Muhongo anaivuruga TANESCO, Magufuli yuko wapi?

Muhongo anaivuruga TANESCO, Magufuli yuko wapi?

Do we noma, na walimu nao wanao wasome bure au siyo.
wàtoto wa wahadhili wasome bure, kazi kqeli kweli, kila mtu na kona yake.
Hapo nimeona uchoyo tulionao baada ya kuona The Boss akisema wafanyakazi wa Tanesco huo umeme ni jasho lao! Dah! Ubinafsi ni hatari. Yaani TRA hizo kodi ni jasho lao! Tuna matatizo ya ubora wa taaluma.
 
Kama maagizo anayotoa yana faida na unafuu kwa mwananchi wa chini hakuna shaka..!! Maamuzi yake yangekuwa yanatugusa sisi wananchi wa chini kama kutoa service chaji, mengine watajuana wenyewe humo ndani. Ilimradi impact isitufikie sisi wananchi.
 
Prof komaa nao hivyo hivyo,maana humo tanesco pia tumeliwa siku nyingi. Aluta continue prof.
 
Tazama hii kutoka gazeti la serikali

Muhongo kutimua mameneja Tanesco

Hii story ina matatizo gani,au ulisoma heading tu ukaanza kumlaumu Prof Muhongo ?

Muhongo kutimua mameneja Tanesco

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameagiza mameneja wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), watakaoshindwa kutekeleza maagizo ya wizara hiyo, waondolewe kazini ifikapo Machi mosi mwaka huu.

Alisema hayo jana wakati wa kikao chake na watendaji wa Tanesco na taasisi nyingine zilizo chini ya wizara hiyo, kilichofanyika katika kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera.

Profesa Muhongo alitaja maagizo hayo kuwa ni kuunganisha huduma kwa wateja wengi, kuwa na makusanyo makubwa ya ankara za umeme, kupunguza manung’uniko ya wananchi katika huduma za umeme na uboreshaji wa mawasiliano kati ya Shirika hilo na wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, ifikapo Machi mosi mwaka huu atatuthibitishia kama mameneja hawa wataendelea na majukumu haya wanayosimamia ama la, na hii itatokana na ufanisi wa utendaji katika majukumu tuliyowapangia,” alisema Profesa Muhongo.

Mbali na mameneja hao, Profesa Muhongo ameagiza Kitengo cha Uwekezaji cha Tanesco, kama hakitakuwa na miradi mipya ya umeme ifikapo Aprili 2 mwaka huu, watendaji katika Ofisi hiyo waondolewe katika nafasi hiyo kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

“Hapa hatuna mzaha kwani mahitaji ya umeme ni makubwa na tuna miradi mingi ya usambazaji umeme kwa wananchi ikiwemo miradi ya Rea (Wakala wa Umeme Vijijini). “Wananchi wanahitaji umeme kwa matumizi ya majumbani na kuanzisha viwanda vidogo, sasa bila miradi mipya ya umeme, tutashindwa kusambaza umeme kwa wananchi hawa kwa kuwa kiasi cha umeme tulichokuwa nacho sasa bado hakitoshi,” alisema Profesa Muhongo.

Profesa Muhongo pia aliwaasa mameneja wa Tanesco wa Kanda, kukaribisha wawekezaji mbalimbali wa umeme ikiwemo miradi midogo ya uzalishaji umeme wa maji, ili nchi iwe na umeme wa kutosha badala ya kuwakatisha tamaa wawekezaji hao.

Alionya watumishi watakaoleta urasimu katika kujadili masuala ya uwekezaji wa nishati, wataachia ngazi kwani ndio wanaokwamisha juhudi za Serikali katika kuongeza kiasi cha umeme nchini.

“Tanesco na Ewura (Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji) kwa sasa pale anapojitokeza mwekezaji wa miradi ya umeme, lazima mjadiliane naye kwa pamoja badala ya mwekezaji husika kwenda Tanesco na baadaye Ewura au TPDC (Shirika la Maendeleo ya Petroli). “Hivyo mwekezaji anapokuja, jadilini naye kwa pamoja ili msitumie muda mrefu katika utekelezaji wa suala moja na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali,” alisema Profesa Muhongo.

Pia amewaagiza watendaji wa TANESCO katika vitengo vya ukaguzi, kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa ikiwemo usimamizi madhubuti wa nguzo za umeme, ambazo baadhi huanguka kila inapofika msimu wa mvua na kusema kuwa suala hilo halikubaliki.

Hatua hiyo ya Profesa Muhongo, imelenga kutekeleza malengo ya Wizara hiyo kuhakikisha asilimia 67 ya vijiji vyote nchini, vitapata umeme katika miaka miwili na nusu ijayo. Mbali na kuunganisha watu wengi na huduma hiyo, juhudi kuongeza uzalishaji wa umeme, Profesa Muhongo alizieleza mara tu alipoapishwa kushika wadhifa huo Desemba mwaka jana.

Katika hafla hiyo, Profesa Muhongo alisema Tanzania ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme, lakini bado umeme unaozalishwa hautoshi na kuwataka wawekezaji wenye uwezo watumie fursa hiyo kuwekeza katika sekta hiyo.

Aidha alisisitiza kuwa ili Taifa lifanikiwe kuwa nchi yenye kipato cha kati kufikia mwaka 2025, ni lazima nchi iwe na umeme wa kutosha, hivyo hadi kufikia mwaka huo, uzalishaji wa umeme unapaswa kufikia megawati 10,000.
 
Mkuu ulichosema ni sahihi kabisa. Hata baathinta maofisa katika wizara yake amewaletea zengwe,akilazimisha wanasheria wa wizara kuwatungia kesi za ubathirifu yote sababu ya chuki ya huyu mjinga anayejihita msomi.

Mengi yatakuja baadaye...
 
Mkuu fuatilia tu media
hata Tanesco kupunguza bei ya kuunga umeme lilikuwa agizo lake
kwa masharti kuwa serikali itatoa ruzuku
ni kweli inatoa ruzuku but haitoshelezi
na ina maana kuwa Tanesco isijiendeshe kwa faida na isijitegemee
isshi kwa ruzuku......na mwisho ndo hayo kwenda kukopa na deni kuongezeka....

soma hata ile hotuba ya Zitto siku ile anafunga ishu ya Escrow
aliitaja deni la Tanesco before Muhongo lilikuwa bilioni 50
now zaidi ya bilioni 300....

Now ameteuliwa tena na Magufuli anakuja na maagizo tele ya dizaini hiyo

Wewe sema tu kwamba kilichokuuma ni bei umeme kupunguzwa sasa ukiwa kama anti Magufuli hilo linakuuma, Pole sana Waziri Muhongo yupo na haendi popote kwa maana tunamuhitaji!
 
Hii story ina matatizo gani,au ulisoma heading tu ukaanza kumlaumu Prof Muhongo ?

Muhongo kutimua mameneja Tanesco

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameagiza mameneja wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), watakaoshindwa kutekeleza maagizo ya wizara hiyo, waondolewe kazini ifikapo Machi mosi mwaka huu.

Alisema hayo jana wakati wa kikao chake na watendaji wa Tanesco na taasisi nyingine zilizo chini ya wizara hiyo, kilichofanyika katika kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera.

Profesa Muhongo alitaja maagizo hayo kuwa ni kuunganisha huduma kwa wateja wengi, kuwa na makusanyo makubwa ya ankara za umeme, kupunguza manung’uniko ya wananchi katika huduma za umeme na uboreshaji wa mawasiliano kati ya Shirika hilo na wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, ifikapo Machi mosi mwaka huu atatuthibitishia kama mameneja hawa wataendelea na majukumu haya wanayosimamia ama la, na hii itatokana na ufanisi wa utendaji katika majukumu tuliyowapangia,” alisema Profesa Muhongo.

Mbali na mameneja hao, Profesa Muhongo ameagiza Kitengo cha Uwekezaji cha Tanesco, kama hakitakuwa na miradi mipya ya umeme ifikapo Aprili 2 mwaka huu, watendaji katika Ofisi hiyo waondolewe katika nafasi hiyo kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

“Hapa hatuna mzaha kwani mahitaji ya umeme ni makubwa na tuna miradi mingi ya usambazaji umeme kwa wananchi ikiwemo miradi ya Rea (Wakala wa Umeme Vijijini). “Wananchi wanahitaji umeme kwa matumizi ya majumbani na kuanzisha viwanda vidogo, sasa bila miradi mipya ya umeme, tutashindwa kusambaza umeme kwa wananchi hawa kwa kuwa kiasi cha umeme tulichokuwa nacho sasa bado hakitoshi,” alisema Profesa Muhongo.

Profesa Muhongo pia aliwaasa mameneja wa Tanesco wa Kanda, kukaribisha wawekezaji mbalimbali wa umeme ikiwemo miradi midogo ya uzalishaji umeme wa maji, ili nchi iwe na umeme wa kutosha badala ya kuwakatisha tamaa wawekezaji hao.

Alionya watumishi watakaoleta urasimu katika kujadili masuala ya uwekezaji wa nishati, wataachia ngazi kwani ndio wanaokwamisha juhudi za Serikali katika kuongeza kiasi cha umeme nchini.

“Tanesco na Ewura (Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji) kwa sasa pale anapojitokeza mwekezaji wa miradi ya umeme, lazima mjadiliane naye kwa pamoja badala ya mwekezaji husika kwenda Tanesco na baadaye Ewura au TPDC (Shirika la Maendeleo ya Petroli). “Hivyo mwekezaji anapokuja, jadilini naye kwa pamoja ili msitumie muda mrefu katika utekelezaji wa suala moja na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali,” alisema Profesa Muhongo.

Pia amewaagiza watendaji wa TANESCO katika vitengo vya ukaguzi, kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa ikiwemo usimamizi madhubuti wa nguzo za umeme, ambazo baadhi huanguka kila inapofika msimu wa mvua na kusema kuwa suala hilo halikubaliki.

Hatua hiyo ya Profesa Muhongo, imelenga kutekeleza malengo ya Wizara hiyo kuhakikisha asilimia 67 ya vijiji vyote nchini, vitapata umeme katika miaka miwili na nusu ijayo. Mbali na kuunganisha watu wengi na huduma hiyo, juhudi kuongeza uzalishaji wa umeme, Profesa Muhongo alizieleza mara tu alipoapishwa kushika wadhifa huo Desemba mwaka jana.

Katika hafla hiyo, Profesa Muhongo alisema Tanzania ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme, lakini bado umeme unaozalishwa hautoshi na kuwataka wawekezaji wenye uwezo watumie fursa hiyo kuwekeza katika sekta hiyo.

Aidha alisisitiza kuwa ili Taifa lifanikiwe kuwa nchi yenye kipato cha kati kufikia mwaka 2025, ni lazima nchi iwe na umeme wa kutosha, hivyo hadi kufikia mwaka huo, uzalishaji wa umeme unapaswa kufikia megawati 10,000.
Huyu Bwana Mm namkubali sana ni Jembe. Tanesco ilishaoza inamwitaji mtu kama Mhongo Aondoe urasimu, uliojenga mizizi ndani ya Shirika hili.
 
Pamoja na kusifiwa usomi uliotukuka lakini nina tatizo moja na huyu mtu, huyu ni wale type ya superiority complex kujiona na kujifanya anajua kila kitu na wengine ni wapuuzi tuu
Muhongo ni kiburi ana dharau majivuno na ubabe....ngoja tuone mwisho wake
kaka wasomi wazamani wa tz bado wanajiona wao ndio wao na hakuna wataalamu zaidi yao kumbe tz ya leo kila mtaa una msomi na mtaalamu ngazi ya chuo kikuu
 
Mtoa hoja ni jipu, na upo tanesco. Ngoja le profeseri akufurahishe....mlizoea vibaya..
 
Kwenye clip Muhongo anawashauri Tanesco (Kanda ya Kusini) kutengeneza umeme wa maji nawaache kutumia umeme wa mafuta ambao ni wa gharama kubwa
Kosa la Muhongo ni lipi hapo ? Inaonekana una personal issue na Pof Muhongo ,links zote ulizoweka hakuna hata kosa alilofanya kama ulivyomtuhumu
 
Kwani ni lini tanesco wamekua na dira au muongozo...!?

kila siku tulikua tunalalamikia utendaji wa tanesco kuanzia bodi mpaka wafanyakazi wake...!?

je ni nani amesababisha umemekufutwa ile charges fee..!?

Hii miradi inayofanywa chini ya tanesco ni nani anasimamia..!?

mkopo wa tanesco kabla ya uongozi wa muhongo ni ulikua ni kiasi gani na sasa hivi ni kiasi gani...!?

matatizo ya tanesco yalikua yapi kabla ya utawala huu na ya sasa hivi niyapi baada ya kuingia utawala mpya...!?

malalamiko ya raia ni yapi kabla ya utawala huu na ni yapi baada ya kuingia utawala huu...!?

em twendeni kitakwimu alafu tuendelee na mengine.
 
soma hii link tu moja halafu useme Menejimenti inafurahia
huku waziri anawaendesha kwa vitisho

Muhongo kutimua mameneja Tanesco
Unaposema Management inafurahia au haifurahii unakuwa unatumia kigezo gani kwa sababu inawezekani unatumia kigezo cha hisia zako katika kujenga hoja.

Hiyo article nimeisoma. Muhongo kama Waziri mwenye dhamana kwenye Wizara ya Nishati na Madini anachofanya ni kutoa maelekezo kwa Management ya TANESCO ambayo ni sehemu ya Wizara yake.
 
Mimi ninapata tabu sana kama mleta mada hii naye ni mtanzania? na kama ni mtumiaji wa huduma ya umeme na pengine kama amewahi kupata hata fursa ya kuangalia namna mashirika haya umeme yanavyoendeshwa na moja wapo ya nchi majirani? lakini pia kumbuka tanesco ni shirika la umma na kumbuka kama wanapata hasara tungejiuliza ni kwa namna gani wanapata hasara hiyo! wateja tunalipa kulingana na matumizi yetu.

leo hii ipo mifano dhahiri ambayo mteja anatoa taarifa tanesco juu ya ubovu wa mita yake tanesco wanakuuliza umeme unapata ukijibu ndiyo wanakuuliza shida yako nini kama mita haisomi haina shida wewe tumia tu na inakuwa hivyo hata zaidi ya miaka mitatu, gharama nyingine inatokana deigning mbove ambayo wapanga vizuri itapunguza gharama (overhead costs) mfano pasipo hitaji nguzo wewe unaweka nguzo n.k

Lipo pia tatizo la kuwa na vibarua wengi na kuwaacha idle bila kazi na mwisho shirika kuishia kulipa gharama, mfano ni shirika kuwa na utaratibu mbovu ktk kuahakikisha vifaa vinakuwepo kwa wakati.

Matatizo ya shirika letu yanachangiwa na geographia ya ukubwa wa nchi yetu na jibu la hili ni pamoja na kuligawa shirika kurahisisha usimamizi wake.

Sijawahi kufikiria Kama kuna mtu atakuwa na nguvu ya kuleta uzi wa kuitetea TaNesco jamani hawa kweli walikuwa na CEO au Ni mausanii ya karne na karne Leo mtu anatumia kivuli cha Waziri sijui nini kuitetea TaNesco na uongozi mzima sijui tunataka marekebisho wapi sisi watanzania inawezekana kweli huyo mnaemsema msomi ana mapungufu yake lakini bora ungemtafutia kisa Hata Kwenye madini huko migodini na kwingineko Sio Tanesco please wote tunajua tumeteseka na bado tunateseka na urasimu plus huduma mbovu na mlolongo wa kishenzi kabisa unaofanywa na watumishi wa tanesco hadi Leo bado Tanesco haijakaa vizuri. Waziri awe na maringo kiburi sijui dharau hivyo umeviona wewe personally ila Tanesco watanzania wote tunajua madharau Yao viburi vyao matusi Yao majibu Yao mabaya na mauchafu Yao yote tuache kutafuta vitu vidogo vidogoo Kwenye hatua zinazochukuliwa kuondoa kero za wateja wa Tanesco ambao Ni Mimi na wewe Kama wewe mleta uzi Ni mtumishi wa Tanesco basi ujue hamkuwa wazuri Hata chembe hadi sasa mnabadilishwa tabia zenu kinguvu na mnaumia kuziacha tabia zenu mbaya zimewaganda Kama ngozi vile
 
mkuu nahisi una shida na muhongo ni yeye tu unayemkomalia kila wakati.
 
Pamoja na kusifiwa usomi uliotukuka lakini nina tatizo moja na huyu mtu, huyu ni wale type ya superiority complex kujiona na kujifanya anajua kila kitu na wengine ni wapuuzi tuu
Muhongo ni kiburi ana dharau majivuno na ubabe....ngoja tuone mwisho wake
Wasomi wengi wako narrow

A PhD holder huwa anafocus kwenye a very narrow and highly specialized study area... watu jamii ya Muhongo huongozwa na maksi alizopata kwenye kujibu swali ambalo si ajabu lilikua hypothetical

it is a fact kwamba Muhongo ni loose fuse na damage yake kwenye system itakuja kugundulika when its too late

Kwa bahati mbaya sana, mfumo mzima wa Tanesco nao ni kama hauna qualities, pamoja na wengi kusomeshwa na kuwa na uwezo, the organizational culture ya tanesco inawanyima uwezo wa kuwa na maamuzi ya kujenga... wamekua more of watu wa kuangalia ya leo

Ushauri... Muhongo agundue kwamba wizara yake ni kubwa sana kuliko tanesco...
 
Mkuu fuatilia tu media
hata Tanesco kupunguza bei ya kuunga umeme lilikuwa agizo lake
kwa masharti kuwa serikali itatoa ruzuku
ni kweli inatoa ruzuku but haitoshelezi
na ina maana kuwa Tanesco isijiendeshe kwa faida na isijitegemee
isshi kwa ruzuku......na mwisho ndo hayo kwenda kukopa na deni kuongezeka....

soma hata ile hotuba ya Zitto siku ile anafunga ishu ya Escrow
aliitaja deni la Tanesco before Muhongo lilikuwa bilioni 50
now zaidi ya bilioni 300....

Now ameteuliwa tena na Magufuli anakuja na maagizo tele ya dizaini hiyo
Acha ujanja ujanja wewe kwa hiyo ulitaka tuendelee kumia ???
 
Hilo tanesco ni shirika la kanisa tuh...management yoote hapo ni waimba kwaya kuanzia juu mpaka chini na hakuna wanachofanya zaid zaid ya wizi na kulitia taifa hasara...ni jipu kubwa kweli kweli...na wasomi wenyewe kama hao kina muhongo basi ni hasara tupu
 
Back
Top Bottom