana katika kuwa na upenzi wa vitu, sehemu au maono. Mambo haya hutokana na aidha malezi au asili nk. Mimi naamini ndoa huanzia katika nyoyo za wawili wapendanao.
Hivyo basi, yanayofuata kuanzia mavazi, malazi na yote yafuatayo ni nyongeza tu. Huyo ambaye hapendi kuvaa pete, anao upendo kwa mwenzi wake? Haigizi ndoa? Kama hayo yapo jumlisha uaminifu wa kweli, wanandoa muishi kwa amani.
Ni kweli ndoa iko moyoni kama ukirudhika kuwa ni sawa mume wako kutokuvaa pete.
 
Hakuna tatizo kama ni muaminifu na unamjua ni mwaminifu
Lakini kinyume na hapo uandike maumivu
Japo pete ya ndoa ni ishara ya kila mmoja kuonyesha anamilikiwa na mmoja tu na kila mtu anapaswa kuliheshimu hilo

Ndoa iheshimiwe na kila mmoja wetu
 
Huyu mbona kaanza kusaliti ndoa mapemaa [emoji23]
Mi nawasiwasi hapo reception kamwona mhudumu kavutiwa naye angalia asije kukutoroka hapo room akaenda kumalizana nae [emoji23]
 
Kusema ukweli he is a husband material na amebeba majukumu yake yote, mke akiridjia hakuta kuwa na neno na pete yake ameihifadhi
Kuna watu tumeumbwa na kuzoea kutojitwisha mavazi au vito vingi mwilini. Zamani hizo, kijijini kwetu mtu akionekana amevaa mipete na mikufu mingi tulimtafsiri kuwa aidha ni mchawi au anajihusisha na uchawi. Lakini leo, maisha yamebadilika na hata uelewa na mtizamo umebadilika.
 
Huyu mbona kaanza kusaliti ndoa mapemaa [emoji23]
Mi nawasiwasi hapo reception kamwona mhudumu kavutiwa naye angalia asije kukutoroka ha room akaenda kumalizana nae [emoji23]
😀😀😀
 
Kuna watu tumeumbwa na kuzoea kutojitwisha mavazi au vito vingi mwilini. Zamani hizo, kijijini kwetu mtu akionekana amevaa mipete na mikufu mingi tulimtafsiri kuwa aidha ni mchawi au anajihusisha na uchawi. Lakini leo, maisha yamebadilika na hata uelewa na mtizamo umebadilika.
Kwenye jamii yetu ya sasa ukiwa huna Pete inamaana bado uko available. Sasa Munro kuonyesha kuwa yuko availabe ni kasheshe
 
Muonekano wa mtu isiwe kigezo cha kumuweka kundi fulani kwa kumdhania tu. Ni vema watu wakawa na ukweli kuhusu mtu. Na huyo mwanandoa, ni heshima na kujitambua ndivyo vitaiacha ndoa salama. Mengineyo ni puruzai tu mbele ya uoni wa wanajamii.
 
Itabidi mke aelewe tu, maana sio kila mtu ni mpenzi wa hayo mavitu (mkufu, hereni, saa, pete nk )

Lakini pia angeweka wazi mapema kabla ya maandalizi ya harusi, mwanamke ajiandae kisaikolojia.

Bwana harusi itampasa kufanya kazi ya ziada kuwatamkia watu kwamba ana mke na anampenda kupunguza wadada kujisogeza Kwake.

Pamoja na yote hayo avae asivae haimaanishi ndoa haipo, ni kitu kidogo sana kulinganisha na mambo mengine muhimu katika ndoa.
 
Siku ya harusi pete zetu zilibarikiwa na mlivalishana. Kamati ya harusi iliandaa usiku mmoja Kempinski kabla hamjasafiri kwenda Serengeti kwa honey moon.

Mmetoka tu reception bwana harusi anapovua suit yake anavua na pete na anakwambia kabisa hawezi kuvaa pete maishani mwake lakini anaahidi kuwa mume bora.

Pamoja na kuwa havai pete, face book profile yake ameweka picha yenu ya harusi na status amechange kuwa married.

Hii imekaaje na wewe utaichukuliaje?
Changamoto io... Ila nanyi mpo wa ivo
 
Hapo inategemea nia ya kufanya hivyo ni ipi kama anafanya hivyo ili kucheat hapo ni shida kama hacheat hakuna shida maana kunawanaovaa pete usiku na mchana na wanacheat usiku na mchana na kuna watu hawana pete na hawacheat. Bora wepi kati ya makundi hayo mawili?
 
Mm wangu alijidai imepotea baharini alipokwenda kuogelea kinachonishangaza hajawahi kuivua tangu siku ya ndoa na haivuki imemkaa kidoleni baharini imetokaje
 
Back
Top Bottom