MUAROBAINI wa UMEME Tz ni nini? Tufanyeje once and for all!

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2008
Messages
2,508
Points
1,195

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2008
2,508 1,195
Hivi, Muarobaini wa tatizo la umeme, au nisema ugonjwa wa umeme Tanzania ni nini? ni solution gani ambayo sisi wana JF hapa tunaweza kuwashauri viongozi wetu ambao kila siku lazima waje humu JF kupakua mawaidha yenye akili...tuwaambie nini, wafanye nini ili kuondoa kabisa Tatizo la umeme Tanzania? hebu tu mention them hapa chini.
 

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2008
Messages
2,508
Points
1,195

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2008
2,508 1,195
Naanza kwa kusema tujenge kinu cha nuke cha kufua umeme kama ilivyo kwa south africa na France. pia, tutumie kufua umeme maji ya rufiji ili yasipotee tu kwenda baharini. kwa maji ya rufiji plus nuclear powerplant, umeme tutauza hata nchi za majirani. nilihuzunika kusikia sumbawanga wamekosa umeme kwasababu ya hitilafu kule Zambia, kumbe wasumbawanga wanatumia umeme wa nchi ya zambia...bukoba umeme wa uganda.
 

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,585
Points
2,000

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,585 2,000
Tuondoe ukiritimba ktk kuzalisha umeme, tanesco wafanywe kama TTCL. Nitakupa mifano hai michache. Bulongwa Makete kuna umeme usiofanya kazi kwa sababu ya sheria za nchi yetu kwamba watu binafsi/taasisi wazalishe mwisho kiasi fulani. Matokeo yake umeme umevutwa toka Mby km 100 kupeleka Makete wakati chanzo cha Bulongwa ni megawat 220,uliopo unatumika na misheni tu ya KKKT.

Ukifika Wino Songea,kuna umeme mkubwa pale,umeishia kutumika RC tu, ukifika kijiji cha Lukani Kilolo,pana umeme wa maji wa kuaminika na kwa upuuzi wa wanasiasa wameliachia kanisa la RC, hata Bomang`ombe Kilolo,kijiji kizima kimepigwa umeme underground na Taliani hadi raha,lakini hawaruhusiwi kusambaza kwingine,Tanesco wamevuta umeme toka Iringa km 50 kupeleka umeme Kidabaga ambapo ni km 5 toka Bomang`ombe. Mwanasiasa anaona fahari kuwaambia wapiga kura nimeleta umeme toka umbali fulani kana kwamba kitendo hicho kina tija.

Tukivuna umeme toka vyanzo vyote vidogovidogo vilivyoko vijijini huko na kuusambaza huko huko vijijini naamini tatizo litakwisha,huu ujinga wa kupeleka umeme mahali penye umeme sijui utakwisha lini. Tuangalie vyanzo rahisi,sio lazima tusubiri miradi mikubwa inayoambatana na wizi ktk ujenzi na mikataba.
 

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
6,566
Points
2,000

Hute

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
6,566 2,000
Turuhusu private companies zingine zije nchini kufanya biashara ya umeme. naona hapo ndo patakuwa patamu...itakuwa kama ilivyokuwa TTCL na makampuni ya simu za mkononi kwasasa. hapo vipi?

vilevile, tusisahau kuwa tunayo urenium ya kufua umeme, mtu rufiji, mto malagalasi kule kigoma etc ni vyanzo tosha. kusema ukweli, tz kuna vyanzo vingi vya umeme, tatizo ni vichwa vigumu vya viongozi wetu walioshika rungu...marungu yangepewa watu wengine wenye akili kama zangu, nchi/inji hii ingeendelea kwa haraka sana. viwanda hatuvutii kwasababu viwanda vikubwa vinahitaji umeme mwingi na wa bei nafuu, nchi zingine zinatupiga bao...sasa sector ya viwanda itakuja kukua lini tz kama umeme wenyewe ni wa mgao hata kwa sisi wenyewe tunaoshawa bulb tu...hahah.
 

Ikimita

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2010
Messages
301
Points
195

Ikimita

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2010
301 195
(1) Ruhusu ushindani katika uzalishaji na usambazi umeme ili kuifanya TANESCO iwajibike, wakishindwa wapoe kama TTCL wengine wapite.
(2) Bei ya umeme iachiwe itambae na soko ili iwe kivutio kwa wawekezaji wapya.
(3) Ondosha au punguza sana kodi kwa sekta yote ya umeme ili kuvutia wawekezaji wapya na kujaribu kuleta unafuu kwa upande wa bei kwa watumiaji.
(4) Umeme uuzwe kwa utaratibu wa lipa kwanza bila kujali mtumiaji ni serikali au mteja mkubwa
(5) ............
 

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
6,566
Points
2,000

Hute

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
6,566 2,000
(1) Ruhusu ushindani katika uzalishaji na usambazi umeme ili kuifanya TANESCO iwajibike, wakishindwa wapoe kama TTCL wengine wapite.
(2) Bei ya umeme iachiwe itambae na soko ili iwe kivutio kwa wawekezaji wapya.
(3) Ondosha au punguza sana kodi kwa sekta yote ya umeme ili kuvutia wawekezaji wapya na kujaribu kuleta unafuu kwa upande wa bei kwa watumiaji.
(4) Umeme uuzwe kwa utaratibu wa lipa kwanza bila kujali mtumiaji ni serikali au mteja mkubwa
(5) ............
tutaepuka vipi syndicates kwa makampuni hayo kujiunga na kumonopolize pamoja soko la umeme kama wanavyofanya wauzaji wa mafuta kwenye shelli zetu...wakiamua bei moja, hata kama inakamua wananchi ndo wameamua ivyo.
 

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Messages
1,728
Points
1,250

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2010
1,728 1,250
Ubungoubungo sitaki kuamini kuwa wahusika hawajui nini cha kufanya ili TZ tuwe na umeme wa uhakika!

Hayo unayosema ni baadhi tu ya mambo ambayo watawala wanayafahamu fika. Nachelea kusema kuwa hizi tabu zote zinatengenezwa kwa makusudi kabisa ili wanasiasa waendelee kunufaika na kuwaweka watz ktk hali ya utegemezi.

Hapa tunazungumzia umeme. Lakini mfano swala la maji dar kuna sources mbili kubwa since time immemorial as if population haiongezeki. Nazungumzia ruvu juu na ruvu chini.

Nasema ni makusudi na kwa manufaa ya wanasiasa ndio mambo yako hivi. Angalia swala la shule watawala wanona sifa kwa kujenga madarasa kama vile ni something extra bila kujua kuwa population ya wanafunzi inaongezeka kila mwaka!! Ukweli ni kwamba huduma za kijamii ndio limekuwa eneo la wanasiasa kupata political scores.

Nafikiri haya matatizo kama umeme usio na uhakika na social services zingine yataendelea kuwepo mpaka utapokuwepo utashi wa kisiasa wenye lengo la kuwa nufaisha walio wengi.

Mungu Ibariki TZ.
 

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
23,337
Points
2,000

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
23,337 2,000
Ubungoubungo sitaki kuamini kuwa wahusika hawajui nini cha kufanya ili TZ tuwe na umeme wa uhakika!

Hayo unayosema ni baadhi tu ya mambo ambayo watawala wanayafahamu fika. Nachelea kusema kuwa hizi tabu zote zinatengenezwa kwa makusudi kabisa ili wanasiasa waendelee kunufaika na kuwaweka watz ktk hali ya utegemezi.

Hapa tunazungumzia umeme. Lakini mfano swala la maji dar kuna sources mbili kubwa since time immemorial as if population haiongezeki. Nazungumzia ruvu juu na ruvu chini.

Nasema ni makusudi na kwa manufaa ya wanasiasa ndio mambo yako hivi. Angalia swala la shule watawala wanona sifa kwa kujenga madarasa kama vile ni something extra bila kujua kuwa population ya wanafunzi inaongezeka kila mwaka!! Ukweli ni kwamba huduma za kijamii ndio limekuwa eneo la wanasiasa kupata political scores.

Nafikiri haya matatizo kama umeme usio na uhakika na social services zingine yataendelea kuwepo mpaka utapokuwepo utashi wa kisiasa wenye lengo la kuwa nufaisha walio wengi.

Mungu Ibariki TZ.
Kwa kuitoa CCM madarakani?
 

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
23,337
Points
2,000

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
23,337 2,000


Stieglers Gorge ni nini hasa?

Stieglers Gorge ni mpalio mwembaba unaopatikana kwenye bonde la mto Rufiji, kilomita 374 toka jijini Dar es salaam. Kwa utafiti uliowahi kufanyika mwishoni mwa miaka ya sabini na mwanzoni mwa miaka ya themanini [ 1978-1980] kwa ushirikiano wa RUBADA [Rufiji Basin Development Authority] na M/s Norplan/Hafslund, ilionekana kwamba mradi wa Stieglers Gorge una uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme mwingi kwa njia ya maji [Hdro-power] zaidi ya umeme ambao Tanzania ilikuwa ikihitaji katika miaka hiyo. Matokeo ya utafiti huo pia yalionyesha kwamba, mpalio wa Stieglers una uwezo wa kuhimili mitambo mitatu mikubwa ya kuzalisha umeme [3 power stations]. Mtambo 'A' wenye uwezo wa kuzalisha megawati mia nne (400MW) ambao ungefungwa upande wa kaskazini mwa bwawa. Mtambo 'B' wenye uwezo wa kuzalisha megawati mia nane (800MW) ambao ungefungwa upande chini ya bwawa, na mtambo 'C' wenye uwezo wa kuzalisha megawati mia tisa (900MW) ambao ungefungwa upande wa kusini mwa bwawa. Jumla megawati elfu mbili mia moja [2100MW].
Ilikadiriwa kwamba, kwa kipindi hicho [1978-1980], ingeigharimu serikali dola milioni 1,200 za kimarekani tu kukamilisha mradi wote.
Lakini cha kushangaza, kwa sababu zisizoeleweka, serikali ikaamua kutoendelea na mradi huu na badala yake ikaamua kuwekeza kwenye vijimradi vidogovidogo kama vile Hale, Mtera, na Nyumba ya Mungu. Matokeo yake, sina haja ya kuyaelezea.
Ndugu watanzania wenzangu, wajibu wa hatma ya nchi yetu umo mikononi mwetu sote. Mustakabali wa taifa letu hautategemea viongozi waoga toka serikali kuu wanaong'ang'ania dhana ya "status quo" kwa kutopenda kujaribu mambo mapya na makubwa ya kimaendeleo. Maendeleo ya kweli hata hivyo, yataletwa na sisi wenyewe, wananchi.
Kwasababu hiyo basi, BongoTz kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi tumeamua kuanzisha movement ya kuishinikiza serikali kutafuta suluhu ya kuridhisha na ya kudumu kuhusu tatizo la umeme/nishati nchini.
Lengo letu ni kukusanya sahihi zipatazo milioni moja na kuziwakilisha kwa Rais Kikwete tukiitaka serikali iwekeze kwenye mradi wa Stieglers Gorge, uliopo kwenye bonde la mto Rufiji wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawatt 2100 [mwingi wa kutosha na hata mwingine kubaki na kuuzwa nje ya nchi] ili tuweze kuondokana kabisa na tatizo hili la kukatikiwa na umeme, tatizo ambalo ni aibu kubwa kwa taifa letu.
Haileti maana kabisa kwa nchi yetu iliyobarikiwa kwa vyanzo vingi vya kuzalisha umeme kama vile makaa ya mawe--Mchuchuma na Kiwira; gesi ya asili "songo songo"--ufukweni mwa bahari ya Hindi na Mnazi bay (Mtwara); pamoja na chanzo kingine rahisi kwa njia ya maji [Hydro-power]--Stieglers Gorge, Rufiji; kuendelea kusuasua kwenye kiza kinene miaka nenda, miaka rudi.
Sio kwamba Rais wetu halijui hili, hapana, analijua fika! Yeye mwenyewe, kwenye ufunguzi wa Bunge jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 30 desemba 2005 alitamka na kuahidi mbele ya wabunge, nanukuu: "Nishati ni sawa na chembe za damu mwilini. Tunapanua wigo na aina ya vyanzo vya umeme na nishati kwa jumla ili kuwa na nishati ya kutosha na yenye gharama nafuu kukidhi mahitaji ya uzalishaji ya viwanda, utoaji wa huduma za kijamii, na matumizi ya nyumbani. Tutayashughulikia kwa kipaumbele cha juu matatizo ya sasa yahusuyo upatikanaji wa umeme nchini... Ilani ya CCM ya uchaguzi wa Oktoba 2005 inasema wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itaharakisha mradi wa kupata umeme kutoka makaa ya mawe ya Mchuchuma. Na Hivyo ndivyo tutakavyofanya. Aidha, Serikali ya Awamu ya Nne itafufua miradi ya umeme ya mto Rusomo na Stiglers [Stieglers Gorge]." Mwisho wa kunukuu..
Ndugu watanzania wenzangu popote pale mlipo: ushirikiano wetu sote unahitajika ili kufanikisha zoezi hili. Tafadhali sign petition hapo chini kisha wafahamishe na wengine pia. Maana tusiposhiriki sasa, nani ajuaye kesho watatuletea hadithi gani tena? Juzi ilikuwa IPTL na Richmond. Jana ilikuwa kununua mvua toka Thailand, wakati Stieglers Gorge ipo. Na kesho je...?
Yes, viongozi wetu kwasasa wanaweza kujidai kuziba masikio wasitake kusikia kilio chetu kama walivyozoea sikuzote, lakini tukumbuke kuwa sahihi 25,000 za wanaharakati wa Seberia wakiongozwa na mwana-biolojia Marina Rhikhvanova ziliilazimu serikali ya Kremlin kusitisha mpango wa kujenga bomba la kusafirisha mafuta karibu na ziwa Baikal, ziwa lenye kina kirefu duniani. Je, itakuweje kwa sahihi milioni moja toka kwa watanzania wenye uchungu na nchi yao? [Sign petition hapa]:
 

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Messages
1,728
Points
1,250

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2010
1,728 1,250
Sio lazima. Kwanza kabla hata kuzungumzia party ipi inaweza kutoa leadership nzuri tunahitaji kuitazama mifumo yetu ya kiutendaji. Mingi ni mibovu kuliko maelezo.

Nikupe mfano kama utakuwa muelewa hutapatashida kuelewa. Kwa mfumo uliopo sasa wa mawaziri utaonekana mzuri tu kama utafanya kazi ndani ya box. Usiwe na wazo jipya ili mradi unasaini vocha on time yaani mambo routine utakuwa ni kiongozi safi ktk serikali. Kama ni muelewa utafahamu kwanini the likes of Mwakyembe, Magufuli si popular serikalini lakini ni popular kwa wananchi. Tizama mfano wa PM na magari ya kifahali serikalini. Mfumo unasema vingine maelezo ya viongozi yanasema vingine.
 

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
23,337
Points
2,000

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
23,337 2,000
Jamaa JK aliongea hivi kunako Oktoba 2005........leo 2010 hajafanya hivyo:

Nanukuu:

"Nishati ni sawa na chembe za damu mwilini. Tunapanua wigo na aina ya vyanzo vya umeme na nishati kwa jumla ili kuwa na nishati ya kutosha na yenye gharama nafuu kukidhi mahitaji ya uzalishaji ya viwanda, utoaji wa huduma za kijamii, na matumizi ya nyumbani. Tutayashughulikia kwa kipaumbele cha juu matatizo ya sasa yahusuyo upatikanaji wa umeme nchini... Ilani ya CCM ya uchaguzi wa Oktoba 2005 inasema wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itaharakisha mradi wa kupata umeme kutoka makaa ya mawe ya Mchuchuma. Na Hivyo ndivyo tutakavyofanya. Aidha, Serikali ya Awamu ya Nne itafufua miradi ya umeme ya mto Rusomo na Stiglers [Stieglers Gorge]." Mwisho wa kunukuu..
 

Nanren

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2009
Messages
1,848
Points
1,500

Nanren

JF-Expert Member
Joined May 11, 2009
1,848 1,500
Tunahitaji kiongozi kama Hugo Chavez, Mugabe, Gadaffi au Fidel Castro, au hata mchina wa zamani Mao Tse tong. Kiongozi asiyehitaji kusifiwa na mataifa ya nje, kiongozi ambaye unoko wake unakuwa mchungu "in short run" lakini ni mtamu in "long run". Nchi yetu imeoza kifkra, hata sehemu kubwa ya wananchi wake. Kila mtu anafikiria ulaji tu, apate pesa kibao atanue.

Hata ukija na wazo zuri la kuanzisha chanzo cha umeme wa kudumu, wazo hilo likikubaliwa, litasababisha ulaji mkubwa wa pesa halafu bado chanzo kisijengwe vizuri kukidhi mahitaji. Halafu Kiongozi atakayekuwepo madarakani ataogopa kuwachukulia hatua walaji eti asikose kura kipindi kijacho, au utakuta naye au jamaa zake wamehusika kwenye ulaji. Wapo Raia wachache wanaoweza kuwa na moyo wa uzalendo kwa nchi na labda wanao hata uwezo wa kuongoza, lakini hatuna namna ya kuwatambua, na hata tukiwatambua, system iliyopo haitoi nafasi kwa raia kama hao kuingia kwenye system. Kifupi ni kwamba tumeliwa!
 

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
6,566
Points
2,000

Hute

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
6,566 2,000
sasa jamani, kwani kikwete anafanya nini? haoni hayo maji ya mto rufiji? au anaogopa kuua kamba pale kwenye mdomo wa kuyamwaga baharini?hahaha, mazalia ya kamba...manake hawa wanawweza wakaokoa kamba na pundamilia tanzania kuliko kuokoa ugumu wa maisha ya mtanzania. tunaomba jk alifanyie kazi hili jambo, tuuze umeme mwingine nje ya nchi, kwasababu tutakuwa nao mwingi hadi wa kumwagika...
 

zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
17,071
Points
0

zomba

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
17,071 0
Kikwete kisha utangaza Muarubaini wa Umeme Tanzania, au hujasikiliza hotuba ya kuzinduwa bunge la kumi?
 

Taso

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2010
Messages
2,053
Points
2,000

Taso

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2010
2,053 2,000
ni solution gani ambayo sisi wana JF hapa tunaweza kuwashauri viongozi wetu ambao kila siku lazima waje humu JF kupakua mawaidha yenye akili...tuwaambie nini, wafanye nini
unajuaje "viongozi wetu kila siku lazima waje humu JF kupakua mawaidha," unajuaje hilo?

na unajuaje wanapokea shauri? Ni kuwa out of touch.

Kilio kimoja kikubwa cha technocrats serikalini ni kwamba viongozi, kama Mawaziri n.k. hawasikii mawaidha ya watu wa chini yao. Ukimshauri anaona kama una mu overshadow, hawataki. Lakini technocrats wa idara husika wanajua matatizo yaliyopo.

Hivi unadhani ni nani anaelewa zaidi tatizo la umeme na nishati nchini kati ya technocrats wa wizara ya Nishati na sisi Jamiiforums hapa tuliobobea katika kutatua masuala ya "Nikim-mega Analia Sana" na "Natafuta Jimama Lenye Watoto Watatu"?
 

Forum statistics

Threads 1,389,740
Members 528,016
Posts 34,033,101
Top