Muda mwingine mchepuko unaweza kuwa wa faida

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
2,166
2,000
JOHN :-Habari yako bwana?

HASSAN :-Nzuri we Nani?

JOHN :-Natumaini hatufahamiani.

HASSAN :-Yes, sikufaham wewe nani nikumbushe..

JOHN :-mimi naitwa mr JOHN au baba Hellen.

HASSAN :-ndio..

JOHN :-Mke wangu ni ANNA ambae kwa sasa ndio mpenzi wako kipenziiii kwa maelezo niliyoyakuta kwenye simu yake.

HASSAN :- (kimyaa)

JOHN :-Leo nakutumia sms hii sio kwa ubaya bali kwa kukupongeza kwa kumbadilisha sana mke wangu.

HASSAN :- (*nisamehe bro, nipo Mwanza kwa Sasa)

JOHN :- Usijai Jana nilikuona unavuka barabara, umekutana na mke wangu mmepanda Bajaji sikujua mlielekea wapi. ..

HASSAN :-(kimyaa)

JOHN :-lakini usijali, kitu ambacho nakupongeza ni kwa kumbadilisha mke wangu.
kitu ambacho hata mapadre na wazazi wake walishindwa.

HASSAN :-(kimyaa)

JOHN :-kwa kweli Anna mke wangu sasa hivi kabadilika sanaaa.
Hanywi tena pombe kupitiliza kama hapo mwanzo, hafokei hovyo watoto na kuwapiga kama mwanzo, harudi nyumbani usiku tena. sasa hivi mke wangu ananipikia na kunifulia.

JOHN :-Unanisikia kaka..

HASSAN :-Ndio

JOHN :-Yaani Nimeshangaa sana. haya mambo niliyasahau muda kutoka kwa mke wangu Anna mpendwa.

HASSAN :-Umejuaje bro

JOHN :-Nimejua, tatizo lilikuwa ni mimi mwenyewe. baada tu ya kunifumania na mwanamke mwengine ndipo mke wangu alibadilika sanaa mpaka nilijuta.

HASSAN :-Aliniambia...Pole Sana

JOHN :-Ansante, yaani kila jitihada zilishindikana za kumrudisha awe kama zamani, ikawa inapotokea nashindwa kutimiza haja zake za kimwili kama zamani basi ni ugomviiii, naonekana kama nimemalizia nguvu huko nje.

HASSAN :-Kwani amebadilika nini?

JOHN :-Ndio, kwa mabadiliko ya hivi karibuni ndio kitu kimenishangaza mke wangu amekuwa na furaha kama mwanzo, amekuwa mcheshi na watoto. anapika na kufua.

HASSAN :-Mbona uwa akija kwangu anafua

JOHN :-Lakini nimegundua sababu kubwa ya mabadiliko haya ni wewe Hassan, toka akupate uwe mchepuko wake amekuwa akikuheshimu sana amekuwa akikusikiliza sanaaa.
Nimekuta sms zako nyingi ukimuuliza mke wangu Anna:

umewapikia watoto?
Mtunze mmeo mimi wa kupita tu
umempikia mme mwenzangu chakula gani
ulivyonipa jana mpe na mzee hivyo hivyo ila usimchoshe..
Anna nimenunua suti na viatu uje kesho uchukue hivyo kwa ajili ya mmeo
msalimie mheshimiwa
Anna uko wapi saa hizi muda wa kurudi mumeo, rudi kwako haraka

Nimefurahi sana kwani nae amekuwa akitii maagizo yako kuliko yangu.

Nimefurahi zaidi kwa kuwa hunywi pombe na hivyo hata yeye umemkataza kunywa pombe na ameacha kabisaaa, hata nilizo nunua mimi ili anywe ziko tu kwenye friji.

Hataki kabisa kunywa pombe kwa kuwa anakuogopa.

Wewe ni mmoja wa wanaume wachache sana ambao hutembea na mke wa mtu na bado akahitaji asiharibu ndoa yake.

Yaani wewe kutembea na mke wangu kumeimarisha sana ndoa yangu.

Hata unapomuudhi wewe huwa najua.

Maana atashinda hana raha kabisa.
Ahsante sana HASSAN.

Ila ninachokuomba mwambie na mie asinisahau sana kwenye tendo la ndoa.

HASSAN :-Sawa nitamwambia....

JOHN :-maana mkiahidiana kukutana wiki ijayo ujue wiki nzima sipewi anakutunziaa.

HASSAN :-Nimekuelewa kaka..

JOHN :-Naomba umwambie hilo.

HASSAN :-Haya..

JOHN :-Mimi ni mtu mzima nahitaji kulea wanangu kwa amani zaidi.

HASSAN :-Ni kweli.

JOHN :pengine nguvu zangu za sasa siwezi mtimizia mahitaji yake ya kimwili.

Bora adui mmoja ninaekujua kuliko akiwa anahangaika ovyo kutafuta kukidhi haja ya mwili wake.

Usimwambie Anna kama nimekujua maana atachukia sana na anaweza nuna mwezi mzima..

HASSAN :-Siwezi kumuambia, ilo nalijua usihofu Bro..

JOHN :- SIKU NJEMA KAKA HASSAN, TUMPENDE MKE WETU.
 

Abuu Said

JF-Expert Member
Jul 5, 2015
3,330
2,000
Kweli km mmezaa ili msiwavuruge watoto inabidi ukubaliane na hayo Mwache tu huru Mkeo atafute furaha yake na wewe tafuta furaha yako
 

Times9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,711
2,000
Hakuna mwanaume anaeweza kukubaliana na mtu/mwanaume mwenzie anae mnyanganya tonge lake mdomoni hata kama amemchoka huyo mwanamke.


Nasema HAKUNA...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom