Muhongo anaivuruga TANESCO, Magufuli yuko wapi?

Muhongo anaivuruga TANESCO, Magufuli yuko wapi?

Tanesco ikifa lawama ni kwa muhongo, kwa sasa yeye ndie mkurugenzi mkuu wa tanesco,mameneja wa kanda wanaripoti kwake,anapokea malalamiko ya temporary break downs,yeye ndie meneja wa huduma kwa wateja wa tanesco,yeye anaamuru meneja huyu wa kanda simtaki huyu namtaka.

Muhongo ni mtaalam wa miamba na mawe asijifanye kuujua umeme,shurika lina hali mbaya kifedha na sasa hali itakua mbaya zaidi kwa maamuzi ya muhongo na sio menejimenti.

Muhongo anaua morali ya wafanyakazi wa tanesco,kuanzia mkurugenzi hadi mtu wa chini,yeye ni maagizo tu bila kujali muundo au mpango wa kazi wa tanesco,shirika sasa halina dira linaongozwa kwa mawazo na maagizo ya muhongo,shirika linatekeleza plans za muhongo na sio zake.

Muhongo ni tishio kwa ustawi wa shirika,muda sio mrefu hili shirika linafilisika.
Moja ya watumbuliwa nini??? Sisi wananchi wa kawaida tunamkubali kwa sabb changamoto nyingi zinatatuliwa chini yake
 
We umewahi fanya kazi na Muhongo?
lini alielezwa kitu akaelewa?

JF ni public forums.....hapa hata Waziri Ndalichako uwaziri wake ulianzia hapa kupigiwa debe
haya sio majungu .....mengi tuliyo yaongea kuhusu Muhongo huko nyuma yamewafikia mabosi wake na walimrekebisha
Hahaha wewe kila siku ni negative tu kuhusu muhongo. Pole sana wananchi twamkubali, ndani na nje ya jamii forum
 
Unasemaje ni assumptions wakati nimeweka link?
maagizo anatoa kwa mameneja wa chini mbele ya media...
unataka ushahidi gani?
yeye sio CEO why atoe maagizo kwa mameneja wa kanda na mikoa?

Sasa ulitaka nani awaagize, Rais? Anayo mamlaka ya kumuagiza yeyote katika sekta anayosimamia
 
Mnyonge Mnyongeni Haki Yake Mpeni, Huyu Bwana Mhongo ni Mtu Mzuri Sana Tatizo la Watanzania Tumepofushwa na Chuki, fitina, na Majungu, hii ndiyo Sumu inaloliangamiza Taifa Hili.

Kila kiongozi Mzuri, lazima Achafuliwe, jamani Katuroga Nani?

Kwa mtu makini hawezi kubeza wala kudharau utendaji wa Prof Mhongo, huyu Bwana, ni Mtendaji kazi na siyo mtu wa siasa, sote bila chembe ya unafiki, tunafahamu jinsi ambavyo amefanya kazi kubwa sana kwa muda mfupi kwenye sekta ya nishati na madini.

Tuacheni jamani majungu bila kuwa na Fact, ikiwa mtu Anafanya vizuri basi tumpongeze, uo ndiyo uhungwana jamani.
Uhungwana dah
 
Nami nimeliona ilo Prof anajisahau sana nadhani huwezi toa order kwa zonal managers/regional managers wa TANESCO moja kwa moja unless umepitia kwa mabosi wao otherwise inakuwa ni KUMUNDERMINE kwa CEO wa TANESCO.
In a long run iyo italeta mtafaluku manake wapo ambao wataharibu na watasema tuliambiwa na waziri meanwhile wao wanareport kwa CEO.
Apo chain of command inakuwa ndivyo sivyo
Kama waziri anaruhusiwa kutoa maagizo pale inapofaa. Mnataka akae nyuma awe anaangalia tu? Wananchi wanapotoa malalamiko lazima achukue hatua. Chain my foot.
 
kuna mwaka wa south Africa waliingia mkataba na Tanesco katika kusimamia utawala tuu hakuna hata mmoja alipiga kelele leo mtanzania mwenzenu kwa maslahi yetu hooo anawaingilia kuna kitu huko kipo kinafanyika sio bure izi kelele.
.
Huyu the boss ni mtumbuliwa au anatumika
 
Kuna watu kwa kweli wanachoongea kama vile vipofu na hawa ndio Iddi Amin alikuwatupa mto Kagera nafuu waliwe tu na mamba .Wanaongea kwa sababu ya chuki zao binafisi ,na yawezekana Muhongo amewabania maslahi yao .
Waziri Muhongo sisi wadau wa umeme tunamukubali 100% ,kazi zake na anachokifanya kina maslahi kwa Taifa kwa ujumla , watendaji wote wa wizara wako chini yake kwa hiyo lazima atoe maelekezo ili mambo yakae sawa .
Kwa hiyo mtoa mada usitake kutuaminisha kwa maneno yako yasiyo na utafiti wa kutosha watanzania wengi tuna muunga mkono na ni moja wapo kati ya mawaziri wachapa kazi katika serikali ya Mhe.Magufuli ,kwa hiyo tusiongee tu kama vile hatufikiri au hatuyaoni mambo mazuri anayoyafanya mheshimiwa Muhongo ,sisi tunampa big upo akaze kamba zaidi.
 
Mkuu fuatilia tu media
Hata TANESCO kupunguza bei ya kuunga umeme lilikuwa agizo lake
kwa masharti kuwa serikali itatoa ruzuku
ni kweli inatoa ruzuku but haitoshelezi
na ina maana kuwa TANESCO isijiendeshe kwa faida na isijitegemee
kuishi kwa ruzuku......na mwisho ndo hayo kwenda kukopa na deni kuongezeka....

Soma hata ile hotuba ya Zitto siku ile anafunga ishu ya ESCROW
aliitaja deni la TANESCO before Muhongo lilikuwa bilioni 50
now zaidi ya bilioni 300....

Now ameteuliwa tena na Magufuli anakuja na maagizo tele ya dizaini hiyo

Unachotaka kutuambia maombi ya mkurugenzi kwa EWURA kuomba kushusha gharama za umeme ikiwa ni pamoja kufuta service Charge yalikuwa maigizo? Unajua mabadiliko ya gharama za Huduma hujadiliwa na kupendekezwa ktk mkutano Wa EWURA na wadau? Muhongo anaingiaje hali kuwa data za uzalishaji zinatolewa na wataalam Wa Tanesco?
 
Prof.Muhongo katusaidia sana watumiaji wa umeme tangu akiwa kwenye serikali ya JK. Alishusha gharama za kuunganishiwa umeme toka tzs 2.2m hadi tzs 700,000 kwa nguzo mbili nami ni kati ya waliofaidika. Sasa service charge out. Mnataka waziri wa namna gani? Mambo ya deni laTanesco hayajaanza leo na yana majibu yake umeme wote utakapokuwa wa gesi na maji. Hii mitambo ya mafuta ya kifisadi ndiyo inaumiza Tanesco na Prof Muhongo hahusiki hata na mtambo moja. Nyie masifadi na wafanyakazi wazembe na wezi wa Tanesco mlioko humu shut up au jinyongeni. Prof Muhongo piga kazi sisi tunakuamini.
Hizi kelele zote sio za bure jamani, watu washazibiwa mirija yao humu. Mnasahau walikuwa wanaagiza nguzo toka South Afrika ya Iringa? Kuunganishiwa umeme sio chini ya mil 1.5 tena kwa umbali usiozidi nguzo 2/3 na zikizidi hizo utalipia kila nguzo pesa kibao!! Tena Mimi nashauri ifutwe menejimenti yote aongoze prof mwenyewe, maana tayari kijijini kwetu Kasenga umeme ushafika sasa.
 
Nimewahi kuweka thread za Waziri Muhongo kuja na sera zake binafsi za kuinyang'anya TANESCO 'uzalishaji na kubinafsisha' so far ni kama amepigwa stop ameacha kuzungumza hayo lakini sasa anachokifanya kwa TANESCO ni hatari zaidi.

Muhongo yeye ni waziri lakini ni zaidi ya CEO wa TANESCO anaingilia utendaji wa kila siku now anatoa maagizo yeye mwenyewe moja kwa moja kwa mameneja wa TANESCO wa kanda mameneja wa wilaya mameneja wa mkoa na watedaji wengi wa TANESCO.

Kilichopo now TANESCO ni kama chaos chochote menejimenti ya TANESCO ikiamua, Muhongo anaagiza wafanye kinyume chake au vile anavyoona yeye inafaaa. Yeye ni kama 'de facto CEO' wa TANESCO ieleweke kuwa yeye Muhongo hajawahi kuongoza chochote huko nyuma kabla ya kuwa Waziri na baadhi ya maamuzi yake na 'amri' zake kwa TANESCO yamepelekea deni la TANESCO liongezeke mara 5 zaidi na mtu yeyote mwenye akili anajua 'athari' za taasisi kubwa kama TANESCO kuwa wanapokea maagizo ambayo mengi siyo ya kitaalamu ni ya kisiasa kwa mtu nje ya shirika.

Ushauri wangu kwa Magufuli kama wana tatizo na menejimenti ya TANESCO ni bora kuibadili kuliko hii ya sasa ambapo menejimenti ipo lakini maamuzi yote anafanya waziri sababu mwisho mambo yakiharibika itakua uonevu mkubwa kuipa lawama menejimenti.

Vikao vya Muhongo na mameneja wa kanda na mikoa wa TANESCO vinaripotiwa hadi na media wakati mwingine vikao hivyo Waziri Muhongo anafanya bila kushirikisha menejimenti ya shirika na maamuzi ni amri tu.

Magufuli anayajua yote haya?

Huu ni mfano mmoja tu wa interference ya waziri kwa menejimenti: Muhongo kutimua mameneja Tanesco

Huu mchango wa member mmoja humu nauweka hapa kwa faida ya wengi;
Mkuu, watu wameshushiwa umeme juzi tu. Unadhani watakuelewa?
 
Kizuri umeme umeshuka haina shida...wew na mengi wako endeleeni kulia lia
 
nilitegemea kukutana na analysis ya kueleweka nakutana na porojo
 
Usiwe unatazama mambo kwa roho ya kimasikini

Wafanyakazi wa Tanesco huo umeme ni jasho lao
ukifanya kazi Daily News gazeti hununui
ukifanya kazi tigo au voda airtime hununui
iko dunia nzima

hata wapiga debe tu daladala hawalipi nauli.....
Ingawa waalimu watoto wao wanalipa ada full !
 
Mkuu fuatilia tu media
Hata TANESCO kupunguza bei ya kuunga umeme lilikuwa agizo lake
kwa masharti kuwa serikali itatoa ruzuku
ni kweli inatoa ruzuku but haitoshelezi
na ina maana kuwa TANESCO isijiendeshe kwa faida na isijitegemee
kuishi kwa ruzuku......na mwisho ndo hayo kwenda kukopa na deni kuongezeka....

Soma hata ile hotuba ya Zitto siku ile anafunga ishu ya ESCROW
aliitaja deni la TANESCO before Muhongo lilikuwa bilioni 50
now zaidi ya bilioni 300....

Now ameteuliwa tena na Magufuli anakuja na maagizo tele ya dizaini hiyo
Nimefuatilia media na hili ndio nililokutana nalo www.majira.co.tz/index.php?page=read_more&name=news&id=8073
 
Poleni sana mlioathirika kwa uwapo wa Muhongo wizara ya Nishati. Swala la kuigawa Tanesco limo katika Ilani ya ccm ya 2015 hivyo kutekelezwa ni muhimu . Muhongo kuitisha wawekezaji katika kuzalisha umeme ni jukumu lake la kutekeleza Ilani
Kama waziri lazima awaeleze watendaji waliochini yake nini anataka na nini hataki ni wajibu wake wala si kutisha. Waziri akisema meneja fulani kaharibu ceo atajua cha kufanya.
Serikali imetoa pesa nyingi kuwekeza katika umeme kinyerezi,ges, rea nk. Kinachofanyika chama kinajua na Rais anajua.
Cha kufanya ni kukubali mabadiriko na tufanyekazi
 
hapa naona tatizo ni "exposure" inawezekana tangu ulivyotoka shule ukaajiriwa tanesco na hadi leo uko tanesco dunia yako ni tanesco. Wapo corporate chairman kama abromovic yeye kila siku ni kutoa maagizo nawewe ceo lazima uendane na kasi yake, anafika wakati anapanga hata wachezaji uwanjani anachotaka ni ushindi bila kujali nani kaleta ushindi mbona hajafirisika ndio kwanza utajiri unaongezeka. wakati ananunua chelsea wataalamu wa biashara walijua kapotea njia na angefirisika hata ndani ya management yake waliupinga uamuzi ule, chakushangaza baada ya mwaka mmoja chelsea ilimwingizia pesa marambili ya zile alizowekeza. nimekutolea mfano mmoja wa watu wenye haiba ya muhongo na wamefanikiwa.

Wewe ndo huna exposure kabisa
sasa tanesco unaifananisha na chelsea?
una akili timamu?

Tanesco ni mali binafsi ya Muhongo?
unajua hata maana ya shirika la umma?
 
Back
Top Bottom