Muda wa maamuzi magumu ni sasa

Team JPM

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,074
1,608
Katika kitabu cha Shaban Robert kiitwacho Kusadikika, Mtunzi anashauri 'Ng'ombe kurejea zizini kusaidiwa baada ya kuvunjika marishoni, sio kosa'.

CCM imevunjika, irejee zizini kusaidiwa ili kusonga mbele.

Maandalizi ya uchaguzi wa 2025 ni sasa hivyo kama chama tufanye maanuzi magumu ili kurejesha imani kwa wanabchi tunapoelekea 2025.

Maamuzi hayo magumu ni kurejea zizini kupata msaada wa kusonga mbele. Najua wapiga dili hawawezi kukubali lakini tunapaswa kurejea zizini ili kusonga mbele.

Kama Mwana CCM Mzalendo, napendekeza maamuzi magumu yafuatayo

1. Kutengua azimio la bunge kuhusu mkataba wa bandari na kumuomba Spika aachie ngazi kwa kushindwa kuliongoza bunge katika kuisimamia serikali kwenye suala la uwekezaji babdarini
2. Kurejesha cheo cha katibu wa Siasa, itikati na uenezi kwa Balozi Polepole
3. Kurejesha Wizara ya ardhi kwa Lukuvi
4. Kumteua Dr. Bashiru kuwa Waziri wa Tamisemi
5. Kumpa NAPE wizara ya michezo
6. Kabudi kumpa Uspika wa bunge
7. Kuwashikisha adabu wote waliotajwa kwenye report ya CAG
8. Kumteua Mh. Luhaga Mpina kuwa Waziri wa Viwanda.

Tukifanya hayo, imani itarejea, uhai wa chama utarudi na kasi ya serikali itaongezeka
 
Sisi tunataka majibu. MKATABA UVUNJWE. FUTA KILA KITU, TUANZE MOJA kutafuta mwekezaji kwa kutangaza Tender, Full stop.

Hayo mengine ya vyeo vya kisiasa vya ulaji. Watajua wenyewe huko
 
Back
Top Bottom