Ukifiwa na kuolewa upya huvai shela au pete ya marehemu

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,189
2,000
Habari wana JF,

Leo nimeota ugomvi ukitokea mahali sababu mume amefiwa na mke na kwa mujibu wa dini yake akaoa/anaoa mke mwingine. Hata hivyo mambo sio mepesi ingawa yote yamefanyika kwa MAPENZI YA MUNGU.

CHANGAMOTO:
- Mume anavaa pete ya mke wa zamani mkono wa kulia na mkono wa kushoto anataka kuvaa pete ya mke mpya.

- Mume bado ameweka picha, nguo, viatu na mazagazaga ya mkewe (marehemu) chumbani, jikoni, sebuleni nk

- Mke mpya haelewi somo, vivyo hivyo kwa watoto na ndg wa pande zote mbili.

MAAMUZI YA PADRI / SHEKHE
- Ugomvi umemfikia Padri / Shekhe na baada ya kusikiliza pande zote mbili ameagiza yafuatayo:-

- Mazagazaga yote ya mke wa zamani ikiwemo pete ya ndoa nk yatolewe na ikiwezekana yapelekwe kwenye kambi za wahitaji, makumbusho nk

MAAMUZI NA YALIYOJIRI
- Watoto wa marehemu wanalia kona zote na hawamuelewi mke wa baba yao. Wapo waliopokea na wengine bado wanaendelea kutulizana.

- Baba mwenye nyumba (mume) ameumia lakini amekubali matokeo. Anawaasa watoto watulie na waheshimu mapenzi ya Mungu.

-Pia amewashauri watoto wake wakubali matokeo maana mke amepatikana kwa mapenzi ya Mungu na sio kwamba yeye ni malaya au hali yoyote ile.

- Baba amemuasa mke mdogo awapende watoto wa marehemu na upendo utaondoa tofauti zote ndani ya muda mfupi.

- Pia ndugu za mke wawapende watoto waliowakuta. Pia watoto waoya wawapende ndg zao. Lazima tujenge familia.

MWISHO
Baada ya maombi mazito ya kufunga na kuomba. Magomvi yameisha na familia inaendelea kubarikiwa sana.

FUNDISHO
Tafsiri yangu inaweza isiwe sahihi asilimia 100 ila naomba uichukulie kwa nia ya kujenga:-

- Baada ya kufariki kwa Rais Mhe. Dr. John Pombe Magufuli kwa mapenzi ya Mungu ndoa ilivunjika ndani ya siku 2. Sasa imejengwa upya baada ya Mhe. Samia kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya sita ya JMT. Hongera mama yetu Mhe. Samia Suluhu Hassan - KAZI IENDELEEE!

- Wale wote waliokuwa wamevaa pete ya Hayati Magufuli (Madaraka ktk Chama na Serikali nk) wanatakiwa kuvua pete ya Magufuli na kuvaa ya pete ya Samia. (Wasivae pete zote 2 - MAMLAKA)

- Mazagazaga ya Hayati Magufuli yawekwe Makumbusho ya Taifa au Nyumba ijengwe Chato yenye kumbukumbu zake zote nk. Rais Samia huwezi kumtendea haki kama bado unazungumzia mazagazaga ya Magufuli (kasoro filosofia nk ikiwemo muendelezo wa miradi, ilani ya CCM nk)

- Wateuliwa wapya au timu ya Mhe. Samia na timu ya Magufuli wote ni ndugu. UPENDO UTAWALE! Kwa kufanya hivyo kutampa raha Mhe. Samia na utawala wake utatulia na utaendelea kubarikiwa. Na JPM ataendelea kuoumzika kwa amani. Msiishi kwa kuogopana na kunangana hayajengi uanakuza mauhasama. Timu mpya somo limepatikana mmeliona kwa wafiwa.. Hili ni somo kubwa kwa kila Mtanzania! KAZI LAZIMA IENDELEEE!!!

- Timu ya Magufuli futeni machozi MAISHA YAENDELEE! Hata mkiona watoto wapya wanawasonda mjue ni muda tuuuu watatulia na kutambua wote ni ndugu. Hata nyie kuna wakati mliwasonda.

- Wana JF tuache zile kauli zinazotugawa na kuligawa Taifa. Hata kwenye mitandao mingine tuwe sasa na kazi moja ya kulijenga Taifa letu la Tanzania.

- Upande uliopoteza usijione yatima na upande uliopata usitambe ukamkufuru Mungu. Wote tukumbuke mama hana makuu, hivyo wapambe tutulieeee tuijenge nchi.

- Panapokorogeka mama yetu kipenzi ndiye anayeumia na kufadhaika. ANATUPENDA WOTE, TUMPE MUDA AIJENGE NCHI YETU NA TUENDELEE KUMUOMBEA.

Asanteni na Mungu awabariki sanaaa.

Queen Esther
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,326
2,000
Unatetea tu MCHWA waliopo ccm, ili waendelee kuifilisi Nchi yetu. Binafsi naomba na hiyo ccm yenyewe nayo ijifie tu! Ili kama Taifa, tuanze upya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom