Mufti Zubeir: Kuna mijitu ilikuwa na kesi za Uhujumu Uchumi, huruma ya Magufuli ikawataka warudishe walizoiba

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,813
Leo katika kongamano la viongozi wa dini ukumbi wa Chimwaga Dodoma, Mufti wa Tanzania, Abubakari Zuberi alipata nafasi ya kusema machache na mojawapo aliongelea wahujumu uchumi nyakati za uongozi wa Rais Magufuli.

''Wenyewe ni mashuhuda, kuna mijitu humu ilikuwa na kesi ya kuhujumu uchumi, kuna watu walikuwa na kesi mnaita za kutakatisha pesa lakini kwa huruma akaona hawa kwanini wasiendelee na masuala ya kushughulika na uchumi zaidi tukapata kodi lakini wakaturudishia pesa walizotuibia!

Jambo hili nililistaajabu nilipolisikia kwa mara ya kwanza lakini ilikuwa ni kazi ya Dkt. Magufuli na aliekuwa makamu wake ambae sasa ni Rais wetu''.

Mufti amesema Rais Magufuli alikuwa Jasiri na mwenye uthubutu ambalo ni jambo muhimu sana kwa viongozi kuwa nalo.

"Yuko mtu mmoja anasema sijapata kuona aibu kubwa katika aibu zote kama mtu anaweza kufanya jambo alafu anashindwa kufanya jambo, hiyo ni aibu kubwa" Alisisitiza Mufti.

Pia Mufti amesema Rais Magufuli amejenga heshma na dunia nzima kufahamu Tanzania ni kitu gani akitolea mfano safari yake mojawapo nje ya nchi na mtu wa immigration aliposoma pasi yake ya kusafiria akamuuliza kama ametoka kwa Magufuli, mtu huyo alimuomba wamuazime Magufuli kwa muda awatatulie masuala yao.

 
Mapambio hayawezi kauka hasa katika swala la kupigania kikombe chako na mkate wako mezani usikauke viongozi wadini walikuwa wa ndimi mbili na wako waliokemea maovu nakuonekana wazalendo tuwe makini na viongozi wetu wa dini has katika nyakati hizi za mwisho kila ataekuja kwa kimvuli cha dini yapaswa kujiridhisha ndani yake kama ndie ane stahili au la
 
mapambio hayawezi kauka hasa katika swala la kupigania kikombe chako na mkate wako mezani usikauke viongozi wadini walikuwa wa ndimi mbili na wako waliokemea maovu nakuonekana wazalendo tuwe makini na viongozi wetu wa dini has katika nyakati hizi za mwisho kila ataekuja kwa kimvuli cha dini yapaswa kujiridhisha ndani yake kama ndie ane stahili au la

Basi subiri siku kiongozi wa dini atakapo ongea yanayo kufurahisha ndio awe kiongozi wako.
 
Sasa Mufti haoni kama hapo sheria imevunjwa? kama kweli mtu amehujumu uchumi kweli na amekamatwa kwa haki kwanini aachiwe kwa huruma na sio sheria ifanye kazi yake?..

Kwa hiyo na wauwaji tuwaachie, wezi waachiwe, wabakaji waachiwe, nk kwa sababu Rais ana huruma.....watch out Mr Mufti..
 
Back
Top Bottom