Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

Mkandara,

..unajua watu kama Tumain na Mwana wa Mungu ingefaa wapelekwe kwenye kambi la wakimbizi[gezaulole] wafungiwe huko kila mmoja ajaribu kumbadili mwenzake dini.
 
Hivi Bakwata au Chombo chchote kinacho ongoza Waislamu, kama baraza la kuendeleza Kuran, wakichagua wanazuoni wao na kuendesha Mahakama hizo za Kiislamu, hususan katika kutoa maamuzi ya ndoa, mirathi nk itakuwa haitoshi? mpaka mahakama hiyo ianzishwe na serikali? ili mradi wahusika wakuu wa hizo kesi wakubaliane kwamba ikiwa ndoa yangu itaingia mgogoro au mirathi yangu basi hatua ya kwanza ni balukta au bakwata. kwa mafano mimi ni mkristo itakapo tokea ya kutokea ni aidha niende mahakama za serikali au niende kwa paroko wangu, hiyo ndio au ndio njia nilizo nazo. period, sina haja ya kugombana na mtu, wa kugomba nami ni nafsi yangu.
Unahitaji kuelimishwa tuu bado hujafahamu vizuri mahakama ya kadhi ...soma zaidi kwanini nchi zingine zilianzisha unafikiri kulikuwa hakuna bakwata yao au balukta ...tafuta zaidi ufahamu kwanini?
 
Mkandara,

..unajua watu kama Tumain na Mwana wa Mungu ingefaa wapelekwe kwenye kambi la wakimbizi[gezaulole] wafungiwe huko kila mmoja ajaribu kumbadili mwenzake dini.
Hakuna kulazimisha katika dini, mimi nimekuwa muislamu baada ya kuwa na akili yangu...kwahiyo ntashukuru kama mwana wa mungu atfahamu haki ...hoja hapa si wewe uwe dini gani? ila kwanini wewe mkristo ujisikie vibaya kwa jambo ambalo halikuhusu..wivu, uchoyo, siasa kali au nini? hapo ndio nashindwa kuwaelewa wakristo?
 
waende wakatafute nchi ya kwao binafsi. waende kule mafia. huyu mufti wao mwenyewe anayetisha ukimwangalia, duh, Mungu na amwondoshee mbali. muda wake naye uko karibu. asipookoka na kumfuata Bwana Yesu, siku zake zinahesabiwa. watu wanaomba sana apotelee mbali na kadhi zake, akahukumiwe nazo huko kuzimu. ameshindwa kwa Jina la Yesu.
Kwahiyo Tanzania ni Nchi yenu siyo? unaota kwelikweli? you are wishing will never materialize na utakufa na chuki zako, zaidi nakuombea uendelee kuishi miaka mingi nakusikia uchungu jinsi waislamu wanavyopeta ikiwemo hii ya mahakama, na mengine mengi ambayo masikio yako hayataki kusikia (ishi miaka 110 mungu ajaalie) ili majungu yawe mengi.
 
Kinachosikitisha sana bongo ni jinsi viongozi wa dini wanavyoelekea kusahau wajibu wao wanaendekeza siasa. Inatakiwa waumini wa dini zote kuwasusia viongozi wote wa dini zao wanaojihusisha na siasa kiwaziwazi. hili jambo likiendekezwa zaidi litaturudisha nyuma kimaendeleo na haswa kisayansi. Waumini waachwe waipe dini ya imani yao nafasi ndani ya mioyo yao bila kupangiwa ukubwa wa eneo ndani ya mioyo ya waumini. Tanzania tunabahati ya kuwa na Baba wa taifa aleyetuongoza kwa busara ya kwamba "Taifa la Tanzania halina dini" ila Watanzania au kila mtanzania w/anao uhuru wa kuabudu dini w/anayoitaka. Tuna mambo muhimu zaidi ya kushughulikia, kutatua, kuvumbua nk. Anayetaka serikali ya Ki-katoliki ahamie Vatican, anayetaka ya Kiislamu ahamie nchi zenye serikali za kiislamu, ziko nyingi sana!
 
Nawaletea maoni ya mtanzania huyu mtanisamehe nimeshindwa kufanya pest vizuri naomba mod unisaidie




additMahakama ya Kadhi: Ahadi nzito iliyoshindikana
ban.maswali.jpg


Ansbert Ngurumo

amka2.gif

IWAPO hoja ya Mahakama ya Kadhi itafika mahali pa kuwakosanisha na kuwagombanisha Watanzania, mgogoro huo utakuwa umesababishwa na woga wa watawala wetu.
Mgogoro huo sasa unaanza kuchukua sura ya kidini, hasa baada ya Waislamu kuituhumu Serikali ya Awamu ya Nne kwamba inawasikiliza Wakristo katika masuala ya Waislamu.
Ni vema niseme tu mapema kwamba Waislamu wana hoja dhidi ya serikali na CCM lakini si dhidi ya Wakristo au Watanzania wa imani nyinginezo.
Sababu kuu ni moja. Serikali na CCM si taasisi za Wakristo. Na tamko la Waziri wa Sheria na Katiba kuhusu Mahakama ya Kadhi, si lake binafsi, ni la serikali, ambayo inagombana na chama chake kilichowaahidi Waislamu kupewa mahakama hiyo.
Lakini yapo mazingira mabaya yaliyojengwa na watawala ambayo Waislamu wanayatumia kujenga hoja yao. Watawala waliingiza siasa zao katika suala la kidini. Na Waislamu, kwa kutaka ulinzi wa kisheria wenye nguvu ya dola, wakakubali hoja ya watawala, na wakasubiri utekelezaji.
Watawala hawakuwa na nia ya kuitekeleza, bali waliitumia kama hoja ya ziada ya kuombea kura. Kwa hiyo, Waislamu wana haki ya kukasirika kwa kuwa wamegundua kuwa imani yao imetumiwa kwa maslahi ya kisiasa.
Kwa hiyo, Waislamu watapata ushindi mnono iwapo wataelekeza nguvu zao zote kwa watawala waliotoa ahadi. Watakuwa wanafanya makosa makubwa ya kimkakati iwapo watawaacha watawala na kuwashutumu wananchi wengine ambao ama wanashabikia au wanakejeli hoja hiyo.
Na hata kama kuna mazingira ya mzozo wa kimadhehebu, hayakuletwa na wafuasi au viongozi wa madhehebu hayo. Wanasiasa ndio wameyatumia makundi ya dini nchini kujipatia madaraka.
Kwa upande fulani, nitamtetea Rais Jakaya Kikwete, ambaye alitumia mbinu na mikakati mbalimbali ‘kuwashinda' maaskofu, makasisi na wachungaji kabla na baada ya kuteuliwa kuwa mgombea urais.
Baadhi yetu tunajua nguvu kubwa aliyowekeza katika kuhakikisha anakubalika kwa viongozi wa dini za Kikristo. Hakuwa na shaka na kura za Waislamu wenzake. Na kama mwanasiasa yeyote, alikuwa na haki ya kuhakikisha anaitumia nguvu ya taasisi za Kikristo kupata anachotaka.
Kwa upande mwingine, mbinu ilikuwa inamjenga kuonekana kama daraja kati ya makundi makubwa haya mawili katika jamii. Na kwa jinsi baadhi yetu tunavyomfahamu, Rais Kikwete si mdini; bali mtu mwenye ustaarabu wa viwango vyake vinavyokubalika.
Kinachogomba, na kinachowaudhi Waislamu ni jinsi ambavyo anashindwa kukaa nao kujadili hatima ya suala hili, lakini yuko tayari kukaa na viongozi wa madhehebu mengine na kulitolea tamko. Hata kama ni kwa nia njema, mkakati wake si mzuri.
Kumbukumbu zangu zinanionyesha kwamba mara ya mwisho Rais alitoa kauli juu ya suala hili Novemba 17, 2007, siku ambapo niliandika katika safu hii na kuwataka Waislamu wambane yeye waachane na Mchungaji Christopher Mtikila.
Niliwaeleza Watanzania kwamba ahadi hii ya CCM ilikuwa ujanja wa kuombea kura. Nikawataka watafakari kuhusu nia, malengo na mkakati wa CCM, iliyomtumia mgombea urais Muislamu kuwaghilibu Waislamu; kwamba tumbane aliyetoa ahadi; na tumlazimishe aitekeleze.
Lakini nilionya, wakati huo, kwamba serikali hii, chini ya Rais Jakaya Kikwete, haikuwa na nia ya kuwapa Waislamu ofisi hiyo; na kwamba serikali ingefanya lolote linalowezekana ama kuiahirisha au kutoa ahadi nyingine mpya, tofauti na ya awali.
Kwa kusisitiza, niliandika hivi:
‘Ni wazi pia kuwa kama serikali ingeamua hata kesho kuwapa Waislamu mahakama yao isingeshindwa kufanya hivyo. Na kama inaona utaratibu wa kisheria kupitia bungeni unaleta mgogoro isingeshindwa kutamka kwamba Waislamu waanzishe mahakama yao wenyewe bila kuishirikisha serikali.
Lakini inajua kwa nini inanyamaza. Haitoi uamuzi kwa sababu haina nia tena ya kuunda mahakama hiyo. Na imepata bahati sasa ya kuwagawa Waislamu…
Itawachukua Waislamu muda mrefu kugundua kuwa wanapambana na mtu asiyehusika na ucheleweshaji wa ahadi ya Rais Kikwete na CCM; na sababu ni moja. Wameamua kusikiliza hotuba nzuri. Hawajapata ujasiri wa kudai matendo ya dhati.
Najua fika kwamba Rais Kikwete binafsi hakupenda wala hapendi suala hili la Mahakama ya Kadhi katika ilani ya uchaguzi ya CCM.
Bahati mbaya hakushiriki kuiandaa, lakini alishiriki kuinadi. Naamini hata yeye leo hajui ni nani aliliingiza suala hilo kwenye ilani. Na hata wakimpata leo, hawataondoa ukweli kwamba yeye (Kikwete) ndiye aliyezunguka nchi nzima analipigia debe.
Ndiye anayepaswa kudaiwa maelezo. Hawezi kubadili ilani ya CCM leo. Waislamu hawawezi kukubali kutumiwa kwa ajili ya kura na baadaye kupuuzwa tu kwa sababu ya hisia binafsi za viongozi wale wale.
Wanachopaswa kufanya ni kumbana Kikwete. Na kama watasubiri hotuba nzuri kuhusu hili, wampe nafasi ataibuka siku moja na maneno matamu ya kuahirisha azma yao. Sijui kama watapiga makofi kumshangilia au watapaza sauti kumzomea.'
Wengi walinielewa, wakati huo; wachache waliitazama hoja yangu kwa macho ya kidini. Lakini baada ya tamko la sasa la serikali, lililotolewa na Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, kwamba serikali haitaunda Mahakama ya Kadhi na badala yake itatafsiri sheria za Kiislam na kuzijumuisha kwenye sheria za nchi, ili zitumike kwenye mahakama za kawaida hapa nchini, naamini sasa tunaanza kuelewana.
Wanaomlaumu waziri kama mtu binafsi wanakosea. Waziri ni mjumbe tu; na mjumbe hauawi! Na wanaoilaumu imani ya waziri wanatenda kosa jingine. Yeye ametumwa na serikali inayoongozwa na chama chake. Huo ndiyo msimamo wao.
Kwa hiyo, watu wanaopaswa kung'ang'aniwa ni watawala. Kwanza, hoja hii ni ya kidini, lakini watawala wameigeuza hoja ya kisiasa. Na wakati mwingine walipoamua kuijadili kidini walitumia uwanja usio mwafaka, kama alivyofanya Rais Kikwete Novemba 17, 2007 mbele ya maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT).
Siku hiyohiyo niliposema Waislamu wambane yeye, rais mwenyewe alijitokeza, akawaambia maaskofu wa KKKT kuwa yeye hahusiki na suala la Mahakama ya Kadhi; akawataja watu waliolitetea na kuliingiza katika mjadala wa chama chake.
Baadhi yetu tulimkosoa kwamba kwa kauli hiyo alifanya makosa mawili. Kwanza, alipaswa kuzungumza hivyo mbele ya Waislam ili wamhoji ajibu maswali yao. Kilichompleka kwa maaskofu kujadili hoja ya Waislamu ndicho kinawapa nguvu baadhi yao kumuona Rais anatumiwa na Wakristo au anawaogopa huku akiwapuuza wahusika katika suala hili.
Pili, licha ya ukweli kwamba yeye hakuhusika kuliingiza suala hili kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM, ndiye aliyeinadi kwa umma na kutoa ahadi ambayo Waislamu bado wanataka itekelezwe.
Kwa hiyo, kama Waislamu wanalalamikia kutumiwa, aliyewatumia ni yule aliyewapa ahadi wakampa kura. Kama hakushiriki kuandika ilani si utetezi tosha wa kumtoa kwenye lawama, labda kama anataka kufuta ilani nzima, maana ndiyo hiyo anayodai anaitekeleza yeye – na si yeye aliyeiandika (na hatukumtarajia aiandike).
Zaidi ya hayo, ndiye mwenyekiti wa CCM na rais wa nchi. Kama amegundua makosa ya ilani yake katika suala hili, ni kipi kinamzuia kukutana na Waislamu akawaeleza msimamo wake mpya (kwamba aliinadi hoja hiyo kimakosa), akasikia hoja zao moja kwa moja, akajibu maswali yao na kuwaondolea wasiwasi?
Kwa nini woga wa rais kukutana na Waislamu usababishe chokochoko za kijamii kati ya Waislamu na waamini wa madhehebu mengine? Kwa nini madaraka yao ya kisiasa yawe sababu ya kuivuruga jamii kwa misingi ya tofauti ya kidini?
Rais na wapambe wake lazima wajue kwamba suala hili litawatafuna hata kama wanadai si wao walioliingiza kwenye ilani, lakini kipimo tunachotumia kupima utekelezaji wake wa ahadi nyingine ndani ya ilani ya chama chake, ndicho hicho tunachotumia kupima kushindwa kwake kutekeleza ahadi hii ya ofisi ya Kadhi Mkuu.
Si kwamba hatujui ugumu au utata wa kisheria, kikatiba na kijamii unaoweza kujitokeza; wala si kwamba sisi ni mashabiki wa suala hili; bali tunataka watawala wawe waungwana, maana halikuingizwa ghafla kwenye ilani.
Na haiwezekani kwamba wasioitaka (akiwamo rais) hawakuliona muda wote huo hadi walipoingia madarakani. Walijua wanachofanya; na hapa walitaka kuwatumia Waislamu kuzoa kura za ushindi wa kishindo. Sasa kama ni waungwana, walipaswa kutimiza ahadi yao, maana Waislamu walishatimiza wajibu wao wa kupiga kura.
Ipo methali ya Kiarabu isemayo: ‘Ahadi ni mawingu, utekelezaji wake ndiyo mvua.' Tunataka rais akubali mvua inyeshe, hata kama itamlowesha, maana yeye ndiye alitengeneza mawingu hayo.
Kwa kuahirisha hoja yao na kutoa tamko jipya sasa, Kikwete anatafuta fursa ya kutekeleza ujanjaujanja wa Mwanafalsafa machachari wa Kitaliano wa karne ya 16, Niccolo Machiavelli, kwamba ‘mfalme hakosi sababu za msingi za kutotimiza na kuvunja ahadi yake.'
Hii ndiyo maana ya kauli ya serikali bungeni, kupitia kwa Waziri Mathias Chikawe wakati akiwasilisha makadirio na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2009/10, wiki hii, kwamba:
''Hivi sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeanzisha mchakato wa kukusanya mawazo na maoni kutoka kwa viongozi wa madhehebu yote ya Dini ya Kiislamu kwa nia ya kuorodhesha misingi ya Dini ya Kiislam, hususan ile inayohusu sheria binafsi kwa madhumuni ya kuihuisha misingi hiyo katika sheria za nchi, kwa kuzingatia sheria ya The Islamic Law Act, sura ya 375 ya mwaka 1964.''
Hiki ndicho wanachokipinga Waislamu, na ndicho kinawalazimisha kuonyesha hasira zao kwamba hawataipigia kura CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, hasa kama atakayegombea ni Rais Kikwete.
Wanasema hivyo wakijua kuwa ndiye atakayegombea; maana maandalizi yameshaanza. Wasichojua ni kwamba yeye alijua hisia zao mapema, na serikali imeamua kuzikabili mapema mwaka huu kuliko kusubiri mwakani ili kupoza hasira zao pole pole kuelekea uchaguzi mkuu.
Sina hakika kama serikali haijaweka mkakati mbadala wa kuwalegeza na kuwagawa ili ichote kura zao kwa staili nyingine, na ahadi nyingine.
Imewachukua muda mrefu Waislam kugundua ujanja wa wanasiasa. Kauli ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) iliyotolewa na Mufti Sheikh Mkuu, Issa bin Shaaban Simba kwamba ‘Rais Kikwete alikuwa akitulaghai ili tumpigie kura' ilipaswa kutolewa siku nyingi. Labda ingekuwa imewasaidia kumsukuma na kumlazimisha kuzungumza nao ana kwa ana.
Sasa wakati umefika, rais aache woga, akutane na Waislamu awasikilize kwa makini; maana sasa ni zamu yako kusikilizwa.
Awaombe radhi kwa kuwatumia katika kampeni kwa suala linalohusu imani yao, ambalo kama wangeambiwa mapema wasingeshindwa kujianzishia Mahakama ya Kadhi Mkuu kama yanavyofanya madhehebu mengine ya dini.
Ajue kwamba kwa jinsi upepo unavyokwenda sasa, wapo Waislamu ambao wanalijadili suala hili bila kutazama udhaifu wa watoa ahadi; bali nguvu ya madhehebu mengine, hasa ya Kikristo, ambayo wanadhani ndiyo yamesababisha serikali kuwakatalia jambo lao.
Na wapo wananchi wa madhehebu mengine wanaoshangilia kushindwa kwa ahadi hii kwa sababu za kidini au za kisiasa, kwamba imesaidia kuonyesha udhaifu na uongo wa serikali inayoongozwa na CCM; na jinsi inavyotii vitisho vya waliokataa Mahakama ya Kadhi.
Naona, nasikia na kuhisi hasira za Waislamu. Ni kweli wameonewa; si tu kwa kunyimwa walichoahidiwa, bali kwa kutumiwa kama ngazi ya wanasiasa kupata madaraka.
Kinachobaki sasa, ni jamii kutazama hatima ya mvutano wa Waislamu na CCM. Utakuwa mvutano wa mabavu au wa hoja? Zitakuwa hoja za kisiasa au za za kidini? CCM itafanikiwa kuwagawa katika makundi na kushinda tena?
Je, wako tayari kushindwa kila harakati zao dhidi ya wanasiasa watawala? Je, CCM ipo tayari kukiri kosa na kuwaomba radhi Waislamu, na kuahidi kutotumia tena masuala nyeti ya imani yao katika majukwaa ya kisiasa?
Je, Waislamu (katika hasira walizo nazo sasa) wanaelewa kuwa ‘wabaya' wao katika hili si Wakristo bali wanasiasa wajanjawajanja wanaofikiri kwamba njia yoyote inayoweza kuwafikisha madarakani ni halali wakati wa kampeni?
Je, serikali inajua kuwa iwapo msimamo wake utaleta mgawanyiko na uadui wa kidini katika jamii, serikali ndiyo itawajibika kwa kuchochea migogoro ambayo ingeweza kuahirishwa kwa uungwana wa watawala?
Matokeo mabaya yanaweza yasitokee katika utawala wake, lakini Rais Kikwete akiondoka madarakani bila kuliweka sawa suala hili atakuwa anajivunia kuacha urithi gani wa chokochoko za kidini? Je, Rais Kikwete bado anatafuta wachawi (walioliingiza suala hili kwenye ilani) wa kubebesha lawama au sasa ameshakomaa na kujua kwamba yeye ndiye rais wa nchi, mwenyekiti wa CCM, na ndiye anapaswa kuwajibika kwa masuala nyetu kama haya? Je, wale wanaoipongeza CCM kwa kutekeleza ilani yake kwa silimia 100, wanajumuisha na udhaifu huu wa Mahakama ya Kadhi? Au hii nayo ni ahadi iliyotekelezwa? Iwe iwavyo; Watanzania wanataka majibu yaliyokamilika.


h.sep3.gif
juu
blank.gif
blank.gif
blank.gif
Habari Mpya | Matangazo | Bei zetu | Wasiliana nasi | Tuma habari
 
Last edited:
Katiba ya nchi ni kanuni ambazo jamii imejiwekea ili zifuatwe katika maisha yao ya kila siku. Kama suala ni kuingizwa kwenye katiba sioni ubaya ili mradi iwekwe wazi kuwa halazimishi mtu kwenye hilo. Mbona Hiyo BAKWATA Ilipoanzishwa wakati wa Nyerere maaskaofu hawakupinga?.

Halafu kama issue ni kuingizwa kwenye katiba, huoni kuwa kwa sheria hizohizo kuingizwa kwenye mahakama za kawaida zinakuwa tayari zimeingizwa kwenye katiba ( Sheria mama?). hoja yako bado imeelemea upande mmoja. Ndoa imefungishwa na Sheikh kwa sheria za dini yao ya kiislamu wewe hakimu Brown Christian unatumia sheria za dini isiyokuhusu kuhukumu wapi na wapi?. Huku ndiyo mwanzo wa kutafuta patashika. Kwa hili serikali imekosea inabidi watu waache idiology zao na kufanya kazi ya nchi sio maaskofu.
Kitu kimoja ambacho nadhani ni vyema kikaeleweka ni kwamba, endapo serikali itakubaliana na matakwa ya Waislam kubadili katiba ili kuweza kuruhusu uanzishwaji wa Kadhi Mkuu (japokuwa haikatazi hilo - kama ni ibada), basi ni dhahiri kuwa kipengele hicho cha Katiba kitawahusu wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakuna uwezekano Katiba ikawa na vifungu vinavyohusu baadhi tu ya watu kwa kuzingatia dini yao na isihusu wengine wote. Kwa minajili hiyo, haiwezekani Katiba hiyo ikaundwa bila kuhusisha watu wote. Hii ni kwasababu;

1. Katiba hubadilishwa na Bunge pekee (Muswada ya mabadiliko ya katiba inaweza kutoka serikalini au kwa Wabunge kwa kufuata taratibu)
2. Hakuna uwezekano wa Bunge kujadili jambo na kuzuia baadhi ya waBunge kuhudhuria au kutumia nafasi yao ya Ubunge kuchangia hoja hiyo

Mkuu Hosfede, umezungumzia ndoa iliyofungwa na Sheikh kuvunjwa na hakimu Brown. Ni kweli kuwa ndoa za kidini kufungwa na Taasisi husika za kidini. Ila kwa sheria za nchi, wanandoa hao pia husaini karatasi ya ndoa ambayo hutolewa na Serikali. Karatasi hiyo ndiyo hutumika sehemu zote ndoa zinapofungwa na ni legal document. Hivyo ili karatasi hiyo ifutwe, ni lazima hakimu akubali hilo kutokea. Hapo ndipo akina Hakimu Brown na Sharif wanapoingia. Wakimaliza kazi yao, utaratibu mwingine wa kuifuta ndoa hiyo kidini/kitamaduni na kadhalika unaweza kufuata.
 
Tatizo si kuwa na mahakama tatizo ni kudhalilishwa na kuonewa waislamu. Mzee Mwanakijiji kuhusu alleged grand corruption cases ni still allegation hakuna substance wala proof katika hilo bali ni accusations tu.

Sasa Mufti ni msomi hawezi kukurupuka tu na kudai fulani ni fisadi pasina kuwa na vielelezo (kumbuka uislamu unataka mtu atuhumiwe kwa vielelezo na sio watu fulani wanamhisi kuwa yeye ni fisadi wengine ni chuki zao binafsi au hasidi zimewatala)

Tukija katika swala la Kadhi hii sio mahakama tu bali mfumo mzima wa maisha ya waislamu. Ni ajabu kama si kichekesho eti sharia za kiislamu ziweke katika mahakama ya circular. Utahukumu vipi kuhusu ndoa wewe hakimu ambaye hujui hata herufi zake zimeandikwaje huoni ni ajabu. Pili unahukumu eti katika tafsiri ya mtu. Kumbuka tafsiri ni mtu aonavyo yeye na sio watu wote waonavyo hivyo basi kuna hatari mahakama zikatawaliwa na mlongo mmoja. Na sio ndoa tu, utawala, ujirani na mengineo mengi je haya tufate kanisa linavyosema au uislamu unavyosema?

Kiufupi CCM naona imejitafutia kaa la moto la hili wamelipata. Waislamu wanakuwa kimya lakini linapotokea jambo kama hili huwa kitu kimoja. Dhambi ya ubaguzi wa dini ni mbaya na Tanzania itachafuka tukielekea huko ule kawaimbo wa amani utatoweka.

I'm sorry for you. That's only the thinking of a corrupt person. Kwa hiyo, Waislamu nchini wataunga mkono tu chama kitakachowaahidi Mahakama ya Kadhi na nchi kujiunga na OIC? Sasa mnaonyesha wazi kuwa mna udini!

Kuhusu 'grand corruption' kwani utaweza kupata 'proof' ya kitu bila ya kuwa na 'allegation' kuwa kitu fulani kinasemekana kutendeka? Na kitu ambacho Watanzania (including waumini wakereketwa wa dini mbalimbali) wamekuwa wakilaani ni kuona resources zetu zinatumiwa kwa manufaa ya wachahche na wengi wanabaki kwenye umaskini wa kutupwa.

Kwa hiyo, unataka kusema kwa 'proofs' zenu, Watanzania wanaishi kwenye neema kiasi cha kufanya viongozi wenu kutojihusisha na matatizo yanayowagusa Watanzania?
 
Last edited:
unajua ccm wanfanya watu kama sijui watoto, sijui mataahira? kama waliwa promise waislamu kuwa watawaanzisha mahakama ya kadhi basi seriali haina budi kuanzisha mahakama hiyo. Hii inaonesha jinsi gani viongozi wetu wa serikali walivyo wasanii. Usanii mtupu umewajaa. Mi nampongeza sana Mufti kwa kutoa msimamo kwa niaba ya Waislamu wote bila uoga. Ingawa mimi ni Mkistru, sioni ubaya wa kuanzishwa mahakama ya kadhi, wa sababu haitavuka mipaka na kufanya maamuzi ya kidini kwa wakatoliki. Mbona mahakam ya Kadhi ipo Zanzibar na hakuna malalamiko kutoka kwa dini nyingine?CCM kitu gani bwana. Asanteee Mheshimiwa Mufti Mkuu
 
Kwahiyo Tanzania ni Nchi yenu siyo? unaota kwelikweli? you are wishing will never materialize na utakufa na chuki zako, zaidi nakuombea uendelee kuishi miaka mingi nakusikia uchungu jinsi waislamu wanavyopeta ikiwemo hii ya mahakama, na mengine mengi ambayo masikio yako hayataki kusikia (ishi miaka 110 mungu ajaalie) ili majungu yawe mengi.
Usipandishe presha maalim,Mtanzania atabakia kuwa mTanzania awe muIslam au mKristo.
Hilo tulijue wazi.
Pili tumeishi kwa kuelewana na kuvumiliana kwa miongo mingi sana.Sasa, naona anaingia Iblisi wa kuwagonganisha waTanzania.
Iblisi huyo asipopigwa na kushindwa basi tutajilaumu sisi wenyewe.
Wa Tz waKristo kwa waIslam tumeoleana na kuelwana kwa miaka nenda rudi.
Hii ajenda ya Kadhi na Mahakama yake isiwe ndo kipaumbele cha kitaifa maana Taifa lina mambo na matatizo mazito zaidi.
Ujinga na umaskini lazima vipigwe vita na wote ili maisha bora yapatikane kwa waTanzania wote.
 
Nao wakristo waungane kuanzisha "mahakama zao kiroho ndani ya katiba"?Nchi hii itakuwaje?anyway siwalaumu ndugu zangu Waislam maana CCM na serikali yake iliwahaidi jambo hili na hata ikawekwa kwenye ilani yao ya uchaguzi,maskini haweakujua kama wanatapeliwa ili watoe kura kama ambavyo ahadi nyingi hewa zilizotolewa!
Bytheway lkn Waislam hawajachambua wazi wanakosa kitu gani kwenye sheria mama zilizopo tz hivi sasa hadi wanapigania mahakama ya kadhi?watapata ni ni ikianzishwa mahakama ya kadhi ambacho sasa hawapati?
ndugu unaoneka na udhaifu wa busara na elimu ya kilimwengu. hizo mahkama za kadhi wanazo dai waislamu hata UK zipo na zemeuhusiwa kisheria kufanya kazi. mahakama hizo , hazihukumu wahalifu ( wezi, majambazi,waporaji na makosa kama hayo). kazi yake ni kuangalia haki za kiislamu kwa wailsamu. katika masula ya ndoa , na urithi na mabo kama hayo. wakristo hawaoi mke zaidi ya mmoja. waislamu wanaruhusiwa kuoa mpaka wa nne. kwa hiyo kunakua na matatizo mengi ambayo sheria ya mahkama ya kawaida inakua tabu kuweka haki sawa.
 
Mufti huyo na wenzake BAKWATA wanategemea ruzuku kutoka CCM wataweza ?

Hakuna shughuli yoyote ya kiuchumi iwe ni shule, vyuo, hospitali, majengo, viwanja, wakfu, mfuko wa zaka na mengineyo kama hiyo ambao jamaa hao wameweza kuanzisha na kuiendeleza bali wao ni kula, kula, kula tu nani atawasikia.

Kabla hujazungumzia kibanzi kwenye jicho la CCM ndugu Mufti nakushauri uangalie jicho lako upya na yale ya wenzako kisha mtoe magogo yaliyoko machoni kwenu ndio muiandame CCM kuondoa banzi jichoni mwake.

BAKWATA iliyokuwa na kila sababu ya kujenga himaya ya Kiislamu yenye utajiri, nguvu za kisiasa, uwezo na mamlaka tosha nchini imechezea nafasi hiyo baada ya kugundua Wakatoliki walivyowapiku ile mbaya dakika ndio inaamka dakika za majeruhi?

Na CCM na serikali yao wajanja kama nini watawaambia subiri na wao kwa kuamini kwenye kauli kama ile ya 'Uislamu ni kusubiri' lakini bila kuangalia kusubiri katika mazingira gani wakaendelea kudanganywa tu watajikuta BAKWATA wote wanamfuata naibu mufti na mahakama ya kadhi wasiione.
Subiri kwa ahadi na mipango, sio subiri, subiri tu! Nini kinachoendelea jiulizeni kwanza? Mnapashwa, mnafahamishwa ? Au mnachukuliwa nyie ni maasubwirina tuu!!!

Ingelikuwa mimi Mufti natangaza mgomo baridi na kisha kuanza kuwarejelea Waislamu wanipe nguvu na nisitegemee nguvu ya kuazima ya CCM au chama chochote cha kisiasa au serikali yoyote ile iwayo. KIla dini na hasa kama hii ya Kiislamu bwana ina uwezo wa kujiendesha yenyewe na kuwa na maguvu tosha ili mradi viongozi wake wasiwe wezi na watu wa dhuluma tu eti!!!
 
ndugu unaoneka na udhaifu wa busara na elimu ya kilimwengu. hizo mahkama za kadhi wanazo dai waislamu hata UK zipo na zemeuhusiwa kisheria kufanya kazi. mahakama hizo , hazihukumu wahalifu ( wezi, majambazi,waporaji na makosa kama hayo). kazi yake ni kuangalia haki za kiislamu kwa wailsamu. katika masula ya ndoa , na urithi na mabo kama hayo. wakristo hawaoi mke zaidi ya mmoja. waislamu wanaruhusiwa kuoa mpaka wa nne. kwa hiyo kunakua na matatizo mengi ambayo sheria ya mahkama ya kawaida inakua tabu kuweka haki sawa.

Nani anazikataa Tanzania? Kinachokataliwa ni kuwa sehemu ya mfumo wa sheria mama. Serikali ilisharuhusu kila dini kuwa huru ili mradi hakuna kuvunja sheria. Ila Waislamu wanataka hii Mahakama ya Kadhi iwekwe kwenye Katiba... (na baadaye OIC..., na baadaye sharia...) etc. Huku kuwekwa kwenye Katiba ndiko kunakokataliwa. Kwani kipengele kinachotoa uhuru wa kuabudu kwa kila dini hakitoshi?
 
Hakuna kulazimisha katika dini, mimi nimekuwa muislamu baada ya kuwa na akili yangu...kwahiyo ntashukuru kama mwana wa mungu atfahamu haki ...hoja hapa si wewe uwe dini gani? ila kwanini wewe mkristo ujisikie vibaya kwa jambo ambalo halikuhusu..wivu, uchoyo, siasa kali au nini? hapo ndio nashindwa kuwaelewa wakristo?

NO!NO!NO! Kuchezea Katiba kunamhusu kila Mtanzania. Kuanzisha Mahakama ya Kadhi nje ya Katiba kunawahusu Waislamu.

Kwa hiyo, hata wewe ujue kitu gani unaongelea! Kuilazimisha serikali iweke Mahakama ya Kadhi kwenye mfumo wa sheria katika nchi ambayo serikali yake haiamini dini ni kuvunja Katiba/sheria mama!
 
hahaha, hii nchi ni ya wakristo na waislam pia, sijasema hii nchi ni ya wakristo peke yao. kwahiyo kama nchi hii ni ya kwetu sote, kwanini wengine wapewe nafasi ya kufanya mambo ya ndani ya dini yao kwenye selikali isiyokuwa na dini? pelekeni dini huko msikitini na kanisani, acheni selikali isiyokuwa na dini ifanye kazi yenu.

tatizo waislam huwa wanapenda kulazimisha mambo, hasa pale utakapowakatalia ndo wanaanza kulia na kutishia kujitoa muhanga. nakuambia hili suala tazamani kwa macho tu na someni tu kwenye magazetu na kuliongea tu mdomoni, HALITAKUJA LIFANYIKE TZ amini usiamini. ni hoja gani mnaihitaji tena?hamuoni mnachanganya dini kwenye selikali isokuwa na dini? ndo maana nasema hii nchi si ya kiislam wala kikristo, ni secular, haina dini. hivyo dini ni kanisani na msikitini. ukienda selikalini hakuna kuvaa shela lako la dini hapa.

tatizo waislam wanalalamika sana, ndo maana wanaishia tu kulalamika na watakuwa nyuma siku zote. walilalamika ati kwasababu wakristo wanaendelea sana na kujenga mashule, wanataka wapewe chuo chao nao,wakapewa cha morogoro, nacho ni sifuli hakina maendeleo yoyote, ni kama hamuna. shule zao ndo zinaongozwa kufeli kwasababu wanaiba nyota na kuwawangia watoto wanaopelekwa pale. watoto wao wanapatikana kichawichawi na kuishi kichawi ndo mana hawabarikiwi walio wengi. kufuga majini na kujiridhisha kuwa utaishi kwa kumwaga majini yapige chuma ulete kwa wakristo na waislam wasokuwa na uchawi mkali. mnaishia hapohapo, maendeleo duni. hadi maeneo yenu yanajulikana, manzese,magomeni, buguruni etc, hamjengi mnapanga na mtaendelea kuwa nyuma milele hadi muokoke. hahaha.

angalieni wakristo wanaomwabudu Mungu wa kweli, tunajenga mashule kibao tena yanayoongoza tz kufanya vizuri, watoto wetu wanaenda shule, tunajenga vyuo kila kukicha. maendeleo ni jadi yetu. angalia, vyuo vyetu tunaruhusu hata waislam kuja kusoma, nyie kule morogoro mnafundhisha magaidi tu. ndo maana mko frustrated muda wote, na sura zenu zinabadilika kuwa kama wakatiliiii, hadi mnatisha kama mnakula watu. nakuambia ukiwa huko maofisini hasa sehemu ya public, muislam mwenye msimamo mkali akija tu unamfahamu hata bila kujitambulisha, utafikiri anakula watu. kama yule mufti wao, na mashehe wooote hakika wako hivyohivyo. MTANDAO WETU TUMEUKAMATA, tunauponda kila siku kwa Jina la Yesu, uchawi wenu utanyong'onyea wenyewewe hadi mtakula mawe. subirini. Maombi yetu Kwa Jina la Yesu yanafanya kazi. nyie wenyewe mnalijua hilo, hadi mtakapookoka na kuacha dini ya ajabu hiyo.
 
Mtizamo mpana wa jambo hili unaweza kukupa picha mbili tofauti zinazokinzana.

Kwanza, ni picha kuwa suala la mahakama ya Kadhi kwa waislamu ni la lazima na CCM ililigundua hilo ndio maana mwaka 2005 ikawa gia kubwa ya kupandia mlima wa uchaguzi.

Tuelewe jambo moja kuwa, ilani ya uchaguzi Tanzania kwa vyama vyetu haiandaliwi na mgombea bali chama kupitia sekretarieti yake.Hivyo Kikwete kama wagombea wengine waliomtangulia alibebeshwa ilani iliyoandaliwa na chama akaitekeleze.

Linapokuja suala la kutekeleza ilani ya uchaguzi mwenye nguvu siyo chama bali serikali.Kikwete anachafanya ni kuangalia katika ilani mambo ya kutekeleza na yapi ayape kipaumbele cha kwanza.

Kigugumizi kinachoonekana kwa Kikwete katika kutekeleza suala la mahakama ya Kadhi ni kutokana na utashi wake na namna alivyokwisha kusoma mambo yalivyo uraiani.Kumbukeni kuwa kila alifanyalo Rais linachangia kesho yake uongozini kwenye jumba jeupe.

Mara nyingi viongozi wetu wanatuteka kwa ahadi nyingi za mabo mengi mazuri nasisi tunawapa kra zetu wakifika waendako wanatugeuzia kibao.Hili ndilo lililotokea kwa waislamu na ahadi ya mahakama ya kadhi.

Tusiikatae CCM kwa hili la mahakama ya kadhi tu bali TUKATAE KUFUNGWA SANDA KIUNONI TUKADANGANYWA NI MSULI NA KITENGE
 
Back
Top Bottom