The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,229
- 116,840
Nimewahi kuweka thread za Waziri Muhongo kuja na sera zake binafsi za kuinyang'anya TANESCO 'uzalishaji na kubinafsisha' so far ni kama amepigwa stop ameacha kuzungumza hayo lakini sasa anachokifanya kwa TANESCO ni hatari zaidi.
Muhongo yeye ni waziri lakini ni zaidi ya CEO wa TANESCO anaingilia utendaji wa kila siku now anatoa maagizo yeye mwenyewe moja kwa moja kwa mameneja wa TANESCO wa kanda mameneja wa wilaya mameneja wa mkoa na watedaji wengi wa TANESCO.
Kilichopo now TANESCO ni kama chaos chochote menejimenti ya TANESCO ikiamua, Muhongo anaagiza wafanye kinyume chake au vile anavyoona yeye inafaaa. Yeye ni kama 'de facto CEO' wa TANESCO ieleweke kuwa yeye Muhongo hajawahi kuongoza chochote huko nyuma kabla ya kuwa Waziri na baadhi ya maamuzi yake na 'amri' zake kwa TANESCO yamepelekea deni la TANESCO liongezeke mara 5 zaidi na mtu yeyote mwenye akili anajua 'athari' za taasisi kubwa kama TANESCO kuwa wanapokea maagizo ambayo mengi siyo ya kitaalamu ni ya kisiasa kwa mtu nje ya shirika.
Ushauri wangu kwa Magufuli kama wana tatizo na menejimenti ya TANESCO ni bora kuibadili kuliko hii ya sasa ambapo menejimenti ipo lakini maamuzi yote anafanya waziri sababu mwisho mambo yakiharibika itakua uonevu mkubwa kuipa lawama menejimenti.
Vikao vya Muhongo na mameneja wa kanda na mikoa wa TANESCO vinaripotiwa hadi na media wakati mwingine vikao hivyo Waziri Muhongo anafanya bila kushirikisha menejimenti ya shirika na maamuzi ni amri tu.
Magufuli anayajua yote haya?
Huu ni mfano mmoja tu wa interference ya waziri kwa menejimenti: Muhongo kutimua mameneja Tanesco
Huu mchango wa member mmoja humu nauweka hapa kwa faida ya wengi;

Tanesco ikifa lawama ni kwa muhongo, kwa sasa yeye ndie mkurugenzi mkuu wa tanesco,mameneja wa kanda wanaripoti kwake,anapokea malalamiko ya temporary break downs,yeye ndie meneja wa huduma kwa wateja wa tanesco,yeye anaamuru meneja huyu wa kanda simtaki huyu namtaka.
Muhongo ni mtaalam wa miamba na mawe asijifanye kuujua umeme,shurika lina hali mbaya kifedha na sasa hali itakua mbaya zaidi kwa maamuzi ya muhongo na sio menejimenti.
Muhongo anaua morali ya wafanyakazi wa tanesco,kuanzia mkurugenzi hadi mtu wa chini,yeye ni maagizo tu bila kujali muundo au mpango wa kazi wa tanesco,shirika sasa halina dira linaongozwa kwa mawazo na maagizo ya muhongo,shirika linatekeleza plans za muhongo na sio zake.
Muhongo ni tishio kwa ustawi wa shirika,muda sio mrefu hili shirika linafilisika.