multmandalin
JF-Expert Member
- Sep 8, 2012
- 2,030
- 576
Ukiongea na vijana wengi sana kwenye ajira hasa za makampuni ya simu, mabenki mashirika mbalimbali nchini ni jambo la kawaida kusikia vijana wazawa wakilalamikia sana wageni na jinsi wanavyowanyanyasa wazawa hata kama elimu yao ni kubwa kuliko hao wageni kipato ni mbingu na dunia!
Ukisikiliza kwa makini utagundua kuna kazi ambazo zingeweza kufanywa na wazawa zinafanywa na wageni. Tuangalie na kushauriana sheria za kulinda ajira zinazoweza kuchukuliwa na wazawa kama njia ya kutatua kama sio kupunguza tatizo la ajira nchini!
Nini kifanyike kukomesha manyanyaso haya ya wageni dhidi ya wazawa? Ukizingatia kwakweli wanaochapa kazi mpaka makampuni haya yakaonekana yanafanya kazi ni wazawa but kipato na manyanyaso kilio ni kikubwa sana!
Kadhambi ka ubaguzi kanakutafuna neno wazawa Mwalimu alilikataa na kuwaita wazawa ni makaburu tu, na aliapa hawezi kuwachekea makaburu hapa Tanzania eti kisa ni weusi kaburu ni kaburu tu!