Muafaka: JK sasa mambo mazito
2008-05-14 16:09:08
Na Usu-Emma Sindila, Buguruni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Jakaya Kikwete sasa amewekwa kwenye mtihani mgumu kufuatia chama cha upinzani cha CUF, kuapa kwamba, kamwe hakitarudi kwenye meza ya mazungumzo.
Kinachofanya mambo yawe mazito kwa kiongozi huyo wa nchi, ni chama hicho kumbwagia sakata hilo zito JK na kukataa kata kata kuendelea kulijadili kama vyama.
Katibu Mwenza wa CUF, Bw. Ismail Jussa Ladhu, kurudi kwenye meza ya mazungumzo na CCM ni kupoteza wakati na kuwahadaa wananchi.
Bw. Ladhu ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Makao Mkuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni, amesema kwa sasa mtu pekee anayeweza kuokoa jahazi
hilo ni rais Kikwete.
``Tukubali, tusikubali rais Kikwete ndiye mwenye uwezo wa kuokoa jahazi hili, na hatuwezi kurudi katika meza ya mazungumzo tena, kwa kuwa ni kupoteza wakati na kuwahadaa wananchi wetu,`` akasisitiza.
Amesema bado nafasi ipo na kwamba kama JK atakaoonyesha nia ya kutaka kuzungumza nao, watampa nafasi na ushirikiano unaotakiwa.
Licha ya chama hicho kumwachia jukumu hilo zito rais Kikwete, kimetaka suala hilo lisichezewe shere kwani ni zito na linahusu mustakabali wa taifa.
Amesema kwa hatua iliyofikiwa sasa, ni budi suala hilo likashughulikiwa kama yalivyoshughulikiwa masuala ya Kenya, Comoro na la sasa la Zimbabwe.
Bw. Ladhu amesema njia pekee za kuweza kufikia makubaliano katika mazungumzo hayo ya muafaka, ni kwa CCM kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na kamati ya mazungumzo ya vyama vyote viwili na endapo Halmashauri Kuu ya CCM imeyakubali kimsingi, basi wakubali kutia saini na utekelezaji uanze mara moja.
Amesema njia nyingine ni kwa Rais Kikwete kuchukua hatua za haraka kuitisha mkutano wa pamoja kati yake na wadau wakuu wa masuala hayo ya Zanzibar, ambao ni Rais Amani Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad kujadili na kukubaliana juu ya mapendekezo yaliyotolewa na NEC.
Chama hicho kimewaomba wanachama wake wa Zanzibar
na Bara kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki wakijua kuwa CUF iko upande wa amani, ukweli na haki.
SOURCE: Alasiri
Mheshimiwa Ismael Jussa Ladhu (Kumbaro wa Shamba) Kwa nini unashadidia tu Rais Karume akutane na Seif. Mdau mkubwa wa suala la muafaka nni CCM Bwana rudi mezani ukutane na Kamati ya mazungumzo iliyoteuliwa.

Jeshi la Polisi nchini, limesema halitawaruhusu ndugu wa watuhumiwa wa `uhaini` waliokamatwa kisiwani Pemba kwenda kuwajulia hali mahala wanakohifadhiwa.
Aidha, jeshi hilo limesema ndugu hao wasiwe na wasiwasi kwani ndugu zao wako salama na wakiumwa wanapatiwa huduma za kimatibabu kama binadamu wengine.
http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/05/15/114417.html
BUBU
Mzee tunakuomba next time post paragraph moja au mili za mwanzo kusha weka lina kwa sababu ya masuala ya copyright.
hilo ni ombi tuu
mfano hivi:
hii itatuondolea kadhia ya kujibu barua za hawa watu wenye mipango ya ku sue na ma lawyers ambao wanahustle kutafuta kesi kwa niaba ya haya magazeti
Nia si kuharibu bali nia ni kuwekana sawa na kulindana
"Maamuzi ya CCM hajabadilisha jambo lolote la msingi katika makubaliano ya Mwafaka –no deviation on fundamental agreement – Tulichofanya sisi ni kuongeza jambo la kuwashirikisha wananchi na kuwataka wanaoendesha majadiliano kulifikiria na hili."
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI..
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL
COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENTS OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI..
Sasa wakati wa kurudi mezani,Rais aviambia CCM and CUFAsema vyama hivyo vinakubaliana kimsingi na kuwa tofauti ni utekelezajiRAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa baada ya vyama CCM na CUF kuwa vimeweka misimamo yao kuhusu Mwafaka hadharani, sasa ni wakati wa kurudi mezani kuendeleza majadiliano.
Rais pia amesema kuwa anaamini kuwa majadiliano hayo hatimaye yatazaa matunda mazuri kwa mustakabali wa Tanzania.Rais ameyaeleza hayo kwa nyakati tofauti leo katika majadiliano na wageni ambao alikutana nao Ikulu,mjini Dar es Salaam.
mazungumzo yake na Waziri wa Nchi wa Ufaransa anayeshughulikia Mahusiano ya Kimataifa na Nchi Zinazozungumza Kifaransa, Alain Joyandet, Rais ametumia muda kumwelezea mgeni historia ya majadiliano ya mwafaka na sababu za msingi zilizopelekea kuanzishwa kwa majadiliano hayo.Naamini mambo yatakwenda vizuri.
Hatimaye tutafanikiwa katika hili la mazungumzo la Mwafaka, amesema Rais Kikwete na kuongeza kuwa, kimsingi, CCM na CUF vinakubaliana kuhusu mambo ya kufanyika juu ya Mwafaka, na kuwa tofauti ni katika utekelezaji wa hayo yaliyokubaliwa.CCM wanataka suala hilo kubwa la msingi liamuliwe moja kwa moja na wananchi.
CUF wao wanataka wanasiasa kuamua kwa niaba ya wananchi. Hivyo, tofauti iko katika namna ya kutekeleza yaliyokubaliwa, amesema.Rais pia amemweleza Waziri huyo kuwa uamuzi wa kuwa na Serikali Shirikishi katika Zanzibar ulichukuliwa miaka saba iliyopita, mwaka 2001, wakati wa majadiliano yaliyozaa Mwafaka wa Kwanza kati ya CCM na CUF.
Rais amesisitiza kuwa uamuzi wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha karibu cha Butiama, Musoma haukubadilisha makubaliano ya msingi kati ya vyama hivyo.Kilichofanyika ni CCM kuongeza mapendekezo mawili ili nayo yajadiliwe na timu za vyama hivyo viwili.Amesema kuwa pendekezo moja ni kuwashirikisha wananchi kuamua utekelezaji wa mwafaka kati ya vyama hivyo,na la pili ni kuweka utaratibu wa ukomo wa utekelezaji (sunset clause) wa mwafaka huo.
Amesema mwafaka unalenga kuitoa Zanzibar katika matatizo ya sasa ya kisiasa. Hauwezi kuwa utaratibu wa daima dumu na kuwa ukifika wakati kuwa mfumo huo wa utawala wa kisiasa umekamilisha kazi yake, basi unaweza kuondolewa na Zanzibar ikarudi katika ushindani wa kawaida wa kisiasa.Amesema kuwa hivyo ndivyo ilivyokuwa katika nchi za Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),na sasa katika Kenya.
Katika mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Adam Woods, Rais amesisitiza kuwa bado iko nafasi ya kuokoa mazungumzo hayo ya Mwafaka.Wote sasa wamezungumza kiasi cha kutosha. Sasa ni wakati wa kukaa chini na kuendelea na mazungumzo, Rais amemweleza Balozi huyo.Amesisitiza: Maamuzi ya CCM hajabadilisha jambo lolote la msingi katika makubaliano ya Mwafaka no deviation on fundamental agreement Tulichofanya sisi ni kuongeza jambo la kuwashirikisha wananchi na kuwataka wanaoendesha majadiliano kulifikiria na hili.
---------------
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Mei, 2008
Crap! Wananchi waamue nini? Mwafaka unakubaliwa kwanza kisha mabadiliko ya katiba ndio kura ya maoni. Wito wa kura ya maoni kwa CCM ni hewa maana hawasemi kura ya maoni ya nini? Utakuwa vipi na kura ya maoni bila mwafaka?