Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

Mbona Dawa Ndogo Sana kwa hili jambo!

Wape mahakama yao, 60% ya waislamu Tanzania watabadilisha dini.
 
Mbona Dawa Ndogo Sana kwa hili jambo!

Wape mahakama yao, 60% ya waislamu Tanzania watabadilisha dini.

Napenda hii. Nani atakubali kikwata mikono, kisa mwislamu. Si bora kuozea lupango ukiwa na viungo vyako vyote, na kanzu ushaitupa!
 
Tatizo si kuwa na mahakama tatizo ni kudhalilishwa na kuonewa waislamu. Mzee Mwanakijiji kuhusu alleged grand corruption cases ni still allegation hakuna substance wala proof katika hilo bali ni accusations tu.

Sasa Mufti ni msomi hawezi kukurupuka tu na kudai fulani ni fisadi pasina kuwa na vielelezo (kumbuka uislamu unataka mtu atuhumiwe kwa vielelezo na sio watu fulani wanamhisi kuwa yeye ni fisadi wengine ni chuki zao binafsi au hasidi zimewatala)

Tukija katika swala la Kadhi hii sio mahakama tu bali mfumo mzima wa maisha ya waislamu. Ni ajabu kama si kichekesho eti sharia za kiislamu ziweke katika mahakama ya circular. Utahukumu vipi kuhusu ndoa wewe hakimu ambaye hujui hata herufi zake zimeandikwaje huoni ni ajabu. Pili unahukumu eti katika tafsiri ya mtu. Kumbuka tafsiri ni mtu aonavyo yeye na sio watu wote waonavyo hivyo basi kuna hatari mahakama zikatawaliwa na mlongo mmoja. Na sio ndoa tu, utawala, ujirani na mengineo mengi je haya tufate kanisa linavyosema au uislamu unavyosema?

Kiufupi CCM naona imejitafutia kaa la moto la hili wamelipata. Waislamu wanakuwa kimya lakini linapotokea jambo kama hili huwa kitu kimoja. Dhambi ya ubaguzi wa dini ni mbaya na Tanzania itachafuka tukielekea huko ule kawaimbo wa amani utatoweka.
 
Sekenke,

Mkuu sasas wewe unaanza udini na kupotosha watu. Mahakama ya kadhi haihusiani kabisa na hukumu za makosa ya jinai Pleasee!.

Kisha kibaya zaidi ktk mjadala huu wamejaa wakristu wasiojua Uislaam ni kitu gani.. acheni waislaam wenyewe tujibu hoja hizi badala ya kutoia majibu yenu huku mmeshika Biblia mikononi.
Mtazame Mwanakijiji ambaye watu kibao wanamuamini humu anakuja na swala ya kuona kama swala hili ni Muhimu kwa Waislaam kuliko yote yanayozungumzwa, utafikiri huwa anapiga kelele yeye peke yake na kanisa lake..Wao, wao...them, them - ndio hoja yake ya msingi!

Mkuu Mwanakijiji, hawa ni Viongozi wa dini na wanawakilisha waumini wa dini, hii ndiyo kazi yao kidini sii kuingilia Siasa ambazo hawana hata hzihusiani na dini wala hawana elimu nayo..Ikiwa Mapadre wenu wanaingilia Siasa hata ktk maswala yasiyohusiana na ibada zenu hiyo ni Ukristu wenu, usitake kuwavuta waislaam pia kuiga yanayopfanywa na Wakristu. Mufti akiingilia siasa hizi basi jua anazungumza kama raia mwninge na anaweza kuja hapa kijiweni kama Mkandara!

Wanabodi,
Nitarudia kusema hivi siku zote HOJA hujibiwa na HOJA ikiwa mnapingana na huyu Mufti njooni na hoja inayoweza kuivunja nguvu hoja ya huyu Mufti lakini kuingia hapa na Gear zenu za Ukristu mnaonekana wapuuzi tu..Hivi akili zetu hukoma kufikiri inapofikia maswala ya dini jamani?
Utafikiri mnamjua yesu kuliko yesu mwenyewe! Looh - salaaaala!

Kuna makosa mengi kayasema huyu Mufti na mtazamo wake umekingwa na vumbi kiasi kwamba anatakiwa kuelimishwa zaidi..Na sii kuja na hoja zilizojaa pumba zaidi ya Mufti mwenyewe.

Hakuna Sura wala sheria yoyote inayosema ni lazima Muislaam jina, ndiye atoe hukumu ya kesi za madai..hasa ktk nchi ambayo Waislaam wanaoana na Wakristu. Hayo madai ya kwamba Mkristu hawezi kumhumu Muislaam ni opofu mkubwa sana kwa sababu kama kweli yeye ni Muislaam safi na madai yake yanafuata elimu yake ya dini basi bila shaka hata mahakama za jinai angepinga hukumu zake! hukumu zake hazilingani wala kufanana na Uislaam, tofauti ya mahakama hizi mbili ni uzito wa kesi zenyewe tu lakini wanaohukumiwa ni pamoja na waislaam...Hivyo basi ni ujinga kukubali hukumu za mahakama moja ukapinga mahakama nyingine tena ndogo zaidi yenye maswala madogo ya madai.

Waislaam wengi hawawezi kumsikiliza mjinga huyu wala kufuata ushauri wake..namwita mjinga kwa sababu hafahamu Utawala na kikubwa zaidi kama Mufti ameshindwa kutazama WATU, MAZINGIRA na Elimu dunia kuwa kigezo kikubwa cha hotuba yake. Ni hawa hawa wajinga wanaofanya waislaam tanzania wanafunga mwqezi wa Ramadhan siku mbili tofauti kwa sababu tu ati mwezi haukuonekana Dodoma au Dar.. Wangejua kwamba huku Canada kuna sehemu inaitwa Yellow Knife Jua huwepo miezi sita bila usiku wa kiza na wakati mwingine Usiku kwa miezi sita vile vile, sijui wao watafunga vipi Ramadhani ikiwa sababu ni kuuona mwezi, hiyo sayansi ya miaka ya nabii Nuhu..Kisha basi Sayansi ambayo ina justify maelezo mengi ya Kuran inaonyesha wazi kwamba dunia nzima tofauti yetu ni kwa masaa 24 tu..Ikiwa na maana hatupishani kwa siku nzima,sasa kwa nini nchi zifunge Ramadhan siku mbili tofauti..

Kisha basi kiibaya zaidi ni kwamba siku ya Idd Hajj sisi hatuongezi ziku moja zaidi wala kusali tofauti na Saudia..Why tuna sababu gani ya kukatiza kufikia Al Hajj lakini tunakataa siku ya mwezi wa Ramnadhan na siku ya Idd El fitr!.. Hawa mai Mufti wa kuchalkiwa na CCM hiyo hiyo!

Wakuu zangu watu kama hawa tuachieni sisi, tunawajua vizuri sana kwamba hawa ni Wanafiki wa Dini, huwezi kuihusisha dini ktk siasa kwa sababu ya Mahakama ya kadhi ambayo hata sisi waislaam wengine tunaona ni kupotosha..

Matatizo yote mnayotaka kuyashughulikia hayana sheria kwa Waislaam zaidi ya kubakia vitabuni. waislaam wanaoa wake bila sababu za msingi na wafungishaji ni hawa hawa Ma Mufti!, Waislaam wanaoa nje ya dini zao, wanazaa nje ya ndoa zao, watoto waliozaliwa mnawaita wana haramu na kuwanyima Urithi..hivi kweli mtaweza kutoa haki kwa wahusika!

Hapana, nasema hapana kwa mahakama ya Kadhi, hatuihitaji ila tunahitaji sheria ziundwe kuwabana wazazi wanaowanyanyasa wake na watoto ktk ndoa na mirathi..Sheria ambazo zinaweza chukua yaliyo bora toka ktk Uislaam na mengine nje ya Uislaam kwa sababu tunachotaka zaidi sisi wananchi Waislaam ni kulinda haki za victims kama hawa watoto mnaowaita haramu, wake mnaowaita Mistress na kadhalika kwa sababu tu ndoa haikufungwa kufuata misngi ya Kiislaam au Kikristu..Sheria ambayo inakuwa msumeno kwa yeyote yule atakaye tumia dini kama kisingizio cha kufanya ayatakayo kinyume cha ustaarabu...
 
Last edited:
Mkandara,

Sasa huko nyuma tulikuwa tunapishana sijui wapi. Nimesoma hadi naanza kupata wasiwasi kama ni wewe umeandika au kosa ni langu huko nyuma nilikuwa sikuelewi/ulikua hueleweki. Nakiri kuwa sasa nimekuelewa na nakiri kuwa unaongelea swala moja muhimu sana. Ila bado naona hili inabidi lihukumiwe katika mahakama za kawaida. Mtoto HARAMU akiachwa pembeni, basi zipimwe DNA (kama mtoto wa Omary Mahita) na ikigundulika kuwa ni mtoto wake, basi jamaa abebeshwe ghalama na ikibidi faini juu kwa kumtelekeza mtoto wake huyo.

Mengineyo kakubaliana kuwa BAKWATA kweli wana utata. Huo ni kama umoja wa CCM ila kwa Waislam vile .....
 
Sikonge,
Msimamo wangu ni ule ule haujabadilika.. Sikubaliani na mahakama ya kadhi toka siku ya kwanza, ila kuna sheria za kiislaam ktk maswala ya madai zinaweza kutumika kwa faida ya wanawake na watoto hasa tukizingatia kwamba wenye imani na Uislaam na Asilia huoa wake zaidi ya mmoja na kuza watoto wasiokuwa na hesabu ktk ndoa tofauti wakati mmoja..

Tunaweza jenga sheria ya kati inayovuta mazuri ya Uislaam yakatumika kwa wale wenye kufuata misingi ya kiislaam ama kiasili..Na huu sio mwisho tunaweza vuta mengine toka nje ya Uislaam pale panapohitajika suluhu inayoppingana na Uislaam lakini wananchi waislaam wanaitumia dhidi ya wanawake na watoto kinyume cha mafundisho ya dini yoyote ile.. Hapa tunatafuta middle ground, kila kitu hakiwezi kuwa black or White ni muhimu kutazama lia gray areas ambazo zinatujumuisha sote kama society moja..

Swala la DNA sio solution, Muislaam unaweza kumlea mtoto sii wake na akawa mwanao na mwenye haki sawa na watoto wako bila maandishi...kuna mambo mengi sana mkuu wangu ambayo siwezi ku cover yote..Kumbuka hadi sasa hivi tunavyozungumza hatuna sheria moja ktk maswala mazito ya madai hasa mirathi na haki za wanawake..Mara nyingi tunafuata sheria za nchi za magharibi ambazo zinakumbatia zaidi Ukristu na ndio maana waislaam wamejkuja na hoja hii ya mahakama ya kadhi..
Mimi sikubaliani nayo kwa sababu Siii waislaam wala Wakristu wanafuata sheria za dini yao ktk matendo yao. Kuwahukumu ni kuwaonea, inatakiwa kwanza tuweze kuwa na mpango madhubuti wa ndoa hizi na nafasi ya watoto ktk familia moja kisha hapo ndipo tunaweza kujenga solution inayoweza kutumika ikiwa tatizo moja limetokea..Hawa masheikh ndio wanaotuharibu kisha leo wanataka kutuletea mahakama ambayo ni ulaji kwao..They care less about religion na mafundisho yake.
Hatuwezi kujenga sheria moja mahakamani hata kidogo kwa sababu katiba yetu haina mtu mmoja ktk maswala haya, inatakiwa ku cover sisi sote pamoja na imani zetu hivyo solution itatokana na ndoa hiyo liyofungwa.. iwe mke mmoja, wawili, wanne, vimada na kadhalika..
Sheria za kiislaam pekee haziwezi kuondoa adha na matatizo ya waislaam ikiwa chanzo cha matatizo haya ni waislaam au niseme viongozi wenyewe wa dini..
 
Last edited:
Mambo yote mengine ambayo sisi tunayapigia kelele hayawafanyi wao kuichukia CCM; yaani yote yaliyofanyika dhidi ya nchi yetu na utajiri wetu wao hayawagusi wala kuwataka waumini wao kuyafanya ya kisiasa na kuiadhibu CCM; yaani yote hayo hayajafikia kiwango cha kuwakera.. isipokuwa hili moja tu?
asante sana mkuu na hayo ndio maajabu ya viongozi wa dini zetu.sasa inamaana ccm wakirekkebisha hilo tu wapewe kura? swala dogo sana hilo kwa ccm kwa kuataka kura.kama wanaweza kutoa rushwa kupata kura watashindwa kuwapa pendekezo lao hili wapate kura?
 
Mambo yote mengine ambayo sisi tunayapigia kelele hayawafanyi wao kuichukia CCM; yaani yote yaliyofanyika dhidi ya nchi yetu na utajiri wetu wao hayawagusi wala kuwataka waumini wao kuyafanya ya kisiasa na kuiadhibu CCM; yaani yote hayo hayajafikia kiwango cha kuwakera.. isipokuwa hili moja tu?

Unazungumzia mambo mabaya ambayo Nyerere aliwafanyia Waislamu?
 
asante sana mkuu na hayo ndio maajabu ya viongozi wa dini zetu.sasa inamaana ccm wakirekkebisha hilo tu wapewe kura? swala dogo sana hilo kwa ccm kwa kuataka kura.kama wanaweza kutoa rushwa kupata kura watashindwa kuwapa pendekezo lao hili wapate kura?

There are two things in our job. Criticism i accept with respect. Disrespect i dont accept and dont respect" - Arsene Wenger.
 
Sijui kama ni sahihi kabisa kusema CCM nadio ina makosa, kuna watu ndani ya CCM ndio tatizo, japokuwa wanaiwakilisha CCM, kuna uwezekano wa kuwaondoa hao wabovu mafisadi na walaghai, na chama kikaendelea vizuri kabisa. Lakini at least hata watu wa dini wameanza kufahamu ukweli wa mambo!!
 
Mambo yote mengine ambayo sisi tunayapigia kelele hayawafanyi wao kuichukia CCM; yaani yote yaliyofanyika dhidi ya nchi yetu na utajiri wetu wao hayawagusi wala kuwataka waumini wao kuyafanya ya kisiasa na kuiadhibu CCM; yaani yote hayo hayajafikia kiwango cha kuwakera.. isipokuwa hili moja tu?
.
NDIO!

Mufti hakuna kurudi nyuma!
 
Ngoma ndio inaanza kupigwa anayeweza aingie na acheze...suala hilo zito sana sana waangalie lisije likaleta machafuko na mpasuko...haya amani yetu tu tusije kuipoteza
.
Kama noma naiwe noma potelea mbali na ivunjike amani.
.
MUFTI UKO SAWA
.
Katika hili umewaunganisha waislam. Hii ndio bakwata
Inayo hitajiwa na waislam.
 
Last edited:
Waisilamu wanahaki ya kupiga kelele kwani ni kweli kwenye ilani ya CCM walisema Mahakama ya kadhi itakuwepo, ila CCM imewapiga mchanga wa macho.

Ila kuna kunahaja shekh mkuu akaangalia ni ahadi ngapi watanzania tupewa changa la macho, maisha bora, utawala wa sheria, je ni waisilamu wangapi wako mahabusu miaka nenda rudi bila kesi zao kusikilizwa.
Je ni waisilamu wangapi wanakufa kwa kukosa huduma za afya.
je ni waisilamu wangapi wapo shule na hakuna elimu bora.
Je ni waisilamu wangapi wanakufa kwa madawa ya kulevya yanayouzwa na vigogo.

Je ni waisilamu wangapi wameathirika na wizi wa EPA, Richmond< Meremeta deepGreen nk.
Haya yote na mengine mengi ndio nilitegemea shekh mkuu angeyafanya kama sababu za kutoichagua CCM.

Wakishindwa kuwa wa kweli kwa wanayoyaahidi hawawezi kutimiza wanayowapaka nayo mafuta, CCM imegundua ina deal na mandondocha hivyo hawajali kesho Kikwete atakuja msikitini atawashika mkono kesho yake wote mnabadili kauli na kuonekana mtu mzima......
Kama kweli basi kidedea mpaka kieleweke tena kwa yote mpaka Rostam aende keko kama Juma na Omari.
 
Mkandara anasema tumjibu Mufti kwa hoja. Zilizotolewa umeona ni vioja? Haya angalia hizi:

  • Mufti anadai Sheria ya Ndoa ya 1970 imewanyima Waislamu haki. Hakuweza kueleza kwani hakielezeki. Si kweli. Na kama ingekuwa kweli basi angesema kipengele husika ni kipi ili kiangaliwe.
  • Mufti kasema Waislamu wanataka mahakama ya kushughulikia mirathi na ndoa. Nani kawanyima kuanzisha? Si lazima iwe sehemu ya serikali.
  • Mufti kasema Waislamu wanapashwa kuwa na mahakama yao kama wafanyabiashara walivyo na mahakama yao. Yaani anataka kusema Waislamu ni kikundi tu kama kilivyo kikundi cha wafanyabiashara? Anawakosea haki Waislamu.
 
Tatizo si kuwa na mahakama tatizo ni kudhalilishwa na kuonewa waislamu. Mzee Mwanakijiji kuhusu alleged grand corruption cases ni still allegation hakuna substance wala proof katika hilo bali ni accusations tu.

Mdondoaji ni kipi hicho unachodondoa jamani mbona ulichoandika kimekaa kaa vibaya hivyo? YAANI UNASEMA ISSUES ZA EPA, RICHMOND, MEREMETA, TANGOLD, DEEP GREEN NA ZINGINE HAZINA PROOF? Did you mean what you wrote au keyboard ilikosa ushirikiano? Kama you meant what you wrote then you have to think twice kwani you could be in a wrong forum I suppose.
 
Hoja ya msingi ni kwamba Waislamu wamekosa demokrasia ndani ya taasisi zao kwa kile tunaita kimombo co-option of few islamic leaders by Government.Taasisi za kikristu kama vile Tanzania Episcopol Council na nyinginezo huwa haziingiliwi na serikali, lakini inapokuja swala zima la uchaguzi ndani ya taasisi za kiislam, serikali ina ingilia(influence) na ndio maana Wapo wanao mkubal sheikh Mkuu na wasiomkubali ndani ya sheikh mkuu. Kwa hiyo hoja ya msingi nikuangalia demokrasia ndani ya taasis za kiislam. Kwa mfano ndani ya kanisa la lutherani (KKT) kumekuwa kunafukuta sehemu mbali mbali kama vile upareni, meru n.k, sababu kubwa utafiti ulibainisha kuwa ni mgawanyo wa rasilimali. Fukuto kubwa ndani ya uisilamu husababishwa na ukosefu wa demokrasia ndani ya taasisi hizo because for some reasons the government does not want the muslims to collectivelly pick the leadership they want. Kwa hiyo hili swala ni lazima litizamwe upya ili lipatiwe ufumbuzi. Wakati civil war inaanza watu huwa hawatangazi ila ilalipuka tu. utasikia tu , fujo mwembe chai, fujo za kkt upareni, vijana wakiislamu wakizuia wazee kuingia misikitini, wakulima wakichinjana na wafugaji, chuo kikuu hakukaliki n.k.
 
Back
Top Bottom