Mukama akumbana na zomea zomea huko musoma. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mukama akumbana na zomea zomea huko musoma.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tindikalikali, May 22, 2011.

 1. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Muda mfupi uliopita ITV imetangaza zomea zomea katika mkutano huo, hali iliyomlazimu katibu mkuu huyo akatishe hotuba yake.
   
 2. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii imetokea kwenye moja ya mikutano ya ccm huko musoma.inasemekana katibu mkuu wa ccm bw wilson mukama alipata mapokezi makubwa lakini watu walitoweka baada ya mkutano kuanza huku wale waliobaki walikuwa wakizomea mara kwa mara hatimaye kupelekea mukama kukatisha hotuba yake.
   
 3. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kutokana na taarifa ya habari ya saa mbili usiku ya ITV, Katibu Mkuu wa CCM, Mukama alipokelewa na umati mkubwa wa wananchi mjini Musoma. Cha kushangaza ni kuwa mpaka afike kwenye mkutano wa hadhara, walikuwa wamebakia watu wachache, na hao wachache waliobakia walikuwa wakimzomez, kitendo ambacho kilimfanya aahirishe mkutano huo.
   
 4. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii imetokea kwenye moja ya mikutano ya ccm huko musoma.inasemekana katibu mkuu wa ccm bw wilson mukama alipata mapokezi makubwa lakini watu walitoweka baada ya mkutano kuanza huku wale waliobaki walikuwa wakizomea mara kwa mara hatimaye kupelekea mukama kukatisha hotuba yake.


  Source:ITV NEWS
   
 5. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  We acha tu ccm wanayo kazi na bado,go to hell ccm.Nimeiona hiyo taarifa na nimeshangaa katibu huyo mkuu wa ccm kasema "ifikapo 2015 hiyo hospitali itakuwa imekamilika"Inamaaana kwa miaka iliyo salia wananchi waendelee kufa?Hawa ccm ni wasanii hiyo ahadi yenyewe waliyoitoa ni hewa sbb mpaka madawati kwa ajili ya shule wanasaidiwa na vodacom?Kabla ccm hamjatuua inabidi tuwawahi
   
 6. z

  zamlock JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  jamani mbona nimeangalia newz sijaona hyo kuzonea zomea ma,bo mengine tusiwe tunazusha kwa sababu ya upinzani wameonyesha ana hutubia ila ambacho sijakipenda ni mbunge wa zamani mathayo kutamka kuwa mbunge wa chadema na wanachadema ni wezi juu ya madawati aliyosema yamechukuliwa na chadema
   
 7. t

  tumpale JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mwanzo tu atazomewa sana mwisho wa siku majiwe, kwani yeye hajiulizi kwanini mwenyekiti wake haendi mikoani, anajua kilichompata yeye, mawaziri na sasa kinaendelea kwa wabunge wao wamuulize nyambari!!
   
 8. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  na bado,.......
   
 9. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,972
  Likes Received: 6,604
  Trophy Points: 280
  Alipokua anaingia msoma amepokewa na watu wengi sana.alipoanza kutoa hotuba yake watu wakaanza kuondoka mmoja mmoja,hadi wakabaki wachache wanamzomea,akaamua kukatisha hotuba yake baada ya kuona zomeazomea imezidi kiwango.
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  safi wabaki na sera zao za udini!!!na madiwani dar nao wasema wamechoka kudharauliwa na viongozi wa juu wa serikali
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Huyu mzee afadhali hata ya Makamba. Mukama hana mvuto wa kisiasa. Bora angebaki na utaalam wake tu. Au angechukua haiba ya Mangula. Sikuwahi kumsikia Mangula akipayuka, na bado alifanya kazi yake vyema. Mukama anaigiza. Namshauri kazi ya kupayuka na propaganda awaachie kina Nape. Nimecheka kimoyomoyo nilipokuwa naangalia itv taarifa ya habari pale Maratu aliporipoti kuwa Mukama alipokelewa na umati mkubwa huko Mara halafu wananchi wakaanza kuzomea huku wakipungua mkutanoni kitendo kilichomfanya kukatisha hotuba. Sijui kama tbc walithubutu kusema ukweli huu. Mukama, aidha uache siasa ama uwe wewe, ama umuige Mangula. Sasa hivi unajiharibia jina tu
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nathibitisha ni kweli kwamba kwa Mujibu wa ITV Mukama hotuba yake ilikuwa inakatishwa katishwa na Zomea Zomea
   
 13. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Mtangazaji alieripoti ndio kasema ilikuwapo hali ya wananchi kuzome zomea ktk mkutano huo hali iliyosababisha Katibu mkuu huyo kukatisha mkutano,ila hawajaonyesha live zomea hiyo japo sababu ya msingi ya kukatisha mkutano huo ni hali ya wananchi kumzomea Mkama wa ccm.Sasa wewe ndio unaleta ushabiki wakati hukuwa makini kusikiliza taarifa ile.Go to hell ccm
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  SAFI SAAAAAAAAAAAAAAAA MUSOMA WA KUPIGA HUYO ZOMEA HAITOSHI WHY HAJAENDA TARIME AISEE
   
 15. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  habari imeripotiwa hivyo, hawajaonesha jins alivyozomea. Kama ni uzush bas aliyeripoti hiyo habari ndiye mzushi
   
 16. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  na bado./////
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  May 22, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli wana kazi ngumu ya kurudisha imani ya chama kwa wananchi!
   
 18. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  SAFII MUSOMA KWA KUMUONYESHA HAKUBALIKI WHY HAJAENDA TARIME?
   
 19. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  hiloooo,zomea hilooooooo
   
 20. z

  zamlock JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  anabwabwaja kichizi
   
Loading...