Ujumbe kwa Heche

Ujumbe kwa Heche

zaza1

Member
Joined
Jun 28, 2018
Posts
58
Reaction score
48
Heche, kupambana kisiasa ni haki yako, na kukosoa mfumo ni sehemu ya demokrasia. Lakini siasa haipaswi kufika mahali ambapo furaha, maendeleo na maslahi ya Taifa yanafanywa kuwa mhanga.


Kama kweli kuna kauli za kuzuia au kuhujumu mambo yenye maslahi mapana kwa Tanzania—ikiwemo michezo, Yanga, au uwezekano wa Tanzania kuwa mwenyeji wa AFCON—basi nadhani huo si mwelekeo sahihi wa mapambano ya kisiasa.


Pambana na system kwa hoja, sera, uwajibikaji na njia za kisheria. Usipambane na Taifa.


Mimi kama raia wa Tanzania, sitaki kuangalia mtu anatoka chama gani. Nitawapima viongozi kwa maono yao, uzalendo wao na namna wanavyolinda maslahi ya wananchi na maendeleo ya nchi.


Sitampa kura yangu kiongozi ambaye, kwa mtazamo wangu, anaonekana kuwa tayari kuzuia au kudidimiza maendeleo na furaha ya Watanzania kwa sababu za kisiasa.


Tanzania ni yetu sote. Tupambane kwa ajili ya kuijenga Tanzania, si kuibomoa.
 
Michezo na burudani haiwezi kutamalaki kwenye chuki,mauaji,fitina,utekaji sema ni vile tu bado wanamichezo hawajakutwa na haya mambo {uko mbele huzingatia sana utu,haki,sheria,aman ndiomaana hufurahia michezo)
 
Back
Top Bottom