Mufti Zubeir: Kuna mijitu ilikuwa na kesi za Uhujumu Uchumi, huruma ya Magufuli ikawataka warudishe walizoiba

Magufuli alimpa pesa kila wakati,alimpa nyumba ya kuishi, alimpa ulinzi na gari ya gharama yaani alikuwa akiishi kifahari kwa hisani ya Magufuli huku waumini wake wengi wakiteseka kwa maisha magumu huku wakidhalilishwa kwa kuitwa magaidi na wala hata hakuthubutu hata kuhoji tu kinachowasibu masheikh wenzake walioshikiliwa gerezani bila kufikishwa mahakamani sasa mtu kama huyo atakosaje kumsifia bwana wake.

Yuko anapambana na MIJITU kwanza mkuu.
 
K

Kama mama Ni sawa na katili mwendasake mbona hskuna aliyeuwawa au kutekwa tangu mama ameingia madarakani? Mbona hakuna anayebambikiziwa kesi za uhujumu uchumi? Mbona Hakuna mfanyabiashara aliyenyang'anywa fedha zao, rambirambi za wahanga zilizoliwa Wala pesa za wakulima wa korosho zilizoporwa? Mbona Hakuna wanyama waliohamishiwa kijijini pasipofaa Wala uwanja wa ndege uliojengwa kijijini kwake mama m kusiko na tija? Au labda unafikiri mama hatopandisha mishahara ya watumishi, hatowapandisha madaraja au wafikiri atajaza kabilla lake serikalini au kuteua makada wa chama chake na kuwapa nafas wasizo na sifa nazo? Mama na muuaji wap na wap? Tangu Mama ameingia madarakani Umeshasikia watu wameokotwa pwani kwenye viroba?

Mwendasake Alijifanya katili Iakin hakujua Kuna katili Zaid yake, aliua wenzake yeye yupo wap Sasa? Tani 7 zinamhusu.

Seti dishi lakovizuri alafu uandike tena.
 
Achana na habari za kumtukana Shekh, mana mazusi ni zao la ujinga, wewe elezea tu unachofikiri utaeleweka bila kutukana.

Magu alikuwa anaangalia hasara na faida, kama ukimfunga fisadi bilioni zake zitabaki kuliwa na wachache lakini akirudisha zinaenda kuweka umeme kwa baba na mamazenu vijijini sasa hapo kizuri kipi.

Hata hao wezi wengine wanapata msamaha kila mwaka.

Kunakitu kinaitwa msamaha wa rais kwa wafungwa, hatahiyo nayo hujui ama unatakaje.
Wewe una uhakika gani hizo pesa zilikwenda kutengeneza hayo unayoyasema? nchi hii inaendeshwa na budget na zaidi sheria. Sasa inabidi mtuambie sheria gani ilitumika hapa maana hata huyo Shekh kasema alishtushwa sana na utaratibu huu haijawahi kutokea. Kama alitaka kuwasamehe angewasamehe baada ya kuhukumiwa sio mahabusu. hao unaosema wafungwa wanasamehewa ni wale labda wametumikia kifungo chao muda mrefu au wagonjwa au wazee na katiba inampa madaraka Rais. sasa tupe sheria gani serikali ilitumika.
 
Ningekuwa Rais ningetekeleza wajibu wangu kwa usahihi. Yeye ametufikisha wapi labda? Hawa waliouwawa hapa kwenye uchaguzi ilikuwa ni kulinda maslahi ya nani? Sasa hivi watu hawauwawi hovyo, je usalama haupo?
Nyerere tu hakuweza kutekeleza kwa usahihi kwakuwa hakuna binadamu mkamilifu,wewe ni nni?wacha unafiki😎
kama mamilioni ya watanzania wameona na wanajua mema yaliyofanyika wewe mnafiki mmoja utamshawishi nani?
 
Unauliza au unapigia jibu mstari? Hebu kaa kwa kutulia ww usidhani unaongea na watoto hapa.
Jibu swali acha taarabu,humu sio facebook,unaweza kuwa mtu mzima na hovyo tu,jibu swali wacha kuzua ujinga ujinga humu.
 
Nyerere tu hakuweza kutekeleza kwa usahihi kwakuwa hakuna binadamu mkamilifu,wewe ni nni?wacha unafiki😎
kama mamilioni ya watanzania wameona na wanajua mema yaliyofanyika wewe mnafiki mmoja utamshawishi nani?
Nilijua lazima utapanick tu. Ni hivi, alikuwa dhalimu na muuaji fullstop.
 
Leo katika kongamano la viongozi wa dini ukumbi wa Chimwaga Dodoma, Mufti wa Tanzania, Abubakari Zuberi alipata nafasi ya kusema machache na mojawapo aliongelea wahujumu uchumi nyakati za uongozi wa Rais Magufuli.

''Wenyewe ni mashuhuda, kuna mijitu humu ilikuwa na kesi ya kuhujumu uchumi, kuna watu walikuwa na kesi mnaita za kutakatisha pesa lakini kwa huruma akaona hawa kwanini wasiendelee na masuala ya kushughulika na uchumi zaidi tukapata kodi lakini wakaturudishia pesa walizotuibia!

Jambo hili nililistaajabu nilipolisikia kwa mara ya kwanza lakini ilikuwa ni kazi ya Dkt. Magufuli na aliekuwa makamu wake ambae sasa ni Rais wetu''

Mufti amesema Rais Magufuli alikuwa Jasiri na mwenye uthubutu ambalo ni jambo muhimu sana kwa viongozi kuwa nalo.

"Yuko mtu mmoja anasema sijapata kuona aibu kubwa katika aibu zote kama mtu anaweza kufanya jambo alafu anashindwa kufanya jambo, hiyo ni aibu kubwa" Alisisitiza Mufti

Pia Mufti amesema Rais Magufuli amejenga heshma na dunia nzima kufahamu Tanzania ni kitu gani akitolea mfano safari yake mojawapo nje ya nchi na mtu wa immigration aliposoma pasi yake ya kusafiria akamuuliza kama ametoka kwa Magufuli, mtu huyo alimuomba wamuazime Magufuli kwa muda awatatulie masuala yao.

Ogopa sana kuwa na viongozi wa dini wasioweza kukemea hata maouvu yanapofanyika waziwazi kwa vile tu
Sasa Mufti haoni kama hapo sheria imevunjwa? kama kweli mtu amehujumu uchumi kweli na amekamatwa kwa haki kwanini aachiwe kwa huruma na sio sheria ifanye kazi yake?..

Kwa hiyo na wauwaji tuwaachie, wezi waachiwe, wabakaji waachiwe, nk kwa sababu Rais ana huruma.....watch out Mr Mufti..
Kusema kweli wengi wa viongozi wetu wa dini kwenye kongamano la jana walizungumzia zaidi hisia na mapenzi kuliko uhalisia.

Mufti ameamua kujitoa ufahamu na kusahau kwamba wengi wa wanaoitwa wahujumu uchumi walifanya hivyo kwa kushurutishwa.

Kuna Mchungaji mwingine alisema kwamba kutokana na imani waliyonayo kwa ccm ndio maana kwenye uchaguzi wa mwaka jana wameichagua ccm kwa kura nyingi sana.

Maana yake ni kwamba mapenzi yake kwa ccm yamemtia upofu kiasi kwamba uchafu wote ulifanyika kwenye uchaguzi ule yeye hakuona na hata kama aliona kwake ilikuwa halali ili mradi waliofanyiwa hiyo dhulma ni wapinzani.
 
Hata wewe hapo ulipo nimchafu kwa matendoyako.

Rais ni kiongozi mkubwa sana kwa cheo chake kwahiyo watu wawili watatu mkiona hakufanya vizuri kwenu basi mjue hichomnachokiona kibaya kilifanyika kwa ajili ya maslahi ya wengi.
Nani kakuambia ni wawili watatu?? Hiyo tafiti umeifanyia wapi?
 
Leo katika kongamano la viongozi wa dini ukumbi wa Chimwaga Dodoma, Mufti wa Tanzania, Abubakari Zuberi alipata nafasi ya kusema machache na mojawapo aliongelea wahujumu uchumi nyakati za uongozi wa Rais Magufuli.

''Wenyewe ni mashuhuda, kuna mijitu humu ilikuwa na kesi ya kuhujumu uchumi, kuna watu walikuwa na kesi mnaita za kutakatisha pesa lakini kwa huruma akaona hawa kwanini wasiendelee na masuala ya kushughulika na uchumi zaidi tukapata kodi lakini wakaturudishia pesa walizotuibia!

Jambo hili nililistaajabu nilipolisikia kwa mara ya kwanza lakini ilikuwa ni kazi ya Dkt. Magufuli na aliekuwa makamu wake ambae sasa ni Rais wetu''.

Mufti amesema Rais Magufuli alikuwa Jasiri na mwenye uthubutu ambalo ni jambo muhimu sana kwa viongozi kuwa nalo.

"Yuko mtu mmoja anasema sijapata kuona aibu kubwa katika aibu zote kama mtu anaweza kufanya jambo alafu anashindwa kufanya jambo, hiyo ni aibu kubwa" Alisisitiza Mufti.

Pia Mufti amesema Rais Magufuli amejenga heshma na dunia nzima kufahamu Tanzania ni kitu gani akitolea mfano safari yake mojawapo nje ya nchi na mtu wa immigration aliposoma pasi yake ya kusafiria akamuuliza kama ametoka kwa Magufuli, mtu huyo alimuomba wamuazime Magufuli kwa muda awatatulie masuala yao.

kuwa na kesi siyo kukutwa na hatia haina tija hiyo,,waangapi wamekutwa na hatia na kufungwa?/
 
Back
Top Bottom