Muhongo anaivuruga TANESCO, Magufuli yuko wapi?

Muhongo anaivuruga TANESCO, Magufuli yuko wapi?

Nimewahi kuweka thread za Waziri Muhongo kuja na sera zake binafsi za kuinyang'anya TANESCO 'uzalishaji na kubinafsisha' so far ni kama amepigwa stop ameacha kuzungumza hayo lakini sasa anachokifanya kwa TANESCO ni hatari zaidi.

Muhongo yeye ni waziri lakini ni zaidi ya CEO wa TANESCO anaingilia utendaji wa kila siku now anatoa maagizo yeye mwenyewe moja kwa moja kwa mameneja wa TANESCO wa kanda mameneja wa wilaya mameneja wa mkoa na watedaji wengi wa TANESCO.

Kilichopo now TANESCO ni kama chaos chochote menejimenti ya TANESCO ikiamua, Muhongo anaagiza wafanye kinyume chake au vile anavyoona yeye inafaaa. Yeye ni kama 'de facto CEO' wa TANESCO ieleweke kuwa yeye Muhongo hajawahi kuongoza chochote huko nyuma kabla ya kuwa Waziri na baadhi ya maamuzi yake na 'amri' zake kwa TANESCO yamepelekea deni la TANESCO liongezeke mara 5 zaidi na mtu yeyote mwenye akili anajua 'athari' za taasisi kubwa kama TANESCO kuwa wanapokea maagizo ambayo mengi siyo ya kitaalamu ni ya kisiasa kwa mtu nje ya shirika.

Ushauri wangu kwa Magufuli kama wana tatizo na menejimenti ya TANESCO ni bora kuibadili kuliko hii ya sasa ambapo menejimenti ipo lakini maamuzi yote anafanya waziri sababu mwisho mambo yakiharibika itakua uonevu mkubwa kuipa lawama menejimenti.

Vikao vya Muhongo na mameneja wa kanda na mikoa wa TANESCO vinaripotiwa hadi na media wakati mwingine vikao hivyo Waziri Muhongo anafanya bila kushirikisha menejimenti ya shirika na maamuzi ni amri tu.

Magufuli anayajua yote haya?

Huu ni mfano mmoja tu wa interference ya waziri kwa menejimenti: Muhongo kutimua mameneja Tanesco

Huu mchango wa member mmoja humu nauweka hapa kwa faida ya wengi;
wacha aingilie tu. hapo tanesco ni kizazi cha nyoka sio rahisi kuwaamini watu tayari wamezoea kupiga dili za mamilioni. maisha yao na miradi yao iko mashakani wasipoendelea na madili. wapo wenye kampuni za milingoti, wapo wenye dili za transforma za india. wengine kampuni zao zitakufa kama hawasupply tanesco kwa bei mbaya, etc etc. yafaa waziri asicheze mbali hadi majipu yakamuliwe usaa yote.
 
Mnyonge Mnyongeni Haki Yake Mpeni, Huyu Bwana Mhongo ni Mtu Mzuri Sana Tatizo la Watanzania Tumepofushwa na Chuki, fitina, na Majungu, hii ndiyo Sumu inaloliangamiza Taifa Hili.

Kila kiongozi Mzuri, lazima Achafuliwe, jamani Katuroga Nani?

Kwa mtu makini hawezi kubeza wala kudharau utendaji wa Prof Mhongo, huyu Bwana, ni Mtendaji kazi na siyo mtu wa siasa, sote bila chembe ya unafiki, tunafahamu jinsi ambavyo amefanya kazi kubwa sana kwa muda mfupi kwenye sekta ya nishati na madini.

Tuacheni jamani majungu bila kuwa na Fact, ikiwa mtu Anafanya vizuri basi tumpongeze, uo ndiyo uhungwana jamani.

Prof.Muhongo katusaidia sana watumiaji wa umeme tangu akiwa kwenye serikali ya JK. Alishusha gharama za kuunganishiwa umeme toka tzs 2.2m hadi tzs 700,000 kwa nguzo mbili nami ni kati ya waliofaidika. Sasa service charge out. Mnataka waziri wa namna gani? Mambo ya deni laTanesco hayajaanza leo na yana majibu yake umeme wote utakapokuwa wa gesi na maji. Hii mitambo ya mafuta ya kifisadi ndiyo inaumiza Tanesco na Prof Muhongo hahusiki hata na mtambo moja. Nyie masifadi na wafanyakazi wazembe na wezi wa Tanesco mlioko humu shut up au jinyongeni. Prof Muhongo piga kazi sisi tunakuamini.
 
usilolijua ni usiku wa giza,eti media ....endeleeni kuweka hisia tu bila kujua ukweli wa mambo!
 
Nami nimeliona ilo Prof anajisahau sana nadhani huwezi toa order kwa zonal managers/regional managers wa TANESCO moja kwa moja unless umepitia kwa mabosi wao otherwise inakuwa ni KUMUNDERMINE kwa CEO wa TANESCO.
In a long run iyo italeta mtafaluku manake wapo ambao wataharibu na watasema tuliambiwa na waziri meanwhile wao wanareport kwa CEO.
Apo chain of command inakuwa ndivyo sivyo
 
Mkuu siamini kama huna elimu hata kidogo ya menejimenti
mameneja wa mikoa na wilaya waripoti kwa waziri we unaona ni sawa?
Waziri kutoa maagizo kwa njia ya simu ni sawa?

hivi labda nikuulize wewe ndo meneja wa wilaya au kanda wa Tanesco
ceo wako akupe maagizo ya nenda kushoto na waziri aje aseme nenda kulia
we unaonaje? ni sawa?

Mawaziri wengine hao wanatimua na kuweka watu wengine....hawafanyi daily tasks...kama Muhongo
Muhongo hajatimua mtu ni kuwapa maagizo yake tu daily
hapa kazi tu # eco prof
 
Pasi na shaka yeyote the Boss ni mmoja wa wakuu wa Tanesco...tatizo la siasa na utalaamu linaimaliza hii nchi...siku hizi ni rahisi sana mwanasiasa kutoa maagizo yanayokinzana na sheria ili mradi aandikwe na gazeti au atangazwe ni hali mbaya kwa kweli na hilo linaumiza mashirika mengi ya umma
 
ebna jipu la hawa tanesco lipo kahama umeme kwetu ni ndoto kukaa masaa 12 bila umeme ni jambo la kawaida ebu pro uje na uku aise i shidaah
 
Pamoja na kusifiwa usomi uliotukuka lakini nina tatizo moja na huyu mtu, huyu ni wale type ya superiority complex kujiona na kujifanya anajua kila kitu na wengine ni wapuuzi tuu
Muhongo ni kiburi ana dharau majivuno na ubabe....ngoja tuone mwisho wake
Majivuno ni sahihi , kwanini asijivune si amesoma ?
 
Ngoja niwaambie Huyu alieleandika taarifa tunajua ni mfanyakazi wa TANESCO aliekubwa na TUMBUA TUMBUA MAJIBU ya kimya kimya. Tuwe wakweli hawa TANESCO wanamadeni mengi zaidi ya milioni 800, wakati Muhongo hakuwepo, tumepata taarifa kuwa hawa TANESCO wanapewa BONASI kila mwaka na mwaka huu wamepewa BOBASI ya karibu trilioni 3 wakagawana, Sasa Wewe unatuambia nini humu, tunajua nyie watumishi mliosomamishwa na Muhongo Ndio mmeanza kusema. Hawa TANESCO badala ya kununua Transfoma za hapa TANZANIA tena kwenye kiwanda chao wanaenda kununua INDIA, halafu MUHONGO akiingilia na kuwaelekeza wanunue hapa mnalalamika mnaingiliwa. Watanzania tuwe macho na hawa vibaraka wanamtumwa kumchafua Muhongo. Tukumbuke TANESCO hawa hawa walikuwa wanakata Umeme eti Kina Cha maji kipo chini, Sasa amekuja Muhongo kakuta Watanzania wanadanganywa akaibua huo uovu na sass tatizo la umeme limekwisha tunaishi kwa raha. Hivi humu Ndani naona kuna watu wamezoea matatizo Yaani Umeme ukikuwa unakatika halafu tunadanganywa Kaja Prof. Muhongo kutatua hayo matatizo tunamuona mbaya.

Muhongo Chapa kazi, waingilie hawa TANESCO hadi majumbani kwao kwani hawa wafanyakazi Kama Huyu aliyeleta hoja hii wanatumiwa kuliibia shirika, wakibanwa wanakimbilia kwenye mitandao ya kijamii.
 
kuna mwaka wa south Africa waliingia mkataba na Tanesco katika kusimamia utawala tuu hakuna hata mmoja alipiga kelele leo mtanzania mwenzenu kwa maslahi yetu hooo anawaingilia kuna kitu huko kipo kinafanyika sio bure izi kelele..
 
s
ruzuku haitoshi huku wafanyakazi wa tanesco wakipeana umeme unit 700 kwa mwezi kwa shilingi elfu 10 tu...

yaani ukiajiriwa tanesco ukitoa elfu 10 unapewa unit 700 za umeme... na hapo hapo shirika linategemea serikali iwape ruzuku... kiukweli watanzania hatuna.shukrani.... tanesco ni jipu kubwa sana na najua mhongo akisaidiana na mwenzake wa kanda ya ziwa jemedari mkuu lazima walitumbue tu... tuwape muda... tanesco haimalizi huu mwaka na management hii hii ya kaskazini iliyozea ujanja ujanja

Siyo unit 700 mkuu ni 720 kwa kila mwezi kwa pesa uloiweka hapo,na kuunganishiwa umeme ni 5000 kwa wafanyakazi wake.
Mleta mada ana chuki zake tu na Muhongo la sivyo angemshauri kufuta huo uhuni.
 
unit 720 ni nyingi sana kama wanapata bure aisee bongo haiishi maajabu huyu mtoa mada leo sijui nini kimemsibu maana leo simuelewi kabisa.
wafanyakazi wa tenesco wako wangapi let say 10000
kwa miezi 12
720x280x10000x12
201600x120000~ 24b
24B KWA mwaka sio hela kidogo
 
Nikiona mtu anawatetea Tanesco namtilia mashaka, atakuwa ni kishoka au mnufaika wa umeme wa wizi, tanesco tuliyoilalamika sana kwa mambo ya kipuuzi, gharama juu huduma duni. Najua kwa upande mwingine Prof. anaingilia kazi za huyo CEO wao, ila kama hafanyi vizuri kumuingilia majukum yake kwa lengo la kuokoa na kutetea maslah ya walaji wa huduma hiyo nalo ni jambo zuri tukiwa tunasubiria utaratibu kamili na usiotoa mwanya wa watu kujiamulia tu upangwe iki hii miingiliano isiwepo, hata raisi asingetakiwa kabisa kugusa sehemu zote zaidi ya kuhangaika na mawaziri wake, lakini kwa hali ilivyo ya kiutendaji na madudu yaliyopo itambidi afanye hivyo kuonyesha mfano.
Miongoni mwa watumishi wa Tanesco ndio wanaongoza kuiba umeme na vifaa, hawa watu ngoja tu waingikiwe majukumu yao mpaka hapo watakapotambua umeme ni huduma muhimu kwa raia
 
Wewe jiongeze mkuu...
una uhakika mnapumua?
ukisikia Tanesco imefilisika ndo mtapumua vizuri

Menejimenti ni ishu za kitaalam
ndo maana watu wanasomea
sasa kama kila Waziri awe CEO wa taasisi zote zilizo chini yake basi tuvunje menejimenti ya hizo taasisi

Kuna faida gani ya kuwa na menejimenti unailipa mishahara huku kazi zote anafanya waziri?
si aiondoe tu hiyo menejimenti ajulikane yeye ndo CEO?
Tunaowaita wataalamu ndo wametufikisha hapa tulipo
Wewe jiongeze mkuu...
una uhakika mnapumua?
ukisikia Tanesco imefilisika ndo mtapumua vizuri

Menejimenti ni ishu za kitaalam
ndo maana watu wanasomea
sasa kama kila Waziri awe CEO wa taasisi zote zilizo chini yake basi tuvunje menejimenti ya hizo taasisi

Kuna faida gani ya kuwa na menejimenti unailipa mishahara huku kazi zote anafanya waziri?
si aiondoe tu hiyo menejimenti ajulikane yeye ndo CEO?
Nchi hii haina wataalamu,ni ujingaujinga tu.
 
Ngoja niwaambie Huyu alieleandika taarifa tunajua ni mfanyakazi wa TANESCO aliekubwa na TUMBUA TUMBUA MAJIBU ya kimya kimya. Tuwe wakweli hawa TANESCO wanamadeni mengi zaidi ya milioni 800, wakati Muhongo hakuwepo, tumepata taarifa kuwa hawa TANESCO wanapewa BONASI kila mwaka na mwaka huu wamepewa BOBASI ya karibu trilioni 3 wakagawana, Sasa Wewe unatuambia nini humu, tunajua nyie watumishi mliosomamishwa na Muhongo Ndio mmeanza kusema. Hawa TANESCO badala ya kununua Transfoma za hapa TANZANIA tena kwenye kiwanda chao wanaenda kununua INDIA, halafu MUHONGO akiingilia na kuwaelekeza wanunue hapa mnalalamika mnaingiliwa. Watanzania tuwe macho na hawa vibaraka wanamtumwa kumchafua Muhongo. Tukumbuke TANESCO hawa hawa walikuwa wanakata Umeme eti Kina Cha maji kipo chini, Sasa amekuja Muhongo kakuta Watanzania wanadanganywa akaibua huo uovu na sass tatizo la umeme limekwisha tunaishi kwa raha. Hivi humu Ndani naona kuna watu wamezoea matatizo Yaani Umeme ukikuwa unakatika halafu tunadanganywa Kaja Prof. Muhongo kutatua hayo matatizo tunamuona mbaya.

Muhongo Chapa kazi, waingilie hawa TANESCO hadi majumbani kwao kwani hawa wafanyakazi Kama Huyu aliyeleta hoja hii wanatumiwa kuliibia shirika, wakibanwa wanakimbilia kwenye mitandao ya kijamii.

Umeandika majungu, uongo naa unafiki.

Acha kufutinisha wafanyakazi wa TANESCO na WANANCHI.
 
Nikiona mtu anawatetea Tanesco namtilia mashaka, atakuwa ni kishoka au mnufaika wa umeme wa wizi, tanesco tuliyoilalamika sana kwa mambo ya kipuuzi, gharama juu huduma duni. Najua kwa upande mwingine Prof. anaingilia kazi za huyo CEO wao, ila kama hafanyi vizuri kumuingilia majukum yake kwa lengo la kuokoa na kutetea maslah ya walaji wa huduma hiyo nalo ni jambo zuri tukiwa tunasubiria utaratibu kamili na usiotoa mwanya wa watu kujiamulia tu upangwe iki hii miingiliano isiwepo, hata raisi asingetakiwa kabisa kugusa sehemu zote zaidi ya kuhangaika na mawaziri wake, lakini kwa hali ilivyo ya kiutendaji na madudu yaliyopo itambidi afanye hivyo kuonyesha mfano.
Miongoni mwa watumishi wa Tanesco ndio wanaongoza kuiba umeme na vifaa, hawa watu ngoja tu waingikiwe majukumu yao mpaka hapo watakapotambua umeme ni huduma muhimu kwa raia
Kufitinisha/kugombanisha watu ni Dhambi kubwa kuliko kuuwa mtu
 
The boss amehongwa na baadhi ya mameneja kuwatetea. Hakuna mtanzania asiyejua udhaifu wa hao ma CEO . Huenda nawe ni miongoni mwao. Pr. Muhongo kaza buti usiogope hayo majipu
 
Back
Top Bottom