As Salafiyyu91
JF-Expert Member
- Jan 11, 2014
- 2,537
- 2,544
Mufti sheikh Abubakar Zubeir amewataka waislamu kote nchini kufanya swala maalum ya kuomba mvua za heri
mufti amewataka waislamu wa taasisi na madhehebu yote nchini kuungana na kuhudhuria kwenye Dua hiyo ya kitaifa itakayofanywa viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Jumapili saa moja na nusu Asubuhi 24/3/2019.
Mufti amewataka viongozi wa taasisi zote za kiislamu, viongozi wa mikoa yote, wilaya na kata zote nchini kuipa umuhimu mkubwa na kufanya juu chini kuandaa swala hiyo siku hiyohiyo.
Amewataka maimamu wote nchini kuomba dua ya Kunuti kwenye swala ya Ijumaa hii kumuomba Mwenyeezi Mungu aliepushe taifa na janga la ukame pamoja na mafuriko.
Kwa upande wake sheikh wa mkoa wa Dar es salaa. Alhadi Musa Salum amesema maandalizi yote kwa ajili ya swala hiyo kitaifa yamekamilika na kuwataka waislamu wa jiji hilo kufurika kumlilia Mwenyeezi Mungu kwa unyenyekevu.
Akawataka masheikh wa wilaya za mkoa huo na masheikh wa kata na maimamu wote kuwajulisha na kuwahamaaisha waislamu pamoja na kuongoza ujio wao kwenye swala hiyo
..............
Courtesy : Sheikh Hassan Chizenga
Katibu Baraza la Ulamaa.
........., .........
Harith Nkussa
Mwandishi maalum wa mufti
Alhamisi 21/3/19
Ofisi ya mufti. Lumumba Str. DSM
Sent using Jamii Forums mobile app