Mufti ataka waislam kuomba mvua

Mufti ataka waislam kuomba mvua

Mufti ana elim ya darasa la ngapi? Kuna sekondari aliyopitia?
 
Namkumbuka mshenzi mmoja alisema anakwenda kuomba mvua thailand atuletee bongo
 
We unataka mvua inyeshe ili iwe nn? Kama ni kilimo mmetumiaje hadi sasa mabonde ya mito kibao yaliyopo nchini. Hii nchi inapenda sana kudeka. Ingekuwa jangwa kama Saudia au Libya sijui wangefanyaje. Labda wangekesha kila siku wanaomba mvua
Mkuu hali haiko sawa hata kiada mvua huwa mpaka sasa inakuwa inanyesha kwa Dar lakini mwaka huu kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea na uwezo wako wa kufikiri. Mungu kawapa mito na mabonde kibao wao badala ya kujiongeza wanaitana wakaombe mvua.

Sasa huko jangwani kama Niger au Saudia kusiko na mvua wafanyeje? Si watakesha kila siku muda wote usiku na mchana kuomba mvua. Wambie hao jamaa waache ujinga hamna sababu ya kuomba mvua waende rufiji, malagarasi, pangank n.k wakalime. Sio wanajibanza hapo Dar wanaomba mvua.
Wakulima wa Tz bado hawana uwezo wa kilimo cha Umwagilaji hiki kilimo kinafanywa na wawekezaji na baadhi ya wakulima wenye uwezo hapa Tz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ANATAKA SIFA HUYO MBONA WENZAKE WAPO KIMYA MUISLAM BAKWATA
 
MUFTI WACHUKUE WASANII MNAZI MMOJA UOMBE NAO MVUA USISAHAU NA KUNDI LAKO LA BAKWATA
 
Hii Swalatu yaitwa " Swalatu istisqa'a." hata Nabii Musa AS aliswali yeye na Qawmu yake !!
Panakuwa na uhaba wa mvua na kipindi kuchelewa!! Basi watakiwa uombe kwa Mwenyezzi Mungu... Nae hujibu kwa haraka ombi Hilo..
Allahu ye3lam !!
MUFTI WACHUKUE WASANII MNAZI MMOJA UOMBE NAO MVUA USISAHAU NA KUNDI LAKO LA BAKWATA


Kwanini Dua isisomwe Ijumaa na hiyo "kunuti" iwe Jumapili? wasipofanya hivyo watakuwa wanataniana na mungu wao kwani siku rasmi kwa waislam ni Ijumaa
 
Hii Swalatu yaitwa " Swalatu istisqa'a." hata Nabii Musa AS aliswali yeye na Qawmu yake !!
Panakuwa na uhaba wa mvua na kipindi kuchelewa!! Basi watakiwa uombe kwa Mwenyezzi Mungu... Nae hujibu kwa haraka ombi Hilo..
Allahu ye3lam !!

Ina maana hapo Mwenyezi Mungu anakuwa hajajua kama kuna sehemu mvua haijanyesha mpaka akumbushwe ndio inyeshe!?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mamlaka ya hali ya hewa wameshasema mvua zinarudi mwezi wa nne!... timing ya hii dua imekaa strategically mwisho wa mwezi kuelekea muda ambao mvua zitarudi... Anyway maendeleo hayana dini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mufti sheikh Abubakar Zubeir amewataka waislamu kote nchini kufanya swala maalum ya kuomba mvua za heri

mufti amewataka waislamu wa taasisi na madhehebu yote nchini kuungana na kuhudhuria kwenye Dua hiyo ya kitaifa itakayofanywa viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Jumapili saa moja na nusu Asubuhi 24/3/2019.

Mufti amewataka viongozi wa taasisi zote za kiislamu, viongozi wa mikoa yote, wilaya na kata zote nchini kuipa umuhimu mkubwa na kufanya juu chini kuandaa swala hiyo siku hiyohiyo.

Amewataka maimamu wote nchini kuomba dua ya Kunuti kwenye swala ya Ijumaa hii kumuomba Mwenyeezi Mungu aliepushe taifa na janga la ukame pamoja na mafuriko.

Kwa upande wake sheikh wa mkoa wa Dar es salaa. Alhadi Musa Salum amesema maandalizi yote kwa ajili ya swala hiyo kitaifa yamekamilika na kuwataka waislamu wa jiji hilo kufurika kumlilia Mwenyeezi Mungu kwa unyenyekevu.

Akawataka masheikh wa wilaya za mkoa huo na masheikh wa kata na maimamu wote kuwajulisha na kuwahamaaisha waislamu pamoja na kuongoza ujio wao kwenye swala hiyo
..............

Courtesy : Sheikh Hassan Chizenga
Katibu Baraza la Ulamaa.
........., .........

Harith Nkussa
Mwandishi maalum wa mufti
Alhamisi 21/3/19
Ofisi ya mufti. Lumumba Str. DSMView attachment 1050706

Sent using Jamii Forums mobile app
Unafiki mtupu, atawasikiliza shetani tu na wala si Mungu. kama huwezi kukemea kuuawa watu, basi wewe hufai kuwa Mufti, labda Mufti wa Ubwabwa!
 
Back
Top Bottom