Muhongo anaivuruga TANESCO, Magufuli yuko wapi?

Muhongo anaivuruga TANESCO, Magufuli yuko wapi?

Ulitakiwa useme sio kweli haingilii maamuzi ya menejimenti
wakati maagizo yake kwa mameneja wa kanda na mikoa ya TANESCO yapo all over the media

Je TANESCO inaendeshwa na Waziri au na menejimenti yake?

nani anaetakiwa kumpa orders meneja wa wilaya wa TANESCO?
waziri au CEO wa TANESCO?
The Boss ukiangalia kwa makini matatizo mengi ya kiuongozi hapa kwetu naona yanaletwa na mambo haya.
1 viongozi wasiojua kuongoza
2 viongozi wasiojua nini maana ya kuamua, kusimamia maamuzi waliyotoa
3 viongozi wasiojua kukasimisha madaraka
4 viongozi wasiojua mipaka yao ya utendaji.
5 viongozi wanaojikweza tu bila kuangalia maslahi mapana ya jamii.
naona sasa hivi idara zilizoko chini ya mawaziri zinaendeshwa na mawaziri na siyo menejimenti zake tena.
 
Nimewahi kuweka thread za Waziri Muhongo kuja na sera zake binafsi za kuinyang'anya TANESCO 'uzalishaji na kubinafsisha' so far ni kama amepigwa stop ameacha kuzungumza hayo lakini sasa anachokifanya kwa TANESCO ni hatari zaidi.

Muhongo yeye ni waziri lakini ni zaidi ya CEO wa TANESCO anaingilia utendaji wa kila siku now anatoa maagizo yeye mwenyewe moja kwa moja kwa mameneja wa TANESCO wa kanda mameneja wa wilaya mameneja wa mkoa na watedaji wengi wa TANESCO.

Kilichopo now TANESCO ni kama chaos chochote menejimenti ya TANESCO ikiamua, Muhongo anaagiza wafanye kinyume chake au vile anavyoona yeye inafaaa. Yeye ni kama 'de facto CEO' wa TANESCO ieleweke kuwa yeye Muhongo hajawahi kuongoza chochote huko nyuma kabla ya kuwa Waziri na baadhi ya maamuzi yake na 'amri' zake kwa TANESCO yamepelekea deni la TANESCO liongezeke mara 5 zaidi na mtu yeyote mwenye akili anajua 'athari' za taasisi kubwa kama TANESCO kuwa wanapokea maagizo ambayo mengi siyo ya kitaalamu ni ya kisiasa kwa mtu nje ya shirika.

Ushauri wangu kwa Magufuli kama wana tatizo na menejimenti ya TANESCO ni bora kuibadili kuliko hii ya sasa ambapo menejimenti ipo lakini maamuzi yote anafanya waziri sababu mwisho mambo yakiharibika itakua uonevu mkubwa kuipa lawama menejimenti.

Vikao vya Muhongo na mameneja wa kanda na mikoa wa TANESCO vinaripotiwa hadi na media wakati mwingine vikao hivyo Waziri Muhongo anafanya bila kushirikisha menejimenti ya shirika na maamuzi ni amri tu.

Magufuli anayajua yote haya?

Huu ni mfano mmoja tu wa interference ya waziri kwa menejimenti: Muhongo kutimua mameneja Tanesco

Huu mchango wa member mmoja humu nauweka hapa kwa faida ya wengi;
sikukuchagua kwa sababu za kisiasa bali kwa utaalam; J P MAGUFULI ( kinyerezi)
 
inasikitisha kuona Muhongo hashauriki hadi sasa kavunja bodi baada ya kutofautina nayo kuhusu bei za umeme v/s madeni makubwa ya TANESCO yanayozidi kuwa makubwa uku wakilazimishwa kushusha bei ya umeme. sijui ni economics ya wapi????????????
 
Nimemuelewa vyema mtoa kinachotakiwa ni kuvunja kwanza mikataba yote inayoifanya TANESCO kulipa zaidi kabla ya kushusha bei ya Umeme ili kulifanya shirika kujitosheleza na kupata faida bila kuhitaji ruzuku ya serikali ambayo ni ndogo sana.

Pili yake bunge lilishauri IPTL mitambo yake yote ibinafsishwe kwa TANESCO na hii inelisaidia zaidi shirika kuliko ilivyo sasa.

Nadhani Muhongo angeutumia UBABE wake kuivunja mikataba yote mibovu inayoliumiza shirika.
 
Hivi kupunguza bei ulitaka nani aseme. Mambo kama kupunguza bei ni siasa yaani ilani ya walioshinda. Mwanasiasa anayetekeleza sera na ilani ni waziri katika wizara kwa niaba ya Rais na chama.
Kingine ndugu yangu ikumbukwe wazi hiyo TANESCO ilishafeli kupita kiasi ndio maana bila booster ya wanasiasa ingekwisha kabisa. Sasa hilo deni la ESCROW Muhongo kalifanyaje tena?
NIlidhani kuna EWURA ambao wana mamlaka hayo
 
hizo protokali ndio zimetufikisha hapa. Na ndizo zilizosababisha jamaa ango'oke ktk utawala ulio pita. Sasa lazima awashukie moja kwa moja ili makosa ya mkurugenzi sijui meneja yasije kumgharimu hapo baadae. twende kazi muhungo
 
Mnyonge Mnyongeni Haki Yake Mpeni, Huyu Bwana Mhongo ni Mtu Mzuri Sana Tatizo la Watanzania Tumepofushwa na Chuki, fitina, na Majungu, hii ndiyo Sumu inaloliangamiza Taifa Hili.

Kila kiongozi Mzuri, lazima Achafuliwe, jamani Katuroga Nani?

Kwa mtu makini hawezi kubeza wala kudharau utendaji wa Prof Mhongo, huyu Bwana, ni Mtendaji kazi na siyo mtu wa siasa, sote bila chembe ya unafiki, tunafahamu jinsi ambavyo amefanya kazi kubwa sana kwa muda mfupi kwenye sekta ya nishati na madini.

Tuacheni jamani majungu bila kuwa na Fact, ikiwa mtu Anafanya vizuri basi tumpongeze, uo ndiyo uhungwana jamani.

Mkuu, utakuwa umelogwa labda wewe peke yako. Watu wanahoji mantiki ya yanayofanywa na kiongozi kwa sababu huyu ni mtumishi wa umma. Wewe unaonaje hatua hiyo kama "kulogwa"? kwa nini huwalaumu "kulogwa" wale wanaosifia kila kitu? nao wako wengi tu.
 
Sasa wewe mwenyewe hushangai?
kipi kina faida? kushusha bei au kuzuia isipande kwa mda mrefu?
Siasa ndo zinaongoza haya mambo now
Mimi ni mshangaaji mkubwa kwa hili. Sijawahi kuona kampuni au shirikalinaloyoa hufuma zake kwa hasara linaomba kudhudha bei ya huduma hizo! Hata kuzuia kupanda kwa mda mrefu katika hali hiyo ni kujidanganya! Haitachukua muda tutalipia hasara hizo tena kwa kiwango kikubwa zaidi.
 
Kwanza mlizoea kula rushwa acha awabane mkipigiwa simu hamfiki kwa wakati katika tukio sisi wananchi ndio tunamtaka mtu kama Mhongo endelea na kamba hiyo Mhongo
 
Usiwe unatazama mambo kwa roho ya kimasikini

Wafanyakazi wa Tanesco huo umeme ni jasho lao
ukifanya kazi Daily News gazeti hununui
ukifanya kazi tigo au voda airtime hununui
iko dunia nzima

hata wapiga debe tu daladala hawalipi nauli.....

Haaa haaa nakumbuka kipindi kile General Tyre tulikuwa na staff price 50% chini sasa wafanyakazi wakaanza kuitumia vibaya unakuta mfanyakazi hana hata pikipiki kila mwenzi anakomba tires 5 pcs.
 
inasikitisha kuona Muhongo hashauriki hadi sasa kavunja bodi baada ya kutofautina nayo kuhusu bei za umeme v/s madeni makubwa ya TANESCO yanayozidi kuwa makubwa uku wakilazimishwa kushusha bei ya umeme. sijui ni economics ya wapi????????????

Hakuna atakaekuelewa now lakini mda utafika
 
The Boss ukiangalia kwa makini matatizo mengi ya kiuongozi hapa kwetu naona yanaletwa na mambo haya.
1 viongozi wasiojua kuongoza
2 viongozi wasiojua nini maana ya kuamua, kusimamia maamuzi waliyotoa
3 viongozi wasiojua kukasimisha madaraka
4 viongozi wasiojua mipaka yao ya utendaji.
5 viongozi wanaojikweza tu bila kuangalia maslahi mapana ya jamii.
naona sasa hivi idara zilizoko chini ya mawaziri zinaendeshwa na mawaziri na siyo menejimenti zake tena.


Hilo la viongozi kutojua mipaka yake sasa ni kubwa mno
halafu mambo yakiharibika wanajifanya hawahusiki huku maamuzi ni yao wenyewe
 
Kama management ya tanesco imekaa muda wote huo lakini wameshindwa kushusha umeme,lakin prof ameanza juz tunaona impact yake,ni heri aendelee hivyo hivyo ili mambo yaende

Mkuu, umeme umeshushwa baada ya kuunganishwa umeme wa gesi kwenye gridi ambao ni umeme wa gharama nafuu, sio kwa maamuzi ya mwanasiasa yeyote.

Ova
 
Mpaka leo najiuliza alimloga vipi magufuli na usukuma wake wote kashfa zote zile za escrow bado akamrudisha palepale au wana uswahiba nini
 
hizo protokali ndio zimetufikisha hapa. Na ndizo zilizosababisha jamaa ango'oke ktk utawala ulio pita. Sasa lazima awashukie moja kwa moja ili makosa ya mkurugenzi sijui meneja yasije kumgharimu hapo baadae. twende kazi muhungo
Watu wamekali protocol tu ila hawaangalii kwamba miaka nenda rudi tumezifuata sasa angalia zilipotufikisha. Wananchi tunajali huduma bora kwanza mambo mengine hayo wataelekezana baadae.
 
Pamoja na kusifiwa usomi uliotukuka lakini nina tatizo moja na huyu mtu, huyu ni wale type ya superiority complex kujiona na kujifanya anajua kila kitu na wengine ni wapuuzi tuu
Muhongo ni kiburi ana dharau majivuno na ubabe....ngoja tuone mwisho wake
itakuwa weww ni mmoja ya walioathirika na posho zikizosimamishwa na Muhongo. umeelezea ushabiki tupu tena ule wa kutumwa na kulipwa. huu utumbo njoo upya mama
 
Back
Top Bottom