Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,840
35,844
Mwendelezo huu wa manung'uniko ya watu dhidi ya yanayojiri, ni dalili ya mkwamo kamili kwenye jitihada zetu za kudai haki. Alikuwepo mzee wa Kiraracha(RIP) akisema sera zake ni siri. Mikakati yetu ya ukombozi nayo ni siri? Viongozi wa vyama vyetu kazi zao au majukumu yao katika kutuvusha ni nini?

Ni vipi tunawapa dhamana viongozi hawa na ili wafanye nini? Haya ni mambo ya kuangaziwa vilivyo sasa na bila ajizi. Muda wa kuzifanya chaguzi zetu kuanzia vyamani na hata kwa nchi kuwa wazi zaidi ni sasa. Washindanishwe watu wote wenye kujidhania wanafaa kama inavyokuwa kwa beberu Biden. Tunahitaji watu walio bora si bora watu.

Watuambie mikakati yao na watakavyotuvusha. Kutuletea hadithi za kuwa umekosa watanzania wa kukuunga mkono, itoshe kuwa hati rasmi na halali ya wewe na timu yako kujiuzuru. Ama kwa hakika tumewavumilia sana. Tusingependa tufikie kwenye kunyang'anyana uongozi kikuku. Vyama hivi si mali binafsi. Wenye uwezo wa kuviongoza wapo. Hayupo mwenye hati miliki.

Habari hii iwafikie wote kutokea Lumumba hadi kwa Hashim Rungwe kokote kule aliko. Kwamba mmeshindwa kuwaunganisha watu kudai haki zao, mmeshindwa kazi tokeni madarakani. Madarakani si kwa ajili ya kulamba asali peke yake.

Habari ndiyo hiyo.
 
..wazo zuri zaidi ni kuanzisha chama kipya.

..kufanya mapinduzi ktk vyama is more time consuming.

..kwanini mtu asitumie muda na rasilimali kuwatetea wananchi badala ya kugombana na kupinduana na Hashim Rungwe, James Mbatia, na wengine?
 
Kuanzisha vyama ni kuwachanganya wananchi. Vyama hivi tumevipigania sote hadi kuvifikisha hapa vilipo.

Kipi tunachoomba kilicho kinyume cha utaratibu:

"Iko wapi mikakati ya ukombozi? Iko wapi mikakati ya kutuvusha?"

Kwanini isiwe asiye na majibu hapo hatufai aingie mwenye majibu?

Ninakazia hivi vyama si mali binafsi.
 
Umoja Party inawasubiri

Karibuni

Tunaamini kuwa uanaharakati ndiyo njia pekee ya kutuvusha:

Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi

Umoja party anayaweza hayo?

Tulipo tunayaweza na masomo tunayo:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Bila uanaharakati walamba asali muache vipi kutusokomeza Tozo na kukiuka haki zetu?

Habari za umoja party ni kujaribu kutupoteza maboya.

Hatudanganyiki!

Tutabanana hapa hapa.
 
Heading yako inataka mapinduzi lakini nikisoma content yako unataka chaguzi vyamani ziwe wazi, hapa umeniacha gizani sijui haswa unalenga nini.

Ila kuhusu huu mkwamo unaouzungumzia, mimi binafsi naona ni kama second chance imepatikana ya kutafuta plan B.

Huu mkwamo umetuletea swali, vipi wale waliokuwa wakitegemewa kutusemea kila siku wanapoamua kunyamaza, what's next?

Pia badala ya kuendelea kulalamika kutaka kubadilisha uongozi ili tupate "wasemaji" wetu wapya, sisi kwanza lazima tujue mipango yetu ni ipi?

Nionavyo, kwa hii tabia yetu ya ukimya hata wakija hao viongozi wapya kutusemea, bado tutakuwa wazito wa kuchukua hatua.

Kumbuka wao wanaongoza tu, lakini wananchi ndio tunatakiwa kuwa watu wa vitendo zaidi ili kuleta mabadiliko, hili tumeliona nchi zote mfano wa karibu ni Sri Lanka.
 
Kuanzisha vyama ni kuwachanganya wananchi. Vyama hivi tumevipigania sote hadi kuvifikisha hapa vilipo.

Kipi tunachoomba kilicho kinyume cha utaratibu:

"Iko wapi mikakati ya ukombozi? Iko wapi mikakati ya kutuvusha?"

Kwanini isiwe asiye na majibu hapo hatufai aingie mwenye majibu?

Ninakazia hivi vyama si mali binafsi.

..sasa hapo unakuwa 50/50

..wewe unaweza kuona waliopo hawana majibu, wenzako wakaona waliopo wana majibu.

..ndio maana nasema ni vizuri kuhamasisha wenzako ambao mnaendana kimisimamo ili muanzishe chama kipya kitakachosukuma ajenda yenu.

..zaidi ningependa kukumbusha kwamba hali mbaya ya kiuchumi kisiasa na kijamii imetokana na utawala mbovu wa Ccm na sera zake.

..Ccm ndio wenye serikali hivyo wanawajibika kutatua shida na changamoto za wananchi.
 
Heading yako inataka mapinduzi lakini nikisoma content yako unataka chaguzi vyamani ziwe wazi, hapa umeniacha gizani sijui haswa unalenga nini.

Ila kuhusu huu mkwamo unaouzungumzia, mimi binafsi naona ni kama second chance imepatikana ya kutafuta plan B.

Huu mkwamo umetuletea swali, vipi wale waliokuwa wakitegemewa kutusemea kila siku wanapoamua kunyamaza, what's next?

Pia badala ya kuendelea kulalamika kutaka kubadilisha uongozi ili tupate "wasemaji" wetu wapya, sisi kwanza lazima tujue mipango yetu ni ipi?

Nionavyo, kwa hii tabia yetu ya ukimya hata wakija hao viongozi wapya kutusemea, bado tutakuwa wazito wa kuchukua hatua.

Kumbuka wao wanaongoza tu, lakini wananchi ndio tunatakiwa kuwa watu wa vitendo zaidi ili kuleta mabadiliko, hili tumeliona nchi zote mfano wa karibu ni Sri Lanka.

Kiswahili ni kifinyu. Mapinduzi ni kwa maana halisi ya neno transformation. Ikiwa na maana ya uhitaji wa mageuzi makubwa vyamani.

Yanahitajika mageuzi makubwa yenye kulenga uwajibikaji. Ifahamike nini wajibu wa kila mtu (kiongozi na mwanachama) ili mtu ajue wazi kama yuko anapostahili.

"Tunataka mikakati ya ukombozi. Tunataka mikakati ya kutuvusha."

Si sahihi sana kudhani kuwa wananchi wamejitenga na viongozi kiasi cha awaye yote kupongezwa kwa kujikalia kimya dhidi ya anaowaongoza.

Anayetuongoza hana option ya kukaa kimya. Wenye shughuli ni sisi. Kwa vile wenye kutuvusha wapo wengi, yakikuzidi na utoke tu vinginevyo tutakufurusha unceremoniously.

Uwazi kwenye chaguzi hilo ni jambo jingine muhimu litakalohakikisha kutokea awali kila wanaotaka uongozi wanajua fika uzito na wajibu wa wanachokitaka.

Mapinduzi haya yataweka wazi kuwa mwenye chama ni nani na hayupo aliye indispensable.

Wenye shughuli ni sisi lakini bila mikakati rasmi ya chama hayupo atakayechukua hatua kwa vitendo. Inatakikana mikakati ya wazi. Mfano majibu kwa maswali hapa yanapaswa kuwepo:

IMG_20220823_134516_288.jpg
 
Kikosi Kazi ndo kinawakwamisha Chadema kwani kinavyozidi kuchukua muda chadema washindwa kuja na hoja juu yetu tunaokutana na Ndugu TOZO.
Lakini haya ni ya muda tu
 
..sasa hapo unakuwa 50/50

..wewe unaweza kuona waliopo hawana majibu, wenzako wakaona waliopo wana majibu.

..ndio maana nasema ni vizuri kuhamasisha wenzako ambao mnaendana kimisimamo ili muanzishe chama kipya kitakachosukuma ajenda yenu.

..zaidi ningependa kukumbusha kwamba hali mbaya ya kiuchumi kisiasa na kijamii imetokana na utawala mbovu wa Ccm na sera zake.

..Ccm ndio wenye serikali hivyo wanawajibika kutatua shida na changamoto za wananchi.

Kwamba naweza kuona hawana majibu kumbe wanayo? Kwani majibu ni siri? Haya si ndiyo ya sera za Mrema basi?

Au wewe unayo majibu ya maswali matatu haya yaliyopo hadharani tangia mwaka jana?

IMG_20220823_134516_288.jpg

Tukubaliane kuwa vyama hivi havina mwenyewe. Tumevipigania sote na kwa muda mwingi tu. Hivyo si sahihi kutokujibu hoja au kujificha kwenye chagizo za kama vipi wengine kwenda kuunda vyama vipya.

Kwanini isiwe sahihi kufanya mageuzi kwa kushawishiana kwa hoja?

Wewe unaona viongozi tuliowapa dhamana ya kutuvusha ni sahihi kukaa kimya kama vile hawapo huku wakitutegemea sisi kumwagika barabarani bila kuwepo mkakati wowote?

CCM ni walamba asali. Kutatua shida ina maana waache kulamba asali. Ajitemeshe vipi huyu tonge mdomoni?
 
Mwendelezo huu wa manung'uniko ya watu dhidi ya yanayojiri, ni dalili ya mkwamo kamili kwenye jitihada zetu za kudai haki. Alikuwepo mzee wa Kiraracha(RIP) akisema sera zake ni siri. Mikakati yetu ya ukombozi nayo ni siri? Viongozi wa vyama vyetu kazi zao au majukumu yao katika kutuvusha ni nini?

Ni vipi tunawapa dhamana viongozi hawa na ili wafanye nini? Haya ni mambo ya kuangaziwa vilivyo sasa na bila ajizi. Muda wa kuzifanya chaguzi zetu kuanzia vyamani na hata kwa nchi kuwa wazi zaidi ni sasa. Washindanishwe watu wote wenye kujidhania wanafaa kama inavyokuwa kwa beberu Biden. Tunahitaji watu walio bora si bora watu.

Watuambie mikakati yao na watakavyotuvusha. Kutuletea hadithi za kuwa umekosa watanzania wa kukuunga mkono, itoshe kuwa hati rasmi na halali ya wewe na timu yako kujiuzuru. Ama kwa hakika tumewavumilia sana. Tusingependa tufikie kwenye kunyang'anyana uongozi kikuku. Vyama hivi si mali binafsi. Wenye uwezo wa kuviongoza wapo. Hayupo mwenye hati miliki.

Habari hii iwafikie wote kutokea Lumumba hadi kwa Hashim Rungwe kokote kule aliko. Kwamba mmeshindwa kuwaunganisha watu kudai haki zao, mmeshindwa kazi tokeni madarakani. Madarakani si kwa ajili ya kulamba asali peke yake.

Habari ndiyo hiyo.
Naona mkuu umeamua kuwa chambua waswahili wanasema “kuwachamba”
 
Ila ni wazo zuri ulilo nalo japo litaleta ukakasi kutekelezeka kuanzia chama tawala[ CCM ] na vyama vyote vya upinzani.
 
Naona mkuu umeamua kuwa chambua waswahili wanasema “kuwachamba”

Haipo namna. Hawana mkakati na eti wanataka mikakati wawe nayo watu mtaani huku wao wakilamba asali:

1. Mkakati wa ukombozi uko wapi?
2. Mkakati wa kuwashirikisha wote wenye nia ya kutuunga mkono uko wapi?
3. Vipi wahanga wetu kwenye ukombozi tunawafidia vipi?

Hata matatu haya kimya. Ila visingizio: watanzania wamejikita kwenye yasiyo na tija? Aaah wapi?

Kwa uongozi upi kwani?

Si watupishe waone?
 
Mwendelezo huu wa manung'uniko ya watu dhidi ya yanayojiri, ni dalili ya mkwamo kamili kwenye jitihada zetu za kudai haki. Alikuwepo mzee wa Kiraracha(RIP) akisema sera zake ni siri. Mikakati yetu ya ukombozi nayo ni siri? Viongozi wa vyama vyetu kazi zao au majukumu yao katika kutuvusha ni nini?

Ni vipi tunawapa dhamana viongozi hawa na ili wafanye nini? Haya ni mambo ya kuangaziwa vilivyo sasa na bila ajizi. Muda wa kuzifanya chaguzi zetu kuanzia vyamani na hata kwa nchi kuwa wazi zaidi ni sasa. Washindanishwe watu wote wenye kujidhania wanafaa kama inavyokuwa kwa beberu Biden. Tunahitaji watu walio bora si bora watu.

Watuambie mikakati yao na watakavyotuvusha. Kutuletea hadithi za kuwa umekosa watanzania wa kukuunga mkono, itoshe kuwa hati rasmi na halali ya wewe na timu yako kujiuzuru. Ama kwa hakika tumewavumilia sana. Tusingependa tufikie kwenye kunyang'anyana uongozi kikuku. Vyama hivi si mali binafsi. Wenye uwezo wa kuviongoza wapo. Hayupo mwenye hati miliki.

Habari hii iwafikie wote kutokea Lumumba hadi kwa Hashim Rungwe kokote kule aliko. Kwamba mmeshindwa kuwaunganisha watu kudai haki zao, mmeshindwa kazi tokeni madarakani. Madarakani si kwa ajili ya kulamba asali peke yake.

Habari ndiyo hiyo.
Mwarobaini wa haya yote uliyo ya zungumza mkuu ni :-
i, Uwanzishwaji wa vyama vipya vya kisiasa vilivyo imara na vilivyo na sera dhabiti zilizo wazi na vinavyo endeshwa kwa misingi ya kidemokrasia ya kweli na sio demokrasia maigizo.

ii, Ugombea binafsi [ mgombea binafsi ] aliye na sera dhabiti za kutuvusha hapa tulipo.
 
Haipo namna. Hawana mkakati na eti wanataka mikakati wawe nayo watu mtaani huku wao wakilamba asali:

1. Mkakati wa ukombozi uko wapi?
2. Mkakati wa kuwashirikisha wote wenye nia ya kutuunga mkono uko wapi?
3. Vipi wahanga wetu kwenye ukombozi tunawafidia vipi?

Hata matatu haya kimya. Ila visingizio: watanzania wamejikita kwenye yasiyo na tija? Aaah wapi?

Kwa uongozi upi kwani?

Si watupishe waone?
Ni kweli kabisa kwa unacho zungumza hakija tekelezwa na vyama vyote vya siasa hapa nchini.
 
Kwamba naweza kuona hawana majibu kumbe wanayo? Kwani majibu ni siri? Haya si ndiyo ya sera za Mrema basi?

Au wewe unayo majibu ya maswali matatu haya yaliyopo hadharani tangia mwaka jana?

View attachment 2333627

Tukubaliane kuwa vyama hivi havina mwenyewe. Tumevipigania sote na kwa muda mwingi tu. Hivyo si sahihi kutokujibu hoja au kujificha kwenye chagizo za kama vipi wengine kwenda kuunda vyama vipya.

Kwanini isiwe sahihi kufanya mageuzi kwa kushawishiana kwa hoja?

Wewe unaona viongozi tuliowapa dhamana ya kutuvusha ni sahihi kukaa kimya kama vile hawapo huku wakitutegemea sisi kumwagika barabarani bila kuwepo mkakati wowote?

CCM ni walamba asali. Kutatua shida ina maana waache kulamba asali. Ajitemeshe vipi huyu tonge mdomoni?

..nimezungumzia mabadiliko ya uongozi kwa njia ya uchaguzi ktk vyama.

..nimesema uchaguzi sio njia ya uhakika, ni suala la 50/50; kwamba, unaweza kupata viongozi wenye dira unayoitaka au usiwapate.

..njia ya uhakika zaidi ya kupata unayoyatamani ni kuanzisha chama kipya huku ukiwaunganisha watu wenye misimamo, mitizamo, na dira ya mabadiliko unayoipendekeza.
 
Heading yako inataka mapinduzi lakini nikisoma content yako unataka chaguzi vyamani ziwe wazi, hapa umeniacha gizani sijui haswa unalenga nini.

Ila kuhusu huu mkwamo unaouzungumzia, mimi binafsi naona ni kama second chance imepatikana ya kutafuta plan B.

Huu mkwamo umetuletea swali, vipi wale waliokuwa wakitegemewa kutusemea kila siku wanapoamua kunyamaza, what's next?

Pia badala ya kuendelea kulalamika kutaka kubadilisha uongozi ili tupate "wasemaji" wetu wapya, sisi kwanza lazima tujue mipango yetu ni ipi?

Nionavyo, kwa hii tabia yetu ya ukimya hata wakija hao viongozi wapya kutusemea, bado tutakuwa wazito wa kuchukua hatua.

Kumbuka wao wanaongoza tu, lakini wananchi ndio tunatakiwa kuwa watu wa vitendo zaidi ili kuleta mabadiliko, hili tumeliona nchi zote mfano wa karibu ni Sri Lanka.
Umezungumza kitu kilicho bora Sana.
 
Mwarobaini wa haya yote uliyo ya zungumza mkuu ni :-
i, Uwanzishwaji wa vyama vipya vya kisiasa vilivyo imara na vilivyo na sera dhabiti zilizo wazi na vinavyo endeshwa kwa misingi ya kidemokrasia ya kweli na sio demokrasia maigizo.

ii, Ugombea binafsi [ mgombea binafsi ] aliye na sera dhabiti za kutuvusha hapa tulipo.

Kuanzisha chama kingine na ikawe option ya mwisho.

Pana watu wameumizwa, wamekufa, wameteswa, nk kwenye harakati hizi tukiwa pamoja. Tumewekeza muda na Raslimali tulipo tunahitaji tu mabadiliko ya tactics.

Inatia tamaa kupambana kutokea ndani kwanza. Mbona pana ufumbuzi hapa!

Tunayoomba mbona yako wazi na halali?
 
..nimezungumzia mabadiliko ya uongozi kwa njia ya uchaguzi ktk vyama.

..nimesema uchaguzi sio njia ya uhakika, ni suala la 50/50; kwamba, unaweza kupata viongozi wenye dira unayoitaka au usiwapate.

..njia ya uhakika zaidi ya kupata unayoyatamani ni kuanzisha chama kipya huku ukiwaunganisha watu wenye misimamo, mitizamo, na dira ya mabadiliko unayoipendekeza.

Uchaguzi wa wazi kama kutokea kwake beberu Biden ukiwa na namna ya wazi ya kumfurusha awaye yote asiyewajibika ipasavyo, hauwezi kutoa kiongozi mbovu.

Ifahamike tunacho hitaji ni mikakati ya kutuvusha. Ina maana kuna dhamira ya kutokutoa hiyo, kama vipi tukaanzishe vyama vipya?

Kwa maana nyingine au unasema yawezekana tuko mahali pasipo sahihi kabisa, yaani kwenye vyama vya walamba asali tu?
 
Kuanzisha chama kingine na ikawe option ya mwisho.

Pana watu wameumizwa, wamekufa, wameteswa, nk kwenye harakati hizi tukiwa pamoja. Tumewekeza muda na Raslimali tulipo tunahitaji tu mabadiliko ya tactics.

Inatia tamaa kupambana kutokea ndani kwanza. Mbona pana ufumbuzi hapa!

Tunayoomba mbona yako wazi na halali?
Jambo unalo zungumza mkuu ni mpango mzuri lakini kasoro iliyopo inayo tia ukakasi wa kutekelezeka kwa mpango wako kwa kuwa vyama vya kisiasa hapa nchi vimekwisha kuwa mali za baadhi ya familia na makunfi yao ya karibu kwa hiyo kuleta mageuzi/ mapinduzi katika mfumo wa namna hii ngumu kutekelezeka labda uundwaji wa vyama vipya vyenye sera dhabiti vitakavyo leta upinzani dhabiti wa hoja na vyama hivi vya sasa vilivyopo nchini . Vyama vipya sharti vinapaswa kuwa na watu ambao falsafa zina fanana na vilivyo wazi kwa wanachama wote.
 
Back
Top Bottom