Muhimu: Kulinda ajira za wazawa Tanzania...

Nape Nnauye

MP Mtama
Dec 26, 2012
99
408
Ukiongea na vijana wengi sana kwenye ajira hasa za makampuni ya simu, mabenki mashirika mbalimbali nchini ni jambo la kawaida kusikia vijana wazawa wakilalamikia sana wageni na jinsi wanavyowanyanyasa wazawa hata kama elimu yao ni kubwa kuliko hao wageni kipato ni mbingu na dunia!

Ukisikiliza kwa makini utagundua kuna kazi ambazo zingeweza kufanywa na wazawa zinafanywa na wageni. Tuangalie na kushauriana sheria za kulinda ajira zinazoweza kuchukuliwa na wazawa kama njia ya kutatua kama sio kupunguza tatizo la ajira nchini!

Nini kifanyike kukomesha manyanyaso haya ya wageni dhidi ya wazawa? Ukizingatia kwakweli wanaochapa kazi mpaka makampuni haya yakaonekana yanafanya kazi ni wazawa but kipato na manyanyaso kilio ni kikubwa sana!
 
Mbona unaleta maneno meengi?
mbona sheria nzuri zipo?
hujui kuwa usimamizi mbovu na rushwa ndo chanzo?

tushauriane nii sasa?

hata madawa ya kulevya utaleta thread mshauriwe nini cha kufanya?

hivi ilikuwaje mkatamani kuongoza wakati hata A ,B , C ZA kuongoza hamzijui?
 
Ukiongea na vijana wengi sana kwenye ajira hasa za makampuni ya simu, mabenki mashirika mbalimbali nchini ni jambo la kawaida kusikia vijana wazawa wakilalamikia sana wageni na jinsi wanavyowanyanyasa wazawa hata kama elimu yao ni kubwa kuliko hao wageni kipato ni mbingu na dunia!

Ukisikiliza kwa makini utagundua kuna kazi ambazo zingeweza kufanywa na wazawa zinafanywa na wageni. Tuangalie na kushauriana sheria za kulinda ajira zinazoweza kuchukuliwa na wazawa kama njia ya kutatua kama sio kupunguza tatizo la ajira nchini!

Nini kifanyike kukomesha manyanyaso haya ya wageni dhidi ya wazawa? Ukizingatia kwakweli wanaochapa kazi mpaka makampuni haya yakaonekana yanafanya kazi ni wazawa but kipato na manyanyaso kilio ni kikubwa sana!
Sera kama hizi Mchungaji Mtikila alikuja nazo "Magabachili" Serikali ya CCM na viongozi wa CCM walimfungulia makesi mengi, kumkamata na kumdhalilisha. Mh Idd Simba alipokuwa waziri wa Biashara, nae alikuja na sera za WAZAWA, serikali ya CCM chini ya mwenyekiti wake wa CCM taifa (Mkapa) walimzima na kuuza rasilimali zetu kwa makaburu. CCM wameuza kali kitu kwa mikataba ya miaka 99, nchi imebaki kavu na wageni wanamiliki mikataba, wewe unakuja na siasa za uhadaa. Tueleze CCM itasaidia vipi kusaidia vijana wasinyanyaswe chini ya hii mikataba ya siri? Tueleze wewe ukiwa kama mmoja wa viongozi wakubwa CCM, Je CCM mlikosa mzawa kushika nafasi ya katibu mkuu wa CCM?
 
kiongozi , unayafahamu makampuni yote na wamiliki ( wengine wamekula kollabo na mafisadi wa ndani ) kwanini usiwa face tu uwape ushauri wako badala ya kutuletea sisi ?
 
Ukisikiliza kwa makini utagundua kuna kazi ambazo zingeweza kufanywa na wazawa zinafanywa na wageni. Tuangalie na kushauriana sheria za kulinda ajira zinazoweza kuchukuliwa na wazawa kama njia ya kutatua kama sio kupunguza tatizo la ajira nchini!
Mkuu,

Soma hapa kwanza, kisha tuendelee na kama unataka zaidi nikushirikishe maana tushaongea sana humu - https://www.jamiiforums.com/habari-...-anawaleta-wahindi-na-kuwaajiri-tanzania.html

Mzalendo mwingine John Mashaka akaandika haya - http://www.thecitizen.co.tz/oped/Ec...tion/-/1840568/1936638/-/10f3ayv/-/index.html
 
Ulikuwa wapi miaka yote kuliona hili la ajira za wazawa? Ni jambo ambalo limepigiwa kelele miaka chungu nzima sasa lakini mlikuwa mmetia pamba masikioni sasa mnaona 2015 inasogea kwa kasi ndio mnaanza kujibaraguza!!! Acha unafiki!!! nchi imewashinda mmevurunda kwa kiwango cha juu kabisa hamstahili kuwepo madarakani hata kwa siku moja achilia mbali miaka mingine mitano.
 
Nakushanga sanaaa, sheria inasema wageni wasizidi 5 katika kampun husika na HR/ CA Wawe wazawa kamasijakose lakini nenda kwenye mashirik/kampun ukajione na unajua sanaaa....
~ Utakuta HRO/CA ni wageni na wanaitwa majina mengine kabisa lakin kazi zao ni hiZo
~ Wakubwa wanakuja kila ijumaa kuchukua 10% zao za kufunika kombe wana haramu apite
~ Kuna sehemu mtu ana Bs. Engr na ni seniour kazini analipwa laki 450,000/ wakati mhindi wenye certificate fulani yakijinga sanaaaaaaaaaa analipwa 3,850,000/ bado unapiga kelele hapa ( na kila ijumaa katibu mkuu wa wizara ya viwanda anakuja kuchukua cheque sijui ya nini)

Mwisho jiungeni na DPP Mwinguru mjifungie msalani mjiulize kwani kuna tatizo ili then mje na majibu sio kuja hapa kutusumbua tu,

MAJIBU YA HAYA NI KUWAWEKA KANDO 2015 MUMECHOKA SANA KIFIKIRA NA KIMAWAZO.
 
Majibu yenu yote mazuri sana tuendelee tutapata jibu tu! Ahsante sana The Boss, Gagnija, Fitinamwiko, Frema, Bak, Erythrocyte na Invisible! kwa mawazo yenu nitayafanyia kazi!
 
Watu wa uhamiaji na Ajira wanawapa wageni working permit hata vigezo na shule hawajaenda kuna. Mfano kuna kampuni moja ya wahindi inaitwa........ energy and infrastructure ni aibu Side manager ni frm 4 ya India mining manager hakuwahi hata kusomea coarse ya mining. Wanabyochimba mgodi ni kichekesho. Na wataalam wa wizara ya Muhongo kila siku wanakuja kukagua na kuondoka kisa kuna nguvu ya mkubwa hvyo hata wataalam wetu washauri vp hawa jama hawawasikilizi
 
Leo hii ndio “mmeona” kuna tatizo la ajira kwa vijana? Mlikuwa wapi siku zote hizo? Au “two timing thinking” inawasumbua?
 
Majibu yenu yote mazuri sana tuendelee tutapata jibu tu! Ahsante sana The Boss, Gagnija, Fitinamwiko, Frema, Bak, Erythrocyte na Invisible! kwa mawazo yenu nitayafanyia kazi!
Mkuu,

Nashauri jaribu kuwa unakuja na issues zisizo za vyama zaidi, sina tatizo na siasa mzifanyazo lakini nadhani taifa letu lina matatizo makubwa yanayohitaji mjadala na kutafutiwa upembuzi makini. Ninyi mkiwa mifano kwa wafuasi wenu kwa kujikita kwenye mijadala ya kufikirisha na kutafuta suluhu ya matatizo yetu basi namna mijadala inavyoendelea humu na kwenye social networks nyingine itabadilika.

Aidha, ni vema mkubali constructive criticism ili kutafuta suluhu ya matatizo ya watanzania. Suala la wazalendo kusahaulika limekuwa gumzo mara nyingi lakini hakujawa na mwitikio wa kueleweka toka kwenu wanasiasa na serikali kwa ujumla.

Hatuna tatizo na wageni kuja hapa, lakini wanapofikia kufanya kazi zinazoweza kufanywa na wazalendo au hata kufanya kazi zilezile lakini wakilipwa mara 10 ya mzalendo anayefanya kazi ileile, ni dalili ya serikali kushindwa vibaya na ni ishara kuwa watawala wanawapuuza waliowaweka madarakani (sahau kuhusu uhisani wao).

Again, mkibadilika na wananchi watabadilika!

BTW, una kauli gani juu ya suala la MADAWA YA KULEVYA? Una kauli gani juu ya Makamba kudai Lowassa ni mtu wa watu na anastahili kuongoza Taifa hili? (Haya unaweza kuja na thread tofauti nasi tutafurahi kuipata kauli yako au ya chama chenu)
 
Sometimes we dogo hua nadhani unatumia ID tofauti, na ninahisi umejikuta unatumia authorize user name kwa bahati mbaya, hasa huu uzi! Hivi nyie si ndio chama tawala? Nani anayewapa vibari vya kufanyia kazi nchini? Nenda migodini huko, yaani utafikiri nchi haina uongozi, wengine serikali ya mkoa au wilaya inawafukuza, wanakuja Dar and then wanarudi na kuendelea na kazi kama kawaida, hili naomba ukawaulize watu wenu humo ccm, ccm ndio isiyopenda wananchi wake.
 
Ukiongea na vijana wengi sana kwenye ajira hasa za makampuni ya simu, mabenki mashirika mbalimbali nchini ni jambo la kawaida kusikia vijana wazawa wakilalamikia sana wageni na jinsi wanavyowanyanyasa wazawa hata kama elimu yao ni kubwa kuliko hao wageni kipato ni mbingu na dunia!

Ukisikiliza kwa makini utagundua kuna kazi ambazo zingeweza kufanywa na wazawa zinafanywa na wageni. Tuangalie na kushauriana sheria za kulinda ajira zinazoweza kuchukuliwa na wazawa kama njia ya kutatua kama sio kupunguza tatizo la ajira nchini!

Nini kifanyike kukomesha manyanyaso haya ya wageni dhidi ya wazawa? Ukizingatia kwakweli wanaochapa kazi mpaka makampuni haya yakaonekana yanafanya kazi ni wazawa but kipato na manyanyaso kilio ni kikubwa sana!

Mr. Nape,
I would like to discuss this issue with you further. However, the main problem is with our immigration system. How do these people obtain work authorization? You don't need to lament on this. The problem can easily be solved if you have the will to

Being in the ruling party. You should advocate on behalf of these Tanzanians. It should be a law, policy and requirement that 90% of the jobs go to the natives. These corporations must prove that such skilled workers cannot be found within our borders. Bottom line, this will work better if you propose sweeping changes in our immigration system.

I met a Chinese national in Zanzibar in 2009 who could barely speak English or Swahili with a Tanzanian passport. I also met another Nigerian national in one of the major global hubs with a Tanzanian passport. The Nigerian was simply a crook, bragging to be an international businessman, and could not tell me the name of Tanzanian registered company
 
[h=1]mkuu nape,kabla ya ajira,je maisha ya watanzania je,watanzanie wanne walifariki kule arusha,kwenye mkutano wa chadema.kikwete hakutoa hata pole

Tanzanian president visits two British women hurt in Zanzibar acid attack[/h] [h=2]The president of Tanzania has visited two British 18-year-old women who were the targets of an acid attack on the Indian Ocean island of Zanzibar late on Wednesday night.[/h]
zanzibar_2638680b.jpg
Kirstie Trup (left) and Katie Gee were the targets of an acid attack by men riding a motorcycle on the Indian Ocean island of Zanzibar Photo: Barcroft

By Mike Pflanz, Nairobi

11:20AM BST 08 Aug 2013

Kirstie Trup, from Hampstead, north London, and Katie Gee both suffered injuries to their faces, chests and hands, and were transferred to a hospital on the Tanzanian mainland where their injuries were described as "mild".

Jakaya Kikwete, Tanzania's president, promised that their attackers would be found.

[SUB]
ZANZIBARPRES_2639042c.jpg
[/SUB]

[SUB]Tanzanian President Jakaya Kikwete, left, at the hospital. (AP)[/SUB]

"It's a shameful attack that tarnishes the image of our country, I order security agents to speed up the investigations and arrest the suspects," he said after visiting the pair in hospital.

[h=2]Related Articles[/h]
 
Ukiongea na vijana wengi sana kwenye ajira hasa za makampuni ya simu, mabenki mashirika mbalimbali nchini ni jambo la kawaida kusikia vijana wazawa wakilalamikia sana wageni na jinsi wanavyowanyanyasa wazawa hata kama elimu yao ni kubwa kuliko hao wageni kipato ni mbingu na dunia!

Ukisikiliza kwa makini utagundua kuna kazi ambazo zingeweza kufanywa na wazawa zinafanywa na wageni. Tuangalie na kushauriana sheria za kulinda ajira zinazoweza kuchukuliwa na wazawa kama njia ya kutatua kama sio kupunguza tatizo la ajira nchini!

Nini kifanyike kukomesha manyanyaso haya ya wageni dhidi ya wazawa? Ukizingatia kwakweli wanaochapa kazi mpaka makampuni haya yakaonekana yanafanya kazi ni wazawa but kipato na manyanyaso kilio ni kikubwa sana!

Kinachotakiwa ni kukiondoa chama dhalimu na kilichoshindwa kuongoza madarakani
 
Mkuu,

Soma hapa kwanza, kisha tuendelee na kama unataka zaidi nikushirikishe maana tushaongea sana humu - https://www.jamiiforums.com/habari-...-anawaleta-wahindi-na-kuwaajiri-tanzania.html
Ni kweli hv kazi za finance manager au chief accountant au accounts payables au accounts receivables, etc, tunahitaji wahindi hata katika hizo kazi?

Mfano hata kwenye kupost invoice tunahitaji wahindi? Hv hii nchi inaenda wapi? Hawa wahindi tunaowapa hizi ajira wamesoma tanzania?

Nafikiri tunahitaji policy reformation juu ya ajira hasa hizi za sekta ya binafsi ili ziwe za wazawa tu maana sasa hv graduates ni wengi wakati job creation ni ndogo nahiyo kidogo bado inamezwa na wahindi, hv jamani kama ni mdogo, mjomba, mtoto, binamu, shangazi, n.k wako kwann wahangaike wakati wageni-wahindi wanakalia ajira zetu?

Tuseme no na tupaze sauti yetu kwa serikali.
 
Mwenyekiti wako si alisema hataki kura za wafanyakazi? hata serikalini tunanyanyaswa tunakatwa kitu ka NHIF afu hata huduma za afya hatupati hatuna housing wala transport allowances huku wengine wakilipana posho za kukaa shughulikien kwanza na hawa wazawa wachache wenye ajira za manyanyaso ndo urukie huko ulipokurupukia jion hii
 
Mawaziri wako wanasema watanzania ni wadokozi.

Wanategemea nini kama wao ni mafisadi? Kama wageni ndo waaminifu basi hata mawaziri tutawata nao watoke nje ili kukomesha udokozi na ufisadi
 
Swali lako ni unafiki na kejeli kwa vijana! Ninyi ndio mnaongoza serikali ambayo imetelekeza vijana. Nafasi za ajira mnapewa watoto na wajukuu utadhani ni serikali ya kifalme! Wewe unafahamu vema. Hapa unataka tukuone unatujali ilhali ukweli unaufahamu! Unafiki mtupu. Ndio maana tumejiunga na cdm maana kuna matumaini!
 
Back
Top Bottom