Muingereza awafananisha Watz na nguruwe

Muingereza awafananisha Watz na nguruwe

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,413
Bibi. Sarah Hermitage ambaye ni Mwanasheria raia wa Uingereza, mwanaharakati wa kupambana na rushwa na pia mwekezaji katika shamba la Silverdale.
Anapatikana CHOMAchomp

Sarah ambaye amekua akiwakashifu viongozi na wananchi wa Tanzania mara kwa mara alivuka mipaka na kufananisha Watanzania na nguruwe, baada ya kulalamikiwa kwa vitendo vyake vya kutoa maneno machafu kwa Watanzania katika mitandao ya kijamii.

Kauli hizo za Sarah amekua akizitoa kupitia mitandao ya twitter kupitia ukurasa wake wa https://twitter.com/Chomachomp kwa muda mrefu sasa bila kuchukuliwahatua zozote na viongozi wala watendaji wa serikali ya Tanzania.

Kauli ya Sarah kuita Watanzania ilianzia pale Mtanzania mmoja ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe Mbaraka Islam, kulalamikia kitendo chake cha kutukana viongozi na Watanzania wote kwa ujumla wao bila kuwa na hoja zinazowahusu.

"Huyu mama (Sarah) amefanya hivyo baada ya kuona Watanzania wamelala na hakuna anayethubutu kumgusa hasa viongozi wetu anaowatukana anavyotaka bila kuguswa na yeyote," alisema Islam na kuongeza kwamba amechukua hatua kadhaa ambazo hajapenda kuziweka hadharani kwa sasa.

Sarah alikerwa na makala aliyoandoka Islam katika gazeti la Raia Mwema, ambayo ilielezea kukerwa na maneno machafu anayoyatoa kwa Watanzania.

Katika makala hiyo, Islam alisema:

KWA takriban miaka mitano sasa, raia mmoja wa Uingereza, Sarah Hermitage amekuwa akiendesha kampeni ya kumchafua Rais Jakaya Kikwete, Serikali ya Tanzania, taasisi muhimu za nchi yetu kama vile mahakama, waandishi wa habari na hata Watanzania ambao wamekua wakimpinga.

Pamoja na kuwa kumekua na mapungufu katika serikali yake na vyombo vyake kama ilivyo kwa serikali nyingine Duniani ikiwamo ya Uingereza, Muingereza huyu amekua akitoa kashfa kwa kila jambo linaloandikwa ama kujadiliwa kuhusiana na viongozi wa Tanzania na taasisi zake na kwa kutumia lugha isiyo na staha.

Watanzania siku zote wakiwamo wanasiasa, waandishi wa habari na wanaharakati, wamekua wakiikosoa na hata kuishambulia serikali na vyombo vyake inapokosea jambo ambalo ni jema na linasaidia kuimarisha utawala bora, lakini kwa staili anayotumia Muingereza huyu ni kupitiliza mipaka na zaidi ya yote ni udhalilishaji usioweza kuvumilika kwa mtu mwenye mapenzi mema na nchi yake.

Dhumuni la Sarah Hermitage na washirika wake wakiwemo baadhi ya Watanzania ni kuzishawishi nchi za Magharibi wakianzia na Uingereza kusitisha misaada na uwekezaji katika Tanzania. Hilo angeweza kulifanya huko kwao kwa kuwasiliana na serikali yake, lakini badala yake amekuwa akitumia mitandao ya kijamii na barua pepe tena kwa kutumia lugha ya kukashifu na kudhalilisha.

Watanzania wote tuna jukumu la kutetea heshima ya nchi yetu, lakini wapo wale ambao tumewapa jukumu la kusimama mstari wa mbele. Jambo la kusikitisha ni kwamba ni watu wachache sana kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ambaye ambaye amekua na ujasiri wa kumkabili Muingereza huyu, kwa kumwambia wazi kwamba kama ni misaada ana haki ya kuishawishi nchi yake kuzuia misaada kwa Tanzania lakini si kwa kudhalilisha Watanzania.

Zitto alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba nchi nyingi tajiri duniani ikiwamo Uingereza, zimejengwa kwa kutumia rasilimali walizozipora katika nchi walizozitawala ikiwamo Tanzania na kwamba nchi hizo zinaweza pia kuendesha shughuli zake bila misaada ya dharau. Bahati mbaya sana watendaji wengine wengi ambao wanapaswa kutetea heshima yetu, hili suala limewapita, pengine kutokana na kutokua na taarifa sahihi ama kwa kutowajibika.

Jambo la kujiuliza, wale ambao miongoni mwa majukumu yao ya kila siku ni kutetea na kulinda hadhi na heshima ya nchi yetu wanafanya kazi gani? Sasa tunawalipa mishahara mikubwa na marupurupu ya nini kama hawawezi kututetea tunapodhalilishwa ama kutukanwa?

Hali hii inatufanya tukumbuke ujasiri wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara kadhaa aliwatunishia misuli viongozi wa mataifa makubwa walipotaka kuidhalilisha nchi yetu, sembuse raia mmoja ambaye amekua akitumia matatizo yake binafsi kutaka kuidhalilisha Tanzania na kutaka kuishinikiza serikali yake na nyingine kuichukia Tanzania.

Jinsi anavyotumia mtandao wa twitter kuchafua Tanzania

Sarah Hermitage amekua akitafuta katika taarifa za vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania vinavyoandika taarifa zozote kuhusu Tanzania na kuziongezea maneno ya kukashifu na kejeli.

Kwa mfano amekua amechukua taarifa inayomunukuu Raia Jakaya Kikwete akiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupambana na rushwa hadi ndani ya Baraza la Mawaaziri, na yeye kuongezea maneno akisema, "kundi moja la majambazi linaliambia kundi lingine la majambazi kukamata mwizi".

Akachukua taarifa iliyochapishwa katika vyombo vya habari ikimnukuu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribisha wawekezaji katika kilimo na yeye kuongeza maneno akisema, "Mheshimiwa Pinda kitakachoendelea kukandamizi uwekezaji katika kilimo cha Tanzania ni uporaji wa ardhi ya wawekezaji katika mtindo wa Mugabe (Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe)."

Amekua akidiriki kukashifu hadi majaji wote wa Tanzania kwamba wana bei akisema, "sina hakika kama unaweza kupata jaji ambaye si mla rushwa. Wote wana bei," kauli ambayo hata Watanzania wanakua wakiitoa kwa uangalifu maana hata kama kuna majaji ambao si waadilifu, haiwezekani wakawa ni wote, kama ilivyo katika taasisi nyingine.

Raia mmoja wa Kenya anayeishi Tanzania, aliyejitambulisha kwa jina la Marigi Patrick aliandika katika mtandao kwa kusema;

"Sisi Wakenya tuna matatizo yetu na tumekua na tofauti kubwa sana za wazi wazi, lakini anapotokea raia wa kigeni kumshambulia kiongozi wetu tena kama Rais wa nchi, tunaungana na kumshughulikia. Kuna wakati Wazungu walimshambulia Rais Mwai Kibaki, sote tukisaidiwa na wabunge wetu na vyombo vya habari tulimshambulia hadi akakoma kutudharau."

Marigi ambaye anajihusisha na biashara ya bima, anasema Watanzania bado ni wachanga katika demokrasia, ama wanadharau kila kitu bila kujua madhara yake katika hadhi na heshima ya Taifa, na ndio maana wanashindwa kutofautisha kati ya demokrasia na udhalilishaji unaofanywa na raia wa nchi nyingine kama alivyo Sarah Hermitage.
 
Serikali yetu ingekuwa imara wala hayo yasingekuwepo,lakini sioni pa kumlaumu huyo mama.Kama Wezi wa EPA waliambiwa warudishe pesa,kuna serikali hapo imara???Nani asiyejua kwamba rushwa imeshamiri sana nchini?Ingawa wazungu wanadharau,lakini ametoa ujumbe.
 
Sheria inasemaje kuhusu tuhuma kwa huyo Mzungu?Umechukua hatua gani za kisheria ili kumkabili?
 
hehehehehe anazidi kutuweka katika ramani ya kimataifa
 
"kundi moja la majambazi linaliambia kundi lingine la majambazi kukamata mwizi".

"sina hakika kama unaweza kupata jaji ambaye si mla rushwa. Wote wana bei,"

Wewe kweli ni boflo mtoto wa fisadi, uongo uko wapi hapo juu?

Huyu mzungu ni mzalendo wa Tanzania zaidi ya watanzania wenyewe! Big up mzungu kwa kuwasema mafisadi bila woga. Haijalishi una malengo gani so long as yale unayosema ni ukweli mtupu.

Mkuu huyu mama anayoyaona ni mabaya tu juu ya Serikali ya Tanzania simply kwa sababu ya ugomvi wake na Mengi! Is it true kuwa hakuna zuri kutoka kwa Watz including wewe? Open your eyes pls!
This is a dirty campaign!
 
Sheria inasemaje kuhusu tuhuma kwa huyo Mzungu?Umechukua hatua gani za kisheria ili kumkabili?

Huyu mama ni mwanasheria kwa hiyo anajua anafanya nini na mtakapompeleka mahakamani kumshtaki atawagaragaza mpaka mtachanganyikiwa.Kikubwa hilo swali lako la sheria inasemaje ulizia sheria inasemaje kuhusu mafisadi na sio huyo mama yaani watazania tunatumia nguvu nyingi kupambana na vitu vidogo lakini kwa vile vitu vikubwa hatuvifanyii kazi
 
Bibi. Sarah Hermitage ambaye ni Mwanasheria raia wa Uingereza, mwanaharakati wa kupambana na rushwa na pia mwekezaji katika shamba la Silverdale.
Anapatikana CHOMAchomp

Sarah ambaye amekua akiwakashifu viongozi na wananchi wa Tanzania mara kwa mara alivuka mipaka na kufananisha Watanzania na nguruwe, baada ya kulalamikiwa kwa vitendo vyake vya kutoa maneno machafu kwa Watanzania katika mitandao ya kijamii.

Kauli hizo za Sarah amekua akizitoa kupitia mitandao ya twitter kupitia ukurasa wake wa https://twitter.com/Chomachomp kwa muda mrefu sasa bila kuchukuliwahatua zozote na viongozi wala watendaji wa serikali ya Tanzania.

Kauli ya Sarah kuita Watanzania ilianzia pale Mtanzania mmoja ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe Mbaraka Islam, kulalamikia kitendo chake cha kutukana viongozi na Watanzania wote kwa ujumla wao bila kuwa na hoja zinazowahusu.

“Huyu mama (Sarah) amefanya hivyo baada ya kuona Watanzania wamelala na hakuna anayethubutu kumgusa hasa viongozi wetu anaowatukana anavyotaka bila kuguswa na yeyote,” alisema Islam na kuongeza kwamba amechukua hatua kadhaa ambazo hajapenda kuziweka hadharani kwa sasa.

Sarah alikerwa na makala aliyoandoka Islam katika gazeti la Raia Mwema, ambayo ilielezea kukerwa na maneno machafu anayoyatoa kwa Watanzania.

Katika makala hiyo, Islam alisema:

KWA takriban miaka mitano sasa, raia mmoja wa Uingereza, Sarah Hermitage amekuwa akiendesha kampeni ya kumchafua Rais Jakaya Kikwete, Serikali ya Tanzania, taasisi muhimu za nchi yetu kama vile mahakama, waandishi wa habari na hata Watanzania ambao wamekua wakimpinga.

Pamoja na kuwa kumekua na mapungufu katika serikali yake na vyombo vyake kama ilivyo kwa serikali nyingine Duniani ikiwamo ya Uingereza, Muingereza huyu amekua akitoa kashfa kwa kila jambo linaloandikwa ama kujadiliwa kuhusiana na viongozi wa Tanzania na taasisi zake na kwa kutumia lugha isiyo na staha.

Watanzania siku zote wakiwamo wanasiasa, waandishi wa habari na wanaharakati, wamekua wakiikosoa na hata kuishambulia serikali na vyombo vyake inapokosea jambo ambalo ni jema na linasaidia kuimarisha utawala bora, lakini kwa staili anayotumia Muingereza huyu ni kupitiliza mipaka na zaidi ya yote ni udhalilishaji usioweza kuvumilika kwa mtu mwenye mapenzi mema na nchi yake.

Dhumuni la Sarah Hermitage na washirika wake wakiwemo baadhi ya Watanzania ni kuzishawishi nchi za Magharibi wakianzia na Uingereza kusitisha misaada na uwekezaji katika Tanzania. Hilo angeweza kulifanya huko kwao kwa kuwasiliana na serikali yake, lakini badala yake amekuwa akitumia mitandao ya kijamii na barua pepe tena kwa kutumia lugha ya kukashifu na kudhalilisha.

Watanzania wote tuna jukumu la kutetea heshima ya nchi yetu, lakini wapo wale ambao tumewapa jukumu la kusimama mstari wa mbele. Jambo la kusikitisha ni kwamba ni watu wachache sana kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ambaye ambaye amekua na ujasiri wa kumkabili Muingereza huyu, kwa kumwambia wazi kwamba kama ni misaada ana haki ya kuishawishi nchi yake kuzuia misaada kwa Tanzania lakini si kwa kudhalilisha Watanzania.

Zitto alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba nchi nyingi tajiri duniani ikiwamo Uingereza, zimejengwa kwa kutumia rasilimali walizozipora katika nchi walizozitawala ikiwamo Tanzania na kwamba nchi hizo zinaweza pia kuendesha shughuli zake bila misaada ya dharau. Bahati mbaya sana watendaji wengine wengi ambao wanapaswa kutetea heshima yetu, hili suala limewapita, pengine kutokana na kutokua na taarifa sahihi ama kwa kutowajibika.

Jambo la kujiuliza, wale ambao miongoni mwa majukumu yao ya kila siku ni kutetea na kulinda hadhi na heshima ya nchi yetu wanafanya kazi gani? Sasa tunawalipa mishahara mikubwa na marupurupu ya nini kama hawawezi kututetea tunapodhalilishwa ama kutukanwa?

Hali hii inatufanya tukumbuke ujasiri wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara kadhaa aliwatunishia misuli viongozi wa mataifa makubwa walipotaka kuidhalilisha nchi yetu, sembuse raia mmoja ambaye amekua akitumia matatizo yake binafsi kutaka kuidhalilisha Tanzania na kutaka kuishinikiza serikali yake na nyingine kuichukia Tanzania.

Jinsi anavyotumia mtandao wa twitter kuchafua Tanzania

Sarah Hermitage amekua akitafuta katika taarifa za vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania vinavyoandika taarifa zozote kuhusu Tanzania na kuziongezea maneno ya kukashifu na kejeli.

Kwa mfano amekua amechukua taarifa inayomunukuu Raia Jakaya Kikwete akiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupambana na rushwa hadi ndani ya Baraza la Mawaaziri, na yeye kuongezea maneno akisema, “kundi moja la majambazi linaliambia kundi lingine la majambazi kukamata mwizi”.

Akachukua taarifa iliyochapishwa katika vyombo vya habari ikimnukuu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribisha wawekezaji katika kilimo na yeye kuongeza maneno akisema, “Mheshimiwa Pinda kitakachoendelea kukandamizi uwekezaji katika kilimo cha Tanzania ni uporaji wa ardhi ya wawekezaji katika mtindo wa Mugabe (Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe).”

Amekua akidiriki kukashifu hadi majaji wote wa Tanzania kwamba wana bei akisema, “sina hakika kama unaweza kupata jaji ambaye si mla rushwa. Wote wana bei,” kauli ambayo hata Watanzania wanakua wakiitoa kwa uangalifu maana hata kama kuna majaji ambao si waadilifu, haiwezekani wakawa ni wote, kama ilivyo katika taasisi nyingine.

Raia mmoja wa Kenya anayeishi Tanzania, aliyejitambulisha kwa jina la Marigi Patrick aliandika katika mtandao kwa kusema;

“Sisi Wakenya tuna matatizo yetu na tumekua na tofauti kubwa sana za wazi wazi, lakini anapotokea raia wa kigeni kumshambulia kiongozi wetu tena kama Rais wa nchi, tunaungana na kumshughulikia. Kuna wakati Wazungu walimshambulia Rais Mwai Kibaki, sote tukisaidiwa na wabunge wetu na vyombo vya habari tulimshambulia hadi akakoma kutudharau.”

Marigi ambaye anajihusisha na biashara ya bima, anasema Watanzania bado ni wachanga katika demokrasia, ama wanadharau kila kitu bila kujua madhara yake katika hadhi na heshima ya Taifa, na ndio maana wanashindwa kutofautisha kati ya demokrasia na udhalilishaji unaofanywa na raia wa nchi nyingine kama alivyo Sarah Hermitage.

Toka ameanza kutoa matamshi yake ni muda. Kwa WALENGWA kuwa kimya=ukweli.

Japo unauma UKWELI utasimama siku zote.
 
...Si mumpeleke mahakamani basi kama amewatukana, badala ya kujaza bandwidth ya JF kila baada ya dakika tano kwa kuirudia rudia hii Issue?????????????
 
ingekuwa enzi za mwalimu angem..........................................
kama alivyomfunza adabu yule jamaa aliyeitukana serikali ya tz enzi zile
 
Sheria inasemaje kuhusu tuhuma kwa huyo Mzungu?Umechukua hatua gani za kisheria ili kumkabili?

Sheria zichukue mkondo kwanza kwa waliohusika na sakata la RADA na Richmond. Watanzania wengi wamekufa kutokana na wizi wa fedha zile. Sasa huyu mama amesema ukweli, wewe unataka achukuliwe sheria gani? Huyu mama amekuwa mstaarabu sana kuwaita watanzania nguruwe. Ametupa heshima kubwa sana kutuita nguruwe, ukizingatia nyama ya kitimoto ilivyo na wapenzi wengi. Ndivyo hivyo hiyo, nchi yetu ilivyo na wapenzi wengi wa kupora rasilimali zetu.
 
Mkuu huyu mama anayoyaona ni mabaya tu juu ya Serikali ya Tanzania simply kwa sababu ya ugomvi wake na Mengi! Is it true kuwa hakuna zuri kutoka kwa Watz including wewe? Open your eyes pls!
This is a dirty campaign!

Mkuu Buchanan ubaya huonekana zaidi kuliko wema, ingawa haya mengine yameletwa na serikali yetu wenyewe, tusiliangalie hili kwa macho ya "mzungu" katukana "watanzania" bali tupime yaliyomo katika anachokiongea na sababu zinazomfanya ayaseme hayo, vinginevyo serikali yetu itatukanwa hadi kesho. Wao wenyewe walimkaribisha now she has grown too big for their shoes, wenzetu hawana utamaduni wa kumeza maneno.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom