Mufti aagiza BAKWATA kuchunguza Mali zake zote zinazomilikiwa na Watu binafsi Kinyume cha Sheria

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,036
Katibu mkuu wa Bakwata Alhaj Mruma amesema Mufti wa Tanzania Shehe Abubakar ameagiza ufanyike Uchunguzi kubaini mali zote za Bakwata, zilipo na uhalali wa umiliki wake.

Alhaj Mruma amesema Bakwata ina mali nyingi sana zikiwemo zinazomilikiwa na Watu binafsi Kinyume cha Sheria.

Baada ya uchunguzi itaandaliwa orodha ya mali zote za Waislamu.

Chanzo: ITV habari
 
Katibu mkuu wa Bakwata Alhaj Mruma amesema Mufti wa Tanzania Shehe Abubakar ameagiza ufanyike Uchunguzi kubaini mali zote za Bakwata, zilipo na uhalali wa umiliki wake

Alhaj Mruma amesema Bakwata ina mali nyingi sana zikiwemo zinazomilikiwa na Watu binafsi Kinyume cha Sheria

Baada ya uchunguzi itaandaliwa orodha ya mali zote za Waislamu

Chanzo: ITV habari
John...
Umenigusa sana kwa kuweka hapa JF taarifa inayohusu, ''Mali za BAKWATA.''
Nimeona ninawajibika lau kwa uchache kueleza kuhusu historia ya hizo mali za BAKWATA.

Nakuweka kipande kidogo kutoka kitabu cha Abdul Sykes ili ikiwa hujui upate uelewa wa mali hizo zilichumwa vipi na vipi zikaja kumilikiwa na BAKWATA na sasa baada ya zaidi ya nusu karne mali hizo zimegeuka kuwa mpata mpatae.

KUPIGWA MARUFUKU EAMWS NA KUUNDWA KWA BAKWATA 1968

Baada ya kuundwa BAKWATA, ili kuondoa wasiwasi na kuwarudishia imani Waislam, Katibu wa Tume ya Waislam, Mussa Kwikima alitoa taarifa iliyosema:

‘’Hakuna anaeweza kutishia kuwepo kwa EAMWS isipokuwa wanachama wake, sheria na serikali, lakini si watu binafsi hata ikiwa mikoa yote 17 ikijitoa haitamaananisha kuwa EAMWS imekufa kwa kuwa kuwepo kwake hakutokani na kuwepo kwa mikoa hiyo kama wanachama isipokuwa kuwepo kwa wanachama wake, Waislam.’’

Wakati ilipotoka taarifa hii BAKWATA ilikuwa bado haijaandikishwa rasmi na Msajili wa Vyama.

Kisheria ilikuwa haiwezekani kwa kundi la Adam Nasibu kuunda jumiya mpya iliyokuwa na malengo sawa na jumuiya ambayo tayari ishaandikishwa.

Kwa muda wa siku tatu BAKWATA na EAMWS zikawepo kwa wakati mmoja. Ilionekana kama kwamba EAMWS itashinda vitimbi vya serikali na vya kundi la Adam Nasibu.

Tarehe 19 Desemba, 1968 serikali kama vile imegutushwa na taarifa ya Kwikima, iliipa BAKWATA ''Cerificate of Exemption,'' na kuifungia EAMWS.Waziri wa Mambo ya Ndani Said Ali Maswanya kwa niaba ya serikali alitoa taarifa fupi:

‘’Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.

Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao.

Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo hilo.

Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.

Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.

Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.

Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali ya Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.

Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kuchukua mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe.

Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu.

BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.

Hivi ndivyo halikadhalika moto wa Waislam uliowashwa kwa kupatikana kwa uhuru waliopigania hadi ukapatikana ulivyokufa.

Moto huu ulikuja ukawaka tena, lakini hiki ni kisa kingine.
Insha Allah Mwenyezi Mungu akipenda tutakuja kukieleza.

1674277528918.png

Moja ya mali za Waislam shule iliyojengwa Dodoma na EAMWS
1674277611709.png

Siku Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipoweka jiwe la msingi la Chuo Kikuu Cha Waislam Chang'ombe kilichokuwa kinajengwa na EAMWS mwaka wa 1968.

Kushoto ni Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akimkaribisha Rais wa Tanzania Julius Nyerere kulia na katikati ni Rais wa Tawi la EAMWS Tewa Said Tewa.​
 
John...
Umenigusa sana kwa kuweka hapa JF taarifa inayohusu, ''Mali za BAKWATA.''
Nimeona ninawajibika lau kwa uchache kueleza kuhusu historia ya hizo mali za BAKWATA.

Nakuweka kipande kidogo kutoka kitabu cha Abdul Sykes ili ikiwa hujui upate uelewa wa mali hizo zilichumwa vipi na vipi zikaja kumilikiwa na BAKWATA na sasa baada ya zaidi ya nusu karne mali hizo zimegeuka kuwa mpata mpatae.

KUPIGWA MARUFUKU EAMWS NA KUUNDWA KWA BAKWATA 1968

Baada ya kuundwa BAKWATA, ili kuondoa wasiwasi na kuwarudishia imani Waislam, Katibu wa Tume ya Waislam, Mussa Kwikima alitoa taarifa iliyosema:

‘’Hakuna anaeweza kutishia kuwepo kwa EAMWS isipokuwa wanachama wake, sheria na serikali, lakini si watu binafsi hata ikiwa mikoa yote 17 ikijitoa haitamaananisha kuwa EAMWS imekufa kwa kuwa kuwepo kwake hakutokani na kuwepo kwa mikoa hiyo kama wanachama isipokuwa kuwepo kwa wanachama wake, Waislam.’’

Wakati ilipotoka taarifa hii BAKWATA ilikuwa bado haijaandikishwa rasmi na Msajili wa Vyama.

Kisheria ilikuwa haiwezekani kwa kundi la Adam Nasibu kuunda jumiya mpya iliyokuwa na malengo sawa na jumuiya ambayo tayari ishaandikishwa.

Kwa muda wa siku tatu BAKWATA na EAMWS zikawepo kwa wakati mmoja. Ilionekana kama kwamba EAMWS itashinda vitimbi vya serikali na vya kundi la Adam Nasibu.

Tarehe 19 Desemba, 1968 serikali kama vile imegutushwa na taarifa ya Kwikima, iliipa BAKWATA ''Cerificate of Exemption,'' na kuifungia EAMWS.Waziri wa Mambo ya Ndani Said Ali Maswanya kwa niaba ya serikali alitoa taarifa fupi:

‘’Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.

Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao.

Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo hilo.

Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.

Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.

Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.

Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali ya Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.

Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kuchukua mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe.

Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu.

BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.

Hivi ndivyo halikadhalika moto wa Waislam uliowashwa kwa kupatikana kwa uhuru waliopigania hadi ukapatikana ulivyokufa.

Moto huu ulikuja ukawaka tena, lakini hiki ni kisa kingine.
Insha Allah Mwenyezi Mungu akipenda tutakuja kukieleza.
Ahsante mkuu kwa hii Elimu murua kabisa!
 
Katibu mkuu wa Bakwata Alhaj Mruma amesema Mufti wa Tanzania Shehe Abubakar ameagiza ufanyike Uchunguzi kubaini mali zote za Bakwata, zilipo na uhalali wa umiliki wake

Alhaj Mruma amesema Bakwata ina mali nyingi sana zikiwemo zinazomilikiwa na Watu binafsi Kinyume cha Sheria

Baada ya uchunguzi itaandaliwa orodha ya mali zote za Waislamu

Chanzo: ITV habari
Wabongo walivyo ukimtaoti kwenye mrija wa utafunani utadikia nimehamia " SHIA"
 
Bakwata ni tawi la ccm kama ilivyo uvccm,hakuna waisalmu bali ni mashehe ubwabwa wamejazana humo.
Ni 'kitengo' kilichoanzishwa na huyo wa kwenye avatar yako ili kudhibiti waislam,si unaona hapo kavunja taasisi ya maana ya waislam (eamws) kaanzisha taasisi Koko kufubaza maendeleo ya waislam,uchaguzi wa mufti bakwata watu wa makumbusho huwa mpela mpela kuhakikisha anaingia mtu anayeaminika
 
Back
Top Bottom