mr gentleman
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,221
- 4,692
hahaaaaa!, ndugu acha kunichekesha, nao naona wamekua kama dawasco, pale kinondoni mkwajuni kuna bomba la maji limepasuka na lina mwaga maji. Nimeliona tangu mwaka jana mwezi wa saba! hadi sasa hivi lina tiririsha maji, alafu si kwamba lipo mafichoni lipo wazi kwenye kituo cha daladala.kwani hawa tanesco wapo hai bado? mana hapa kwangu kuna waya zimeshuka mpaka watoto wanataka kubembea na wakina mama wanataka kuanikia nguo......jamaa hawaji hata uwafate na masidisi benzi...
Wewe inaelekea Ulikuwa na mirija ya Ulaji Tanesco Sasa Muhongo kaziba line zako umeamua kumshambulia sana .Nimewahi kuweka thread za Waziri Muhongo kuja na sera zake binafsi za kuinyang'anya TANESCO 'uzalishaji na kubinafsisha' so far ni kama amepigwa stop ameacha kuzungumza hayo lakini sasa anachokifanya kwa TANESCO ni hatari zaidi.
Muhongo yeye ni waziri lakini ni zaidi ya CEO wa TANESCO anaingilia utendaji wa kila siku now anatoa maagizo yeye mwenyewe moja kwa moja kwa mameneja wa TANESCO wa kanda mameneja wa wilaya mameneja wa mkoa na watedaji wengi wa TANESCO.
Kilichopo now TANESCO ni kama chaos chochote menejimenti ya TANESCO ikiamua, Muhongo anaagiza wafanye kinyume chake au vile anavyoona yeye inafaaa. Yeye ni kama 'de facto CEO' wa TANESCO ieleweke kuwa yeye Muhongo hajawahi kuongoza chochote huko nyuma kabla ya kuwa Waziri na baadhi ya maamuzi yake na 'amri' zake kwa TANESCO yamepelekea deni la TANESCO liongezeke mara 5 zaidi na mtu yeyote mwenye akili anajua 'athari' za taasisi kubwa kama TANESCO kuwa wanapokea maagizo ambayo mengi siyo ya kitaalamu ni ya kisiasa kwa mtu nje ya shirika.
Ushauri wangu kwa Magufuli kama wana tatizo na menejimenti ya TANESCO ni bora kuibadili kuliko hii ya sasa ambapo menejimenti ipo lakini maamuzi yote anafanya waziri sababu mwisho mambo yakiharibika itakua uonevu mkubwa kuipa lawama menejimenti.
Vikao vya Muhongo na mameneja wa kanda na mikoa wa TANESCO vinaripotiwa hadi na media wakati mwingine vikao hivyo Waziri Muhongo anafanya bila kushirikisha menejimenti ya shirika na maamuzi ni amri tu.
Magufuli anayajua yote haya?
huu ni mfano mmoja tu wa interference ya waziri kwa menejimenti
Muhongo kutimua mameneja Tanesco
huu mchango wa member mmoja humu nauweka hapa kwa faida ya wengi
Tanesco ikifa lawama ni kwa muhongo, kwa sasa yeye ndie mkurugenzi mkuu wa tanesco,mameneja wa kanda wanaripoti kwake,anapokea malalamiko ya temporary break downs,yeye ndie meneja wa huduma kwa wateja wa tanesco,yeye anaamuru meneja huyu wa kanda simtaki huyu namtaka.
Muhongo ni mtaalam wa miamba na mawe asijifanye kuujua umeme,shurika lina hali mbaya kifedha na sasa hali itakua mbaya zaidi kwa maamuzi ya muhongo na sio menejimenti.
Muhongo anaua morali ya wafanyakazi wa tanesco,kuanzia mkurugenzi hadi mtu wa chini,yeye ni maagizo tu bila kujali muundo au mpango wa kazi wa tanesco,shirika sasa halina dira linaongozwa kwa mawazo na maagizo ya muhongo,shirika linatekeleza plans za muhongo na sio zake.
Muhongo ni tishio kwa ustawi wa shirika,muda sio mrefu hili shirika linafilisika.
Mleta mada kaamua kusaka huruma JF Kwa njia za ujanja , lakini Muhongo anachapa kazi hata Kama ana mapungufu yake Kama binadamu lakini mazuri ni mengi kuliko mabaya ,Kama management ya tanesco imekaa muda wote huo lakini wameshindwa kushusha umeme,lakin prof ameanza juz tunaona impact yake,ni heri aendelee hivyo hivyo ili mambo yaende
Kwani huyu muheshimiwa ni mkabila gani vile?maana kama ni yale makabila ya pale maeneo flani kujisifia huwa ni kawaida yao wao huwa wanajua kila kitu.Pamoja na kusifiwa usomi uliotukuka lakini nina tatizo moja na huyu mtu, huyu ni wale type ya superiority complex kujiona na kujifanya anajua kila kitu na wengine ni wapuuzi tuu
Muhongo ni kiburi ana dharau majivuno na ubabe....ngoja tuone mwisho wake
Wafanyakazi wa tanesco umeme ni jasho lao? U must be kidding...kupewa 700kWh kwa mwezi ni sawa na shs ngapi, while the company makes no profit.Usiwe unatazama mambo kwa roho ya kimasikini
Wafanyakazi wa Tanesco huo umeme ni jasho lao
ukifanya kazi Daily News gazeti hununui
ukifanya kazi tigo au voda airtime hununui
iko dunia nzima
hata wapiga debe tu daladala hawalipi nauli.....
Ili la kushusha bei lilishangaza, mpaka EWURA wanakuwa na wasiwasi kuhusu punguzo linaloombwa! Lakini tunashangaa nini kwa stahili ya sasa tunaiona mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya n.k. wote wanafuatilia 'utendandaji' hadi kwa maofisa wasiowajibika kwao na tena kwa kuruka mamlaka zinazowahusu maofisa hao. Wanawawajibisha bila mamlaka zao kujua au hata kujulishwa - wanazisikia bombani!Mkuu fuatilia tu media
hata Tanesco kupunguza bei ya kuunga umeme lilikuwa agizo lake
kwa masharti kuwa serikali itatoa ruzuku
ni kweli inatoa ruzuku but haitoshelezi
na ina maana kuwa Tanesco isijiendeshe kwa faida na isijitegemee
isshi kwa ruzuku......na mwisho ndo hayo kwenda kukopa na deni kuongezeka....
soma hata ile hotuba ya Zitto siku ile anafunga ishu ya Escrow
aliitaja deni la Tanesco before Muhongo lilikuwa bilioni 50
now zaidi ya bilioni 300....
Now ameteuliwa tena na Magufuli anakuja na maagizo tele ya dizaini hiyo
Naona unaongelea a hear say, na hoja yako inarudi kwa Muhongo wa wakati ule wa awamu iliyopita eti reference yako ni escrow na maandiko ya Zito Kabwe.Mkuu fuatilia tu media
hata Tanesco kupunguza bei ya kuunga umeme lilikuwa agizo lake
kwa masharti kuwa serikali itatoa ruzuku
ni kweli inatoa ruzuku but haitoshelezi
na ina maana kuwa Tanesco isijiendeshe kwa faida na isijitegemee
isshi kwa ruzuku......na mwisho ndo hayo kwenda kukopa na deni kuongezeka....
soma hata ile hotuba ya Zitto siku ile anafunga ishu ya Escrow
aliitaja deni la Tanesco before Muhongo lilikuwa bilioni 50
now zaidi ya bilioni 300....
Now ameteuliwa tena na Magufuli anakuja na maagizo tele ya dizaini hiyo
Yaani uoni yanayoendelea! Haujashangaa kwa shirika linalofanya hasara kuomba kushusha bei ya huduma zake? Haya ndiyo yalichangia kuua mashirika yetu huko nyuma. Ebu tuache mashirika yanayotoa huduma kibiashara yafanye hivyo ili tusije beba mzigo mkubwa huko siku za usoni.Wafanyakazi wa tanesco umeme ni jasho lao? U must be kidding...kupewa 700kWh kwa mwezi ni sawa na shs ngapi, while the company makes no profit.
Nimewahi kupanga nyumba ya mfanyakazi wa tanesco, umeme ulikuwa bure...bure kabisa! Kama mpo radhi wafanyakazi wa tanesco wale "jasho lao" while mwingine atanunua 1kWh kwa 290tsh mtakuwa na yenu.
Mleta mada umelalamika tu, toa facts angalau tano ili mada yako iwe tangible.
kweli kabisa mkuu,kitendo cha muhongo kuamuru kuondolewa kwa service charge hakikubaliki kabisaWatu hawajui kuwa unaweza kuwa msomi lakini usiwe umeelimika....! Na Hilo ndio Naona linalomsibu prof.....!
Kama wana makosa lazima watimuliwe maana hakuna namna.
Nadhani unajichanganya sasa.Usiwe unatazama mambo kwa roho ya kimasikini
Wafanyakazi wa Tanesco huo umeme ni jasho lao
ukifanya kazi Daily News gazeti hununui
ukifanya kazi tigo au voda airtime hununui
iko dunia nzima
hata wapiga debe tu daladala hawalipi nauli.....
Nilitaka kuandika hivyo pia, tangu jamaa aingie wizarani umeme umekuwa stable kwa zaidi ya 75%. Tumepunguziwa bei kwa 2%(japo sio kubwa sana), tumeondolewa service charge(5220tsh)....tunataka nini zaidi, especially sisi ambao hatuhusiki huko?Tokea prof ateuliwe, UMEME haukatiki ovyo, no service charges, TUNATAKA NINI TENA WATZ????
Prince nakuunga mkono, watz wakisimamiwa wanaleta longolongo, kimsingi hakuna shirika lenye watu wazembe na wapenda rushwa kama tanesco.Mnyonge Mnyongeni Haki Yake Mpeni, Huyu Bwana Mhongo ni Mtu Mzuri Sana Tatizo la Watanzania Tumepofushwa na Chuki, fitina, na Majungu, hii ndiyo Sumu inaloliangamiza Taifa Hili.
Kila kiongozi Mzuri, lazima Achafuliwe, jamani Katuroga Nani?
Kwa mtu makini hawezi kubeza wala kudharau utendaji wa Prof Mhongo, huyu Bwana, ni Mtendaji kazi na siyo mtu wa siasa, sote bila chembe ya unafiki, tunafahamu jinsi ambavyo amefanya kazi kubwa sana kwa muda mfupi kwenye sekta ya nishati na madini.
Tuacheni jamani majungu bila kuwa na Fact, ikiwa mtu Anafanya vizuri basi tumpongeze, uo ndiyo uhungwana jamani.
Ni nzuri Kwa upande wa wananchi lakini ingekuwa bora Zaidi gharama Kwa unit zingeshuka......!kweli kabisa mkuu,kitendo cha muhongo kuamuru kuondolewa kwa service charge hakikubaliki kabisa