Eee sawa mkuu mliangalia uwezekano sasa mme wezekana!
Uroho wenu wa kura mnarukia vitu ambavyo vinaivunja katiba! eti iingizwe kwenye katiba, lakini waislamu tu ndo watoe maoni? na waislamu tu ndo wawe mahakimu? Kwahiyo itabidi serikali isomeshe mahakimu wa kiislamu kwa ajili ya kuhudumia mahakama hizo? yaani yaaani...
..Kikwete alishachomoa kuhusu ahadi ya Mahakama ya Kadhi.
..alidai waliotumbukiza suala hilo kwenye ilani ni Philip Mangula[mkristo] na Ngombale Mwiru[hana dini].
Tatizo si kuwa na mahakama tatizo ni kudhalilishwa na kuonewa waislamu. Mzee Mwanakijiji kuhusu alleged grand corruption cases ni still allegation hakuna substance wala proof katika hilo bali ni accusations tu.
Sasa Mufti ni msomi hawezi kukurupuka tu na kudai fulani ni fisadi pasina kuwa na vielelezo (kumbuka uislamu unataka mtu atuhumiwe kwa vielelezo na sio watu fulani wanamhisi kuwa yeye ni fisadi wengine ni chuki zao binafsi au hasidi zimewatala)
Tukija katika swala la Kadhi hii sio mahakama tu bali mfumo mzima wa maisha ya waislamu. Ni ajabu kama si kichekesho eti sharia za kiislamu ziweke katika mahakama ya circular. Utahukumu vipi kuhusu ndoa wewe hakimu ambaye hujui hata herufi zake zimeandikwaje huoni ni ajabu. Pili unahukumu eti katika tafsiri ya mtu. Kumbuka tafsiri ni mtu aonavyo yeye na sio watu wote waonavyo hivyo basi kuna hatari mahakama zikatawaliwa na mlongo mmoja. Na sio ndoa tu, utawala, ujirani na mengineo mengi je haya tufate kanisa linavyosema au uislamu unavyosema?
Kiufupi CCM naona imejitafutia kaa la moto la hili wamelipata. Waislamu wanakuwa kimya lakini linapotokea jambo kama hili huwa kitu kimoja. Dhambi ya ubaguzi wa dini ni mbaya na Tanzania itachafuka tukielekea huko ule kawaimbo wa amani utatoweka.
Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM
Na Ummy Muya
Alisema serikali imedhihirisha kuwa inaendeshwa na Wakristo na si kweli kama serikali haina dini na akamtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kubatilisha kauli hiyo kwa kuwa inamchafua Rais Jakaya Kikwete mbele ya umma wa Waislamu.
Source: Mwananchi
CCM watajuta kuweka swala la Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani yao uchaguzi ya 2005.
Waziri ametuthibitishia kama Rais Kikwete alikuwa akitulaghai ili tumpigie kura kwa kigezo kuwa suala hilo litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi na sio kuchanganywa kama ilivyokuwa mwaka 1970 katika Sheria ya Ndoa na kuwanyima haki Waislamu,alisema.
Imetosha kuwa ujumbe umewasilishwa au umefika sasa kama wataenda ikulu au uwanja waTaifa hayo ni maslahi binafsi ,kama ni kuruka nae mufti ameruka kwa kuwakabidhi waislamu uhuru wao wa kuchagua badala ya kuing'ang'ania CCM iliyojaa uwongo kwa kuthibitika kuwepo kwa ahadi hewa lukuki.
serikali itambue kuwa Bakwata iko hai hao Wakristo walikuwa wapi wakati sisi tukipigania uhuru,alihoji.
Wakati huohuo, Sheikh Salum Rwambo alisema anawashangaa wabunge Waislamu ambao baadhi ni mahajat na malhaj wanakaa kimya na kushindwa kutetea hoja za msingi na kudai kuwa huo sasa ndio mwisho wao wa kuwaita masheikh na kutaka waombewe dua ili wasipate wepesi katika kampeni zao. Sheikh Rwambo pia alimsifia mbunge wa Nzega Lucas Selelii kwamba ni miongoni mwa wabunge katika Bunge hilo wanaozungumza ukweli na kwa kujiamini tofauti na wengine ambao wanaenda kukaa bila kufanya kazi zilizowapeleka.
Toka lini msimamo wako kuhusu hili umebadilika?Tusichanganye DINI na SIASA