Mufti aagiza BAKWATA kuchunguza Mali zake zote zinazomilikiwa na Watu binafsi Kinyume cha Sheria

Katibu mkuu wa Bakwata Alhaj Mruma amesema Mufti wa Tanzania Shehe Abubakar ameagiza ufanyike Uchunguzi kubaini mali zote za Bakwata, zilipo na uhalali wa umiliki wake

Alhaj Mruma amesema Bakwata ina mali nyingi sana zikiwemo zinazomilikiwa na Watu binafsi Kinyume cha Sheria

Baada ya uchunguzi itaandaliwa orodha ya mali zote za Waislamu

Chanzo: ITV habari
bakwata kazi yake kuuza viwanja majumba ya waqf
 
View attachment 2489631
Moja ya mali za Waislam shule iliyojengwa Dodoma na EAMWS
Hii EAMWS pamoja na nia njema waliyokuwa nayo waanzilishi wake, yapo makosa waliyoyafanya ambayo hata bila kuingiliwa na serikali wangekuja kusambaratishana wenyewe.

Huwezi kuwaweka waislam wa shia, sunni, khoja... chini ya chombo kimoja ukataraji watadumu chini ya chombo hicho kwa utulivu miaka yote.
 
Gagnija,
EAMWS ilikuwapo toka 1945 bila ya matatizo.

Hapakuwa na suala la madhebu.

Tatizo lilijitokeza pale EAMWS ilipokuwa sasa inajenga Chuo Kikuu Cha Waislam.

Kuna watu hili liliwatia hofu wakaamua lazima EAMWS ipigwe marufuku.
 
Ni 'kitengo' kilichoanzishwa na huyo wa kwenye avatar yako ili kudhibiti waislam,si unaona hapo kavunja taasisi ya maana ya waislam (eamws) kaanzisha taasisi Koko kufubaza maendeleo ya waislam,uchaguzi wa mufti bakwata watu wa makumbusho huwa mpela mpela kuhakikisha anaingia mtu anayeaminika

Acha kumhusisa JKN na upuuzi wa waganga njaa.
 
Gagnija,
EAMWS ilikuwapo toka 1945 bila ya matatizo.

Hapakuwa na suala la madhebu.

Tatizo lilijitokeza pale EAMWS ilipokuwa sasa inajenga Chuo Kikuu Cha Waislam.

Kuna watu hili liliwatia hofu wakaamua lazima EAMWS ipigwe marufuku.

Mzee acha kupotosha kwa upuuzi wako,vyuo vya kiisalmu dunia hii mbona vipi vingi hata morogoro kipo mlipewa ila mmebakiza majungu na kuchapa fimbo wanafunzi kama wapo madrasa.
 
Katibu mkuu wa Bakwata Alhaj Mruma amesema Mufti wa Tanzania Shehe Abubakar ameagiza ufanyike Uchunguzi kubaini mali zote za Bakwata, zilipo na uhalali wa umiliki wake

Alhaj Mruma amesema Bakwata ina mali nyingi sana zikiwemo zinazomilikiwa na Watu binafsi Kinyume cha Sheria

Baada ya uchunguzi itaandaliwa orodha ya mali zote za Waislamu

Chanzo: ITV habari
Dr. Bashiru yupo Idle sana apewe hii kazi huyu ni ndugu yetu katika imani na ana uzoefu kwenye ukaguzi wa mali za ccm
 
KUPIGWA MARUFUKU EAMWS NA KUUNDWA KWA BAKWATA 1968

Baada ya kuundwa BAKWATA, ili kuondoa wasiwasi na kuwarudishia imani Waislam, Katibu wa Tume ya Waislam, Mussa Kwikima alitoa taarifa iliyosema:

‘’Hakuna anaeweza kutishia kuwepo kwa EAMWS isipokuwa wanachama wake, sheria na serikali, lakini si watu binafsi hata ikiwa mikoa yote 17 ikijitoa haitamaananisha kuwa EAMWS imekufa kwa kuwa kuwepo kwake hakutokani na kuwepo kwa mikoa hiyo kama wanachama isipokuwa kuwepo kwa wanachama wake, Waislam.’’

Wakati ilipotoka taarifa hii BAKWATA ilikuwa bado haijaandikishwa rasmi na Msajili wa Vyama.

Kisheria ilikuwa haiwezekani kwa kundi la Adam Nasibu kuunda jumiya mpya iliyokuwa na malengo sawa na jumuiya ambayo tayari ishaandikishwa.

Kwa muda wa siku tatu BAKWATA na EAMWS zikawepo kwa wakati mmoja.

Ilionekana kama kwamba EAMWS itashinda vitimbi vya serikali na vya kundi la Adam Nasibu.

Tarehe 19 Desemba, 1968 serikali kama vile imegutushwa na taarifa ya Kwikima, iliipa BAKWATA ''Cerificate of Exemption,'' na kuifungia EAMWS.

Waziri wa Mambo ya Ndani Said Ali Maswanya kwa niaba ya serikali alitoa taarifa fupi:

‘’Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.

Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao.

Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo hilo.

Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.

Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.

Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.

Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali ya Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.

Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kuchukua mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe.

Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu.

BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.

Hivi ndivyo halikadhalika moto wa Waislam uliowashwa kwa kupatikana kwa uhuru waliopigania hadi ukapatikana ulivyokufa.

Moto huu ulikuja ukawaka tena, lakini hiki ni kisa kingine.

Insha Allah Mwenyezi Mungu akipenda tutakuja kukieleza.
 
Nant...
Kwa nini unaniuliza swali hili?
Anglican wamepewa shule waliyojenga Kikuyu, leo ni chuo chao kikuu cha Mt John.

Kwanini nanyi msidai shule yenu mliyojenga Dodoma na madai mengine mliyonayo? Japo sina hakika ombi lenu likiridhiwa atakabidhiwa nani.

Taarifa nilizonazo shule ya Dodoma uliyoiweka kwenye picha ilijengwa na Agha Khan.
 
EAMWS agha Khan ndani,alikua muweka hazina sijui, waislam wote walikua kitu kimoja, Julius akaona akiwaacha kanisa halitafika kanaani
 
Hiyo shule iliyojengwa na waislam Dodoma ipo hadi leo. Kama Anglican walipewa iliyokuwa Kikuyu ambayo leo ndiyo St John university, basi na waislam wapewe shule yao.
Hahaha, hebu taja shule zenu hata 5 nchi hii na uwe na uhakika nazo

Mngekuwa na shule zenu Akina J.M Kikwete na Lipumba wangesoma Christian Seminaries mpaka wabadilishe na majina?

Kama Ilboru, Pugu, Mringa, Azania na zinginezo zingeendelea kuwa za kikristo na kusajili Wanafunzi wa Kikristo tu....nakuambia kwa hakika mngebaki nyuma sanaa kuliko sasa

Mlipaswa kumshukuru Nyerere aliyeamua kuzitaifisha wakasoma wanafunzi wa dini zote, ila ninyi hamna Shukurani kabisa
 
Back
Top Bottom