Hebu soma link hii tu uone ni sawa kwa waziri kuongea haya?
yeye ndo ceo?
Muhongo kutimua mameneja Tanesco
Hapo nimeona uchoyo tulionao baada ya kuona The Boss akisema wafanyakazi wa Tanesco huo umeme ni jasho lao! Dah! Ubinafsi ni hatari. Yaani TRA hizo kodi ni jasho lao! Tuna matatizo ya ubora wa taaluma.Do we noma, na walimu nao wanao wasome bure au siyo.
wàtoto wa wahadhili wasome bure, kazi kqeli kweli, kila mtu na kona yake.
Mkuu fuatilia tu media
hata Tanesco kupunguza bei ya kuunga umeme lilikuwa agizo lake
kwa masharti kuwa serikali itatoa ruzuku
ni kweli inatoa ruzuku but haitoshelezi
na ina maana kuwa Tanesco isijiendeshe kwa faida na isijitegemee
isshi kwa ruzuku......na mwisho ndo hayo kwenda kukopa na deni kuongezeka....
soma hata ile hotuba ya Zitto siku ile anafunga ishu ya Escrow
aliitaja deni la Tanesco before Muhongo lilikuwa bilioni 50
now zaidi ya bilioni 300....
Now ameteuliwa tena na Magufuli anakuja na maagizo tele ya dizaini hiyo
Huyu Bwana Mm namkubali sana ni Jembe. Tanesco ilishaoza inamwitaji mtu kama Mhongo Aondoe urasimu, uliojenga mizizi ndani ya Shirika hili.Hii story ina matatizo gani,au ulisoma heading tu ukaanza kumlaumu Prof Muhongo ?
Muhongo kutimua mameneja Tanesco
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameagiza mameneja wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), watakaoshindwa kutekeleza maagizo ya wizara hiyo, waondolewe kazini ifikapo Machi mosi mwaka huu.
Alisema hayo jana wakati wa kikao chake na watendaji wa Tanesco na taasisi nyingine zilizo chini ya wizara hiyo, kilichofanyika katika kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera.
Profesa Muhongo alitaja maagizo hayo kuwa ni kuunganisha huduma kwa wateja wengi, kuwa na makusanyo makubwa ya ankara za umeme, kupunguza manung’uniko ya wananchi katika huduma za umeme na uboreshaji wa mawasiliano kati ya Shirika hilo na wananchi.
“Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, ifikapo Machi mosi mwaka huu atatuthibitishia kama mameneja hawa wataendelea na majukumu haya wanayosimamia ama la, na hii itatokana na ufanisi wa utendaji katika majukumu tuliyowapangia,” alisema Profesa Muhongo.
Mbali na mameneja hao, Profesa Muhongo ameagiza Kitengo cha Uwekezaji cha Tanesco, kama hakitakuwa na miradi mipya ya umeme ifikapo Aprili 2 mwaka huu, watendaji katika Ofisi hiyo waondolewe katika nafasi hiyo kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.
“Hapa hatuna mzaha kwani mahitaji ya umeme ni makubwa na tuna miradi mingi ya usambazaji umeme kwa wananchi ikiwemo miradi ya Rea (Wakala wa Umeme Vijijini). “Wananchi wanahitaji umeme kwa matumizi ya majumbani na kuanzisha viwanda vidogo, sasa bila miradi mipya ya umeme, tutashindwa kusambaza umeme kwa wananchi hawa kwa kuwa kiasi cha umeme tulichokuwa nacho sasa bado hakitoshi,” alisema Profesa Muhongo.
Profesa Muhongo pia aliwaasa mameneja wa Tanesco wa Kanda, kukaribisha wawekezaji mbalimbali wa umeme ikiwemo miradi midogo ya uzalishaji umeme wa maji, ili nchi iwe na umeme wa kutosha badala ya kuwakatisha tamaa wawekezaji hao.
Alionya watumishi watakaoleta urasimu katika kujadili masuala ya uwekezaji wa nishati, wataachia ngazi kwani ndio wanaokwamisha juhudi za Serikali katika kuongeza kiasi cha umeme nchini.
“Tanesco na Ewura (Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji) kwa sasa pale anapojitokeza mwekezaji wa miradi ya umeme, lazima mjadiliane naye kwa pamoja badala ya mwekezaji husika kwenda Tanesco na baadaye Ewura au TPDC (Shirika la Maendeleo ya Petroli). “Hivyo mwekezaji anapokuja, jadilini naye kwa pamoja ili msitumie muda mrefu katika utekelezaji wa suala moja na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali,” alisema Profesa Muhongo.
Pia amewaagiza watendaji wa TANESCO katika vitengo vya ukaguzi, kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa ikiwemo usimamizi madhubuti wa nguzo za umeme, ambazo baadhi huanguka kila inapofika msimu wa mvua na kusema kuwa suala hilo halikubaliki.
Hatua hiyo ya Profesa Muhongo, imelenga kutekeleza malengo ya Wizara hiyo kuhakikisha asilimia 67 ya vijiji vyote nchini, vitapata umeme katika miaka miwili na nusu ijayo. Mbali na kuunganisha watu wengi na huduma hiyo, juhudi kuongeza uzalishaji wa umeme, Profesa Muhongo alizieleza mara tu alipoapishwa kushika wadhifa huo Desemba mwaka jana.
Katika hafla hiyo, Profesa Muhongo alisema Tanzania ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme, lakini bado umeme unaozalishwa hautoshi na kuwataka wawekezaji wenye uwezo watumie fursa hiyo kuwekeza katika sekta hiyo.
Aidha alisisitiza kuwa ili Taifa lifanikiwe kuwa nchi yenye kipato cha kati kufikia mwaka 2025, ni lazima nchi iwe na umeme wa kutosha, hivyo hadi kufikia mwaka huo, uzalishaji wa umeme unapaswa kufikia megawati 10,000.
kaka wasomi wazamani wa tz bado wanajiona wao ndio wao na hakuna wataalamu zaidi yao kumbe tz ya leo kila mtaa una msomi na mtaalamu ngazi ya chuo kikuuPamoja na kusifiwa usomi uliotukuka lakini nina tatizo moja na huyu mtu, huyu ni wale type ya superiority complex kujiona na kujifanya anajua kila kitu na wengine ni wapuuzi tuu
Muhongo ni kiburi ana dharau majivuno na ubabe....ngoja tuone mwisho wake
Unaposema Management inafurahia au haifurahii unakuwa unatumia kigezo gani kwa sababu inawezekani unatumia kigezo cha hisia zako katika kujenga hoja.soma hii link tu moja halafu useme Menejimenti inafurahia
huku waziri anawaendesha kwa vitisho
Muhongo kutimua mameneja Tanesco
Mimi ninapata tabu sana kama mleta mada hii naye ni mtanzania? na kama ni mtumiaji wa huduma ya umeme na pengine kama amewahi kupata hata fursa ya kuangalia namna mashirika haya umeme yanavyoendeshwa na moja wapo ya nchi majirani? lakini pia kumbuka tanesco ni shirika la umma na kumbuka kama wanapata hasara tungejiuliza ni kwa namna gani wanapata hasara hiyo! wateja tunalipa kulingana na matumizi yetu.
leo hii ipo mifano dhahiri ambayo mteja anatoa taarifa tanesco juu ya ubovu wa mita yake tanesco wanakuuliza umeme unapata ukijibu ndiyo wanakuuliza shida yako nini kama mita haisomi haina shida wewe tumia tu na inakuwa hivyo hata zaidi ya miaka mitatu, gharama nyingine inatokana deigning mbove ambayo wapanga vizuri itapunguza gharama (overhead costs) mfano pasipo hitaji nguzo wewe unaweka nguzo n.k
Lipo pia tatizo la kuwa na vibarua wengi na kuwaacha idle bila kazi na mwisho shirika kuishia kulipa gharama, mfano ni shirika kuwa na utaratibu mbovu ktk kuahakikisha vifaa vinakuwepo kwa wakati.
Matatizo ya shirika letu yanachangiwa na geographia ya ukubwa wa nchi yetu na jibu la hili ni pamoja na kuligawa shirika kurahisisha usimamizi wake.
Wasomi wengi wako narrowPamoja na kusifiwa usomi uliotukuka lakini nina tatizo moja na huyu mtu, huyu ni wale type ya superiority complex kujiona na kujifanya anajua kila kitu na wengine ni wapuuzi tuu
Muhongo ni kiburi ana dharau majivuno na ubabe....ngoja tuone mwisho wake
Acha ujanja ujanja wewe kwa hiyo ulitaka tuendelee kumia ???Mkuu fuatilia tu media
hata Tanesco kupunguza bei ya kuunga umeme lilikuwa agizo lake
kwa masharti kuwa serikali itatoa ruzuku
ni kweli inatoa ruzuku but haitoshelezi
na ina maana kuwa Tanesco isijiendeshe kwa faida na isijitegemee
isshi kwa ruzuku......na mwisho ndo hayo kwenda kukopa na deni kuongezeka....
soma hata ile hotuba ya Zitto siku ile anafunga ishu ya Escrow
aliitaja deni la Tanesco before Muhongo lilikuwa bilioni 50
now zaidi ya bilioni 300....
Now ameteuliwa tena na Magufuli anakuja na maagizo tele ya dizaini hiyo
Mbona poa tu kwani tatizo nini hapo nchi hii bila amri haindi safi sana mhongo