Muhongo anaivuruga TANESCO, Magufuli yuko wapi?

Mkuu The Boss sina wasi wasi na Bandiko lako lkn naomba "Supporting Evidence" ili kulipatia nguvu zaidi.

Mfano: Maamuzi aliyotoa na athari zake.

NB:

Viongozi wa Awamu ya 5 wamevurugwa na Kutumbua Majipu.... Hawana muda wa kufuata kanuni za Uongozi.

Mzee!.
 
Nimewahi kuweka thread za Waziri Muhongo kuja na sera zake binafsi za kuinyang'anya TANESCO 'uzalishaji na kubinafsisha' so far ni kama amepigwa stop ameacha kuzungumza hayo lakini sasa anachokifanya kwa TANESCO ni hatari zaidi.

Muhongo yeye ni waziri lakini ni zaidi ya CEO wa TANESCO anaingilia utendaji wa kila siku now anatoa maagizo yeye mwenyewe moja kwa moja kwa mameneja wa TANESCO wa kanda mameneja wa wilaya mameneja wa mkoa na watedaji wengi wa TANESCO.

Kilichopo now TANESCO ni kama chaos chochote menejimenti ya TANESCO ikiamua, Muhongo anaagiza wafanye kinyume chake au vile anavyoona yeye inafaaa. Yeye ni kama 'de facto CEO' wa TANESCO ieleweke kuwa yeye Muhongo hajawahi kuongoza chochote huko nyuma kabla ya kuwa Waziri na baadhi ya maamuzi yake na 'amri' zake kwa TANESCO yamepelekea deni la TANESCO liongezeke mara 5 zaidi na mtu yeyote mwenye akili anajua 'athari' za taasisi kubwa kama TANESCO kuwa wanapokea maagizo ambayo mengi siyo ya kitaalamu ni ya kisiasa kwa mtu nje ya shirika.

Ushauri wangu kwa Magufuli kama wana tatizo na menejimenti ya TANESCO ni bora kuibadili kuliko hii ya sasa ambapo menejimenti ipo lakini maamuzi yote anafanya waziri sababu mwisho mambo yakiharibika itakua uonevu mkubwa kuipa lawama menejimenti.

Vikao vya Muhongo na mameneja wa kanda na mikoa wa TANESCO vinaripotiwa hadi na media wakati mwingine vikao hivyo Waziri Muhongo anafanya bila kushirikisha menejimenti ya shirika na maamuzi ni amri tu.

Magufuli anayajua yote haya?
Hebu weka mifano ya baadhi ya maamuzi ambayo Muhongo amewai kuyaingilia na hakutakiwa kufanya hivyo!

Una imani na Magufuli?Na lini umeanza kumuamini?
 
Still unaendelea kumtuhumu mtu kwa assumption,hadhi ya JF ni kubwa scandal nyingi nchi hii zimeibuliwa hapa
  1. Labda uko Tanesco ,tuletee hayo maagizo ambayo Muhongo ametofautiana na CEO wa Tanesco ?
  2. Tuonyeshe hayo maagizo Muhongo alilyoyatoa Tanesco kwa njia ya simu ?

Unasemaje ni assumptions wakati nimeweka link?
maagizo anatoa kwa mameneja wa chini mbele ya media...
unataka ushahidi gani?
yeye sio CEO why atoe maagizo kwa mameneja wa kanda na mikoa?
 
Mkuu fuatilia tu media
hata Tanesco kupunguza bei ya kuunga umeme lilikuwa agizo lake
kwa masharti kuwa serikali itatoa ruzuku
ni kweli inatoa ruzuku but haitoshelezi
na ina maana kuwa Tanesco isijiendeshe kwa faida na isijitegemee
isshi kwa ruzuku......na mwisho ndo hayo kwenda kukopa na deni kuongezeka....

soma hata ile hotuba ya Zitto siku ile anafunga ishu ya Escrow
aliitaja deni la Tanesco before Muhongo lilikuwa bilioni 50
now zaidi ya bilioni 300....

Now ameteuliwa tena na Magufuli anakuja na maagizo tele ya dizaini hiyo
Sijaona hoja hata moja hapo ya kumtia hatiani Muhongo! Ulivyo andika uzi ni tofauti na mifano unayo itoa..

Hoja hizo ni dhaifu kabisa labda kuna zingine!
 
The Boss, I hope wewe ni mwajiliwa wa Tanesco. Au!... Kwa nafasi yake niliamini anafanya hayo yote baada ya mawasiliano ya ndani na menejiment. Kama sivyo kunaweza kuna tatizo lakini pia hali ya taaisi za serikali ilivyokuwa inaendeshwa inatia mashaka.

Bodi za wakurugenzi zilikuwa ni vikundi vya makubaliano ya mambo ya kipuuzi kabisa yenye maslahi kwao wana bodi. Hayo ni kote tangu NSSF, PPF, PSPF, TBS, TPDC, Universities, etc. etc. Kwa mwanasiasa ambaye ndo anayekuwa punching bag kuitetea Tanesco kule Bungeni, inakuwa aibu kubwa kuanza kusema hayo ni maamuzi ya menejimenti. Huyo CEO inafikia hatua huwezi kumuamini kumuachia aamue anachotaka.

Kwa hizo ruzuku pia namtetea kiasi. Yaonekana Tanesco wanataka kuendesah shirika bila investment. Kukiwa na ongezeko la mahitaji wao wanasukuma gharama kwa watumiaji badala ya wao kuweka mtaji na baadaye wapate faida. Watumiaji wanachangia REA wakati hiyo kwa Tanescvo ni investment na baadaye watakaopata faida siyo wachangiaji, ni Tanesco!

Tanesco itapata faida baada ya kuongeza idadi ya watumiaji umeme. Hao watumiaji umeme wataongezekaje kama unaweka gharama ambazo ni exorbitant! Mbona mbinu ni rahisi. Hata konda anakudai nauli baada ya kuwa umepanda na kuondoka kituoni.

Inawezekana wewe hunielewi
siko hapa kuitetea menejimenti
ndo maana nikasema kama ana tatizo na menejimenti basi aibadili...

hapa kuna kitu very very simple....hata ukiwa na elimu ya darasa la kwanza tu inatosha kuelewa

unamuajiri mfano mlinzi akulindie nyumba...
halafu na wewe unakesha na bunduki nje ya nyumba usikukucha...
huku ukimpa maagizo huyo mlinzi....

why usimfukuze kama unaona hafai?
 
Mkuu The Boss sina wasi wasi na Bandiko lako lkn naomba "Supporting Evidence" ili kulipatia nguvu zaidi.

Mfano: Maamuzi aliyotoa na athari zake.

NB:

Viongozi wa Awamu ya 5 wamevurugwa na Kutumbua Majipu.... Hawana muda wa kufuata kanuni za Uongozi.

Mzee!.

Hebu soma link hii tu uone ni sawa kwa waziri kuongea haya?
yeye ndo ceo?
Muhongo kutimua mameneja Tanesco
 
unit 700 ni laki mbili tu...
zisikutoe roho.......
unafikiri wafanyakazi wakinyimwa hizo unit ndo hali ya umeme itaboreka?
na motisha kwa wafanyakazi itaongezeka?
200000x10000x12= 24000000000
wew unaona ni kidogo hizo kwa mwaka
 
Nimewahi kuweka thread za Waziri Muhongo kuja na sera zake binafsi za kuinyang'anya TANESCO 'uzalishaji na kubinafsisha' so far ni kama amepigwa stop ameacha kuzungumza hayo lakini sasa anachokifanya kwa TANESCO ni hatari zaidi.

Muhongo yeye ni waziri lakini ni zaidi ya CEO wa TANESCO anaingilia utendaji wa kila siku now anatoa maagizo yeye mwenyewe moja kwa moja kwa mameneja wa TANESCO wa kanda mameneja wa wilaya mameneja wa mkoa na watedaji wengi wa TANESCO.

Kilichopo now TANESCO ni kama chaos chochote menejimenti ya TANESCO ikiamua, Muhongo anaagiza wafanye kinyume chake au vile anavyoona yeye inafaaa. Yeye ni kama 'de facto CEO' wa TANESCO ieleweke kuwa yeye Muhongo hajawahi kuongoza chochote huko nyuma kabla ya kuwa Waziri na baadhi ya maamuzi yake na 'amri' zake kwa TANESCO yamepelekea deni la TANESCO liongezeke mara 5 zaidi na mtu yeyote mwenye akili anajua 'athari' za taasisi kubwa kama TANESCO kuwa wanapokea maagizo ambayo mengi siyo ya kitaalamu ni ya kisiasa kwa mtu nje ya shirika.

Ushauri wangu kwa Magufuli kama wana tatizo na menejimenti ya TANESCO ni bora kuibadili kuliko hii ya sasa ambapo menejimenti ipo lakini maamuzi yote anafanya waziri sababu mwisho mambo yakiharibika itakua uonevu mkubwa kuipa lawama menejimenti.

Vikao vya Muhongo na mameneja wa kanda na mikoa wa TANESCO vinaripotiwa hadi na media wakati mwingine vikao hivyo Waziri Muhongo anafanya bila kushirikisha menejimenti ya shirika na maamuzi ni amri tu.

Magufuli anayajua yote haya?

huu ni mfano mmoja tu wa interference ya waziri kwa menejimenti

Muhongo kutimua mameneja Tanesco

huu mchango wa member mmoja humu nauweka hapa kwa faida ya wengi

Tanesco ikifa lawama ni kwa muhongo, kwa sasa yeye ndie mkurugenzi mkuu wa tanesco,mameneja wa kanda wanaripoti kwake,anapokea malalamiko ya temporary break downs,yeye ndie meneja wa huduma kwa wateja wa tanesco,yeye anaamuru meneja huyu wa kanda simtaki huyu namtaka.

Muhongo ni mtaalam wa miamba na mawe asijifanye kuujua umeme,shurika lina hali mbaya kifedha na sasa hali itakua mbaya zaidi kwa maamuzi ya muhongo na sio menejimenti.

Muhongo anaua morali ya wafanyakazi wa tanesco,kuanzia mkurugenzi hadi mtu wa chini,yeye ni maagizo tu bila kujali muundo au mpango wa kazi wa tanesco,shirika sasa halina dira linaongozwa kwa mawazo na maagizo ya muhongo,shirika linatekeleza plans za muhongo na sio zake.

Muhongo ni tishio kwa ustawi wa shirika,muda sio mrefu hili shirika linafilisika.
Punguza majungu kwa muhongo kila siku nakuona unamdiss jamaa sijui kakufanyia nn
 
Haina shida ilimradi maagizo yake yana manufaa kwa taifa
 
Mbayahayo madeni unakuta wana katenchao aisee inauma sanaaaaa kilaaa nikimfikiriaaa
 
Tanesco ikifa lawama ni kwa muhongo, kwa sasa yeye ndie mkurugenzi mkuu wa tanesco,mameneja wa kanda wanaripoti kwake,anapokea malalamiko ya temporary break downs,yeye ndie meneja wa huduma kwa wateja wa tanesco,yeye anaamuru meneja huyu wa kanda simtaki huyu namtaka.

Muhongo ni mtaalam wa miamba na mawe asijifanye kuujua umeme,shurika lina hali mbaya kifedha na sasa hali itakua mbaya zaidi kwa maamuzi ya muhongo na sio menejimenti.

Muhongo anaua morali ya wafanyakazi wa tanesco,kuanzia mkurugenzi hadi mtu wa chini,yeye ni maagizo tu bila kujali muundo au mpango wa kazi wa tanesco,shirika sasa halina dira linaongozwa kwa mawazo na maagizo ya muhongo,shirika linatekeleza plans za muhongo na sio zake.

Muhongo ni tishio kwa ustawi wa shirika,muda sio mrefu hili shirika linafilisika.
Tanesco naife tu ikifa watakuja akina symbion eskom songas, mbona ttcl ilivyokufa wakaja vodacom tigo, atc imekufa wamekuja fastjet. Impact ya uwepo wa muhongo tunaiona, mgao umepungua nguzo zinasambazwa vijijini mita tunapata tena kwa bei poa ya elfu 30 kinyerezi I imeshaanza kutema umeme mbona hamkufanyahayo kabla ya muhongo? tumeona impact alivyoondolewa kwenye sakata la escrow kila kitu kikasimama, huku kwetu nguzo zilianza kuliwa na mchwa mita zikaanza kuwa za kuhongana, bora tanesco ife tena mwaka huu.

Nani asiyejuwa watumishi wa tanesco ni miunguwatu, kuanzia mameneja hadi wabeba nguzo, waziri simbachawene mwenyewe alipiga simu huduma kwa wateja akaambulia matusi ya nguoni, kwanini muhongo asisikilize kero mwenyewe? Tanesco munanunua umeme iptl 120/kwh nyie munatuuzia 340/kwh halafu munalalamikia mikataba kama sio ujuha ni nini?
 
Inawezekana wewe hunielewi
siko hapa kuitetea menejimenti
ndo maana nikasema kama ana tatizo na menejimenti basi aibadili...

hapa kuna kitu very very simple....hata ukiwa na elimu ya darasa la kwanza tu inatosha kuelewa

unamuajiri mfano mlinzi akulindie nyumba...
halafu na wewe unakesha na bunduki nje ya nyumba usikukucha...
huku ukimpa maagizo huyo mlinzi....

why usimfukuze kama unaona hafai?
Hapan! Mfano mzuri ni kumuajili mwalimu halafu huna muda wa kuangalia madaftari ya mwanao kwa sababu tu eti unaamini uwezo wa Mwalimu.

Simutetei Muhongo kwa tabia yake ya ku harass watendaji kwa kutumia neno usomi. Tunajua amesomea madini, hakusomea umeme. Tatizo langu ni watendaji walivyo. Hao unaotaka awaondowe, siyo wateule wa waziri! Yeye kama waziri kweli asubiri mpaka mkiti wa bodi aondolewe? Mkurugenzi mkuu aondolewe?

Angalia utendaji wa serikali na ujiulize kwa nini hata PM anamsimamisha daktari kwa rushwa badala ya kusubiri immediate boss wake. Tukubali nchi ina mapungufu makubwa.
 
Nimewahi kuweka thread za Waziri Muhongo kuja na sera zake binafsi za kuinyang'anya TANESCO 'uzalishaji na kubinafsisha' so far ni kama amepigwa stop ameacha kuzungumza hayo lakini sasa anachokifanya kwa TANESCO ni hatari zaidi.

Muhongo yeye ni waziri lakini ni zaidi ya CEO wa TANESCO anaingilia utendaji wa kila siku now anatoa maagizo yeye mwenyewe moja kwa moja kwa mameneja wa TANESCO wa kanda mameneja wa wilaya mameneja wa mkoa na watedaji wengi wa TANESCO.

Kilichopo now TANESCO ni kama chaos chochote menejimenti ya TANESCO ikiamua, Muhongo anaagiza wafanye kinyume chake au vile anavyoona yeye inafaaa. Yeye ni kama 'de facto CEO' wa TANESCO ieleweke kuwa yeye Muhongo hajawahi kuongoza chochote huko nyuma kabla ya kuwa Waziri na baadhi ya maamuzi yake na 'amri' zake kwa TANESCO yamepelekea deni la TANESCO liongezeke mara 5 zaidi na mtu yeyote mwenye akili anajua 'athari' za taasisi kubwa kama TANESCO kuwa wanapokea maagizo ambayo mengi siyo ya kitaalamu ni ya kisiasa kwa mtu nje ya shirika.

Ushauri wangu kwa Magufuli kama wana tatizo na menejimenti ya TANESCO ni bora kuibadili kuliko hii ya sasa ambapo menejimenti ipo lakini maamuzi yote anafanya waziri sababu mwisho mambo yakiharibika itakua uonevu mkubwa kuipa lawama menejimenti.

Vikao vya Muhongo na mameneja wa kanda na mikoa wa TANESCO vinaripotiwa hadi na media wakati mwingine vikao hivyo Waziri Muhongo anafanya bila kushirikisha menejimenti ya shirika na maamuzi ni amri tu.

Magufuli anayajua yote haya?

huu ni mfano mmoja tu wa interference ya waziri kwa menejimenti

Muhongo kutimua mameneja Tanesco

huu mchango wa member mmoja humu nauweka hapa kwa faida ya wengi

Tanesco ikifa lawama ni kwa muhongo, kwa sasa yeye ndie mkurugenzi mkuu wa tanesco,mameneja wa kanda wanaripoti kwake,anapokea malalamiko ya temporary break downs,yeye ndie meneja wa huduma kwa wateja wa tanesco,yeye anaamuru meneja huyu wa kanda simtaki huyu namtaka.

Muhongo ni mtaalam wa miamba na mawe asijifanye kuujua umeme,shurika lina hali mbaya kifedha na sasa hali itakua mbaya zaidi kwa maamuzi ya muhongo na sio menejimenti.

Muhongo anaua morali ya wafanyakazi wa tanesco,kuanzia mkurugenzi hadi mtu wa chini,yeye ni maagizo tu bila kujali muundo au mpango wa kazi wa tanesco,shirika sasa halina dira linaongozwa kwa mawazo na maagizo ya muhongo,shirika linatekeleza plans za muhongo na sio zake.

Muhongo ni tishio kwa ustawi wa shirika,muda sio mrefu hili shirika linafilisika.
Wakosaji bwana,utawatambua tu.Endelea kufurahisha jamvi ndg.Shilingi ikidondoka ktk shimo la choo huwa ni nadra sana kuipata lkn yeye aliipata.
 
Inawezekana wewe hunielewi
siko hapa kuitetea menejimenti
ndo maana nikasema kama ana tatizo na menejimenti basi aibadili...

hapa kuna kitu very very simple....hata ukiwa na elimu ya darasa la kwanza tu inatosha kuelewa

unamuajiri mfano mlinzi akulindie nyumba...
halafu na wewe unakesha na bunduki nje ya nyumba usikukucha...
huku ukimpa maagizo huyo mlinzi....

why usimfukuze kama unaona hafai?
hapa naona tatizo ni "exposure" inawezekana tangu ulivyotoka shule ukaajiriwa tanesco na hadi leo uko tanesco dunia yako ni tanesco. Wapo corporate chairman kama abromovic yeye kila siku ni kutoa maagizo nawewe ceo lazima uendane na kasi yake, anafika wakati anapanga hata wachezaji uwanjani anachotaka ni ushindi bila kujali nani kaleta ushindi mbona hajafirisika ndio kwanza utajiri unaongezeka. wakati ananunua chelsea wataalamu wa biashara walijua kapotea njia na angefirisika hata ndani ya management yake waliupinga uamuzi ule, chakushangaza baada ya mwaka mmoja chelsea ilimwingizia pesa marambili ya zile alizowekeza. nimekutolea mfano mmoja wa watu wenye haiba ya muhongo na wamefanikiwa.
 
Analeta siasa tu kwenye mambo ya kitaalam....
halafu lawama iwashukie Menejimenti

Mimi ninapata tabu sana kama mleta mada hii naye ni mtanzania? na kama ni mtumiaji wa huduma ya umeme na pengine kama amewahi kupata hata fursa ya kuangalia namna mashirika haya umeme yanavyoendeshwa na moja wapo ya nchi majirani? lakini pia kumbuka tanesco ni shirika la umma na kumbuka kama wanapata hasara tungejiuliza ni kwa namna gani wanapata hasara hiyo! wateja tunalipa kulingana na matumizi yetu.

leo hii ipo mifano dhahiri ambayo mteja anatoa taarifa tanesco juu ya ubovu wa mita yake tanesco wanakuuliza umeme unapata ukijibu ndiyo wanakuuliza shida yako nini kama mita haisomi haina shida wewe tumia tu na inakuwa hivyo hata zaidi ya miaka mitatu, gharama nyingine inatokana deigning mbove ambayo wapanga vizuri itapunguza gharama (overhead costs) mfano pasipo hitaji nguzo wewe unaweka nguzo n.k

Lipo pia tatizo la kuwa na vibarua wengi na kuwaacha idle bila kazi na mwisho shirika kuishia kulipa gharama, mfano ni shirika kuwa na utaratibu mbovu ktk kuahakikisha vifaa vinakuwepo kwa wakati.

Matatizo ya shirika letu yanachangiwa na geographia ya ukubwa wa nchi yetu na jibu la hili ni pamoja na kuligawa shirika kurahisisha usimamizi wake.
 
Pamoja na kusifiwa usomi uliotukuka lakini nina tatizo moja na huyu mtu, huyu ni wale type ya superiority complex kujiona na kujifanya anajua kila kitu na wengine ni wapuuzi tuu
Muhongo ni kiburi ana dharau majivuno na ubabe....ngoja tuone mwisho wake
Wengine tulisemahapa kuhusu kibri ya huyu jamaa lakini tukashangaa anarudi zile kauli tu za kusema wauza juisi na skendo za Escrow zilimfanya asiwe na sifa ya kuwa waziri,anyway kila shetani na mbuyu wake lakini jamaa bado hajifunzi kwani sasa anawananga wabaya wake kuwa kiko wapi ?nimerudi palepale.
 
Usiwe unatazama mambo kwa roho ya kimasikini

Wafanyakazi wa Tanesco huo umeme ni jasho lao
ukifanya kazi Daily News gazeti hununui
ukifanya kazi tigo au voda airtime hununui
iko dunia nzima

hata wapiga debe tu daladala hawalipi nauli.....

Do we noma, na walimu nao wanao wasome bure au siyo.
wàtoto wa wahadhili wasome bure, kazi kqeli kweli, kila mtu na kona yake.
 
Pamoja na thread ikiambatanishwa na link kama evidence bado Muhongo hana tatizo labda tu kama amegusa maslahi binafsi, tasisi km Tanesco zimeoza sio kufukuzwa tu hao mameneja hata CEO mwenyewe walifanya shirika kama mali yao, kubambika madeni, gharama za umeme za ajabu, nyumba vyumba 3 utafikiri mtu anayeyusha vyuma ukiuliza wanatuchanganya na teminology zao tariff 4,3 au 1 yoyote ukichagua unaliwa km mchezo wa karata 3 na kekundu, foleni ya kuwekewa ndio usiseme hao si ndio wamezalisha Vishoka? Weka hoja zenye mashiko bwana
 
Back
Top Bottom