Hotuba nzito na muhimu ya Mufti Shekh Abubakar Zubeir

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,209
4,706
HOTUBA MZITO NA MUHIMU YA MUFTI SHEKH ABUBAKAR ZUBEIR

Kutoka Ukurasa wa Sheikh Ibrahim Ghulaam

Asema BAKWATA ndiyo mama wa Taasisi zote za Kiislamu nchini

Taarifa kwa hisani ya Harith Nkussa
Mwandishi maalumu wa Mufti

đź”·Ofisi ya Mufti yawataka Viongozi wa taasisi za kiislamu kote nchini na waislamu wote kuisikiliza mpaka mwisho, waiandike na kufanyia kazi vipengele vyote vya hotuba hiyo.

âś” Akariri, BAKWATA ndiyo taasisi mama inayosimamia waislamu na taasisi zao zote pasina kujali makundi au madhehebu yao kisha ataja sababu.

✔Akiri kuna taasisi nyingi za kiislamu ambazo zinafanya vizuri kwenye maeneo fulani, lakini asisitiza kuwa zote hizo zinafanya kazi chini ya mwamvuli wa Bakwata.

✔Akariri wito kwa wasomi wa kada mbalimbali na waislamu wote kuleta maoni, fikra mpya na ushauri kwa lengo la kuleta maendeleo kwa waislamu na kwamba milango ya BAKWATA iko wazi muda wote. Awataka waislamu watumie fursa hiyo badala ya kulalamika, kunungunika au kusemea pembemi

âś” Akumbusha kuwa kazi ya BAKWATA ni kuwatumikia waislamu wote na taasisi zao zote na madhehebu yao yote na kwamba BAKWATA sasa inatimiza wajibu na jukumu lake hilo kikamilifu na kwamba inawasahilishia waislamu na kamwe haimkwamishi yeyote kutimiza wajibu wake

âś” Aonya desturi mbaya ya kuwaona masheikh hawakusoma. asisitiza masheikh ni wasomi muhimu sana wenye akili na wanaoona mbali sana na kuwataka masheikh wasikubali kudharaulika kwa hali yoyote.

âś” Awahimiza masheikh kusoma elimu za kisekula ikiwa ni pamoja na lugha mbalimbali. awaambia hakuna ugumu wowote.

âś” Apongeza ushirikishwaji wa viongozi wa Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine kwenye kazi na shughuli za kimaendeleo za kiislamu. Apongeza sana mchamgo wa wadau hao.
 
Attachments

  • 1698311927838.jpg
    1698311927838.jpg
    9.9 KB · Views: 3
Bakwata iliundwa na Nyerere kwa lengo la kufifisha uislam na waislam baada ya kuvunja taasisi ya maana zaidi,uchaguzi wa mufti askari kanzu kibao,Kuna shughuli ya bakwata 1990s ilifadhiliwa na kanisa,bakwata Mali za wakfu inauza..kwa nini waislam waamini bakwata!?.. waislam waliunda chombo kingine miaka ya tisini,Baraza kuu..Hilo ndiyo mama wa taasisi za kiislam,Kama anabisha tuitishe kura ya maoni
 
Umeiweka sawa kabisa
 
Ninachojua CCT,Bakwata na TEC zimeundwa kwa sheria moja.Je Nyerere alikuwa na nia ya kufifisha ukatoriki na uprotestant kwa kutumia mabaraza haya?

Sent from my Nokia 2.4 using JamiiForums mobile app
 
Asalaaam Aleykhum warahmatullah Wabarakatul...!

Ni vizuri tuheshimu mamlaka iliyo juu na uzuri zaidi Mufti amesema kama kuna wenye maoni wayapeleke vizuri tu na atayafanyia kazi
 
Bakwata iliundwa na Nyerere kwa lengo la kufifisha uislam na waislam baada ya kuvunja taasisi ya maana zaidi,uchaguzi wa mufti askari kanzu kibao,Kuna shughuli ya bakwata 1990s ilifadhiliwa na kanisa,bakwata Mali za wakfu inauza..kwa nini waislam waamini bakwata!?.. waislam waliunda chombo kingine miaka ya tisini,Baraza kuu..Hilo ndiyo mama wa taasisi za kiislam,Kama anabisha tuitishe kura ya maoni

Wewe mjukuu wa mzee side kaa kutulia,taasisi na jumuia za kiislam nchini ziko chini ya mwamvuli bakwata.

Bila kusahau bakwata ni tawi la kijani kama ilivyo uwt.
 
Hawana lolote hao vibaraka wa serikali.
BAKWATA haisimamii maslahi ya Waislam bali dola, sisi sio wajinga.
Nitawaunga mkono pindi watakapobadilika ila sio sasa.

Nipo tayari kumsikiliza Sheikh Ponda sio Sheikh Mkuu.

Kumbe nyie wengine mko against mamlaka ya nchi,sajilini viwe vyama vya siasa ijulikane moja.
 
Point ya 2&3 kutoka mwisho zinakinzana,hii inadhihirisha wazi mashehe wengi ni felia.
 
Sawa ila mamlaka inayowatambulisha na kuwawakilisha waislam hapa nchini ni bakwata,uzuri bakwata inawakaribisha nyote kujenga jumuia bora ya kiislam tanzania.
Sawa lia , ila bakwata ni tawi la kanisa, na hili sasa hivi wengi wamelijua
Likidhihirika serikali itapata shida sana
 
Back
Top Bottom