Tatizo sio uhaba wa umeme nchini. Tatizo kuu ni mazoea tuliyojijengea

Mwl Athumani Ramadhani

JF-Expert Member
Sep 10, 2022
1,282
2,508
Kama Taifa tumejijengea mazoea mabaya na yanatuumiza wenyewe!

Mazoea ya kuwa maji ndio chanzo KIKUU cha umeme kwenye Taifa ndio yanatuumiza,ni nani alituloga!!?

HIVI hapa nchini maji pekee ndio chanzo cha umeme!? Ina maana ukame ukitokea tu umeme wa kipimo na hakuna namna nyingine ya kufanya!?

Haiwezekani umeme wa maji pekee ukawa tegemeo kwetu wakati jua linawaka zaidi ya asilimia 90 ya mikoa yote Tanzania,wakati kinyesi cha wanyama kipo kila kona ya nchi ni tatizo la kisheria pekee ndilo linarudisha NYUMA usindikaji wa kinyesi kwa ajili AJILI ya umeme, bado upepo na vyanzo vingine vingi sana.

Kama taifa ni aibu kubwa sana eti kuwe na umeme wa kipimo na wananchi wateseke KWA kukosa umeme!!kuna tatizo mahali hata kama tanesco na serikali wanafanya Biashara Basi hiyo biashara inatakiwa iwe advanced kuendana na mahitaji yaliyopo.

Wenye dhamana na hili waanze kufikiri upya namna ya kutatua changamoto hii ya KILA mwaka nchini!

Mungu ibariki TANZANIA
 
Hakuna ubunifu na ujasiri wa maamuzi. Kipindi cha awamu ya nne hali ilikuwa mbaya, kidogo ikawa nafuu awamu ya tano. Kwa sasa tatizo limekuwa mara mbili iko shida mahala. Mtabadilisha watu haitoshi. Akicheza hata Dotto atachemka, vyanzo vya nishati, sera, sheria na mifumo ya uzalishaji na usambazaji iangaliwe upya. Hii ni pamoja na teknolojia na mitizamo ya watendaji wa Tanesco.
 
Umeme wa nyuklia unawezekana ila kwa mazoea na mchango wa ccm kinaweza kulipuka na kushindwa kumudu.
Kama kiwanda Cha magodoro kinaungua kwa uzembe au bandari serikali kushindwa kuiendesha tutaweza ili
 
Umeme wa nyuklia unawezekana ila kwa mazoea na mchango ccm kinaweza kulipuka na kushindwa kumudu.
Kama kiwanda Cha magodoro kinaungua kwa uzembe au bandari serikali kushindwa tutaweza ili
 
Umeme wa nyuklia unawezekana ila kwa mazoea na mchango ccm kinaweza kulipuka na kushindwa kumudu.
Kama kiwanda Cha magodoro kinaungua kwa uzembe au bandari serikali kushindwa tutaweza ili
 
Lakini kwa sasa umeme wa gesi (thermal) ndio chanzo kikuu cha umeme kwa Tanesco. Labda ikiwashwa Stiglers ndio itakuwa hydropower inaongoza.
 
Umeme unaotokana na maji ni mzuri kwasababu maji hayo yatatumika Kwa matumizi mbalimbali baada ya kuzalisha umeme
 
Umeme unaotokana na maji ni mzuri kwasababu maji hayo yatatumika Kwa matumizi mbalimbali baada ya kuzalisha umeme
Ni kweli. Lakini hizi mvua zisizoeleweka, zinaathiri sana uzalishaji wa umeme. Mabadiliko ya tabianchi yamefanya hydropower isiwe chanzo cha kuaminika cha uzalishaji umeme. Lakini pia kama nchi , hatujawekeza kwenye umeme wa upepo na umemejua. Huko tuna potential ya kutosha sana
 
Wewe unasema nini. Tulishatoka huko umeme asilimia kubwa ni gesi. Kuhusu vyanzo vya maji tangu mama ameingia na kuweka kipara ngoto waziri wa nishati wamepuuza magufuli alivyosema maji yanaachiwa kusudi kwenye mabwawa ikiwa ni mchongo wa wauza magenerator na sasa solar panels.

Pia kwenye uzalishaji kwa gesi kuna hujuma nyingi tu maana hata hao wenye kusupply gesi mpamgo ni kuwepo daima shortage ya umeme.

Kwa ufupi kuna hujuma nyingi za wapigaji bila magufuli wanafugwa na kulelewa na vigogo wenye lengo moja tu la kujilimbikizia mali.
 
Tanesco iache monopoly katika uzalishaji iruhusu wazalishaji wawe wengi kutoka private sector yeye awe mnunuaji mkuu au shirika livunjwe vunjwe liwe na zone ambazo zinajitegemea maana monopoly inauwa creativity inauwa competition dhidi ya soko na inaleta stagnancy na udumavu mkuu ktk sekta. Angalia TBC ilivyochangamka kwa kuwa inapata ushindani kutoka media house nyingine na haibebwi sasa shirika likiwa moja halina ushindani linalala tu.
 
Tatizo Si umeme wa maji, tatizo ni mabwawa kufunguliwa makusudi Ili wawekezaji wakubwa mashamba Yao yapate maji wakati wa kiangazi,

Nadhani ukipewa KAZI ya kuhakikisha mabwawa hayafunguliwi utaweza vizuri comred!!
 
Back
Top Bottom