Mukama akumbana na zomea zomea huko musoma.

Kutokana na taarifa ya habari ya saa mbili usiku ya ITV, Katibu Mkuu wa CCM, Mukama alipokelewa na umati mkubwa wa wananchi mjini Musoma. Cha kushangaza ni kuwa mpaka afike kwenye mkutano wa hadhara, walikuwa wamebakia watu wachache, na hao wachache waliobakia walikuwa wakimzomez, kitendo ambacho kilimfanya aahirishe mkutano huo.

Hapo kazi ipo. Huko Musoma ndio nyumbani kwake anazomewa sasa Mwenyekiti wake ****** akija huko itakuaje? Jamani ukombozi wa Mtanganyika umekaribia.
 
Kama hukusikia,hebu tupe sababu ya Mkama kukatisha mkutano huo?

jamani nimeomba sorry siwezi pingana na wana harakati au wanamageuzi wa jf sikuwa makini kusikiliza kwa sababu naona waliowengi wamenipinga basi nivye,a nikakubaliana nao kuwa sikuwa makini
 
Ningekuwa na uwezo wa kuiambia Tanzania nzima wafanye hivyo, ningezunguka ila mahali!
Mkama anaona kama vile anapendwa sana, umbe anatia kinyaa!
 
mkama hana mvutoooo kabsaaaaa kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza mangula was a cool brother! hutu mkama ccm wanamtafutia presha mapemaaa hawezi fitna za siasa huyu
 
mkama hana mvutoooo kabsaaaaa kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza mangula was a cool brother! huyu mkama ccm wanamtafutia presha mapemaaa hawezi fitna za siasa huyu
 
CCM waondoke madarakani mara moja kabla ya umwagaji damu.Ni ushauri tu.Wameshindwa kazi ni wakati wa kuondoka.
 
msingi wa taarifa hiyo upo katika kukatishwa kwa mkutano, na taarifa ya zomea zomea wala sio picha gani zilionekana kwenye TV, haya nyie tuambieni kwa nini mkutano ulikatishwa kama ilivyoripotiwa, CCM kwisha habari yake
 
Mukama hata sijui kwa nini JK alidhani kwamba ana maana na anaweza kukubalika . Musoma walitaka kumuona tu anafananaje lakini siamini kama walienda kumsikiliza . Hosp wanayo iongelea imekaa miaka mingi na ina matatizo mengi . Ilikuwa ya Kanisa katoliki CCM wakachukua imewashinda kujenga .Kanisa limeomba irudi kwao waimalizie lakini bado wanaletea siasa . Mathayo kusema hayo aliyo yasema ni sawa maana ana pesa kweli ila akili yake haina akili
 
Mkama atapeleka salamu alizopewa na wanamusoma kwa Mwenyekiti wake, na kwa staili hiyo mwenyekiti atachanganya na za mbayuwayu hatuta muona kuja kushukuru wananchi "waliomchagua"!
 
Back
Top Bottom