Ushauri: Rais Samia inaweza kuwa ni maamuzi magumu lakini hapa tulipofikia hakuna budi

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,603
29,746
Mheshimiwa Rais
Nakuamkua kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tunajua kuna juhudi unafanya tena kubwa ili kuivusha Tanzania kutoka kwenye hali ya uchumi wa chini kuelekea uchumi wa juu.

Lakini sisi wakosoaji wako, tuna lengo la kukussidia kuona nyufa zinazotengenezwa kwa makusudi na wasaidizi wako. Tumekuwa tunafichama majina yetu halisi hapa mtandaoni kwa sababu serikali yako bado imekumbatia sheria kandamizi ya kuwashughulikia Watanzania wanaotumia haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni. Kimsingi kwenye eneo la HAKI hatuna imani na serikali yako kwa sababu Haki kwa nchi hii inategemea huruma zako na siyo taratibu za kisheria.

Neno TUMEFIKA HAPA ni pana sana Mheshimiwa Rais. Mimi raia wako ambaye ninakuletea ushauri wangu kwako, simaanishi kwamba una ulazima wa kufuata ushauri wangu. Hata kama ushauri wangu ukionekana hauna tija lakini angalau nimeweza kutoa ya moyoni.

UHALISIA
Mheshimiwa,

Mtaani au huku chini mambo hayaendi vyema kwenye uchumi wa mtu mmoja mmoja. Sehemu kubwa ya raia wako ni kuanzia uchumi wa kati kushuka chini, sasa uhakika wa kipato unategemea mshahara kwa walioajiriwa, waliobaki wanabangaiza wapate mahitaji ya siku ili waione kesho.

Lipo kundi la wachache ambao kipato chao wana uwezo wa kuishi miaka hata 20 bila kufanyakazi na bado wasitetereke. Kundi hilo pia limejaa maafisa ngazi za juu serikalini na baadhi ya watoa maamuzi. Wateule wako wengi hawakosekaniki kwenye kundi hili.

Siwachongei la hasha, bali najaribu kukupa picha ya uwiano halisi wa maisha ya Watanzania wako.

kutokana na uhalisia wa uhakika wa kuyakabili maisha ya kila siku, raia wako vifua vimejaa na ikitokea ukaweza kufunua mioyo ya Watanzania wengi, utakuta wananung'unika na hasa hasa kujenga chuki kwako. Sababu ya sononeko dhidi yako kuongezeka, ni kwa sababu wateule wako wengi kuanzia Halmashaurini huko, Wilayani na ngazi za juu wamegeuza matatizo ya Watanzania kama.mitaji yao ya kisiasa na utakuta kwa dhati wanaweza kuwa ndiyo wanaoweka mikakati ya kuendeleza changamoto ili zitumike kwa faida yao ya kisiasa.

Umesimamia zoezi la kuhakikisha maji safi na salama yanamfikia kila Mtanzania lakini pamoja na mabomba kutandazwa maeneo mengi nchini bado uhakika wa maji kupatikana ni mdogo sana. Mabomba yanatoa maji siku chache mno na hakuna maelezo ya kina aidha ya kiufundi au mgao.

Umeme napo ni tabu. Laiti ungeliona wafanyabiashara wanaokula hasara kubwa ya kuharibikiwa bidhaa zao zinazoregemea umeme hakika ungewafuta machozi. Pia Mhe. Rais, kuna wale ndugu zetu wanategemea umeme kwa ajili ya matibabu yao, hatujui ni wangapi maisha yao yamekatishwa kwa sababu ya tatizo la.umeme ambalo hutokea bila hata taarifa kwa maeneo mengi....

Elimu yetu napo ni maboresho kila kukicha, na maboresho hayoyanaigharimu serikali fedha nyingi lakini kasoro za mitaala hazikokesaniki na hqtujui zinawekwa kwa makusudi au ni udhaifu wa kibinadamu

Leo wafanyabiashara Kariakoo wameanza mgomo, na inaonesha wana kilio chao ambacho laiti wateule wako wangewaita na kuzungumza nao ikiwemo kuwaelimisha isingefikia tukio laaibu la mgomo unaoendelea leo.

Imefika mahala kila Mtanzsnia anatarajia kauli yako kwenye kila jambo au changamoto zinazotokea ka siku.

Tulitarajia kuona wssaidizi wako wakikimbizana kutatua changamoto zinazotukabili lakini badala yake tunawaona wakijinemeesha rasilimali za ncbi wanazozisimamia maeneo yao ya kisekta.

Tanzania ya leo tunafikia kuamini kuwa uteuzi ni fursa na siyo dhamana ya kiutumishi uliotukuka.

USHAURI
Mheshimiwa Rais

Kama ikikupendeza ulivunje Baraza la Mawaziri ufanye uteuzi upya ili luweka watu sahihi kwenye kuipeleka nchi kwenye maendeleo ya kweli. Muda ni rafiki kwako na hakika utakaowateua tena ni Watanzania katika nafasi za kulusaidia.

Chukua tahadhari kubwa na sifa nyingi zinazotolewa mitandaoni, wengi wanalinda nafasi zao kwani kukusifia bila kuonesha wao wenyewe wamefanya nini ni kukupaka mafuta kwa mgongo wa chupa

Ndimi,
Msanii
 
Asisahau jana magari ya kutoka nji ya Morogoro kuingia Dar na kinyume chake yaliwekwa karanteen yasitembee kwa massa 8 toka saa 11 jioni hadi saa 6 usiku.

Nimeambiwa kumbe eti mwenge ilikuwa unapiunapita ndo sababu ya kufunga hibarabara kwa massa 8 na shida ya uamuzi huko kamwe wengi hawataisahau leo wala kesho.

Hivi mabasi, malori na vyombo vyote vinazuiliwa kwa muda wote huo alafu liwe jambo la kawaida tena usiku kiasi hicho, unajiuliza abiria anayefika mbezi stand saa 7/8 usiku na anatakiwa kwenda Chanika, Tegeta ama Mbagala anafikaje huko usiku huo wa mnane?

Hivi mwenge unatufanya tunakuwa mazuzu kiasi hiki ama ni hujuma hii kwa nchi?

Naona sahivi pila litembee tu
 
Wachapakazi hawajui kusifu hivyo ni vigumu kuonekana kwa mama.

Kuna watu wazuri tu kwa kazi ila hawajui kujipendekeza.

Mama angazia halmashauri za wilaya hadi wizarani. Wasiojua kujipendekeza hawapewi fursa.

Watafute watu hawa ndio watakaokusaidia
 
Wachapakazi hawajui kusifu hivyo ni vigumu kuonekana kwa mama.

Kuna watu wazuri tu kwa kazi ila hawajui kujipendekeza.

Mama angazia halmashauri za wilaya hadi wizarani. Wasiojua kujipendekeza hawapewi fursa.

Watafute watu hawa ndio watakaokusaidia
Siyo kwamba hajui ila kuwa na hadhari sana na hili neno DOKEZO....

Nchi imekuwa under Dokezo for decades.

Mama abadiliahe haya mambo
 
Sidhani hata kama akisoma atafanya lolote. Dawa na tiba ya hizi kero zote ulizoandika ni kuitoa CCM madarakani na wanachama wake na viongozi watiwe mbaroni na kusomewa mshitaka ya kuhujumu taifa na raia.
 
Wachapakazi hawajui kusifu hivyo ni vigumu kuonekana kwa mama.

Kuna watu wazuri tu kwa kazi ila hawajui kujipendekeza.

Mama angazia halmashauri za wilaya hadi wizarani. Wasiojua kujipendekeza hawapewi fursa.

Watafute watu hawa ndio watakaokusaidia
Hii tabia ya watu kujipendekeza inaua nchi kabisa...Imefika sehemu hao hao waliojipendekeza ndiyo waliojaa kila nafasi na hivyo wao pia wanatafuta ambao wana tabia kama zao. Mwisho wa siku hakuna ubunifu wala ufanisi ni kufanyiana tu usanii na kukenuliana meno kinafiki huku mioyo yao na akili ipo katika kujinufaisha binafsi na siyo kujenga nchi
 
Siyo kwamba hajui ila kuwa na hadhari sana na hili neno DOKEZO....

Nchi imekuwa under Dokezo for decades.

Mama abadiliahe haya mambo
Naona manmpigia mbuzi gitaa. tangu aingie hapo kuna maamuzi yoyote kama amri jesh mkuu ameyafanya ili na hili liwe la pili
 
Naona manmpigia mbuzi gitaa. tangu aingie hapo kuna maamuzi yoyote kama amri jesh mkuu ameyafanya ili na hili liwe la pili
Ni kama kweli vile, kwa sababu maamuzi mengi ni kutubana sisi wa chini na kuwapa haueni majizi.

Teuzi za kufutana machozi na kupeana maisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom