Muhimbili watoa Rai: Watanzania tuchangie damu

Nchi hii imejaa siasa za ujinga sana, Viongozi wa Chadema (Katibu), alitoa wito kwa Wanachama chake wajiyokeze kuchangia damu kwani kuna uhaba mkubwa sana wa Damu Mahospitalini, Serikali kwa kuona kuwa ni Chadema ndio watakaokuja kutoa damu inawakamata na kuwatia ndani, kuvaa fulana za Chadema sio kuwa damu yao haifai, kila siku huwa tunaona kila kikundi kinachokwenda kutoa damu huwa wanafaa fulana za Taasisi zao wanazoziwakilisha, iweje iwe shida kwa Chadema?

Siasa zinaangamiza taifa,
Jumuiya ya Ulaya imetoa pesa za kujenga Barabara ya kutoka kituo cha mawasiliano, kupitia Sinza, Tandale mpaka Magomeni, lakini Serikali haitaki hiyo barbara ijengwe kwani Mayor wa Ubungo na Mbunge watapata sifa, kila kukicha Bonface anaangaika sana na hiyo Barbara lakini CCM hawataki

Ndo maana mimi ilisema na nasema tena hatuna mtetezi wa wanyonge

Hapa tuna mtu mwenye agenda zake za siri
 
Waweke na condition tusiende zaidi ya watu wawili kwenye uchangiaji utakua ni mkusanyiko haramu
 
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kitengo cha dharura wametoa rai kwa watanzania kujitolea kwa hiyari kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaopokelewa hospitalini hapo.

Akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililofanyika kwa siku mbili mwishoni mwa wiki katika eneo la Karume jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo,amebainisha kuwa zoezi hilo ni muhimu sana kwani litasaidia kuokoa maisha ya
wagonjwa wenye uhitaji huo wanaopokelewa hospitalini hapo kama vile waliopata ajali, wakina mama wajawazito na watoto.

“Hospitali ya Taifa Muhimbili inahitaji wastani wa chupa za damu 100 lakini tunafanikiwa kupata wastani wa chupa 40 hivyo kuwepo na upungufu wa chupa 60 kila siku. Hali hii inapelekea kuhudumia
wagonjwa wenye uhitaji wa dharura tu huku wengine wakisubiri.” Alisema

“Wataalamu wananiambia kuwa kwa kawaida, damu inaweza kuhifadhiwa kwa muda wa takribani mwezi mzima kabla ya muda wake wa kutumika kwisha, na kutokana na uhifadhi wa damu kwa muda mfupi ndiyo maana tunasisitiza umuhimu wa watu kuchangia mara kwa mara. Kitaalamu mwanamume anaweza kuchangia mara nne kwa mwaka na mwanamke mara tatu kwa mwaka.” Aliongezea

“Katika wakati wa kutoa huduma ya tiba ya dharura, haswa kwa wagonjwa wa ajali, watoto na wamama wajawazito, upatikanaji wa huduma ya Ambulance na damu kwa wakati huongeza nafasi ya
kuishi kwa wahitaji kwa kiasi kikubwa mno na huduma hizi huokoa maisha ya mamilioni ya wagonjwa kila mwaka duniani kote,” alisema na kumalizia,

“Natoa rai kwa wakazi wa Dar es slaaam na Watanzania wote kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara ili nchi iwe na akiba ya damu ya kutosha, kwani asilimia moja ya Watanzania wakiamua kuwa wachangiaji damu wa kujirudia Mpango wa Taifa wa Damu Salama utaweza kukidhi mahitaji ya damu nchini.”

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, kampuni inayojishughulisha na uuzaji na usambazaji wa ving’amuzi kwa ajili ya matangazo ya dijitali ambao walidhamini zoezi hilo amesema kuwa hii ni mara ya pili wao kudhamini zoezi hilo kutokana
na umuhimu wake katika kuokoa maisha ya watanzania wote kwa ujumla.

“Hakuna asiyefahamu katika maisha yetu yanayotuzunguka ajali zimekuwa nyingi zinazopelekea watu kupoteza maisha maelefu kubaki mejeruhi wenye uhitaji mkubwa wa damu ili kupata matibabu. Kama
tunafuatilia vyombo vya habari basi tutakuwa tunasikia ni mara ngapi kwa wiki ajali zinatokea barabarani na kuacha majeruhi wengi. Kwa upande wa akina mama wajawazito wanahitaji damu kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kujifungua.

Hatuwezi kukaa pembeni na kuwatizama wakikosa msaada wakati uwezo huo tunao.” Aliongezea “Tumejisikia faraja sana kuwa wamojawapo wa wadau walioshiriki kufanikisha zeozi hili na tunaahidi kuendelea kushirikiana na Muhimbili katika kuwahamasisha watanzania wajitokeze zaidi.

Kwa mujibu wa wataalamu tunaweza kujitolea damu mpaka mara nne ndani ya mwaka, nina
uhakika kila mtanzania akifanya hivyo basi benki yetu ya damu itajaa na tutaweza hata kusaidia wengine wan chi za jirani wenye uhitaji.” Alimalizia Makamu wa Rais kutoka kampuni ya StarTimes

My Take
Mods sijakosea Jukwaa,sijakosea kabisa

Huku ndiko Lissu alitakiwa alazwe mahali ambapo hata DAMU hawana kazi ipo
 
Kama itakugundulika nitakuwa na damu nyingi kupita kiasa. ni bora hata nikajikata na damu yangu nikazimwagia mbwa zikanywa huenda mbwa zitanishukuru hata kwa kutikisa mkia.

Lakini sio nikaenda kuichangia damu yangu kwa maelekezo ya watu wasio julikana.
 
Back
Top Bottom