sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Umenikumbusha mbali sana.Niliwahi kuleta hapa hii maada takribani miezi miwili iliyopita ila mnisamehe bure nilisahahu kuleta mrejesho
Walimu wanamsingizia kiuonevu mwanangu, je ni hatua gani nichukue kama mzazi?
Ipo hivi, mwanangu anasoma shule fulani English medium, mimi haya mambo ya schoolbus niliyakataa kabisa maana kuna wenzake wengi tu wanatembea na hata mimi baba yake siijui school bus maisha yangu ya elimu, ila pia niliona atembee tu ili kunyoosha miguu kwa afya yake. Sasa pale shuleni kwao...www.jamiiforums.com
kiufupi niliitwa shuleni kama mzazi mimi pamoja na wazazi wengine, mwanangu wakimsingizia kushawishi watoto zao waache kupanda schoolbus wawe wanatembea kama mwanangu na wenzake wachache wasiopanda school bus.
Naweza kusema kesi niliishinda kirahisi mno, maana hata watoto hao wanaodhaniwa wanashawishiwa kutopanda school bus, walikiri hawajashawishiwa ila ni wao tu hawataki kupanda school bus, wao wanataka wawe wanatembea.
Licha ya hivyo wazazi walifuka na kukandia hasara za kutopanda schoolbus, point zao zilikuwa ni usalama wa watoto, watoto kuwahi kufika shule, watoto kufika shuleni wakiwa hawajachoka, nk.
Mimi point yangu ya kwanza ilikuwa kama mwanangu hajawashawishi watoto wao wasipande school bus ila ni wenyewe tu wanataka kumwiga mwanangu je mwanangu anahusikaje
Kiufupi nilianza kutiririka sababu za mimi kuamua mtoto wangu kutopanda school bus ( ghaama ya school bus kwangu sio tatizo kabisa)
1. Afya ya mtoto huimarika kwa kufanya zoezi la kutembea, umbali wa nyumbani hadi shuleni ni dakika kama 20 tu kwa mwendo wa kawaida kabisa, mara chache chache mimi au mke wangu tunampa lifti ya gari tunapoenda kwenye shughuli zetu
2. Kuna mamilioni ya watoto wa shule za msingi hasa za serikali huwa wanatembea kwenda shuleni, shida iko wapi mwanangu kambatana na wenzake kwenye kutembea, kuna shule ipo karibu yao ni ya serikali, wenzake wengi tu huwa wanakutana njiani na hakuna tatizo.
3. Kwa sasa naweza nikawa na uwezo wa kulipia hiyo school bus, ila hali yangu ya kiuchumi ikibadilika mtoto wangu atapata shida.
hizo ndizo zilikuwa sababu zangu, ila zaidi ya hapo, kuna mtoto flani anajiamini sana hana uwoga akaelezea sababu zake
Yeye kwa niaba ya wenzake alisema walikuwa wanapenda wanavyoona mtoto wangu pamoja na wenzake wachache wasiopanda school bus pale wakitoka shuleni, kuna shule karibu sana ya serikali kuna uwanja wa mpira, hapo huwa wakitoka shuleni wanapata nafasi ya kujumuika na wenzao wa hio shule wanacheza na kujumuika na watoto wa shule hio ya kata, si mnajua tena watoto wanavyopenda kucheza.
Lakini pia hapo uwanjani wanapokutana na watoto wengine, mwanangu na rafiki yake aliemzidi darasa moja ambae nae hapandi school bus, walijifunza sarakasi kadhaa na hata mimi nikiri tu kwamba kipaji cha sarakasi cha mwanangu si haba, sasa wakirudi hio shule yao wakianza kuruka ruka hizo sarakasi wenzao wanakusanyika kushangaa, hii nayo ndio ikawa inapelekea nao wengine kugoma
Kiufupi sababu ndizo zilikuwa hizo, lakini licha ya hivyo wazazi waliona watoto wao bado ni wadogo sana waliokuwa wakiongea utoto mwingi n.k kwa hio waliwakataza kabisa watoto zao kurudia tena kuibua upya haya mambo.
Leo nimeandika hii maada baada ya mtoto flani kuwa kiburi na kutaka kufosi nae asiwe anapanda school bus, wazazi wake wanamtandika sana lakini ikifika mida ya kutoka anakwepa school busila watoto bwana.
ni hayo tu ndugu zangu
haya sasa, mtu anaona anampa mateso mtoto kutembea mita chache tuUmenikumbusha mbali sana.
Tulikua tunatembea almost 10km per day
mtoto usimpe kila kitu na wala usimnyime kila kitu, hio ndio kauli yanguVitu vingine kweli ni kujiendekeza,mi pia mtoto wangu anatembea tu baada ya kubadilishiwa ratiba ya school bus kuwekewa sa 12 kasoro. Saizi anaamka saa 12 na nusu kwa raha zake. Mwanzoni alikua anaona kama hatumpendi ila saizi humwambii kitu anaona school bus miyeyusho maana yeye anafika home nusu saa au lisaa ndio school bus inapita kushusha. Siku mojamoja namsindikiza nikijiskia kumpa kampani tunapiga mastory njia nzima maana kurudi kwangu night kali washalala. Na actually ni kama mwendo wa dakika 15 hadi 20. Vitu vingine tunajiendekeza.
Watatekwaa huyo mkeo ni limbukeni tuNdoa yangu itavunjikankwa ajili ya watoto mke hataki watoto watembee shule iko km 1.2 toka home watoto wamenenepa ...mwaka unaisha sasa anawapeleka kwa gari anaogopa salaam geti watatekwa asahi mijasho na wanachoka .....anayetaka mrejesho artichoke January 17 nawatakia mapuNziko mema ya mwisho wa mwaka ....
Ni sahihi mkuu Sky soldiermtoto usimpe kila kitu na wala usimnyime kila kitu, hio ndio kauli yangu
Hata sijui school bus hufananaje. Kule kwetu kijijini hakuna. Maisha yetu ni mguu to and flow. Halafu kwapani kuna daftari zangu na mgongoni nimening'iniza mpira wa kushonwa kwa matambara.Vitu vingine kweli ni kujiendekeza,mi pia mtoto wangu anatembea tu baada ya kubadilishiwa ratiba ya school bus kuwekewa sa 12 kasoro. Saizi anaamka saa 12 na nusu kwa raha zake. Mwanzoni alikua anaona kama hatumpendi ila saizi humwambii kitu anaona school bus miyeyusho maana yeye anafika home nusu saa au lisaa ndio school bus inapita kushusha. Siku mojamoja namsindikiza nikijiskia kumpa kampani tunapiga mastory njia nzima maana kurudi kwangu night kali washalala. Na actually ni kama mwendo wa dakika 15 hadi 20. Vitu vingine tunajiendekeza.
Mwanamke ana tabia ya kumlinda sana mtoto.Ndoa yangu itavunjikankwa ajili ya watoto mke hataki watoto watembee shule iko km 1.2 toka home watoto wamenenepa ...mwaka unaisha sasa anawapeleka kwa gari anaogopa salaam geti watatekwa asahi mijasho na wanachoka .....anayetaka mrejesho artichoke January 17 nawatakia mapuNziko mema ya mwisho wa mwaka ....
Wanawake wapo very insecured na over protective, mbaya zaidi ni kazi sana mwanamke peke yake kumkuza mvulana kuwa mwanaume,Watatekwaa huyo mkeo ni limbukeni tu
Mastory gani mnapiga na dogo? 🤣🤣Vitu vingine kweli ni kujiendekeza,mi pia mtoto wangu anatembea tu baada ya kubadilishiwa ratiba ya school bus kuwekewa sa 12 kasoro. Saizi anaamka saa 12 na nusu kwa raha zake. Mwanzoni alikua anaona kama hatumpendi ila saizi humwambii kitu anaona school bus miyeyusho maana yeye anafika home nusu saa au lisaa ndio school bus inapita kushusha. Siku mojamoja namsindikiza nikijiskia kumpa kampani tunapiga mastory njia nzima maana kurudi kwangu night kali washalala. Na actually ni kama mwendo wa dakika 15 hadi 20. Vitu vingine tunajiendekeza.
Wanawake wapo very insecured na over protective, mbaya zaidi ni kazi sana mwanamke peke yake kumkuza mvulana kuwa mwanaume,
Hahahaaa mastori mengi si unajua ukiwa na dogo yeye ndo anakuuliza maswali unajibu na kutoa maelezo kana kwamba ye ndo bossMastory gani mnapiga na dogo? 🤣🤣