MUAFAKA: Kusuasua na Ufafanuzi wa Kikwete - Je, Yote ni Msukumo Kutoka Nje?

Ndugu Zitto,
Mimi naomba sana kueleimishwa ktk hili..
Ni sababu zipi zinazotunga huu Muafaka wa vyama viwili jinsi ya kutawala nchi zima?..
je unatokana na uchaguzi wa mwaka 2000 au 2205 na kama ndivyo... Je matokeo ya uchaguzi huo yako wapi ambayo yanahallalisha kuundwa kwa Muafaka huu.
Tatizo langu kubwa sio kufikia Muiafaka wa kisiasa kati ya CCM na CUF isipokuwa vipengele vilivyosimamiwa..
Kwa nini iundwe serikali ya Mseto - what if - Jahazi Asili au United People Demokratic (UPDP) cha Fahmi Nassoro kikishinda uchaguzi mwaka 2010 kutakuwepo na utaratibu gani..
Sina wasiwasi na Chadema kwa sababu nyie tayarc mmekwisha jenga muafaka kati yenu na CUF hivyo siwezi kuingilia zaidi isipokuwa kwa chama kama CCM< nashindwa kuelewa sababu inayounda muafaka unaohusu Mustakabali wa nchi nzima kusimamiwa na vyama viwili tu.
Na mwisho, napenda kuuliza what's wrong kuuliza wananchi kwanza? kuna tatizo gani hapa ikiwa CCM wanataka swala hili liamuliwe na wananchi badala ya vyama viwili.. Kama alivyosema JK hili ndilo tatizo hadi sasa hivi kwa nini CUF hawatakli wananchi washirikishwe hali sauti hii ikipelekwa kwa wananchi itawageuka CUF zaidi kwa kutaka kuingia mkataba kisiri...
Je, Muafaka huu una kwa jinsi wanavyotaka CUF una tofauti gani (kwa wananchi) kati yake na ile mikataba ya madini?


Ndugu Mkandara,

Suala zima la mwafaka wa kisiasa ni lazima liwe na wachezai wakuu yaani key players. Hapa ni CCM na CUF. Ndio maana katika miafaka baada ya makubaliano yanayohusu wananchi watatawaliwa namna gani, inabidi kwenda katika kubadili sheria au kubadili/kuandika katiba ya nchi. Hapa suala linakuwa kubwa zaidi ya vyama. Linakuwa ni suala la wananchi wote kabisa. Key players wanakuwa ni chachu tu na ndio maana katika sheria hakitatajwa chama cha siasa bali yatatajwa mazingira ya kisiasa.

Kwenye suala la Zanzibar, CCM wanataka wananchi waulizwe mnataka mwafaka au sio! Kimantiki hili haliwezekani, kwani wakikujibu ndio maana yake ni kuwa ni lazima ukabadili katiba ya nchi na kutunga baadha ya vifungu upya. Wakisema NO ni mbaya zaidi kwani hutakaa uwe na mwafaka hata kama ukihitajika siku za usoni. Ndio maana taratibu ni wanasiasa kuongea, wanasheria kuandaa muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba ua kuandika katiba mpya kabisa na kisha wananchi wanaulizwa mnataka katiba hii au hamtaki. Wakikataa, katiba ya zamani inatumika, wakikubali katiba mpya inatumika na hivyo unakuwa ni mwafaka wa umma na sio wa vyama.

Mwafaka wa sasa ni kufuatia hali ya kisiasa ya zanzibar toka uchaguzi wa mwaka 1995,sio uchaguzi uliopita tu. CCM wanacheza siasa na CUF kuna makosa ya kimsingi kabisa wanafanya. Kwa mfano suala hili ni lao tu na sio vyama vingine, wanakosa mawazo mbadala na kujikuta hata mapendezo ya mwafaka kuonesha picha ya wao tu (narrow picture).

Matokeo yake nchi ipo katika hatari sana wakati huu, na itakuwa hatari zaidi kwani viongozi hawajitokezi kuprovide leadership. Malumbano ya kijinga kabisa (UVCCM) ambayo hayana chembe ya utamaduni wetu wa kisiasa
 
GT itakuwa vizuri kama utaiweka hapa ukumbini hiyo article au link kuhusiana na wenye magazeti kutaka kufungua kesi dhidi ya habari zao kuwekwa hapa ukumbini au ukumbi mwingine wowote.
 
Mwafaka wa sasa ni kufuatia hali ya kisiasa ya zanzibar toka uchaguzi wa mwaka 1995,sio uchaguzi uliopita tu. CCM wanacheza siasa na CUF kuna makosa ya kimsingi kabisa wanafanya. Kwa mfano suala hili ni lao tu na sio vyama vingine, wanakosa mawazo mbadala na kujikuta hata mapendezo ya mwafaka kuonesha picha ya wao tu (narrow picture).

Matokeo yake nchi ipo katika hatari sana wakati huu, na itakuwa hatari zaidi kwani viongozi hawajitokezi kuprovide leadership. Malumbano ya kijinga kabisa (UVCCM) ambayo hayana chembe ya utamaduni wetu wa kisiasa
Haya maneno!...
sasa vyama vingine mnajishughulisha vipi kuhusiana na Muafaka huu.
Je, CUF ni mwakilishi halali wa vyama vya Upinzani Visiwani ktk kujenga mapendekezo au ndio kama ulivyosema hapo juu..
Mengine ya CCM tuyaache kama yalivyo kwa sababu hakuna asiyejua kwamba CCM siku zote ni waburuzaji kisiasa lakini wananchi hawatategemea kuona chama kingine cha Upinzani kikijaribu kuburuza Visiwani na CCM kuwa ndio kinga pekee ya Uburuzaji huo.
Mwisho mkuu hukunijibu sababu zilizojenga hoja hii ya Muafaka. Matokeo ya mwaka 1995, 2000 na hata 2005 kwa kiasi fulani ni matokeo yaliyopikwa... why now wakati muafaka wa kisiasa kulingana na uchaguzi hudumu miaka yake mitano tu kabla ya uchaguzi unaofuata kwa hiyo sioni bado connection ya mambo ya mwka 1995 kuyaleta leo hali kilichotakiwa ni kuboresha zaidi katiba yetu ktk sehemu za uchaguzijambo ambalo haliwahusu CUF wala CCM peke yake.
Mbali na yote haya, watu wote wanafahamu kuwa CCM alicheza mchezo mchafu miaka yote hiyo lakini tunapokuja kubali mchezo ule na kuujengea ngome nyingine ya Muafaka ambao utajenga mseto wa vyama viwili nje ya mapendekezo ya wananchi unafikri hii ni haki?..Ikiwa Karume l;eo hafai kusimama pale inakuwaje mnampa mshirika wakati hafai kuwa rais kulingana na matakwa ya kura za wananchi?..
Ikiwa wananchi wameisha chagua chama iwe CCM ama CUF kuwa ndio mshindi iweje serikali iundwe kwa kushirikisha chama kilichoshindwa ili mradi tu kuondoa uhasama kati ya vyama viwili ambavyo vyote vinakubali mwongozo mzima wa Demokrasia ktk kutawala. je, kuna ujenzi wa aina mpya pinzani na ule unaowapa wananchi nguvu ya kuchagua mtawala?
Hata Uhuru wetu ulipatikana kwa kura za wananchi baada ya TANU kushinda lakini kama tutataka kucheza mchezo waliokuwa wakicheza Zanzibar chini ya Utawala wa sultan toka uchaguzi wa mwaka 1959, sidhani kama hii italeta suluhu ya utawala mzima na pengine utajenga zaidi uhasama.
Binafsi nadhani jambo la kufanya ni kundwa kwa kamati maalum ambayo itahusisha wanasiasa, Wanasheria, Wazee wa baraza wote toka pande mbili kwa sababu swala hili ni zaidi ya mkataba wa madini wa Buzwagi ama Richmond!..kwa sababu athari zake zinaweza jitokeza ktk National Security.
 
BUBU

Mzee tunakuomba next time post paragraph moja au mili za mwanzo kusha weka lina kwa sababu ya masuala ya copyright.

hilo ni ombi tuu

mfano hivi:




hii itatuondolea kadhia ya kujibu barua za hawa watu wenye mipango ya ku sue na ma lawyers ambao wanahustle kutafuta kesi kwa niaba ya haya magazeti

Nia si kuharibu bali nia ni kuwekana sawa na kulindana

Wewe nawe unajifanya kuwa unajua kila kitu hapa jamiiforums. Kazi yako kupondea wanachofanya wengine. Hakuna wa kumshitaki bubu kama amesema kilichobandikwa hapa kimetoka wapi.

Unajifanya kujua kila kitu kumbe bange tu. Ndio maana ulikurupuka na maneno ya Chenge kunywa sumu.
 
GT itakuwa vizuri kama utaiweka hapa ukumbini hiyo article au link kuhusiana na wenye magazeti kutaka kufungua kesi dhidi ya habari zao kuwekwa hapa ukumbini au ukumbi mwingine wowote.

Bubu wewe endelea na kazi yako na uachane na huyo GT. Yeye kila siku kazi yake ni kupinga kila kinachofanyika hapa.

Wengi tunapenda unavyoweka habari hadi na maoni ya wasomaji ili kuweka picha kamili ya habari.
 
Unajua napata PM toka remote areas kama namabengo kule songea na kwingineko wanasema link zinawapa shida kuzifungua kwa hiyo wameniomba niendelea kuweka habari kama ninavyoziweka. Mpaka hapo nitakapoona article inayodai wenye magazeti yao wanataka kufungua kesi dhidi ya habari zao kuwekwa hapa, mimi nitandelea kuziweka habari kama kawa.
 
Tukubali Rais wetu hana msimamo! Haya mambo angekuwa ameyamaliza Butiama! Yaani hakuwa hata na uwezo wa kutabiri migogoro kama hii! Kiongozi asiyeweza hata kutabiri vitu vidogo namna hii kweli anashangaza! Sasa anaanza kujikosha, si ni yeye aliyewatuma akina Kingunge nk kutema fitina, leo anajifanya mazungumzo yatafanikiwa! Kwani yeye ni nani, mpaka aseme hivi! (He represents one of parties to the negotiations) Sana sana angeweza kusema mazungumzo hayawezi kufanikiwa kwa sababu yeye na chama chake hadi sasa wameonyesha kuwa they are capable of spoiling! Kufanikiwa kwa mazungumzo ni pande mbili kuridhia (it takes two to tango).

JK ni mpenda sifa jamani na anaogopa sana lawama ndio maana tumefika hapa tulipo! Rais hana maamuzi jamani! CUF kurudi kwenye mezani kwa style iliyopita haitakuwa na maana! Mimi nadhani la msingi, maadam Rais wetu anaweza kugeuka ili kufarahisha watu basi sasa na ageuke aseme chama chake kimeridhia muafaka kama ulivyokuwa!

Mimi hata sielewi hivi huyu Karume wanamwogopea nini! Jeshi hana, akili hana! Sasa nini cha kumwogopa mpaka wamweche aharibu nchi yake? Viongozi, watawala - waachienie watanzania angalau amani tu. Uchumi mnaharibu, majizi mnafuga, basi tuachieni angalau amani! Mtu leo unaamka kwenda kusuluhisha mgogoro wa Uganda na DRC, Kenya, Comoro nk wakati kwako kunawaka moto? Hivi kweli hiyo migogoro ndio inayokukosesha usingizi kuliko huu wa nyumbani! Mbona hamjifunzi, mkapa alidhani yeye ni mtu wa kimataifa, leo hii amemaliza urais anaishi Tanzania na magazeti anayosoma na watu 'wanaompungia' mikono ni watanzania! Si angeishi uingereza au Uswisi.

Hizo sifa mnazopenda hazitawasaidia sana. Sanasana mnawafanya wasioijua Tanzania waanze kutake interest, and one striking thing they immediately see is the problem in Zanzibar!! Hawaoni Kilimanjaro wala Ngorongoro! Kwa sababu kwa wazungu kilimanjaro ngorongoro na zanzibar havitengani (they are three in one). Najua kwa nini mnaogopa kumface Mugabe! Ni kwa sababu hatawakopesha, atawaambia mmeshindwa kushughulikia madogo ya Zanzibar mnakuja huku!!! Mungu ibariki Tanzania. Kama mmeshindwa kila kitu, tuachieni angalau amani na udugu basi!
 
danganya toto kwa ajili ya umaarufu nje ya nchi na si vinginevyo. fungua macho JK nyumba inateketea
 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa baada ya vyama vya CCM na CUF kuweka misimamo yao kuhusu muafaka wa Zanzibar hadharani, sasa ni wakati wa kurudi mezani kuendeleza majadiliano.

Rais pia amesema kuwa anaamini kuwa majadiliano hayo hatimaye yatazaa matunda mazuri kwa mustakabali wa Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana, ilisema kuwa rais aliyaeleza hayo kwa nyakati tofauti katika majadiliano na wageni ambao alikutana nao Ikulu, mjini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yake na Waziri wa Nchi wa Ufaransa anayeshughulikia mahusiano ya kimataifa na nchi zinazozungumza Kifaransa, Alain Joyandet, rais alitumia muda huo kumwelezea mgeni historia ya majadiliano ya muafaka na sababu za msingi zilizosababisha kuanzishwa kwa majadiliano hayo.

“Naamini mambo yatakwenda vizuri. Hatimaye tutafanikiwa katika hili la mazungumzo ya muafaka,” alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa, kimsingi, CCM na CUF vinakubaliana kuhusu mambo ya kufanyika juu ya muafaka, na kuwa tofauti ni katika utekelezaji wa hayo yaliyokubaliwa.

“CCM wanataka suala hilo kubwa la msingi liamuliwe moja kwa moja na wananchi. CUF wao wanataka wanasiasa kuamua kwa niaba ya wananchi. Hivyo, tofauti iko katika namna ya kutekeleza yaliyokubaliwa,” alisema.

Rais pia amemweleza waziri huyo kuwa uamuzi wa kuwa na serikali shirikishi katika Zanzibar ulichukuliwa miaka saba iliyopita, mwaka 2001, wakati wa majadiliano yaliyozaa muafaka wa kwanza kati ya CCM na CUF.

Aidha, rais alisisitiza kuwa uamuzi wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha karibuni cha Butiama, mkoani Mara, haukubadilisha makubaliano ya msingi kati ya vyama hivyo.

“Kilichofanyika ni CCM kuongeza mapendekezo mawili, ili nayo yajadiliwe na timu za vyama hivyo viwili,” alifafanua.

Alisema kuwa pendekezo moja ni kuwashirikisha wananchi kuamua utekelezaji wa muafaka kati ya vyama hivyo, na la pili ni kuweka utaratibu wa ukomo wa utekelezaji wa muafaka huo.

Katika mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Adam Woods, rais alisisitiza kuwa bado iko nafasi ya kuokoa mazungumzo hayo ya muafaka

Source: Tanzania Daima
 
"Naamini mambo yatakwenda vizuri. Hatimaye tutafanikiwa katika hili la mazungumzo ya muafaka," alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa, kimsingi, CCM na CUF vinakubaliana kuhusu mambo ya kufanyika juu ya muafaka, na kuwa tofauti ni katika utekelezaji wa hayo yaliyokubaliwa

KIKWETE STOP BLUFFING..!!!!!

Mambo hayaendi vzr, kila mtu anajua, watu hawawezi kuwa wamewekwa kizini na ndugu zao wasiruhusiwe kwenda kuwaona, kwa kutuhumiwa uhaini halafu useme mambo yanaenda vizuri

Mambo hayaendi vzr, kila mtu anajua, haiwezi kuwa pemba wamegoma kusafirisha chakula unguja (hasa dunia ikuwa inatikisika kwa uhaba wa chakula) ikiwa inajulikana kuwa unguja inategemea kuasi kikubwa cha chakula kitokacho pemba halafu useme mambo yanaenda vizuri

Mambo hayaendi vzr, kila mtu anajua, CUF hawawezi kutoa kauli ya kutorudi tena mezani kujadili muafaka halafu useme mambo yanaenda vizuri

Mambo hayaendi vzr, kila mtu anajua, ikiwa kiongizi wa UVCCM kutoa vitisho kwa CUF na kutoa kauli kama hizi "Muda wa kuwabembeleza CUF umepita, na UVCCM inawasubiri uwanjani katika uchaguzi mwaka 2010 na siyo kulilia ushindi wa mezani," hawawezi kutoa kauli ya kutorudi tena mezani kujadili muafaka halafu useme mambo yanaenda vizuri
 
CCM hawako serious waseme kabisa hakuna muhafaka mpaka baada ya uchaguzi wa 2010 kwani karume alishasema alishinda kihalali na hana mpango wa kugawana madaraka na mtu yeyote, kuwa wakweli kutawafanya CUF wajue wanafanya nini badala ya kuwambia kuwa watapewa nafasi za uwaziri wakati si kweli.

Majadiliano yasimamiwe na raisi mwenyewe kuonyesha kuwa yuko committed.
 
Bwana namba kuuliza kwanza tafadhali nitoeni ushamba. Jamani hii Jamii forums ndo ile Jambo forums? Sijakuwepo kijiweni hapa kwa kitambo kidogo sasa naona mabadiliko,
 
Nshukuru sana ndugu Tuandamane kwani kwa ufisadi huu watu wanaweza kutupiga kiini macho
 
Hayo yalikuwa mazungumzo na wazungu,tena ikulu,Tunataka atokee sasa ktk mazungumzo na wananchi wote ambao mwafaka unawagusa moja kwa moja.

Tanzania DAIMA walikuwepo ikulu au walipewa tu taarifa na Salva?Tutathibitishaje kama Rais katoa hiyo kauli maana kwa siku za hivi karibuni kila kukicha tunasikia kauli nyingi za watu tofauti tofauti kuhusu huo mwafaka.

Let him appear to the public and adress it
 
Nshukuru sana ndugu Tuandamane kwani kwa ufisadi huu watu wanaweza kutupiga kiini macho


Hawawezi tena moto unawawakia kila kona ya nchi watu wamaamka, na huu ni mwanzo na hawa jamaa hawajaamka bado wanakoroma tuu..... siku zao Zimefika
 
kikwete anajibabaisha kwa kuwa ameulizwa kuhusu muafaka na wazungu.
ccm haina msimamo, kila anayetaka anafungua tu mdomo na kutoa maoni yake, mengine ya kichochezi pia.
the guy is not serious, na muafaka haupatikani kwa leo wala kesho
 
CUF nafikiri kauli yao huyu Kikwete hajaisikia ,nakumbuka kila wanaporapu CUF wanasema hawarudi tena.
 
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL
COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI..
Sasa wakati wa kurudi mezani,Rais aviambia CCM and CUFAsema vyama hivyo vinakubaliana kimsingi na kuwa tofauti ni utekelezajiRAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa baada ya vyama CCM na CUF kuwa vimeweka misimamo yao kuhusu Mwafaka hadharani, sasa ni wakati wa kurudi mezani kuendeleza majadiliano.
Rais pia amesema kuwa anaamini kuwa majadiliano hayo hatimaye yatazaa matunda mazuri kwa mustakabali wa Tanzania.Rais ameyaeleza hayo kwa nyakati tofauti leo katika majadiliano na wageni ambao alikutana nao Ikulu,mjini Dar es Salaam.

mazungumzo yake na Waziri wa Nchi wa Ufaransa anayeshughulikia Mahusiano ya Kimataifa na Nchi Zinazozungumza Kifaransa, Alain Joyandet, Rais ametumia muda kumwelezea mgeni historia ya majadiliano ya mwafaka na sababu za msingi zilizopelekea kuanzishwa kwa majadiliano hayo.“Naamini mambo yatakwenda vizuri.

Hatimaye tutafanikiwa katika hili la mazungumzo la Mwafaka,†amesema Rais Kikwete na kuongeza kuwa, kimsingi, CCM na CUF vinakubaliana kuhusu mambo ya kufanyika juu ya Mwafaka, na kuwa tofauti ni katika utekelezaji wa hayo yaliyokubaliwa.“CCM wanataka suala hilo kubwa la msingi liamuliwe moja kwa moja na wananchi.

CUF wao wanataka wanasiasa kuamua kwa niaba ya wananchi. Hivyo, tofauti iko katika namna ya kutekeleza yaliyokubaliwa,†amesema.Rais pia amemweleza Waziri huyo kuwa uamuzi wa kuwa na Serikali Shirikishi katika Zanzibar ulichukuliwa miaka saba iliyopita, mwaka 2001, wakati wa majadiliano yaliyozaa Mwafaka wa Kwanza kati ya CCM na CUF.

Rais amesisitiza kuwa uamuzi wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha karibu cha Butiama, Musoma haukubadilisha makubaliano ya msingi kati ya vyama hivyo.“Kilichofanyika ni CCM kuongeza mapendekezo mawili ili nayo yajadiliwe na timu za vyama hivyo viwili.†Amesema kuwa pendekezo moja ni kuwashirikisha wananchi kuamua utekelezaji wa mwafaka kati ya vyama hivyo,na la pili ni kuweka utaratibu wa ukomo wa utekelezaji (sunset clause) wa mwafaka huo.

Amesema “mwafaka unalenga kuitoa Zanzibar katika matatizo ya sasa ya kisiasa. Hauwezi kuwa utaratibu wa daima dumu na kuwa ukifika wakati kuwa mfumo huo wa utawala wa kisiasa umekamilisha kazi yake, basi unaweza kuondolewa na Zanzibar ikarudi katika ushindani wa kawaida wa kisiasa.†Amesema kuwa hivyo ndivyo ilivyokuwa katika nchi za Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),na sasa katika Kenya.

Katika mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Adam Woods, Rais amesisitiza kuwa bado iko nafasi ya kuokoa mazungumzo hayo ya Mwafaka.“Wote sasa wamezungumza kiasi cha kutosha. Sasa ni wakati wa kukaa chini na kuendelea na mazungumzo,†Rais amemweleza Balozi huyo.Amesisitiza: “Maamuzi ya CCM hajabadilisha jambo lolote la msingi katika makubaliano ya Mwafaka –no deviation on fundamental agreement – Tulichofanya sisi ni kuongeza jambo la kuwashirikisha wananchi na kuwataka wanaoendesha majadiliano kulifikiria na hili.â€
---------------
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Mei, 2008
 
Bwana namba kuuliza kwanza tafadhali nitoeni ushamba. Jamani hii Jamii forums ndo ile Jambo forums? Sijakuwepo kijiweni hapa kwa kitambo kidogo sasa naona mabadiliko,

Mzee Angalia date of joining? Angalia thanks na post zako.. kwa vyovyote vitakuelezea jambo fulani..

Usiku Mwema.
 
Back
Top Bottom